Ankal Michuzi, Good Morning!
Naomba nitandikie hii kwenye Globu yetu ya Jamii.
Ni miezi sita tangia nimelipia Luku njia tatu kwa jengo langu pale Mivumoni, Madale (nitakupelekea scan ya risiti). Nimelipia milioni moja (1.0 M TAS) kwenye Ofisi ya TANESCO Kinondoni Kaskazini.
Mimi ni mstaafu ninayetegemea kuanza mradi wa kunipatia kipato. Ofisini kwao walikuwa wamebandika mabango kuwa tutaunganishiwa umeme baada ya mwezi mmoja na mpaka sasa sijaunganishiwa. Miaka michache ilopita walimfukuza kazi meneja wa kanda hiyo lakini huduma bado kuboreshwa. Except lip services.
Wengine wanafungiwa kwa mlango wa nyuma eti kwa tiketi ya mradi maalumu/viongozi. Ziko stoo zinatolewa kinyemela kwa rushwa. Sisi tusotoa rushwa twaambiwa tukanunue za laki nne (Sh. 400,000) zilizoko Achelis. This is pure collusion and corruption. Iweje tulipe mara mbili??. Rushwa chafu, Wizi mtupu!!! Ogopeni Mungu!!

Mrithi wa Dr. Rashid, Mkurugenzi Mkuu mpya Mhandisi Wiliam Geofrey Mhando ameahidi kutoa huduma kwa ufanisi bila kuwafumbia macho mafisadi. Iweje mpaka leo sijapata umeme na kila siku watendaji/Engineers wake wanatoa ahadi kuwa luku zipo zinashushwa kwenye meli bandarini, ni Jumatatu, wiki kesho, kesho kutwaa , mtondogo …??
Nimepiga vumbi/ mguu hapo ofsini mpaka soli imeisha . Kwa Ankal hii ndo kasi mpya nguvu mpya Eng. Mhando anisaidie kwa hili. Natambua uadilifu na uchapaji kazi wake tangu opereshini TIJA pale G- Coy Bulombora JKT tukijenga taifa. Baada ya kuteuliwa aliahidi kujipanga kukabiliana na tatizo sugu la usambazaji umeme.
Mungu ibariki Tanzania Yetu!!
Mdau Madale

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2010

    Globu ya jamii hoyee!!. Afadhali umeaniaka uozo huu. Shear lack of public responsibility. Kakobe hakukosea kuwaambia wamwogope Mungu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2010

    Hee hili tatizo ndio limemkuta mama yangu huko bongo. wamemfungia Luku ya njia tatu bomu kila mara umeme unakata. kwenda kuwalalamikia eti wanamwambia akanunue mtambo mwingine unauzwa laki nne. WTF?? nani mwenye kosa mama au hao waliomfungia luku bomu??? Huo ndio ufisadi na hilo duka nani analimiliki?? kigogo ama? TANESCO acheni kuwaumiza wateja/ wananchi! Shame on U

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2010

    umeme ukikatika mafundi wa tanesco wakija kurekebisha wanataka kitu kidogo sivyo utalala kiza wiki 2

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2010

    Hili jambo sio tu Dar, Arusha nimengoja mpaka nikamua kuacha kila siku ni maneno, hakuna nguzo ama boss hayupo bali wanataka hela, project ya kina mama je tutaendelea kweli na hawa akina mama watajifunza lini computer mwaka gani? hela wamelipwa miezi 8 ilyopita.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2010

    poleni wakuu ndio maisha bora hayo kwa kila mtanzania.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2010

    SERIKALI IPO NA INAYAONA HAYA LAKINI HAWAYASEMEI, WANANCHI TUANDAMANE KWA MAMBO KAMA HAYA SI KWA VITU VYA KIPUUZI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...