Marehemu Mzee JOHN STEVEN MUSHI aka MZEE MIWANI

Ni mwaka mmoja umepita tangu baba yetu mpenzi umetutoka.Majonzi mengi umetuachia lakini kwa sababu ni kazi ya Mungu nasi hatuna budi kumshukuru kwa kila jambo. Baba, pamoja na kwamba haupo pamoja nasi kimwili, lakini upendo wako, busara zako, ucheshi wako, utoaji wako na malezi bora uliotupa bado vipo pamoja nasi na ndio maana hatutakusahau.

Tunaamini kwa mazuri uliyoyafanya sio kwetu sisi tu bali na kwa watu wengine wengi; huko ulipo Mungu amekupumzisha mahali palipo pema zaidi. Baba haukupenda kuona mtu anateseka, ulikuwa tayari kuteseka ili familia yako tunufaike.

Ulitufundisha kuwa elimu ni silaha muhimu sana ambayo mtu hataweza kukunyang'anya: bali itakuwa nawe siku zote. Unakumbukwa sana na mke wako mpenzi Martha John Steven MUSHI, watoto wako Penda, Dr Kunda, Dr Cleopa, Shanande, Ufoo na FranciaWajukuu wako wanaokupenda sana na kuyafaidi matunda mema uliowaachia wazazi wao, Catherine, Ngapani Jr, Michael, Rodney, Mcshield, Moshe, Alinda, Sia na Doreen.

Kutakuwa na ibada ya shukrani itakayofanyika anapokaa mjane wa marehemu


REGENT ESTATE, 236 UKOMBOZI STREET tarehe 29/July saa 11 jioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2010

    Tunamkumbuka sana mzee mushi, mhangaikaji na mtafutaji sana, kapumzike mzee. Poleni sana wakina doc Kunda

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2010

    Mzee wa watu RIP

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2010

    RIP mzee Miwani, tunakukumbuka

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2010

    Huyu mzee kafariki lini tena? namfahamu tokea akiwa meneja wa mamlaka ya pamba, poleni sana wanafamilia

    Maleo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2010

    Babu mzee wa Range mererani tunamkumbuka sana tokea ameondoka vijana wako wamesambaratika sana. Mungu akuleza pema peponi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2010

    Penda,Kunda,familia ya mushi poleni sana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2010

    Mzee Mushi jamani,Mungu akulaze pema peponi. Tunakukumbuka sana na machine za kusaga pale Mwananyamala. RIP

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 28, 2010

    Mzee Mushi unakumbukwa sana pia na wanaregent wote na majirani wote mwenyezi mungu aistiri roho yako pahali pema panapostahili ,upo kwenye sala na maombi yetu ya kila siku RIP

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 28, 2010

    Mungu akupe furaha, pumziko na amani ya milele mzee, umesaidia watu wengi Mungu ndiye ayajua. mcheshi mpenda watu na mtoaji asiye kinyongo na mtu, hatutakusahau mzee mushi poleni sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...