Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ,Mh. Hussein Mwinyi akikabidhi kombe la ushindi kwa muwakilishi wa kampuni ya Sigara Tanzania,Simon Maha mara baada ya kutangazwa washindi wa tuzo za Chama Cha Waajiri Tanzania (Association of Tanzania Employers) zilizotolewa jana katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana,Mh. Juma Othman Kapuya akikabidhi kikombe cha ushindi wa pili kwa muwakilishi wa benki ya Standard Chartered katika hafla ya utoaji tuzo kwa makampuni yaliopo nchini. tuzo hizo zilitolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (Association of Tanzania Employers) jana katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.
Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Nchini,Adv. Cornelius Kariwa,akikabidhi kikombe na cheti cha ushindi wa tatu kwa muwakilishi toka BP Tanzania.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mawasilano wa TBL,Steven Kilindo akipokea kikombe pamoja na cheti cha ushindi walioupata wa Taaluma ya Afya na Usalama (Occupational Health and Safety) katika hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika jana usiku katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.
Wafanyakazi wa TBL wakifurahia Tuzo yao waliyoipata.toka kulia ni Lilian Erasmus, Steven Kilindo (Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mawasiliano),Stephen Kolimba,Rosedomina Swai,Lilian Makau na Sarah Zayumba
Mdau Alfred Martin wa PPF (kulia) akikabidhi kikombe pamoja na cheti cha ushindi kwa mwakilishi wa kampuni ya Sigara Tanzania,Victor Kimaro ambao ndio walionyakuwa vikombe vingi katika tuzo hizo.Wafanyakazi wa kampuni ya Sigara wakiwa na Vikombe vyao vya ushindi
washindi woote walipata picha ya pamoja na Mgeni rasmi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2010

    Hongereni sana watu wa TCC hasa bwana Somon Mate. Huyo jamaa ni MASHINE mnapaswa kumkubali maana ameibadilisha kampuni.
    Gunda Straton Mushy Faazaa faazaa Mnatakiwa kufuata nyayoooo! Hongereni sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2010

    hongereni wote mlopata tuzo.Ila mm nina swali,labda kwa uelewa wangu mdogo sijui kupata tuzo kutoka chama cha waajiri TZ nn kitu gani kinazingatiwa.Nilidhani ni wale waajiri wanaoajiri waTZ labda au wale wanaotoa ajira kwa public kwa any media, kwani hao TCC, BP na wengineo cjawahi ona wametangaza kazi.Au jamani ni criteria zipi zimeangaliwa hapo???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...