January akizindua kitabu kuhusu Bumbuli
Nimewaiteni kwa mambo mawili. Kwanza, kuzindua kitabu nilichokiandika. Pili, kuzungumzia uvumi na minong’no kwamba natarajia kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bumbuli.
Nianze na jambo la pili. Baada ya kutafakari kwa kina, na kuzungumza na wana-Bumbuli wenzangu, nimeamua niombe fursa ya kuwa sauti yao, kuwawakilisha na kuwasemea Bungeni, kuwatumikia na kushirikiana nao kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jimboni kwetu.
Kuendelea hadi mwisho wa tamko hili la January BOFYA HAPA
haya mambo yamewadia. Nimefurahishwa sana kuona January kaaza safu kwa ajili ya Kujikita katika kinyanganyiro cha Ubunge.
ReplyDeleteHii inanipa faraja kwani sasa tutegee akina Dr Shayo, John Mashaka nao wako mbioni. Hii itaongezea chachu ya vijana wetu bungeni.
Dr Shayo wewe unaweka sera bayana Lini? Jimbo yako la Vunjo ninakuhitaji.
usiwaangushe wazee
KWELI SIASA NI MCHEZO MBAYA HASA KATIKA NCHI ZETU HIZI ZA WATU WENYE NJAA ZA DUNIA YA TATU NA HASA AFRIKA, WATU WANALILIA VYEO KUGANGA NJAA ZAO TU SI KUINUWA MAENDELEO YA WATU NA HII IMEONESHWA NA JANUARY MAKAMBA MWENYEWE KATIKA KITABU CHAKE JINSI ILIVYOKOSOWA HALI HALISI YA BUMBULI NA HIYO NI BUMBULI TU, NA SEHEMU KUBWA YA TANZANIA IKO HIVYO, HAMNA SHULE WALA MABENKI, HATUTOFIKA KOKOTE KULE KAMA HATUTOKUWA WAKWELI WA DHAMIRA ZETU, SOMA KITABU CHA JANUARY UTAONA JINSI TULIVYOOZA
ReplyDeleteHaya watanzania umefikia wakati wa kupokezana uongozi, kila kiongozi ampigie debe mtoto au ndugu yake apate kula, Ridhwani nawe gombea, sisi walala hoi tukale wapi. Hivi kuna mtu anategemea akichuana na Januari au Ridhwani.
ReplyDeletehongera baba!!waondoeni hao wazee,tunataka vijana zaidi.
ReplyDeletemichuzi na mie natangaza nia kugombea uwanja wa fisi.
ReplyDeleteNi haki yake kikatiba...lakini mhhh!!!! it tells the direction we're. Siku moja tusishangae tukiwa kwenye serekali za kifalme kwa staili nyengine, Gabon imeshatokea, DRC ndo hivyo tena, Znz imeshatokea, USA ndo walisha-nusa hili, anyways yato haya hayajalisi as long as he's a good leader,but tuwe macho yanakuja!
ReplyDeleteAnkal sikukuona kwenye kashuguli haka au ulipigwa chini,mimi leo nilivyosikia huyu jamaa anaenda kutangaza nia nikasema ngoja nikamuone kwasababu nimemsikia sana hasa kwenye mitandao kuna mtandao mmoja kila siku kuna topic mpya juu yake,nikasema ngoja nikamuone ingawa sikupangiwa huu mzigo mimi hapa newsroom sasa kwanza nimeshangaa kukuta ukumbi umejaa,yaani wahariri mabosi wetu pekee walikuwa zaidi ya ishirini, nikasema ya leo kali anaumbuka mtu,jamaa kachelewa kama dakika kumi,kukatokea mkangayiko kwanza. Shuguli hii kaandaa nani kwasababu mc alikuwa nevile meena halafu tena walikuwepo kinadada wengine sijui wa kampuni gani,sasa bwana mdogo kaingia na suti yake na tai ya ki-obama obama.katumbulishwa akaanza kuzungumza ndipo nikashangazwa.hakuwa anasoma popote kazungumza kwa dakika kama 25 bila kusoma karatasi na kwa ufasaha nikashangaa kwamba huyu sio yule wanayesema kilaza kule jf?sisi tumezoea hapa press conference mtu anakusomea statement yake mwenyewe katazama chini,lakini huyu bwana mdogo alionyesha kujiamini sana na kuzungumza kwa kutulia,mimi kwa hili pekee amenivutia,jambo la pili ni kwenye maswali na majibu,kaulizwa maswali ya kizushi kayapangua yote bila shaka tena mengine kwa utani na hadi watu wakaishiwa na maswali,nimetoka pale nimebadilika sana mawazo kuhusu bwana mdogo.ana safari ndefu kwenye nchi hii
ReplyDeleteNdugu Kalwalwa,
ReplyDeletesio "nyengine" ni "nyingine" hahahaha nakutania tu ndugu yangu ni umetoa wazo la kweli.
mdau, massachussets
Yale yale Namimi nibadirishe last name yangu. SIJUI NIJIITE MICHUZI?
ReplyDeleteBosi nakuona na suti kubwa ndugu yako wa Galanos aka Nguvumali Sec, bweni la Pamba. Big up bosi ila usitusahau kwenye ufalme, toka zamani ulionekana kiongozi. Tulikuchagua Depurty Head Boy nakumbuka baada ya muda ukataka kujiuzulu baada ya Mama Msemo kutulazimisha kulima kwenye saa za kipindi cha darasani na ukagoma kusimamia zoezi lile na ukamwambia mama wa kipare yule achukue cheo cheo tangu siku ile nilijua utakuja kuwa kiongozi wa watu.Nakumbuka ulikuwa huli na wanoko wengine viongozi kwenye ofisi ya uongozi ile iliyokuwa kwenye njia ya mabanda ya kuku ulikuwa unakula na sisi bwaloni,labda hukumbuki.Songa mbele songa mbele bosi
ReplyDeleteJamani wadau huyu bwana ana uwezo wake binafsi acheni ushamba wa kumgasi kwasababu tu ya ubini wake. Mumuhukumu kwa dhambi zake sio kwa ubini wake kama baba yake yumo kwenye siasa yeye anakosa haki ya kuingia kwenye siasa mimi nimeshangazwa kwasababu ni mmoja wa watu waliokuwa wanaamini kwamba anabebwa sasa nimemuona mwenyewe nimesoma maelezo yake nimesoma blogu ana uwezo mkubwa kuliko asilimia tisini ya watu humo serikalini.
ReplyDeleteLove him or hate him January ni mmoja wa very few smart Tanzanians. Watu wengi watasema ooh sijui baba yake or sijui nini lakini kwa tunaomjua jamaa tunakubali ni very smart.
ReplyDeleteEniwei, I will bet you guys $ 100 jamaa atagombani urais 2015.
Ankal zote siasa hizi na wanasiasa kwa changa la macho ndio wenyewe lakini angalau huyu hata kama ni changa la macho lakini lina akili kidogo,kajitahidi kaonyesha njiaTunasubiri utekelezaji. GodBless!
ReplyDeleteLookin' good future prezzo! Usitusahau na wala usianze kula rushwa.
ReplyDeleteMimi nashindwa kuelewa hawa watu wanaishi mjini, wamekulia mijini shida za watu huko utazijuaje?
ReplyDeleteIna maana ukipata ubunge utahamia huko Bumbuli au ndio itakua safari moja kwa mwaka...We need to be serous... na watu wenye majimbo yenu muwe makini. Mumpe kura mtu anaye waelewa na atakayewatete haki zenu sio muwape kura watu kwa popularity zao...
Na utupe hii kapuni pia...
WAPAMBE WENGI DAH , KWELI WAPAMBE NOMA.
ReplyDeleteSomeni historia yake kwenye blogu za mitaani. Alipomaliza shule ya msingi alikwenda shule ya kulipia. Alipomaliza sekondari ikabidi tena aende shule ya kulipia. Alipomaliza high school, ikabidi afanye kazi kule alikokuwa baba yake Kigoma. Kwa nini? Tuseme tu kwamba tunamuunga mkono lakini kwamba ana sijui akili, wala hakuna kitu kama hicho. Kasoma Marekani kwa pesa za baba yake tena baada ya kusota miaka Kigoma, kwa nini hakutinga mlimani pale penye waliofaulu form six?
ReplyDeleteushatangaza sasa jiandae kwa wenye chuki kuanza kukuonea wivu na kukutukana.
ReplyDeleteBUMBULI - Yesterday, Today and tomorrow! ndivyo kinavyoitwa kitabu hicho.
ReplyDeleteMimi nina asili ya Bumbuli natamani sana kukisoma kitabu hicho, ila lugha inanipiga chenga, kipo cha kiswahili chake??
Mnyarugusu
Mkuu Jan Makamba sasa jiandae na chuki sasa za waosha vinywa ambao hata hawakujui na hawajui uwezo wako. nimeona wengine washaanza humu eti oh anakaa mjini oh...ujuha mtupu! viongozi siku zote ni elites huo ndio ukweli, hata wanamapinduzi wote walikuwa elites wamesoma zaidi na wanakaa mijini. Nenda mbele kaza buti mkuu! tunasubiri matokeo.
ReplyDeleteMdau wa july 06, 05:47:00, Kama humjui Januari Makamba kaa kimya. Kasoma Galanos, shule ya Serikali. Kasoma Forest Hill Moro na kwa mujibu wa hoja yako anapungukiwa na sifa ya uongozi kwa sababu eti kasoma high school ya kulipia. Ujuha mtupu! Na kwasababu hakusoma Mlimani basi hafai kuwa kiongozi? Ujuha mtupu! Tatizo lako umelisema mwenyewe kwamba unasoma blog za mitaani. Get the facts!
ReplyDeleteGuys this is the courage we need among our young people. I am very proud of the future of our country. A young has decided to do something. There are two type of people: - those who roll their sleeves and go to work, and those who are there to comment on what is happening or has happened. This young man has rolled his sleeves. Let us join him! I don't care where he went to school or who his father is, I am judging him for what he has done and as far as I am concerned this is admirable. No one can argue that this is not admirable.
ReplyDeleteShule ni Shule tu iwe ya kulipia ama Goverment la muhimu ni mwisho wa siku utoke na Elimu bora kwa manufaa yako na Jamii inayo kuzunguka kwa ujumla. Sisi hayatuhusu kama amesoma USA ama Kigoma kama amesoma kwa fedha za baba yake ama Goverment na vile vile kusoma Mlimani siyo ndio kufaulu form six wangapi tunaona wanapewa nafasi Mlimani kwa Rushwa?
ReplyDeleteHukumu ya huyo mgombea ni October kama Raia watamkubali awatumikie ama vinginevyo. Kila la kheri Watanzania wenzangu ktk Uchaguzi Mkuu.
Leo headlines magazeti yote Bongo ni Bumbuli funika mbaya. Hata sheni hajawahi kupata hii.
ReplyDeleteSWALI LANGU BADO LIKO PALE PALE. HIVI MTU HAWEZI KUSHIRIKI KATIKA KULETA MAENDELEO KATIKA JAMII YAKE BILA KUWA MBUNGE?
ReplyDeleteUBUNGE NI KWA FAIDA YA MGOMBEA AU YA WANANCHI?
HOFU YANGU NI PALE WATU WANAPOFANYA UBUNGE KUWA AJIRA YA KUENDESHA MAISHA YAO.
umeula uuu,rudi kwenu kijijini.
ReplyDeleteJAMANI UKIPERNDA CHONGO UAITA MAKENGEZA, AKILI KILA MTU ANAZO, NA KAMA UMEJIANDAA NA KITU HAKUNA HAJA YAKUSOMA TOKA KWENYE KARATASI, SI MTU MWENYE KICHWA HIVYO KAMA WATU MNAVYOSEMA MBONA AMEKUWA AKISOMA KWA KUUNGA UNGA HIVYO NGAZI ZOTE ZA HUKU CHINI ZA MSINGI ALIFELI ALIFELI DARASA LA SABA, ALIFELI DARASA LA KUMI NA MBILI NI PESA TU NDIZO ZILIZOMELEKA HAPO ALIPO SO MTU YOYOTE KAMA AMESOMA HADI ALIPOFIKIA YEYE ANAWEZAKUCHAMBUA MAMBO KAMA ALIVYOCHAMBUWA YEYE. KILA MTU AKIPATA NAFASI ANAWEZA KUONYESHA UWEZO WAKE NI KWAMBA WATOTO WA MASIKINI HAWANA NAFASI NA HAWAJAPEWA NAFASI YA KUONYESHA UWEZO WAO
ReplyDeletemaswali mengine yamekaa kiushuzz tu, ati mtu anauliza utakuwa unakaa bumbuli au mjini, ina maana wabunge woote bongo wanaishi kwenye majimbo yao walikochguliwa??? mfano mzuri tu mbunge mo' dewji wa singida mjini, anaishi dar lakini kila mara yuko jimboni kwake akishirikiana na wananchi wake bega kwa bega, na asilimia 90 ya wabunge hawaishi majimboni kwao huwa wanakwendaga kwa msimu tu!
ReplyDeleteCopies za hiki kitabu ‘BUMBULI’ zisije zikawa ‘sold out’, maana huko Beijing wa-chinese na wanafunzi wao walivyo wacheshi watamsoma ‘BUMBULI’ mapema mapema tu - ‘sold out’
ReplyDeleteMimi narudi tena kuchangia suala hili, napingana na hoja nyingi hapo juu, huyu jamaa simjui ila nasikia tu kama baba yake ni katibu mkuu wa ccm na yeye ni msaidizi wa rais japo sijui katika eneo gani, ila tusimuhukumu kwa ubini wake kwa kuwa ni haki yake kikatiba, na suala la kama kasoma kigoma ama USA iwe kwa kulipiwa na pesa za baba yake ama la. Jamani wote tunajua mazingira ya Tanzania kufaulu ama kuto faulu kwa mtu kunatokana na factors nyingi mno, suala la UDSM kuwa ni sehemu ioneshayo uwezo wa mtu kichwani nakubaliana nalo, japo wapo watu wengi tu waliokatiza hapo na bado ufanisi wao na fikra zao zinakuwa na walakini, hebu tujiulize kwenye Bunge letu wangapi wamepita pale UDSM, je ni wote wenye kufanya mambo ya msingi? so scientifically hatuwezi ku-conclude kwamba UDSM ni suluhisho la viongozi bora! najua mnanielewa. Sasa nije kwenye hoja yangu ya msingi, ningekuwa mimi ndo January nisinge tangaza kugombea ubunge sasa, ningekuwa mimi mzee makamba nisingeruhusu mwanangu agombee ubunge sasa, ningekuwa mwana ccm nisinge ruhusu huyo kijana agombee sasa, kwa mwanasiasa makini,chama makini, na "mtu makini kama January," maana sina uhakika ni watu tu ndo wanatoa sifa kedekede, nisingegombea wakati huu, katika hali hii hamna mtu atakaye amini ni uwezo wake bali ni kubebwa na baba mwenye wadhifa mkubwa ndani ya chama,hii ni kuzidi kuondoa imani kwa baba yake, chama na yeye mwenyewe, maana nasikia amesomea conflict resolution ameshindwaje kuliona hili, ni kwa namna gani baba ata acha kutumia mabavu yake kuhakikisha mwanae anapita, maana wote twamjua mzee makamba,sipingi kwa yeye kugombea ila anataka ubunge kipindi ambacho tunaamini kuna "conflict of interest," kitu ambacho kinanitoa imani ya yeye mwenyewe kama mtu makini, nadhani ange concentrate na kumshauri Rais, ama angesubiri mpaka baba aondoke madarakani, hii inaonesha namna baadhi ya viongozi wasivyo waadilifu, narudia tena KWA WATU MAKINI HAWAWEZI KUFANYA HIVI, na kwa kujua sisi Watanzania huwa tunalalamika kwa kunong'ona tu ndo wanakandamiza, tusubiri tuone hii filamu ya UCHAGUZI 2010.
ReplyDeleteMimi ni mwandishi wa habari na mara kibao nimekuwa kwenye misafara ya rais ndani na nje ya rais. January nimekuwa nikikutana naye mara kwa mara na nadiriki kusema HE IS A LEADER. Kweli sitashangaa kumwona siku moja anakuwa rais wa nchi hii. Ni mtu mwema asiyependa makuu. Kwa baba yake naye kuwa mwanasiasa, that is just accidental. Go January go.
ReplyDelete