Leo Yanga imetangaza kikosi cha cha maangamizi chenye wachezaji 28, wakiwamo 10 waliowasajili upya huku ikiwamwaga wachezaji wengine watatu.
Wachezaji wapya watakaokipiga kwenye klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani ni pamoja na wanaochezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 'Ngorongoro Heroes' ni Salum Telela, Abuu Ubwa Zuberi, na Omega Seme pia imemnyakua mshambuliaji wa Africa Lyon Yahaya Tumbo mlinzi wa kati wa Mtibwa Sugar Chacha Marwa.
Pia klabu hiyo ya Jangwani imemuongeza kwenye kikosi chake mshambuliaji Nsa Job, Ibrahimu Job huku wachezaji wa nje ni Waghana kiungo Ernest Boakye, Isaack Boak (mlinzi wa kati), Kenneth Asamoah (mshambuliaji) na mlinda mlango kutoka Serbia Ivan Knezevic ambaye anachukua nafasi ya Obren Curcovich ambaye ametimkia Afrika Kusini.
Mbali na wachezaji hao pia ofisa habari wa Yanga Lous Sendeu aliwataja wachezaji wa zamani waliowabakiza kwenye kikosi chao ni mlinda mlango Yaw Berko, Nelson Kimath, Shedrack Nsajigwa, Stephen Mwasika, Nadir Haroub 'Canavalo', Mohamed Mbegu, Nurdin Bakari, Godfrey Bony, Athuman Idd 'Chuji', Kigi Makasi, Abdi Kassim 'Babi' Jerryson Tegete, Idd Mbaga, Razack Khalfan na Fred Mbuna.
Wachezaji walioachwa kwenye kikosi cha Yanga msimu huu ni Wisdom Ndlovu, Stephen Marashi na Stephen Bengo.
Hata hivyo wachezaji Wisdom Ndlovu na Stephen Marashi ambao walimwaga wino kuichezea Yanga msimu huu mapema mwezi Aprili wameshtaki Yanga kwa TFF ili waweze kulipwa haki zao.
Wakati huo huo uongozi mpya wa Yanga umeendelea kulipa fadhila baada ya kumrejesha kwa mlango wa nyumba Emanuel Mpangala kwa kumpa umeneja wa timu. Awali Mpangala alikuwa katibu wa kamati ya mashindano kwenye uongozi uliopita chini ya mwenyekiti wake Iman Madega.
Sendeu alisema kuwa Mpangala atakaimu nafasi hiyo hadi hapo atakapopatikana meneja mwingine wa kuajiri.
nimefurahi kuwa Tegete na Canavaro wapo ndani ya nyumba
ReplyDelete