kikosi cha zimamoto kutoka kampuni ya ultimate security kikijaribu kuuzima moto uliokuwa umepamba kwenye jengo hili lililowaka moto kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa ni shoti ya umeme iliyoanza katika moja wa maduka yaliyokuwepo katika jengo hilo jioni hii maeneo ya manzese kwa bahressa, jijini dar.
wakazi wa maeneo ya jirani na pamoja na waliokuja kushuhudia tukio hilo,wakiwa katika msongamano kwenye njia iliyokuwa inaelekea katika tukio hilo la moto lililotokea leo,manzese kwa bahresa,jijini dar.
hawa nao walikuwa wakiushuhudia moto huo na wengine wakipata taswira nzima ya tukio hilo kupitia simu zao za mikononi.
kila mtu alitaka kuona na kujua kilichokuwa kinaendelea katika eneo hilo la tukio.
jengo hilo likiendelea kuteketea kwa moto huku juhudi za kuuzima moto huo zikendelea kutoka kwa kampuni ya ultimate security baada ya zile gari za faya kuishiwa maji katikati ya tukio huku watu kibao wakishuhudia tukio hilo.
watu kibao walifika kushuhudia tukio.hakuna mtu hata mmoja aliepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Wabongo kazi kweli. Sasa msongamano wa nini? Wakiona itawasaidia nini? badala ya kuondoka ili waweze kuacaha nafasi ya first responder wao wanabanana hapao. Au ujanja tu wanataka kwenda kuwahi chochote kitakachokuapo hapo

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na Anon. hapo juu. Yaani wabongo moto unatokea ndio kwanza watu wanakimbilia huko. Hata zimamoto lingini likija itakuwa kazi kufika eneo la tukio kwani njia imezibwa na kundi la watu. Lol we have a long way to go kwa kete hii.

    ReplyDelete
  3. Moto huo ni mission posibo, hakuna cha umeme wala nini.

    ReplyDelete
  4. Ningeshangaa kama gari za zimamoto toka halmashauri ya jiji zisingeishiwa MAJI! Hivi huu msamiati wa gari kuishiwa maji utaisha lini..? Umekuwa kama ni wimbo masikioni mwetu. Aibu yenu halmashauri ya jiji, Dar kukosa gari la kisasa linaloweza kukidhi mahitaji!
    Mithupu hata ukibania comment yangu habari ndio hiyo!

    ReplyDelete
  5. sasa hawo watu nao wanafanya nini ? serikali tafadhali weka sheria kuhusu watu kusongama katika maeneo ya hatari ili watoa huduma wafanye kazi zao kwa nafasi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...