Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akizungumza na Wachimbaji wadogo katika machimbo yasiyo rasmi ya Nyakagwe wilayani Geita muda mfupi kabla ya kutoa amri ya kufungwa kwa machimbo hayo baada ya kutokea uvumi wa kufukiwa kwa wachimbaji zaidi ya 70 wiki iliyopita.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akipata maelezo ya uvumi wa kufukiwa kwa wachimbaji wadogo zaidi ya 70 katika machimbo ya dhahabu ya Nyakagwe kutoka wa Ofisa madini mkazi wa wilaya ya Geira Donald Mremi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Nonosius Komba (Kulia) akiteta jambo
na Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Geita SSP Kasabango.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa mwanza Nonosius Komba akizungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Nyakagwe muda mfupi kabla ya zoezi la ufukuaji wa wachimbaji wadogo 70 waliodaiwa kufukiwa katika machimbao hayo juzi
Greda la kampuni ya GGM ambao ni wamiliki wa mgodi wa Geita wakifanya zoezi la ufukuaji katika machimbo yasiyo rasmi ya Nyakagwe baada ya kusikika kwa madai ya kufukiwa kwa zaidi ya wachimbaji wadogo 70,hata hivyo hakuna mwili hata mmoja uliopatikana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Haya mambo ya ushabiki usio na msingi ndio yanayoleta umaskini na wizi Tanzania. walikua wanasema ni uzushi tuu hakuna waliokufawakati leo wameibuliwa maiti toka migodini. Baadhi ya wabunge wa CCM na wakuu wa wilaya waliudanganya umma hivihivi kipindi kile wananchi walio pembezoni mwa mto Tigite walivyoathirika na sumu wao wakawa wanapuuza ukweli ule

    ReplyDelete
  2. kama kampuni inafanya ufukuaji kwa hiyo sio uvumi ni ukweli kwamba watu wamefukiwa machimboni? machimboni watu wanakufa na kufukuwa kama sio binadamu.Hii serikali yetu inafanya kazi gani,Kuna haja gani ya kuwa na wizara zisizofanya kazi zake?

    ReplyDelete
  3. Hii nchi haithamini roho za watu.

    ReplyDelete
  4. Asalam allekyum,

    I would like to get Michuzi email..i have a question that I would like to ask him...please email me at thacosigner@yahoo.com.

    Thank you

    ReplyDelete
  5. Tanzania, please respect human life and stop playing politics with it...

    Michuzi, I have lost a distant cousin in that accident, FACT. Yet politicians out here still say no one was burried in there.

    Those people went down in narrow holes of about 100m. Those holes collapsed, yet you bring a grader that digs no more than 50m and satisfy yourselves that no one was burried in there.

    I weep. Not only for my relative, but also for my country. I bleed, I weep and I am distraught for Tanzania. How much of this shall we keep seeing? What is happening to us? And all this just to keep somebody's political goodwill?

    DAMN!

    ReplyDelete
  6. Jamii ya Wachimbaji duniani huwa wana solidarity sana matatizo kama haya yanapotokea. Sishangai GGM kuacha kazi zake za uzalishaji na kukimbia hapa kwa wachimbaji hawa wadogo wadogo kusaidia. Najua pia siyo mara yao ya kwanza kwani wameshajihimu pia kwenye ajali kule Mererani.

    Mimi ni mmoja wa wanamigodi na naungana na wahanga wote wa hili ajali. Vilevile, nimeshaomba misa kwa ajili ya kuwaombea wale wanamigodi walikuwa trapped kule Chile.

    Labda cha kujifunza hapa ni kuwa hawa tunaowaita wachimbaji wadogo wadogo wanafanya kazi katika hali hatarishi sana. Uchimbaji mdogo mdogo huu unaleta tija ndogo sana, unaajiri watu wachache sana na hata kipato cha wahusika ni kidogo sana.

    ReplyDelete
  7. Comrade Ngeleja, tayari una kura yangu. huku kwenye mashina kazi inaendelea. Hatutachoka. J. Manyanda.

    ReplyDelete
  8. we annoni wa Wed Sep 01, 07:17:00 AM upo dunia gani? usiwe unaandika hovyo hovyo tu. Ngoja nikupe mfano kidogo wa faida ya wachimbaji hawa unaowatukana. Kwanza wakipata madini huwekeza kwenye ujenzi wa nyumba bora, mahoteli na aina mbalimbali za biashara hufungua hapahapa nchini hilo we huoni kama ni faida kwa watanzania? Mafundi wajenzi hupata ajira za kujenga, biashara ya vifaa vya ujenzi inaimarika, viwanda vya pombe vinaongeza uzalishaji kutokana na wanywa bia kuongezeka,hivyo kulipa kodi serikalini, we haya huyaoni kama yanaletwa na pato la mchimbaji mdogo?

    ReplyDelete
  9. wazalendo ndio wanakufa na kupata shida wazungu {mabwana wa viongozi wetu}wao wanachukua tu mali mandege kwa mandege haooooo kwao ...sisi wazalendo watz hakuna chochoteeee tufaidikacho zaidi ya viongozi wetu na familia zao.mkae mjue hao watu weupe wakiimaliza nchi mtafurahi.mkae mkijua furaha yenu hapa dunia ni majuto tuendako .poleni wate mliopatwa na matatizo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...