Na Mwandishi Maalum, Madrid, Hispania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaja sababu kuu za umasikini wa Bara la Afrika, na kupendekeza mambo saba ambayo anasema kuwa yakifanyika yatachangia kuliondoa Bara hilo katika udhalili wa umasikini wa sasa.
Aidha, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Bara la Afrika limeboreka sana katika miaka 15 iliyopita, na sasa liko tayari kutoa mchango wake katika jumuia ya kimataifa kama juhudi za pamoja za Bara hilo na Jumuia ya Kimataifa zitaendelezwa kuboresha hali katika Bara hilo.
Rais Kikwete alisema hayo kwenye ufungaji wa Mkutano wa Kimataifa Kuhusu Maendeleo ya Afrika na Nafasi ya Siasa za Maendeleo katika Bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara uliofanyika katika Jumba la Palacio de Congresos de Madrid, mjini Madrid, Hispania.
Rais Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi wa kimaendeleo kutoka Bara la Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na chama tawala cha Hispania cha Socialist and Workers Party of Spain (PSOE), chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) pamoja na taasisi isiyokuwa ya kiserikali yenye uhusiano wa karibu na PSOE ya Fundacion Idea.
Pamoja na Rais Kikwete kwenye ufungaji wa Mkutano huo walikuwa ni Rais wa Cape Verde, Mheshimiwa Pedro Pires; Waziri Mkuu wa Hispania, Mheshimiwa Jose Luis Rodriguez Zapatero; Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi; Rais wa zamani wa Serikali ya muda ya Liberia, Mheshimiwa Amos Sawyer; na Rais wa chama tawala cha FPI cha Ivory Coast, Mheshimiwa Pascal Affi N’Guessan.
Wengine walikuwa ni Rais wa chama tawala cha Ghana cha National Democratic Congress, Mheshimiwa Kwabena Adjei na Katibu Mkuu wa Chama cha Kisoshalisti cha Senegal, Mheshimiwa Ousmane Tanor Dieng ambaye pia alikuwa mgombea urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu uliopita.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Rais Kikwete alitaja sababu kuu na chanzo cha umasikini wa Afrika kuwa ni pamoja na mazingira adui ya kimataifa dhidi ya Bara la Afrika ambayo ni pamoja na ukoloni, mfumo adui kabisa wa kiuchumi duniani ikiwa ni pamoja na nafasi finyu za Afrika kufanya biashara na ukosefu wa masoko ya uhakika ya Afrika kuuza bidhaa zake, tena kwa bei ya haki.
Rais Kikwete amesema kuwa sababu nyingine za umasikini wa Afrika ni siasa za nchi za Afrika zenyewe ambazo huko nyuma hazikuzaa matunda yaliyokusudiwa na zilizolazimishwa kwa nchi za Afrika na taasisi za kimataifa za Bretton Woods – yaani Benki ya Dunia na Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani (IMF).
“Lakini makosa mengine yalikuwa ya kwetu wenyewe, ikiwa ni pamoja na sera ambazo hazikuzaa matunda na mgawo mkubwa mno wa ukosefu wa utulivu wa kisiasa, mapigano, upinduaji wa Serikali,” amesema Rais Kikwete na kuongeza huku akishangiliwa na mamia ya washiriki wa mkutano huo:
“ Tulikuwa hakuna nafasi ya kufikiria jinsi ya kuondoa umasikini na kuendeleza watu wetu kwa sababu tulikuwa na kazi na shughuli za kupigana, kugombea madaraka na kuuawa.”
Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa hali ya Afrika imebadilika sana katika miaka 15 iliyopita. “Hili siyo tena Bara la ovyo, siyo Bara ombaomba tena. Tuna utulivu mkubwa zaidi wa kisiasa, ukiondoa Somalia, Bara la Afrika halina mgogoro wa kisiasa ambao kwa sasa hauna majibu yake. Demokrasia inapaa, kuna hali bora zaidi ya utawala bora, tunapambana kweli kweli na rushwa, tunajali haki za binadamu. Tunafanya vizuri, lakini tunahitaji kufanya vizuri zaidi kwa kuwekeza katika hali na maisha ya watu wetu.”
“Sasa tufanye nini?” Rais Kikwete alijiuliza mwenyewe na kuanza kutoa majibu ya kuongeza kasi ya kulitoa Bara la Afrika na watu wake katika umasikini akisisitiza:
“La kwanza ambalo lazima tufanye ni kudumisha na kulinda mafanikio ambayo tumeyapata mpaka sasa. La pili ni kuwekeza zaidi katika watu wetu. Tunahitaji kuboresha zaidi elimu, kuwapa watu wetu maji safi na salama, tunahitaji kujenga miundombinu bora zaidi kwa maana ya barabara, njia za umeme, kuboresha mifumo ya reli na bandari zetu.”
Rais Kikwete amesema kuwa jambo la tatu linalostahili kufanyika ni kufanya mageuzi ya kuboresha kilimo cha Afrika.
“Asilimia 70 ya watu wetu wanaishi katika sehemu za mashamba na shughuli yako kubwa ni kilimo. Hii ndiyo njia rahisi ya kuwatoa watu wetu katika umasikini. Afrika ina asilimoa 10 tu ya wakazi wote wa dunia, lakini Bara letu lina asilimia 30 ya watu wote masikini zaidi duniani.”
Rais Kikwete amezitaja njia nyingine za kulitoa Bara la Afrika katika umasikini haraka zaidi kuwa ni pamoja na kuanza mageuzi ya ujenzi wa viwanda hasa vile za kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.
“Hatuwezi kuendelea kuuza mazao ghafi kwenye masoko ambayo yanabadilisha thamani ya mazao hayo na kutuuzia mazao yetu wenyewe tena kwa gharama kubwa zaidi.”
Ameongeza kuwa njia nyingine za kulitoa Bara la Afrika katika umasikini ni kuongezeka kwa uingiaji wa mitaji katika Bara hilo. Kwa sasa Bara la Afrika linapata asilimia mbili tu ya mitaji yote ya uwekezaji duniani.
Rais Kikwete ametaja ongezeko kubwa zaidi la biashara kama njia nyingine ya kupunguza umasikini wa Afrika. Kwa sasa Afrika inachangia asilimia mbili tu katika biashara duniani. Pia ametaja umuhimu wa kuongeza kasi ya ushirikiano wa kikanda miongoni mwa nchi za Afrika na umuhimu wa kumalizika kwa mazungumzo ya kuleta mfumo mpya wa kibiashara duniani chini ya majadiliano ya Doha.
Akizungumza baada ya hotuba ya Rais Kikwete, Waziri Mkuu Zapatero alikubaliana na mapendekezo mengi ya Rais Kikwete na kuahidi kuwa Hispania imeamua kuwa sehemu na kuchangia ya maendeleo ya Afrika. “Napenda kutangaza kuwa kuanzia leo hii Hispania iko ndani ya Afrika, na Afrika iko ndani ya Hispania.”

JK ameongea point tupu. I think Industrial revolution ndio inayotakiwa Africa. We don't have to keep depending on kilimo peke yake. Tukumbuke Industrial revolution itaboresha hata kilimo chetu duni na kukifanya kuwa kilimo cha kisayansi.
ReplyDeleteIndustrial revolution italeta ajira kwa watanzania. Jaribu kufikiria ni vitu gani tunaweza kuzalisha wenyewe nyumbani? We don't produce anything right now. Kila kitu tunaagiza nje.
Eniwei, Spain wenyewe wako miguu juu sasa hivi. So hamna haja ya kuwategemea kutusadia.I think we can do on our own. Mambo ya kutegemea misaada yameshapitwa na wakati. We can raise money toka kwenye Internationa Capital Markets, blanace our budget and help our people.
Long Live Africa!
Nadhani ubinafsi, kukosa uzarendo na kutopanga vipaumbele vinavyostahili ndio sababu kubwa ya umaskini Afrika.
ReplyDeleteAmesahau na ubinafsi wa viongozi wa afrika wa kujilimbikizia mali na pesa kuliko hata uwezo wao.Waafrika ni wabinafsi sana kwa hio nionavyo mimi maendeleo ni ndooto za mchana.waache wapige domo tu hapo.
ReplyDeleteu have a poit jk.go jk
ReplyDeleteTarehe Tue Jul 20, 12:47:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous
ReplyDeleteNadhani ubinafsi, kukosa uzarendo na kutopanga vipaumbele vinavyostahili ndio sababu kubwa ya umaskini Afrika.
#Tarehe Tue Jul 20, 12:54:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous
Amesahau na ubinafsi wa viongozi wa afrika wa kujilimbikizia mali na pesa kuliko hata uwezo wao.Waafrika ni wabinafsi sana kwa hio nionavyo mimi maendeleo ni ndooto za mchana.waache wapige domo tu hapo.
Nakubaliana nanyi. Aache visingizio vingine maana vimekuwa kama santuri mbovu inayojirudia rudia. Tuangalie mapungufu yetu kwanza-uongozi wa kijambazi ulioweka vipa umbele wao kwanza kuliko maendeleo ya wananchi ndio sababu kubwa ya umaskini. Ukitatua tatizo hilo, utatatuzi wa matattizo ya nje yatakuwa rahisi sana kutatua. Angalia nchi zilizokuwa maskini, lakini kwa kupitia uongozi bora na sera zinazowalenga wananchi wameweza hata kushinda matatizo ya kimataifa...mfano nchi za Asia kama China, Singapore n.k.
Viwanda tumeua na sasa tunaomba tujengewe vingine.Nadhani bado naamini Sera za mwalimu zilikuwa sawa kabisa ila wabinafsi waliziingilia na kuzitilia mizengwe mingi na leo hii ndio tunapata tabu.Wakulima wa Pamba walikuwa wanajua ni wapi watauza pamba zao na wakulima wa korosho ni hivyo hivyo sasa leo hii hakuna viwanda na inabidi tutegemee masoko ya nje na bei za kupangiwa.
ReplyDeleteUjamaa na Kujitegea ndio jibu ukichanganga kwa maarifa siasa ya Ubepari, na sio kukurupuka na kuchukua kila kitu cha siasa za capitalism, Ndio maana tunaona milipuko ya bei za nyumba na kodi za nyumba kwenye nchi yetu ambazo ni sawa kabisa na za ughaibuni.
Tumekurupuka kufuata mifumo ambayo haiendani na hali yetu ya nchi.mfano bei za vitu kuwa kwa fedha za kigeni, hili ni tatizo kubwa.
Mjusi
Majibu ya jumla yasiowakuna wabadhilifu na wabinafsi. Kwa kuwa ulikuwa ugenini pengine isingekuwa busara kumwaga kuku kwenye mtama mwingi. Tunaomba ukirudi ongelea sababu za msingi za watanzania kuendelea kuwa maskini na mapendekezo ya suluhisho.Hizo hadithi zipo hata kwenye vitabu vya historia. Elezea mpango mzima, umeshajifunza urais, NDIO tumeona sasa fanya mambo n not bla blaa!!!
ReplyDeletetalk too much do very little....a big problem.Actions are required than too much words
ReplyDeleteMimi naona kama antucheza shere tu....the lessons learnt are there we just always keep on repeating same choirs and songs....kilimo kilimo kilimo...Mbona budget haiboreshwi..., Viwanda vinakuja baada ya uzalishaji kuwa mkubwa, maana hapo ndipo watu wanapo thik big on how to improve the storage and added value, industrial revolution malighafi utatoa wapi? Tulikuwa na viwanda vingapi na vimekufa kwa uzembe wao hao waliomadarakani....Yeye JK asubiri muda wake upite akapumzike tutampa mwingine naye hivyo hivyo huku tunaendea kufa kwa njaa na magonjwa.
ReplyDeleteTatizo la africa ni vipengere vya sheria vimewapa viongozi mamlaka ya kuwa dicteta,wizi wa mali ya umma, corruption, unqualify friends, chama kina wenyewe and elimu duni ya viongozi.
ReplyDeleteMKUU WA NCHI WA SPAIN NI RAIS NA SI WAZIRI MKUU, MARA NYINGI VYOMBO VYA HABARI VYA NJE YA SPAIN HUPOTOSHA JAMBO HILI KWA VILE WANAFIKIRI KILA NCHI YENYE KUONGOZWA NA MFALME/MALKIA BASI MKUU WA NCHI NI WAZIRI MKUU, NO, THAT IS ONLY FOR THOSE COUNTRIES FOLLOWING WESTMINSTER SYLE OF GOVERNMENT, AND SPAIN IS NOT ONE OF THEM. KUHUSU KIKWETE AMEONGEA VYA MAANA, LAKINI PIA VIONGOZI WETU PIA NI WENGI WAO NI WABOVU HAWANA UELEWA WA KWA NINI MAENDELEO YANAHITAJIKA KWA WATU WOTE. VITA PIA NI HUTOKANA NA UMASIKINI, SIASA MBOVU NA ZA GIZA NA UONEVU PIA NI KWA SABABU YA UMASIKINI NCHI KAMA IKO WAZI NA NI AFADHALI KATIKA UMASIKINI HAYO YOTE YATATOWEKA, WATU HUUWANA ILI KUSHIKA DOLA WAIBE ILI WAONDOKANA NA UMASIKINI LAKINI KAMA KUNA NAFASI SAWA YA WATU KUJISHUGHULISHA KATIKA MAPAMBANO YA MAISHA YAO HAKUTAKUWA NA SABABU YA VITA NA WIZI USIO NA SABABU HIVI VYOTE VITAKWISHA NA AMANI ITAKUWEPO. WATU WAPEWA NAFASI SAWA KULINGANA NA UWEZO WAO NA MATAKWA YAO UPENDELEO WA WAZI NA USIO WA SABABU TUANCHANE NAO KAMA TUNATAKA KUJENGA AMANI NA MAENDELEO YA WATU WOTE. VIONGOZI WAACHA KUFIKIRIA WAO NA NDUGU ZAO WAFIKIRIE NCHI NZIMA NA WATU WOTE WANAWAONGOZA, NDUGU ZAO PIA WAACHEZE TABIA YA KUWABUGUZI VIONGOZI WETU KWA KUTAKA UPENDELEO USIO WA LAZIMA WAJE HUKU TULIKO SISI TUCHEZE PAMOJA KATIKA UWANJA MMOJA WA KUYATAFUTA MAENDELEO ILI WAWAPE VIONGOZI WETU NAFASI YA KUTUFIKIRIA SISI SOTE, WAACHE HIYO TABIA YA KUINGIA KATIKA CHUMBA CHA MWAMUZI WAJE KATIKA CHUMBA CHE SISI WACHEZAJI NA TUKITOKA NCHI UWANJANI TUCHEZE SAWA KWANI SOMETIMES DAMU NI NZITO KULIKO MAJI WATAKAPOKUWA WANAKILIMBLIA MARA KWA MARA KWA MFANO KWA RAIS NA RAIS NI NDUGU ZAKE NI LAZIMA ATATOWA UPENDELEO HATA KAMA HAWASITAILI NA VIVYO HIVYO KWA VIONGOZI WOTE BASI NA SISI WANANCHI WENYEWE LAZIMA TUJUWE CHEO NI DHAMANA NA KWA AJILI YA SISI SOTE TUWAPE NAFASI VIONGOZI WETU KUONGOZA NCHI VIZURI KWA USAWA NA KWA WOTE. VIONGOZI WA LEO WANATAKIWA WAWE NA VISION FOR THE FUTURE, WAWE NA MAWAZO YA KIKWETE WAWE NA UCHUNGU WA NCGHI NA WANANCHI WAKE WOTE, WAONE MBELE NA WATAKE KUONA NCHI YA YA BAADAYE ITAKUWAJE, CHA MSINGI NI UTAWALA WA WAZI, BORA, HAKI NA UNAOFUATA SHERIA, MFANO WA KUIGWA NI WA CHINA PAMOJA NA KUWA CHINA INASEMEKANA INAKIUKA SANA HAKI ZA BINADAMU LAKINI CHINA HAKUNA HATA KIONGOZI MMOJA MWEZI ANAYEJILIMBIKIZIA UTAJIRI KWANZA UKIGUNDULIKA NI KITANZI NA KIFO NI CHAKO. CHINA BAADA YA MIAKA KUMI HIVI IJAYO ITAKUWA NCHI TAJIRI KULIKO ZOTE DUNIANI HADI SASA NCHI ZOTE ZA WAZUNGU WANAKOPA PESA TOKA CHINA. JUZI NILISOMA VIONGOZI TAJIRI DUNIANI KATIKA LIST HIYO KUNA KIONGOZI MMOJA WA AFRICA NA NCHI YAKE NI NDOGO KAMA MKOA WA MOROGORO SASA JAMANI JUST IMAGINE KA NCHI KADOGO KAMA HAKO KIONGOZI YUKO KATIKA LIST YA VIONGOZI TAJIRI DUNIANI! HUU UTAJIRI AMEUPATAJE? KAMA SI WIZI? KENYA MBUNGE ANAPATA KARIBU SHILINGI 18,000,000.00 KWA MWEZI KWA KAZI GANI, HIZI PESA NI ZA WALIPA KODI NA ZINGEWEZA KUJENGA SHULE NYINGI TU KWA AJILI YA ELIMU

ReplyDeleteZapatero ni rais na si prime minister
ReplyDeleteNashukuru Raisi wetu ameongelea mambo muhimu ambayo yanalikwamisha Bara la Africa, mtu unasikiliza kwa machungu ukiona kumbe kiongozi au viongozi wa Afrika wanajua tatizo, ila hatuna kiongozi wa kutenda yale yanayoongelewa. Kwa sababu haya mambo tumeyaongelea saaaaaaana. Kwa nini hatutendi??
ReplyDeleteKuongelea ukoloni sasa hivi nafikiri kumepitwa na wakati. Sera za nyuma sio tena jambo la kuongelea. Kuuana kwa nyuma sio jambo (infact, hatujafikia mauaji yaliyotokea Ulaya!!).
Halafu, hatuna taifa la kushirikiana nalo?? Ahadi za Mh. Jose ......Zapatero nazitilia mashaka kwani Spain ni kati ya nchi maskini za Ulaya (yumo kwenye PIIGS), sijui kama ana msaada kwa sasa. Na kwa kweli hatuna msaada mkubwa tunaouhitaji kutoka popote nje, zidi ya kuwekeza kwa binadamu wa Bara hili. Juhudi za Raisi wetu kwenye Elimu linaonekana, lakini sio speed itakayowakomboa wananchi kwenye ufukara wa akili.
Na mkutano wa mambo ya Afrika (Sub-saharan Africa)kufanyika huko nje kuna maana gani? Tunakimbia nini Dar es Salaam?? au Abuja, Accra, Kinshasa hata Chigali??
Ama kweli!!Alishawahu kusema mwana wa Afrika Steve Biko kuwa "The most powerfull weapon in the hands of the oppressor is the mind of the oppressed!!"
Tujitambue sasa!!
Matatizo ya Africa hayafanani, na kwa kiongozi kama JK kugeneralize matatizo ya Africa ni kukosa uwajibikaji. Ameongelea vita na ukosefu wa utulivu, Tanzania hatukuwahi kupitia huko, nchi imekuwa salama toka tupate uhuru MBONA Tanzania bado ni masikini na ni moja ya nchi maskini kabisa barani Africa. Hii tabia ya viongozi wetu kucopy notes za walimu wa IDS sijui itaisha lini. Practically JK ambaye amekaa madarakani for nearly five yrs kama Raisi anashindwaje kuzungumzia practical problems za nchi yake with reference to Africa, anaongelea historia? Kwa nini tatizo la uongozi mbovu na rushwa hakulitaja kwa nguvu na la kwanza, amelificha ficha, anahighlight capital flow bila kujiuliza kama mazingira ya kufanya biashara ni mazuri. Mwekezejai wa kawaida anazungushwa na kutakiwa kutoa rushwa, matokeo yake genuine investors wanaondoka, wanakuja wapenda rushwa. JK kwa miaka yake amefanya nini kwenye viwanda. Kilimo, ni hivi majuzi tu kakurupuka na kilimo kwanza, miaka yake mitatu ya uongozi hakujua kilimo kitawapa ajira watu wengi? Na hicho kilimo kwanza cha kutegemea mvua na trekta za mgawo na wakati miti yote imeshakatwa na nchi ni jangwa, kweli kuna kilimo kwanza au ni slogan ya kujipatia kura toka kwa maskini wasiojua hata maana ya kura yenyewe. Kikwete anasema kuna good governance Africa? is he serious lol, yeye serekali yake ina good governance, anadai kuwa wanaheshimu haki za binadamu, huyu ndiye aliyesema kuwa ni muamuzi wa mwisho, hata mahakama ikiamua yeye akisema no ni no. Ni wakati muafaka kwa JK kuzungumza from his head and not from talking points alizoandaliwa na wanafiki wanaomsaidia. Halafu kuna watu wanasema JK katoa points, zipi? Ni kipi katika alichosema JK Mtanzania wa kawaida hajawahi kukisikia Swala la rushwa linaimbwa hadi kwenye nyimbo za injili, leo hii Kiwete kusema anapambana na rushwa bila kukiri kuwa rushwa ipo ni point? Kila nchi Africa imepitia mambo tofauti, sio nchi zote africa ni masikini, zile tu ambazo zimekuwa na uongozi mbovu na ufujaji wa mali za wananchi na ubinafsi wa kujilimbikizia mali ndizo zinaelea kwenye lindi la umaskini ikiwemo Tanzania. Mbona nchi zilizopitia kwenye vita zinafanya vizuri tu? Rwanda! Mbona nchi kama Botswana ziko vizuri tu, Liberia chini ya uongozi wa mwanamke yule chuma cha pua na wala huzioni kwenye mikutano feki kama huo wa Uhispania. Watembeza bakuli na wapenda vitrip ndio utawakuta kwenye vikongamano hivi, na nchi zao zinazidi kudidimia kila wanapochezea hela za walipa kodi kusafiri nje. JK anadai kuwa Africa imepiga hatua katika miaka 15 hii, lakini anashindwa kujua sio nchi zote za africa zimesonga mbele, Tanzania imerudi nyuma, angalia takwimu za umaskini zimeongezeka, so wakati wengine wanakwenda mbele, JK na watu wake wanasagura kurudi nyuma. Pia anasindwa kujua kuwa mabadiliko haya si kwa sababu ya juhudi za waafrika na viongzi wao wabovu, ni kubadilika kwa mfumo wa uchumi duniani. Africa imekuwa dampo LA BIDHAA HAFIFU, hatuzalishi bali tunaletewa vilivyozalishwa huko, sasa sijui JK anaongelea hatua gani? vita? sasa wale waliokuwa wanatuuzia silaha wameacha kwani wanataka stability ili waweze kutuuzia bidhaa zao feki, zenye faida kuliko silaha,by implication vita vitakwisha tu. Africa haijabadilika, ila imebadilishwa kuwa destination ya uchafu wote wa nchi matajiri na zile zinazoendelea kama China etc. Mbona Mwai Kibaki haendagi kwenye huo upuuzi, Watanzania mnaoufuatilia habari za nchi jirani, last time Kibaki kusafiri nje ya nchi ilikuwa ni lini? Mbona wawekezaji wanamiminika Kenya? Kwani lazima uwafuate? Kwani JK hajui ule usemi unaosema kibaya chajitembeza, kizuri chajiuza. Wawekezaji wanajua a-z ya hizi nchi kabla hawajatia timu kwenye nchi yoyote, hawahitaji JK kufunga msafara na watu ambao hawajui hata kufungua midomo kuja kuwaambia wakawekeze nchini? nchi isiyokuwa na umeme na maji ya uhakika Lol. Mungu ibariki TZ
ReplyDeleteNdugu mambo ni hayo hayo, hizo ni kelele za kila siku. Je nyumbani amefanya nini zaidi ya kuweka marafiki zake wanaokula bila huruma, nchi iko kwenye hali mbaya. Eti watu na akili zao wako na kijani, aibu tupu. Hivi anaona watu wote wajinga! Tujitambie kwa yapi?
ReplyDelete1. Kugeneralize matatizo ya Africa ni kukosa uwajibikaji.Africa ni bara, lenye nchi zaidi ya 50,na kila nchi ina historia yake na kiwango cha umaskini na maendeleo.The fact kwamba ni Africa then unazungumzia matatizo ya africa kiujumla ni ishara tosha kuwa JK hafahamu mengi kuhusu bara letu
ReplyDelete2. Kuna nchi Africa ambazo hazikuwahi kukumbwa na vita hata baada ya ukoloni. Tanzania ni mojawapo. Ghana ilitawaliwa na mapinduzi ya kijeshi na wanajeshi ndio waliirejeza Ghana nyuma, lakini sasa Ghana inawika na imeiacha mbali TZ
3. Tz tumeenjoy amani toka mkoloni alivyoondoka. Lakini tumerudi nyuma kwa kiasi kikubwa kuliko alivyotuacha mkoloni. Kuna barabara za enzi ya mkoloni. Baada ya uhuru tukajitahidi kujenga viwanda, tukajenga tabaka la kati, wataalamu wa kuharibu walivyopewa uongozi wakaharibu, wakaua tabaka la kati, wakajiwekea utajiri wachache, na wale wa tabaka la kati wakatupwa kwenye umaskini. Why JK analaumu vita, TZ haijawa kuwa na civil war,labda vita ya Uganda, sasa JK anavyohusisha vita na matatizo ya africa haoni kuwa anaingiza waliokuwemo na wasiokuwemo. Kenya imekuwa na vita vya ukabila, lakini iko juu kiuchumi kuliko TZ. Kwa nini JK asizungumzie Tanzania ambayo anaijua then afanye reference na nchi zingine za africa?
3. Na mengi mengi-- shida hapa si ukoloni,mkoloni aliondoka akaacha infrastructure intact, shule akaacha, reli akaacha, sisi tukaviharibu, why JK anaulaumu ukoloni uliotokea decades ago? Kwani mkoloni alivyokuja alitukuta tuna maendeleo gani? na alivyoondoka aliacha nini? Zimbabwe inaweza kulaumu ukoloni? sio uongozi mbovu umeididimiza ile nchi?
4. JK kwa nini asingekuwa tu mkweli akaweka "uongozi dhaifu" kama tatizo NO 1 la Africa
5.Na kwa nini JK amekuwa msemaji wa Africa, wakati nchi yake na wananchi wake wanaogelea kwenye lindi la umaskini, hiyo credibiliy ya kuongelea shida za Africa ameitoa wapi, wakati uongozi wake ni dhaifu?
6. JK anasema kuna good governance, alikuwa ana refer nchi zipi, TZ? Huwezi kutoa mifano ya jumla, kimsingi mawazo yake ni ya jumla, hayako specific, na ndio maana hakuna kitu kipya alichosema ambacho watanzania na waafrica hawajawahi kukisikia
7. Uchumi wa dunia umabadilika, Africa inaangaliwa tofauti, inaangaliwa kama destination ya uchafu na fujo zote zinazotokea kwenye nchi tajiri na zinazoendelea, Africa ni kichwa cha mwenda wazimu, bidhaa dhaifu peleka AFRICA, madawa dhaifu kafanyie research Africa. Kwa mtizamo wa JK anasema Africa imebadilika within last 15 yes, lakini hajasema specifically what attributes to the change. Kama mkuu wa nchi huwezi kutoa blanket statement kama hizo. Kachambua matatizo then akatoa majibu ya matatizo hayo, asilimia 90 ya majibu yapo ndani ya uwezo wetu na wa viongozi wetu na wala hayahitaji nguvu toka nje, sasa mbona yeye hafanyi?
8.Mbona viongozi wengi wa africa waliohudhuria ni watu wa chini na sio wenye hadhi ya ukuu wa nchi? JK alikuwa na sababu gani za kwenda? je TZ imefaidika na nini kwa kwenda kwake, kwa sababu ameeleza matatizo ya africa na majawabu yake anayo, kwa nini asingeachia kongamano likatoa mawazo mbadala badala ya yeye kusoma talking points zake alizoandikiwa na watu wanaocopy teaching notes za maprofessor wa IDS? Je kuan jipya alilojifunza?
9.Mbona zipo nchi za Africa zinafanya vizuri tu? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ili tuendelee tunahitaji mambo manne, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Labda kwa maisha ya sasa tunahitaji ICT pia. Tanzania ni yapi katika mambo hayo manne yanayokosekana, watu kibao, siasa sio mbaya, nchi ina utulivu,ardhi ni nyingi tu ya kumwaga. Uongozi-- hapo ndio kwenye shida!!
10.JK anajua ule usemi usemao, kibaya chajitembeza, chema chajiuza, wawekezaji wanaijua africa kuliko sisi waafrica wenyewe, wanajua pa kwenda, wanajua ni wapi kuna mazingira mazuri ya kufanya bishara, mbona Mwai Kibaki hatembezi bakuli la kuomba misaada, lakini wawekezaji kibao wako Kenya?
11. JK kwa mtizamo wako huo, sidhani kama tutafika. Rasilimali tulizonazo zinatosha kutufanya tuwe na kiburi, wenyewe watakuja tu bila kufuatwa. Kusanya nguvu za ndani, hamasisha umma kujenga nchi.
Wakuu si ni huyu alisema hajui kwa nini Tanzania ni masikini iweje leo azungumzie kuhusu Africa nzima??
ReplyDeleteAu sasa ndiyo amejua???
hapo Mh president kasema ukweli na mambo sahihi kabisa kwa Africa, ambacho hajakisema ni kutokujipanga kwa watawala wa nchi za kiafrica,pia hakuna priorities nini kianze na kifuate kipi,pili hakuna kujibana ktk matumizi makubwa ya viongozi ili kuelekeza funds,mind zote ktk uchumi,hakuna integrity kwa 80% ya watawala wa kiafrica,utawala wa kimabavu even if wanapreach democracy,vyama tawala huwa kama miungu,they can do anything at any cost to sustain their existence!
ReplyDeleteanony 2:36 pm true words you said. yale mazuri tuyasemayo hatuyandendi bali tunayoyachukia ndiyo tuyatendayo.. fed up already!!?
ReplyDelete