Tyson with his hosts in Madinah Friday


Former boxing champion Mike Tyson, who embraced Islam while serving a prison sentence in the 1990s, is on his first visit to the Kingdom to perform Umrah. He arrived in the holy city of Madinah on Friday to perform prayers at the Prophet’s Mosque.

While in Madinah, Tyson met Dr. Muhammad Al-Oqala, president of the Islamic University, who briefed the world heavyweight champion on the services being rendered by the university to students from across the world.
From Madinah, Tyson will travel on to Makkah to perform Umrah, press reports said. He will also visit Jeddah, Abha and Riyadh as part of his Saudi tour. His visit to Saudi Arabia was arranged by the Canadian Dawa Association (CDA) as part of visits it organizes for new Muslim celebrities to the Islamic sites in the Kingdom.
Shazad Mohammed, president of CDA, was present at Prince Muhammad International Airport in Madinah to receive Tyson.

Mohammed, an ambassador of peace with the United Nations, said Tyson would be in the Kingdom for one week, visiting the holy places as well as important landmarks in the country and meeting with Saudi people to get to know their culture and traditions.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2010

    mashallah

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2010

    subiri komenti za upande wa pili sasa. mtaona watu wanaanza kumtaja holifidi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2010

    Sisi tunaomba msimkane Tyson pindi atakapofanya utumbo wowote. Msije mkasema hakuwa mwenzenu. Ni tahadhari tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2010

    big up Tyson,hata kina Loon walifika hapo mwaka jana na kutembelea sehemu mbali mbali madina

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2010

    kwani nani humkana akifanya utumbo,mshaanza,nyie mnamkana elton john na george michael kisa magay

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 06, 2010

    Mashaallah, may Allah protect and help Tyson and us.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2010

    Kwa sisi tunaoishi Marekani tunajua kuwa Wamarekani weusi wengi wanaojulikana wanapenda kujiita Waislamu, ni hama fashion tu. Kuna wanafunzi wengi wanajiita waislamu chuoni lakini hawajui dini wala koran ni nini. Mike Tyson kama anataka kuwa Muislamu inabidi aondoe tattoo usoni ambayo si sheria kama unataka kuswali na ailimu na jina la kiislamu. Kuna akina Charles wengi tu Marekani wanajiita Waislamu.

    Vile vile utakuta macelebrity wao wanakimbilia Afrika Kusini kama vile ni "nyumbani" kwa kuwa Afrika Kusini imeendelea na wanaona karibu sawa na Marekani kimaendeleo. Tuliosoma historia ya ukoloni na Utumwa tunajua kuwa Waafrika waliopelekwa kama watumwa Marekani walitokea Magharibi mwa Afrika kama Nigeria, Senegal, Togo na kadhalika. Kwa nini hawaendi huko kutembea?

    Pia, utakuta Wamarekani Weusi wanasheherekea "Kwanzaa Day". Hii ni sherehe ambayo wanatumia lugha ya kiswahili (kibovu) na kutunga kuwa "nyumbani" wakulima wanasherekea Kwanzaa ina nguzo saba na kwa miaka mingi walikuwa wanadanganya watu kuwa hizi nguzo saba zimetoka Afrika. Mara nyingi huwa nawaambia kuwa hatuna hizi nguzo saba katika sherehe zetu na Afrika ni kubwa sana, kuna mila chungumzima, na hizi sherehe zimetungwa na Mmarekani mmoja anayejiita DR. Maulana Karenga ili nao wawe na sikukuu yao kama wazungu na watu wengine.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 06, 2010

    Nasubiri pale atakapomrushia ngumi mwarabu atakayejisogeza kumtaka a sign autograph. Tyson hatabiriki.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 06, 2010

    Mashallah
    kwa wanaoamini
    TTAKBIRRR SAY ALLAH AKBAR

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 06, 2010

    Mike Tyson was the man back then.Sasa hivi anakula pork tu sio muislam wala nini.Just Fronting.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2010

    ukiona intavyu zake mike tyson utasikitika manake wamempiga kichwa mpaka kauli yake ni kama ya mtu mgonjwa, labda hivi alivyomrudia mola watamwombea arudi kwenye chati, ila sababu utu uzima tena ndio tuombe mungu. enzi yake aliwika sana. sasa hivi anabaki kupiga mapaparazi si ya kuchekesha ila saa zingine hawa watu maarufu wana matatizo sana.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2010

    Uliyetoa comment za mambo ya ugay kuna watu au jamii kama ya kiarabu yenye kuenzi ushoga? Au kwa sababu unaona nchi za magharibi zinaruhusu unadhani uarabuni hakuna utumbo huo? Angalia maeneo yote waliyokaa waarabu yana hurka za kishoga Zanzibar, Tanga, Dar, Mombassa, Malindi, Lamu na kwingineko

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 06, 2010

    Uliye taja mambo ya Evender Hollifield unanikumbusha mpambano wao na Tyson nilishangaa kuona waislamu wote wanashabikia Tyson sababu tu walisikia kasilimu wakati wakristo walikuwa wamegawanyika wengine Tyson na Wengine Evender kwa hiyo muache kuwa single minded na ushabi wa kidini usio na maana dini zenyewe zimeletwa na watu wa nje yaani waarabu na wazungu za dini za kwetu ilikuwa kuabudu milima na mababu zetu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 06, 2010

    mla masikio

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 06, 2010

    sasa ww unaesema waarabu wanaenzi ushoga,kama ww ni mmoja wapo hebu jaribu kwenda hapo saudia uone cha moto.Unajua adhabu yake nn.KATA KICHWA.
    Unajua nchi zisizo za kiislam hasa zile za magharibi wanapromote hii kitu in public.Sasa hiyo inawaexpose vijana wadogo na wao kujiingiza kirahisi katika ushoga tofauti na nchi za kiarabu.Usitake kusema nchi inayoruhusu haya mambo ni sawa na isiyoruhusu.

    ReplyDelete
  16. Hold up people....
    Anon 03:14am. Sio fasheni wanavyojiita waislam, wengi wanamwelekeo mzuri ila baadhi hawajapata mafunzo sahihi. Wapo 5% Nation of islam, wapo Nation of Islam, na wapo sunni Muslims...hayo ni makundi makubwa ya wanaojiita waislam. Aliyesema kama mtu anatatoo inabidi aiondoe ili aweze kuswali kasema nani?, na nani kasema mwislamu lazima awe na jina la kiarabu?....Unaweza ukaitwa Charles Johnson na ukawa better muslim than anayeitwa Abdallah bin Muhammed. Sio lazima kubadili jina ndio uwe mwislam.

    Watu wengune kazi yao ku-judge tu, Tyson ni mwislam....na alikuwa mwislam tangu aliposilimu jela. Lakini Tyson ni human being with his baggages and problems, like all human beings. Yes he's been on the edge, yes he's been a thug, yes he's a lil crazy, yes he probably still smoke leaves...But that doesn't take him from Islam. Besides he's still alive and he's making Tawbah. Hata kama anakula nguruwe, bado anachance ya ku-improve.

    Just leave the man alone....let him do what he wants, can't you see that he's trying to improve his life and be a better man?

    May God forgive him and continue to guide him in the straight path. May god forgive us all.Ameen!

    ReplyDelete
  17. Lazima atulie maana ukienda hayo maeneo matakatifu lazima utatulia na kuwa mcha mungu wa ukweli.MAY GOD BLESS U TODAY AND FOREVER TYSON.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 06, 2010

    PLAIN SIMPLE FACT IS THAT TYSON AMEISHIWA HANA HATA SENTI MOJA ANACHOFANYA HAPO NI KUTAFUTA KULA, ANAJUWA UPANDE HUO UNA PETRO DOLLARS ATAZIKOMBA KIULAINIIIIII, NAJUWA KINACHOFANYIKA HAPO KWA UPANDE WA DINI NI KUPATA CHEAP POPULARITY WANAMTUMIA TYSON KAMA MARKETING TOOL YAO KWA VILE WANAJUWA DUNIANI KOTE WATU WATAFUATILIA JAMBO HILI NA LITAKUZA MASWALA YA DINI NA KUIENEZA, KWANI WANGAPI WANAJIUNGA NA DINI HIYO HAPA DUNIANI? NI WENGI TU MBONA!NA KWA NINI HAWATANGAZWI? NI KWA VILE SI WATU MUHIMU KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE, THEY ARE NOT ENOUGH MARKETING TOOLS, SO TYSON ANATUMIKA KAMA KITANGAZA DINI LAKINI KWA UPANDE WAKE ANA GANGA NJAA, NI NIPE NIKUPE ILI MRADI TUMBO LIJAE,

    KUHUSU MA-GAY JAMANI WAPO KIBAO UPANDE HUO WA DUNIA AMBAKO DINI ZETU HIZI ZILIANZIA, NIMEONA MWENYE DOCUMENTARY ZA REAL INTERVIEWS ZA MA-GAY IRAN, ISRAEL, SAUDI ARABIA, AFAGHSNSTAN, PAKISTAN, MALAYSIA, SYRIA, LEBANON WAPO WENGI TU WA KUMWAGA PAMOJA NA MADAWA YA KULEVYA. SO THAT IS NO A POINT TO RAISE HERE AT ALL, MASHOGA WAPO DUNIANI KOTE HATA MALAWI, EVEN PROSTITUTE WAKO KIBAO SEHEMU HIZO. MASWALA YA DINI NI MAMBO YA MTU BINAFSI KAMA WEWE NI MTU WA DINI SHIKA NA FUATA DINI YAKO USIJIONE KUWA WEWE NI WA DINI FULANI BASI UKAONA YA KWAKO NI BORA KULIKO YA MWINGINE HUO NI UPOTOVU WA DINI YAKO KWANI DINI ZOTE ZINASISITIZA UPENDO, KWANZA HAMNA USHAHIDI WOWOTE WA KUONYESHA KUWA HIZI DINI NI MAMBO YA KWELI, WACHA TU TUSIFUATE KUDUMISHA AMANI DUNIANI KWA FAIDA YETU SOTE. NIMEZALIWA NIMEKUTA WAZEE WANGU WAKIABUDU DINI NINAYOABUDU SIKUWA NA UCHAGUZI AS SIMPLE AS THAT, AND THAT IS THAT, JAMANI NENDENI MAKTABA MUKASOME MASWALA YA DINI I MEAN HISTORY OF RELIGIONS KAMA TUMBO LAKO SI KUBWA NA KIFUA CHAKO CHEPESI UTAACHA DINI SIKU HIYO HIYO.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 06, 2010

    Mi nashaaanga watu ohh tyson utafikir wai hizo tatoo hawana au umaluuni hawafanyi na niwaislam na misikitin kutwa.binaadam huws tunajisahau yetu kukalia ya wenzetu.ukifatilia sana wengi ni waislam majina ijapikuwa wamesoma na wanaielewa vizuuuri sana dini nayo.binaadam sisi nyoyo zetu dhaifu kwa mambo ya dunia most of ppl hiyo kitu tunayo so muacheni tu tson kwani hata nyie mnayo yenuuuuu.mnasema waislam wa usa nyie mnafatilia dini yenu ipasavyoooo au basi tu mnajikosha hapa kwa ankalllll wengine kufunga tu panakushindeni kutwa nzima kulaaaa

    Yabinty

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 06, 2010

    KAMA MTU ANAFUATA DINI FULANI BILA KUJUA KAMA DINI HIYO NI BORA KULIKO ZOOTE BASI BORA AWE HUMATARIAN TUU. MAANA ATAEPUKA MADHARA MENGINE BURE.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 06, 2010

    sis watanzania tunashindwa hata kujadili mambo muhimu. nimesoma comments nyingi lakini naona wengi ya wanaotuma comments hawajui nini wanachokisema au ni malimbukeni.baadhi ya watu wanamtukana tyson kwasababu ya tatoo. hivi kweli kama watu wote wangelikuwa wanalingania wako kama wewe annoy wa hapo juu wangeuwona ukweli wa dini????

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 06, 2010

    UKWELI MTAJARIBU KUSEMA KILA JAMBO KULINDA AMA KUTETEA ITIKADI MLIZONAZO!!
    UKWELI NI KWAMBA TAYSON YUPO JUU KIHESHIMA KATIKA ULIMWENGU WA MACELEBRET ANAHESHIMIKA NA HAKUINGIA KTK UISLAM KWA AJILI YA HELA BALI AMEINGIA KWENYE UISLAM BAADA YA KUHELIMISHWA AKAUJUA UISLAM!NYINYI MNAESEMA AMEINGIA BAADA YA KUISHIWA KWANI TYSON AMEINGIA LEO KWENYE UISLAMU?
    WAMAREKANI WENGI WENYE ELIMU WAINGIA KWENYE UISLAM KWA WINGI!!NA WANASAYANSI WENGI TU DUNIANI KOTE!!
    NAKUHUSU HUYO ALIYESEMA SIKUKUU YA KWANZA NI WAMAREKANI WAPIGANIA HAKI ZA WEUSI WANASSHEREHEKEA SIKUKU HIYO KWA MOYO MOJA KUPINGA SIKUKUU ZA WAZUNGU KAMA KRISTISSMAS WAMELIPA JINA LA KISWAHILI KUTOKANA LUGHA YA KISWAHILI INACIVILISATION YA UNITE NA UPENDO!!
    KUHUSU KUTAMKA MANENO YA KISWAHILI HIYO INATEGEMEA HATA MSUKUMA AMA MMASAI KUTAMKA VIZURI MANENO YA KISWAHILI HAWEZI ITAKUJA KUWA WAO!!HEBU ACHENI INFERIORITE COMPLEX.
    PIA WATUMWA HAWAKUTOKA WEST AFRICA TUU HATA HUKU KWETU WALICHUKULIWA WENGI TU NA WAKINA VASCO DAGAMA.
    USHOGA UPO HATA SHINYANGA,MBEYA NA KAGERA!!ILA MIJI HIYO MLIYOITAJA NIKWAKUWA NDIYO MIJI MIKUBWA NA MIJI MIKUBWA UTAKUTA KUNAWAHAMIAJI NA WATU WA TABIA MBALIMBALI.
    WAARABU KWAO USHOGA NI HARAMU NA KOSA KUBWA ILA WAZUNGU WAMEUALALISHA HADI MAPADRI NI MASHOGA!!HATA NDANI YA VYAMA VYA SIASA NA SERIKALI WANANGUVU KUBWA.HII INAONESHA NI JINSI GANI MASHOGA WALIVYO NA THAMANI UTAKUTA MTU ANAMKE NA WATOTO SHOGA WANAWAKE ZAO ASILIMIA 96 WANAPENDA MAPENZI KUNYUME NA MAUMBILE

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 06, 2010

    Kwa nini wadau mnaijadili hii ya tyson kuwa Muislam. Yeye ameamua kua Muislam, Mungu wake ndio mwenye kuona lililo rohoni, sisi hatuna budi kukubaliana nae na kumpongeza kwa kuchagua Dini ilio bora. Hio baadhi ya wadau wanaodai wamarekani wanaingia katika uislam ni utapeli, huna uhakika, kwani hivi ndivyo sisi waislam tunavyotegemea , watu wataingia kwenye dini ya kiislam makundi kwa makundi. Kama ntanukuu maneno ya marehemu Michael jackson kwa kaka yake alieingia uislam, hi was realy admiring him. Uislam ni mzuri hata baba yake bikira maria na aliemlea maria walikua waislam , narudia Muislam- tafura suratulimraan. Michuzi naomba uitoe hii comment yangu usiibanie. ili wengine wajue uislam ulikuapo na upo, nawataka wote wasome hio sura na waielewe.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 07, 2010

    Waislamu wenzangu mna presha sana. Kwanza, katika sheria za kusali, maji lazima yashike ngozi ukitawadha. Tattoo hairuhusu maji yashike ngozi kwa kuwa rangi ipo katikati ya ngozi na maji. Ndio maana Mwislamu haruhusuwi kuweka tatoo katika mwili kwa kuwa hawezi kuwa msafi anapotawadha.

    Pili, mtu akislimu, lazima awe na jina la kiislamu. Ni Marekani peke yake utaona mtu anaitwa Charles lakini anajiita Mwislamu kwa kuwa ni fesheni. Ni fesheni kwa kuwa wengi wao hawaijui dini kabisa. Nenda nchi yoyote yenye Waislamu wengi na utaambiwa kuwa ukisilimu, jina lako lazima liweze kuandikwa kiarabu. Hukuti Charles wala Johnson wala David Mwislamu isipokuwa Marekani na nchi za ulaya ambapo hamna watu wengi wa kiislamu na kwa hivyo hawaelewi dini na sheria zake.

    Tatu, hio Nation of Islam sio Waislamu kwa kuwa wanamfuata mkuu wao kama Mtume. Labda kwa Marekani ni sawa lakini si sheria kwa dini ya Kiislamu kufuata mtu. Kila anachosema mkuu wao wanamfuata mpaka akina Mohamed Ali na Malcolm X wakatoka katika Nation of Islam kwa kuwa waliambiwa wao sio waislamu tena kwa kuwa wanakataa kufuata masharti yake kama vile dini ya Kiislamu kaianzisha yeye Alijah Mohammed.

    Kila binadamu ana hitilafu zake lakini ukweli lazima usemwe. Kila mtu hata Mtanzania anaweza kusilimu lakini pia asifuate masharti ya dini kama waumini wengi wanaokunywa pombe japokuwa ni waislamu. Lakini ukweli ni kuwa wanaojiita waislamu Marekani wengi wao hawaijui dini kabisa hasa katika vyuo nilivyokwenda. Sijapata kuonana na Mwislamu Mmarekani mweusi anayeweza kuswali au kujua sheria yoyote ya dini au kusoma Kuran. Kwao, wanaona kuwa dini ya kikristo si yao kwa kuwa walipewa na wauzaji wa Utumwa.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 07, 2010

    we all took america history there is no party of that history say thatkwanzaa is africa holyday!! so sto lying ass hole!!!! kwanzaa is for the son of slave their, holyday!! to reminding them about they history so get that right you pussy!!!!!!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 07, 2010

    Anony unayeandika kwa herufu kubwa (unapiga makelele ukiandika hivyo)naomba usome zuri nilivyoandika kuhusu utumwa.

    Nilisema kuwa Mtumwa aliyepelekwa Marekani mara nyingi ametokea Afrika Magharibi sijasema hamna utumwa Afrika Mashariki. Wale waliopelekwa Marekani walitokea Afrika Magharibi kwa kuwa ni rahisi na karibu ukitumia njia hio kuliko kuja Mashariki na kwenda Marekani. Watumwa wa Mashariki walipelekwa katika visiwa kama Jamaica, Ulaya na kadhalika. Naomba usime historia ya utumwa kama nilivyosoma mimi kabla ya kuropoka.

    soma zaidi:
    Philip D. Curtin's book, The Atlantic Slave Trade, (1969).



    PROJECTED EXPORTS OF THAT PORTION OF THE FRENCH AND ENGLISH SLAVE TRADE HAVING IDENTIFIABLE REGION OF COAST ORIGIN IN AFRICA, 1711-1810.

    Senegambia (Senegal-Gambia) * 5.8%

    Sierra Leone 3.4%

    Windward Coast (Ivory Coast) * 12.1%

    Gold Coast (Ghana) * 14.4%

    Bight of Benin (Nigeria) * 14.5

    Bight of Biafra (Nigeria) * 25.1%

    Central and Southeast Africa (Cameroon-N. Angola) * 24.7%

    Sasa kama asilia kubwa walitokea Afrika ya Magharibi, kwa nini hawaendi huko kama wanavyomiminika Afrika Kusini kila siku? Kila mmoja anataka kumbusu Mandiba kama mjomba wake wakati ndugu zao hasa wako huko Ghana na Nigeria (75%). Kama sio fesheni ni nini? Wanaona Lagos ni vumbi tupu hakuna mpango lakini Cape Town ni kama kwao, kwa hivyo lazima iwe "nyumbani" tu walipotoka vizazi vyao.

    Pili, kupinga sikukuu za wazungu na kutunga sikukuu yako na kusema kwamba imetoka Afrika ni vitu viwili tofauti. Una haki ya kutunga lakini huna haki ya kudang'anya watu. Nilisoma vitabu vingi tu katika maktaba na vyoye vinasema Kwanzaa imetoka moja kwa moja barani Afrika. Huu usemi si wa kweli na ndio ilikuwa pointi yangu. Hatuna sherehe hizo nyumbani.

    Nakubaliana na wewe kuwa mashoga wapo katika kila nchi na jumuiya. Tofautu yetu na ya wenzetu ulaya na marekani ni kuwa wao wamejitokeza na kuomba haki ya kuwa shoga bila ya kufunguliwa mashitaka au kunyanyaswa na jamii. Na sasa nchi nyingi za kwao wanaruhusu ndoa yao vile vile.

    Lakini, japokuwa ushoga ni haramu katika dini nyingi, utakuwa upo sana kwa nchi za kiarabu hasa Saudi Arabia kwa kuwa wanaume na wanawake wametengwa na bubanwa sana. Ndio maana unasoma habari kuwa wanaume wengi wanakamatwa kwa nguvu kila siku (mwanamke hana haki ya kutembea au kusafiri au kuendesha gari peke yake). Hii ni sawa na kuwa jela katika nchi yoyote hata Tanzania. Binadamu ana mahitaji yake na kama hapati mwanamke basi atatafuta mwanamme, kama utamwita shoga hii ni juu yako kwa vile yupo jela.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 07, 2010

    Mtu akiwa jela na kufanya mapenzi na mwanamume mwenzake utamwita shoga au anatimiz amahitaji yake ya kibinadamu? Arabuni, hasa Saudi Arabia,wanaume wengi wanakamatwa kwa nguvu (kama jela) kwa kuwa hawana uhuru wa kuwa na mchumba wa kike kabla ya ndoa. Nchi za kitajiri zimewapa rukhsa mashoga haki ya kuwa shoga bila ya kupelekwa jela. Sisi tunao mashoga wengi tu ila hawawezi kujitokeza bila ya kupelekwa rumande. Lakini hata kama hatupendi kuwapa uhuru wa kuwa mashoga, sheria za binadamu za umoja wa mataifa hazituruhusu kuwapeleka jela kwa kosa la kuwa shoga ila inaheshimu sheria za nchi za kutotaka kuwapa haki za ndoa.

    Watumwa wengi wa Marekani walitokea Afrika ya Magharibi sio Mashariki. Mdau unaopiga makelele (kwa kuandika kwa herufi kubwa) sijasema kuwa hakujakuwa na utumwa Mashariki ila ni rahisi kwa meli zao kuchukua Magharibi watumwa kwa kuwa ni rahisi kinjia. Soma historia ya Utumwa kama mimi hapa:

    Philip D. Curtin's book, The Atlantic Slave Trade, (1969), p. 221.


    Senegambia (Senegal-Gambia) * 5.8%

    Sierra Leone 3.4%

    Windward Coast (Ivory Coast) * 12.1%

    Gold Coast (Ghana) * 14.4%

    Bight of Benin (Nigeria) * 14.5

    Bight of Biafra (Nigeria) * 25.1%

    Central and Southeast Africa (Cameroon-N. Angola) * 24.7%

    Sasa kama ndugu zao wengi (75%) wametokea Nigeria na Ghana, kwa nini macelebrity wao hawaendi huko bali wanamiminika Afrika Kusini na kusema wamefika "nyumbani"? Kama sio fesheni ni nini? Wanajua Lagos ni vumbi tu, ndio maana wanakwenda Cape Town.

    Sijasema hawana haki kuwa na sikuu zao ila wasidanganye watu kusema kwamba Kwanzaa imetoka Afrika. Hii ni tofauti na kusema kuwa tunataka sikukuu yetu sio ya wazungu. Vitabu vyote nilivyosoma katika maktaba ya chuo vinasema kuwa Kwanzaa imetoka moja kwa moja barani Afrika, hii ndio pointi yangu.

    Dini ni imani yako. Kuna wengi wanajiita Waislamu au Wakiristo lakini hawafuati sheria zake. Pia naamini kuwa hamna mtu ana haki ya kukuchambua kama wewe ni kweli Muislamu au Mkiristo n.k isipokuwa Mola wako.

    Kwa hivyo kama Tyson amesilimu kama wafungwa wa Kimarekani (weusi)wengi ni poa tu. Kama amekwenda kwa kulipwa ni poa pia, kwa kuwa arosto sasa, kapoteza milioni 300. Nilichosema mwanzo ni kuwa wananchi wengi wa Marekani walioslimu na nilioongea nao chuoni ni waislamu wa jina tu. Hawaijui dini, koran wala sheria za dini.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 07, 2010

    Jamani waTZ inabidi tuwe na uelewa wa mambo katika karne hii. Tunatakiwa kujua kutofautisha.
    moja: Uikristo na Uzungu, waikristo na wazungu (Nchi za magharibi)
    pili: Uislam na Uaraabu, waislamu na waraabu.

    Niliposoma "Comments" hapo juu nimesikitika sana, kwani watu wenye upeo kwa kiasi chao lakini bado wanachanganya mambo.

    Dini zina mfumo wake wa maisha na jamii zetu ka waaraabu, wazungu, wachina, wahaya, wasukuna n.k nazo zina mfumo wake wa maisha.

    HAPO ANONY WA Wed Jul 07, 02:45:00 AM
    SIJUI WEWE NI DIDNI GANI LAKINI KWA NINAVYOJUA UISLAM HAKUNA SEHEMU INAPOSEMA MTU LAZIMA AWE NA JINA LA KIARABU NDIO AWE MUISLAMU.

    UISLAM UNAFUNDISHA TUWAPE WATOTO WETU MAJINA MAZURI. JINA ZURI LINAWEZA KUWA KATIKA LUGHA YOYOTE ILIMRADI LINA MAANA NZURI KWA HATA HAYO MAJINA YA KIARABU YANA MAANA ZAKE. KWAHIYO MTU AKIITWA DAVID AU DAUDI AMBOLO NI JINA MOJA LUGHA TOFAUTI HAKUNA TATIZO.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 07, 2010

    anonymous wa tue/july06,03:24:00.hujui uislam,kaa kimya,nani kakwambia uislam unatangazwa na tyson,uislam unajitangaza wenyewe na ndio maana mataifa ya magharibi hawalali kufikiria namna ya kuuvunja lakini wapi,hii ni dini ya mungu,mungu ndio anaitangaza kwa namna yake mwenyewe anayoijua lakini sio tyson kwakuwa kaingia ktk uislam basi kwakuwa ni maarufu eti ataitangaza,koma kabisa kuongea hivyo,tyson kaona umaarufu wa uislam ni mkubwa sana ndio akaamua kuingia ili aujue ukweli wake,so jua baada ya kuisoma na kuufahamu utaona mabadiliko makubwa sana kutoka kwake.hii dini haitangazwi kama ukristo unavyotangazwa,hii inajitangaza yenyewe,qoran inasema kuna time itafika watu watajiunga na uislam makundi kwa makundi na ndio kipindi hichi unachokiona sasa.wewe kaa na mawazo yako potofu uliyonayo lakini ukweli hauko mbali.thanks

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 07, 2010

    Nilipoandika kuwa majina ya kikristo ni Mali sana kwa nini mmekataa kutoa comment zangu. Jamani acheni wivu.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 07, 2010

    Hakuna majina ya kikristo au ya kiislamu. Majina yaliyopo ni either ya Kiyahudi, au ya Kiarabu. Au Anglo. Kwa mfano, Yaser Arafat aliyekuwa kiongozi wa Palestine alikuwa mkristo mwenye jina la kiarabu. Tariq Aziz aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Iraq wakati wa Sadam, ni mkristo mwenye jina la kiarabu. Mfano mwingine, Malcolm X, alikuwa muislamu mwenye Anglo/Irish name.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 07, 2010

    BADALA YA KUTAFUTA HELA NYIE ENDELEENI TU KUJADILI MAISHA BINAFSI YA WATU YASIYOWAHUSU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...