Home
Unlabelled
omba omba apata mkong'oto
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
SAFI SAAANA, KINA MAMA OYEEE!!! UNAMIKONO YOTE MUNGU KAKUJALIA, VIUNGO VYOTE VIMETIMIA!! NI KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YAKO NA WATOTO WAKO, MAANA HATA SIJUI HAO WATOTO WAKE WANAJIFUNZA KITU GANI HAPO SASA? KWAMBA LIFE NI KUAMKA ASUBUHI NA KUOMBA? MIMI NAFIKIRI TUANZE KUSAKANA MITAANI, NIKIKUKUTA UMEKAA HAPO HUNA ULEMAVU UNAOMBAOMBA, NI KONDE ZITO LA PUA, KAENI TAYARI.
ReplyDeleteNimeipenda hii changamoto kutoka Arusha maana kina mama wengine wanapenda kuwa watoto wa kike na sio wanawake..Mikoa yote ikiiga mfanao huu nadhani hata hao watoto wanaozagaa barabarani watapungua.
ReplyDeletewakina mama waliompiga hawana akili wanaweza wakafungwa gerezani kwa miaka mitano kwa walichokifanya.
ReplyDeletena wajuwe binadamu anauhuru wa kuishi maisha anayotaka ilimradi havunji sheria.
Marekani wakiamua kuwapiga omba omba wao watapiga karibia kila omba omba (wake kwa waume). Yaani ni wazima kabisa, na tena wanakuambia uwape kiasi fulani cha dola. Wengine waomba hela ili wakawanunulie mbwa wao chakula. CNN nk. wenyewe wanaangaza Afrika tu, ya kwao wanayaficha. Tena angalau Afrika omba omba wetu mara nyingi utakuta wana ulemavu, wa kwao wazima kabisaaa!
ReplyDeletejamani mimi natakakujua hapo ni arusha sehemu gani ? mnijuze wapendwa
ReplyDeleteBora wamemtolea uvivu huyu mama nadhani yuko maeneo ya metropo.Anamtuma mtoto wake aombe afu ukimpa 50 mtoto anakataa anataka kuanzia 100. Yani maza kaona hayo ndo maisha hataki kujishighulisha.
ReplyDeleteBig up sana wamama mliojitoa kimasomaso
We anony wa saa 05:55 unachekesha kweli,.Na wewe kafanye hivyo basi tujue ndio style ya maisha unayotaka tuone,Acha kulea upumbavu angalau ujinga unaweza kufutwa..
ReplyDeleteanon wa Sun Aug 22, 05:55:00 PM wakinamama wa ARUSHA WOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE; SAFI SANAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
ReplyDeleteNina laani kitendo cha huyu mama kupigwa! Watanzania inabidi tujifunze kuwa uchukuwaji sheria mikononi sio kitendo cha kujivunia. Pili, ni muhimu kutambua kuwa kila mtu ana haki ya kushi anavyotaka, ili mradi havunji sheria za mahala husika...
ReplyDeletePamoja na hayo, simuungi pia mkono huyu mama aliyeamua kuendesha maisha yake kwa kuombaomba, ni kitendo dhaifu na cha kumdhalilisha yeye, familia yake na nchi kwa ujumla.
Wito wangu ni kwamba vikundi vya kinamama wenye uchungu wa kukomesha hali ya kuombaomba wajitahidi kuunda vikundi zaidi vya maendeleo na kuelimisha wakina mama ombaomba ili watoke mitaani. Nina imani kuwa endapo huyu mama(ombaomba) angeelimishwa na kupewa msaada wa kiuchumi, basi asinge kaa hapo na hatimaye kuambulia kipigo.
Waheshimiwa wana wa Tanzania wezangu mambo niaje!
ReplyDelete"No body is above the law" sasa hao wakina mama waliompiga tena mbele ya watoto wake wamefanya kosa kubwa mno tena kama mnawajua waripotini wakafungwe kabisa.
Kuomba sio tabia mzuri tena kama hauna kilema ni kujidhalilisha mwenyewe na jamii kwa ujumla, lakini kumpiga tena mbele ya watoto wake ni kumdhalilisha zaidi, kumvunjia heshima na kumuonea kabisa.
Kama kweli walikuwa nauchungu wangemsaidia mradi au wampatie kazi ili ajiendeleze kimaisha.
Wanasheria waTanzania nawaomba mumsaidie huyo mama aliyepigwa kwa kuwa sue hao waliompiga ili apate pesa za mtaji.
Mh Michuzi au aliyepigapicha na kutoa habari thanx kwa kutumia kipaji chako kukemea na kuwaumbua hao wakinamama mabully sasa ni jukumu la polisi kuwasaka ili sheria ichukue mkondo wake.
Nini swali moja, ao kina mama waliokuwa wanampa viboko huyo mama hivi walifikiria uchungu wa ao watoto walioshuhudia mama yao akitandikwa?? Angalia huyo mtoto anavyomfajiri mama yake, hili jambo limeishamharibia maisha huyo mtoto. Sisi wenyewe ndiyo tunaocreate majambazi. Ni bora tu wangemfukuza huyo mama aondoke katika eneo hilo badala ya kumpiga.
ReplyDeleteTukianza kuwapiga na omba omba je na wezi? Tutafikia wapi?
Police wa tanzania kazi zenu ni kulinda raia na mali zao, sasa lazima muwasake wale wote waliomshambulia ombaomba huyu ili waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.
ReplyDelete"why lie I need a beer" hao ndio omba omba wa marekani.tena kuna kipindi cha MSNBC TV station "what would you do" ambacho waliset scenerio kama hiyo watu kupiga homeless tena mwanamke haukupita hata dakika moja walitokea wasamalia wema kuingilia. Sasa nyinyi mnaoshabikia uvunjaji huo wa sheria need to be changed.
ReplyDeleteKama ilivyozoeleka Watanzania wenzetu humu kwenye blogu wanashabikia vitendo vya kihuni na uvunjaji sheria walivyofanya wakina Mama wa Arusha.!!
ReplyDeleteHuyu Mama na watoto wake kosa lao lilikuwa nini? Kuomba tu? Tangu lini kuomba ni kinyume cha Sheria. Halafu walimpigia wapi? mbele ya mtoto wake!!!
Hao kinamama wanatakiwa waende Kanisani/Msikitini au Mlimani wakatubu kwa Mungu wao kwa kitendo hiki.
Hii nchi inakwenda wapi na uonevu wa kiwango hiki. Sasa mkishapiga omba omba mtaenda kuwapiga changudoa pia??!!!!
Soames,
Reading, UK.
Wapigwe na Dar! Wamezidi. Wanaona bora kuwa omba omba kuliko kufanya kazi au kulima!
ReplyDeletenina dola 100 ya mama alitekua anaomba.michuzi naomba niwekee contact za mama ombaomba
ReplyDeleteya marekani tuwaachie wa marekani msijidai mnaijua america kihiivyo bebeni maboxi huko, kitu kidogo tu mnapenda kukompea na marekani, kwendeni huko mara flying over sijui nini, mnajifanya hamjazaliwa bongo wakati mlikuwa mnakunywa mataptap leo mko huko mnaanza kunyea kambi, bongo vumbi sijui upupu kibao, iacheni bongo ikae ina siasa zake na mambo yake pamoja na mipaka zake
ReplyDeletehapo kinachopaswa kuangalia kwa undani zaidi ni jinsi gani ya kuwaondoa ila kumpiga tena mbele ya watoto wake sio jambo zuri kwani linawaathiri hata watoto kisaikolojia kushuhudia mama yao akipigwa bakora.
ReplyDeleteHata hivyo hapa Dar es Salaam maeneo ya Ocean Road karibu na Gymkhana pia kuna mama mmoja mwenye nguvu zake tena pande la mama, ana watoto 5 hivi sasa ananyonyesha, anakuwa pale muda mwingi kuanzia asubuhi na mapema na hata mpka usiku yaani kafanya kama ndio makazi yake, haieleweki ni ombaomba au ni kitu gani na tunapita tunamtizama tunamuacha tu, je angekuwa huko arusha si angeshauawa tayari? asaidiwe vipi na yeye??
Mtaji wa ombaomba ni kukosa "HAYA" (aibu)period!!!.
ReplyDeleteMdeki.
Wadau huyu mama anaomba sehemu nyingi ila anapenda kuomba maeneo ya uwanja wa sheik amri tena ana matusi mbaya na hao watoto wake wanawavuta wapita njia ukikataa kumpa hela ana kutukana yaani watoto wamefundishwa kutukana na mama yao hicho kipigo kimemsatahili kabisa mnaokataa hamumjui tu msiongea kitu
ReplyDeletePOA TUU. KAZI HATAKI KUFANYA. ULEMAVU HANA LAKINI 'KAZI' YA KUTENGENEZA WATOTO ANAJUA. KIBANO SAIZI YAKE.
ReplyDeletehizi sanaa hata hapa bongo zipo sana kuna sikumoja nilimkuta mama mmoja pale ubungo karibu na geti la songas akaniambia amepungukiwa nauli na anaumwa anaelekea kibaha nikampa miambili huku nikimwambia pokea hii mama utaongezea ili ikusaidie matokeo yake alikaataa nakupayuka kwa nguvu akisema we vipi hiki kimia mbili ndio kinanifikisha kibaha? alinishangaza sana na akaniganda kwa kele ikabidi nimuongezee tena ndipo alipo tulia , cha ajabu baada ya siku mbili nikamkuta tena pale pale na habari yake ile ile ya nauli na kuumwa hivyo nawapa big up sana wana harusha
ReplyDeleteAisee, ingawa kupiga sio suluhisho zuri sana lakini wanamama kama huyu(hata wanaume wanaoomba mtaani na si walemavu)wapate funzo. Kwani wale wanojiajiri wenyewe hata kuuza vitumbua, maandazi, n.k. wana maisha mazuri? na wao wangeweza kuomba kama nyinyi tu lakini wametumia akili na kujitafutia kazi. Watanzania wengi tumezoea kuishi kwa kutegemea wengine na ndio maana misaada kutoka nje haiishi. Tuanze kujifunza jamani!
ReplyDeleteKwa wale msiojua, Bongo kazi ya ombaomba inalipa sana.
ReplyDeleteKuna ombaomba namjua, yeye kwa siku analaza zaidi ya laki moja, kijiwe kisipochanganya analaza sitini na ushee, hesabu hizo unakuwa bado hujahesabu vijisenti vya chenji. Lakini pia ana nyumba tatu: mbili ziko Mbagala na moja iko Sinza. Ameoa wanawake watatu na kila mmoja anamtimizia mahitaji yote ya kimwili na kiroho. Wabeba box mpo!!
Nkyabo - Bongo
Sio kweli wote tunaoishi marekani tunabeba mabox, na hata tukubeba mabox tunaingiza kipato halali. Hapa topic ni Ombaomba kupigwa, Tulikuwa tunajaribu kusema ombaomba wapo kila mahali ulimwenguni.Sawa na mdau hapo juu kufananisha na ombaomba tapeli wa ubungo. Hawa ni binadamu kama kila mtu na wanahaki ya kuheshimiwa japo hatukubaliani na njia zao za kuingiza kipato. Sasa ndugu zetu wa Arusha ambao wanamfahamu huyo mama na tabia yake ya kutukana watu pamoja na watoto wake kuwa kero kwa wapita njia ahsante kwa kutuelimisha sisi tusiomjua.
ReplyDeleteBasi serikali iingilie kati kumwadhibu huyo mama na wengine wanaotumia matusi, kashfa au vitisho kwa raia wema. Hakuna haja ya kukashifiana kwa mahali tunapoisha au kazi tunazofanya, wote ni Watanzania.
mdau unaodhani watu wanaoishi marekani wanabeba mabox? pole sana na mawazo hayo. Angalia baadhi ya viongozi wetu hapo Tanzania wamesoma wapi?Watoto wao wapo wapi na wanafanya nini? mimi nimepata uraia wa marekani lakini nakuja nyumbani kila mwaka na nasoma magazeti ya nyumbani katika mtandao kila siku. Tena nipo very proud na Ubongo wangu.Sio mimi alone tupo wabongo wengi hapa America happy na asili yetu. Hata Bro Michuzi analijua hilo na alijionea mwenyewe alipofika hapa na ndugu zetu wengi wakitanzania waliofika hapa wanajua ukweli huo. Hatujatupa jongoo na mti wake kama unavyofikiria wewe Mheshimiwa. Tulikunywa matap tap hatujayasahau na hatutoyasahau kama unavyofikiri "man without past and culture, same as tree withuot roots" Nakubali wapo wachache wanaojibadili, lakini sio vizuri kutumia lugha ya ujumla na ya kashfa.
ReplyDeleteheheheh wabeba maboksi imewauma ... sawa sawa mmezidi kudharau bongo , mnajifanya kama mko peponi !! mnatumwa tu huko ... mkija huku hata kiswahili mnajifanya mmesahau yaani kaazi kweli kweli ...nyinyi ni masikini wa akili .. afadhali sisi huku ni masikini wa mali na sio akili kama nyinyi ...
ReplyDeletependa chako na sifia chako khaaa !!
na kuhusu huyo mama roho imeniuma sana hasa pale anapopigwa na mtoto wake anamkumbatia , jamani hatuna hata huruma ... siwasapoti hata kidogo kitendo walichofanya , sio kizuri tena isitoshe mwezi mtukufu huu wa ramadhani inabidi tusaidie zaidi ya kusaidia ...
wabeba maboksi msikasirike ni kazi mnazofanya huko na hamna ubaya wowote..
Hata mie wa mama wa Arusha mmenifurahisha sana kwasababu mama mwenyewe pia ana maneno machafu.Ukimwambia huna anakukashifu.
ReplyDeletemaneno maneno jamani..kama imekuwa dhambi watu kwenda usa kha! wanaobeba mabox ni wale walioachia vyuo njiani and out of status(japo wengine wana kazi nzuri pia),wenye kusahau kiswahili ni wale malimbukeni ambao ukiangalia background zao hawakutarajia kama wangetoka tanzania hata kwenda kenya. Otherwise poleni na fikra that kila mtu anabeba box, people got their lives!
ReplyDeleteMdau unaodhani sisi tunaoishi marekani tuna umasikini wa akili angalia lugha uliyoitumia ukilinganisha na ligha tunazozitumia, nani ni masikini wa akili? "penda chako na sifia chako" haujui fimbo ya mbali haiui nyoka? sasa changu mimi ni hiki nilichokuwa nacho hapa " cash in hand not at bank". do you know what is sequence and series?
ReplyDeleteUkiwa masikini wa akili next itakuwa masikini wa mali. Lakini ukiwa masikini wa mali kama tajiri wa akili, basi utajua kutafuta mali hivyo umasikini utakutoka.Tungekuwa tunadharau bongo basi tusingeongea na mtu kama wewe uliokuwa na ueleo mfinyu."If you don't give a sh*t about anything, you don't bother to talk about it" sisi hatuidharau bongo ndio maana tunasoma na kuongea habari za nchi yetu nzuri. Pia tukipata nafasi tuna safiri masaa kibao kuja kupumzika na ndugu , jamaa na marafiki. "Mnatumwa huko" what does it mean? kwani uko nyumbani hamtumwi? au wewe jeuri ndio maana masikini wa mali? "mnajifanya mko peponi huko" nani kakudanganya marekani ni peponi? tembea ujionee usingojee kuambiwa. Ndio maana tulisema hata marekani kuna ombaomba."mkija huku hata kiswahili mnajifanya mmesahau yaani kaazi kweli kweli" nadhani wewe ni msichana ambaye kuna mtu alikuhaidi kitu sasa baada ya kurudi akakukuta hadhi yako imeshuka akakutema. Umebaki na chuki please get over and find some positive to do. Kumbuka "you can do, we can help"
Asante sana anony wa Mon Aug 23 saa 10:46:00 PM kwa kuwaelezea hali halisi hao wanaotuita wabeba mabox. Unadhani tusingejali nchi yetu tungesumbuka kuweka comment katika hii mada?!
ReplyDeleteNa kuna watanzania wengi tu wanaojifanya kuwasema waishio nje na wakati wao wenyewe hawana lolote na hawajali nchi yetu inapoelekea. Mimi binafsi inanisikitisha sana kila nikirudi nyumbani na kukuta maendeleo yanarudi nyuma na malalamiko kibao kutoka kwa wananchi. Ndiyo maana naelewa kuwa kuzidi kwa ombaomba kiasi cha wengine kufanya ni sanaa ya kupata hela inaonesha jinsi hali inavyoendelea kuwa mbaya. Natumaini watu watajifunza kutokana na kipigo alichokipata huyu mama!
P.S: Tungekuwa maskini wa akili, wengi tusingefika Marekani!!