Rais Jakaya Kikwete pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange na viongozi wengine wa jeshi wakitoa heshima zao leo wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita kuu ya Dunia 1939-1943.maadhimisho hayo yamefanyika leo asubuhi katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange akielekea kutoa heshima za kijeshi kwa kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita kuu ya Dunia 1939-1943,Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete akiongoza viongozi mbalimbali katika maadhimisho ya kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita kuu ya dunia 1939-1943,Mnazi mmoja leo.
Askari wa JWTZ wakitoa heshima za kijeshi
Rais Jakaya Kikwete akiweka ngao na mkuki kwenye mnara uliopo Mnazi mmoja wakati wa maadhmisho ya siku ya mashujaa,yaliyofanyika leo.
kiongozi wa mabalozi akiweka shada la maua.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wazee waliopigana vita kuu ya dunia 1939-1943 katika viwanja vya Mnazi mmoja leo.
Rais Aman Karume akisalimiana na wazee.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ally Hassan Mwinyi akifuatiwa na Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Fredrick Sumaye na viongozi wengine walipokuwa wakiwasalimia wazee waliopigana vita kuu ya Dunia 1939-1943 katika maadhimisho ya siku ya mashujaa leo.
Gwaride kwa Askari wa JWTZ
Gwaride kwa Askari wa FFU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2010

    Haya waosha vinywa . Semeni tena basi kama askari wetu wananjaa.

    Nafikiri mtataka kuweka vigezo kuwa askari awe na tumbo kama mimba changa ndiyo mseme wameshiba :-)

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2010

    Vita ya pili ya dunia ilipiganwa mwaka 1939-1945 na sio 1943!

    Tafadhali weka rekodi zako sawa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2010

    MAGEREZA WAKO WAPI?

    MBONA PORISHI WAMO KWANI NAO NI WAJESHI? AU WALIPIGANA?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2010

    akina Ras makunja wamependeza kweli na gwaride lao

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2010

    HAWA JAMAA WAMEKULA CHUMVI NA MUNGU AMEWAJALIA NA BADO WANAONEKANA WANA NGUVU MUNGU AWAWEKE KWA MUDA MREFU UJAO NAWATAKIA KILA LA KHERI, HAWA WATU WANASTAHILI HONGERA SANA NA PIA NASHAURI WAPATA KUTEMBELEA UPANDE WA NCHI WALIOKUWA WANAPIGANIA KAMA NI UINGEREZA BASI QUEEN AFANYE MWALIKO WATAMBELEE UINGEREZA, INAVYOONEKANA HUKU ULAYA WAMESHA SAHAU MCHANGO MKUBWA ULIOTOLEWA NA ASKARI WA NCHI ZA KI-AFRIKA, PIA WANASTAHILI PENSHENI NA MALIPO KIDOGO KWA MCHANGO WAO.

    NILIKUWA NA BABU YANGU ALIPIGANA VITA HII ALISHAFARIKI ZAMANI SANA ALICHUKULIWA TOKA LUATALA KIJIJI KILICHOKO WILAYA YA MASASI MKOA WA MTWARA ALITUHADITHIA SANA SAFARI YAO YA ADI BURMA, INDIA, CHINA NA MAAENEO MENGINE YA ASIA NA AFRIKA. WAKATI ANATUHADITHIA HABARI HIZO MIAKA YA 60 MWISHONI ALIKUWA BADO ANA UNIFORM ZAKE INTACT.

    LA MWISHO KAMA NILIVYOTOWA OMBI HAPO JUU WATU HAWA NI MUHIMU KWA HISTORIA YA NCHI YETU WATUNZWE VIZURI NA WAANDISHI WA HABARI JARIBUNI KWENDA KWA HAWA WAZEE WETU MUPATE HABARI YA KUWAELEZA WATANZANIA WA LEO JUU YA VITA KUU YA DUNIA YA PILI

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2010

    Mzee mmoja hapo kavaa kofia hizo ndo kofia zao zilikuwa ameitunza hadi leo anastahili sifa

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2010

    Hongera kwa maadhimisho, lakini nina hoja ya kujadiliwa hapa. Hivi harufu ya ukoloni itaendelea mpaka lini? Kwa nini kila tunapowakumbuka mashujaa wetu hukusanya wazee wa vita kuu ya pili ambao kimsingi haikuwa vita ya WATANZANIA?. kama ni kuwashukuru waliopigana hizo vita basi mashujaa wetu halisi, waliopigana kwa ajili ya TANZANIA tuliyonayo washirikishwe kwa dhati: Tunao, walioshiriki, Mapindizi Zanzibar, Comoro 1st & 2nd, Ushelisheli, Uganda, Mozambique 1st & 2nd, Zimbabwe, Africa ya kusini, Liberia nk. Wapo mashujaa wetu kweli kweli, waliojitoa mhanga kwa taifa letu. Wazee wa WW2 hao tunawaheshimu lakini ni pensioner wa Malkia, kwa nini wao?????????? Tujadili.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2010

    Picha ya saba hapo JK akisalimia na mzee mmoja amefanana na Thabo Mbeki, mie nikajua na Mbeki amepigana vita vya pili ya dunia ..LOL

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 26, 2010

    vita vya ushelisheli/comoro 1 vilikuwa vya baba mtakatifu nyerere sio vya kusherekewa,comro 2 vya jk, kama kweli anataka kuingilia vita vya watu/inchi za watu wengine atume jeshi somalia/mogadishu tuone ubabe wetu!!!!

    ReplyDelete
  10. This is amazing....veterans wa world war 2 asilimia 85 wa Marekani wapo kwenye wheel chair, in bad shape. Lakini hawa wanajeshi wapo wima na imara!

    Najiuliza....life expectancy ya Africanz iko chini sana kulinganisha na Wamarekani...je ni kweli?

    Hata kama ni kweli...ukiangalia, in real sense wazee wa huku West ndio wengine wanaishi mpaka 100+ years...lakini angalia hali zao, pacemakers, dementia, can't breathe on their own, they pop 20+ pills everyday...wa Tz sawa, labda ni kweli sio wengi wanaoishi Karne...lakini wanaoishi afya zao ziko imara zaidi.

    So this Western pride and bragging of Life expectancy is nonsense...afterall all our lives are in the hands of God!. Mtu anapatwa stroke 4 times, heart attack 8 anatibiwa...thanx for medical tech, But if all he can do is just laying down...everything is done by some machinery nae anahesabiwa miaka!!!...in realty he's DEAD!. If the heart cant pump blood through the system by itself, lungs cant function, brain is virtually dead......Is that person really alive?. It's the machines doing everything.

    This is controversial I know....criticize me if u want, but it's my opinion.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2010

    Ya vita vya WWII siyo vyetu.

    N hivyo muitavyo vyetu ni vya viongozi wetu.

    Na hao wanajeshi hawapigani bure wanalipwa kila mwezi mishahara mikubwa.

    Kwa nini mnasema wajeshi wamejitoa mhanga kwa nchi wakati ni ajira wanalipwa?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2010

    JESHI LA TANZANIA NI JESHI LA UKOMBOZI NA AMANI KUSINI MWA AFRIKA NA AFRIKA NZIMA.

    MBONA SOMALIA HAMPELEKI WAKASAWAZISHE AMANI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...