JK akimnadi Charles Kitwanga a.k.a Mawe Matatu, mgombea ubunge wa CCM wa jimbo la Misungwi Mwanza leo, akiwa ni mbunge wa kwanza kunadiwa na mwenyekiti huyo wa CCM ambaye kaanza rasmi ziara ya mikoani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Ankal
    Ulivyojitahidi kwa coverage ya ccm ufanye na vivo hivyo kwa vyama vingine. Maana ni kijani na njano tu, inaboa sasa.
    Take home message: Be fair to all political parties! Watanzania tumechoka na ushabiki tunataka sera na kiongozi anayetufaa.

    Hata kama utabana, msg delivered moyo wangu ni mweupe hasa mwezi huu mtukufu!

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  2. Si wa CUF tushazoea walau nyie wa Chadema mnapata kidogo coverage

    ReplyDelete
  3. KAKA MICHUZI LEO CUF TUMEZINDUA KAMPENI TEMEKE MWISHO MBONA PICHA HAKUNA? ANGEKUWA DR SLAA AU KIKWETE KWELI USINGEWEKA? TUNAOMBA UWE FAIR KAKA HATUTAKI KUPENDELEWA JUST BE FAIR

    ReplyDelete
  4. Mimi si mshabiki wa CCM lakini hii blog ni blog binafsi na mwenye blog yake ana haki ya kuwa mwanachama au mshabiki wa chama anachokitaka. Hii blog siyo mali ya serikali, na hivyo basi Michuzi halazimiki kisheria kuwa msawa kwa vyama vyote.
    Ingawa ni kweli ingekuwa vizuri zaidi na kama vyama vingine vingepata nafasi ya kutangazwa kama CCM.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa Sun Aug 22, 10:44:00 PM, kama hii no blog binafsi, kwa nini iitwe blogu ya jamii? Kwa kweli hii sio fair kwa watanzania kuwafichia habari. Michuzi bania tuu hii this is not fair. JK ni binadamu kama sisi na kusema kweli kama binadamu nimesikitishwa na yaliyomtokea. Yaani wasomaji wa blogu yako hawatakutrust tena. Kuna siku uliweka video ya mtu mmoja akizikwa live kiislamu. That video was so bad nikacomplain ukabania maoni yangu. Leo bania tena maoni yangu lakini najua hapo ulipo roho yako inakusuta. Najiskia kama kulia.

    ReplyDelete
  6. Mdau unayesema hii ni blog ya binafsi ya Michuzi yaelekea ni mgeni humu. Michuzi alishaweka bayana hii ni blog ya jamii, ndio sababu habari anazotoa zinagusa jamii ya Watanzania popote pale walipo. Si hivyo tu, ameshapata kutoa mada binafsi kuhusu nafasi ya blog kama vyombo vya habari ndani ya blog hii hii.
    Blog hii ni sawa na vyombo vya habari vya binafsi kama magazeti ya Mwananchi na Michuzi ameshapata kusema hana upendeleo. Pale chombo cha binafsi kinapokuwa chombo cha propaganda huwa kinajitambulisha kabisa mfano magazeti ya Uhuru ni ya Chama Cha Mapinduzi.

    ReplyDelete
  7. Mr.3 Stones, tunakutakia Ushindi wa kishindo.

    ReplyDelete
  8. Hii blog ni ya michuzi hata kama inaitwa ya jamii hilo ni jina tu kijana anzisha ya kwako na wewe ukitaka, keep in mind CCM ndio unayomuweka michuzi mjini.
    Raia asiyependa politics

    ReplyDelete
  9. Hii blog ni blog binafsi ya Michuzi. Kuitwa Blog ya jamii ni uungwana tuu kama vile unapoenda hotelini ukaambiwa kwamba "mteja ni mfalme"; haina maana kwamba eti wewe ni mfalme.

    ReplyDelete
  10. Jamani eeh hata magazeti barabarani yanaitwa magazeti ya jamii sijui jamii imefanya nini, sijui kwanza jamii, sijui jamii yetu na mbona hayagaiwi bure?

    Mwenyewe keshasema hachagui habagui na bado tunaona bure bileshi hao sijui CUF sijui Chadema wameishafanya hiyo mikutano yao ya kampeni au ndio mnaanza kulia lia mapema mkishindwa mseme hamkutendewa haki? Na je kama wameshafanya mikutano yao wamemletea Michuzi picha akazitia kapuni? Matarajio yenu yamekuwa sivyo ndivyo! Mtaluona mwaka huu!

    Michuzi endeleza libeneke, globu kibao mbona hawaweki hizo picha kwanini watu wakushikie bango wewe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...