Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu JuliusMsekwa ambaye ni mtoto wa Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwanyumbani kwao Bongoyo Oysterbay, jijini Dar asubuhi ya leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwamarehemu Julius Msekwa ambaye ni mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCMBara Pius Msekwa wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwawazazi wa marehemu , Bongoyo Oysterbay jijini Dar es Salaam janajioni.Marehemu Julius Msekwa aliyefariki wiki iliyopita huko NicosiaCyprus ambapo alikuwa akifanya kazi ya mtaalamu Mshauri bingwa katikafani ya teknolojia ya Mawasiliano, alizikwa jana katika makaburi yaKinondoni jijini Dar jioni hii
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,(wapili kushoto) Makamu Mwenyekitiwa CCM Bara Pius Msekwa(kushoto) na mkewe Mama Anna Abdallah(watatukushoto) pamoja na Rais mstaafu awamu ya tatu Mzee Ali HassanMwinyi(kulia) wakishiriki ibada ya mazishi ya kumuombea MarehemuJulius Msekwa aliyefariki huko Nicosia Cyprus wiki iliyopita nakuzikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar jioni hii. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Poleni familia ya mzee Msekwa.Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.Fikra na sala zangu zipo nanyi.

    Mungu amsamehe dhambi zake na ampokee kwenye utukufu wake.

    ReplyDelete
  2. PETER NALITOLELASeptember 21, 2010

    IM ASKED QUESTIONS OF OUT OF TOPICS TO YOUR BLOGGERS BUT IS NOT CONFIDENCE YOU ARE SAYING I DOES NOT CARE THE MAIN TOPIC, MY QUESTION ARE WHY ARE THE PEOPLE OF TANZANIA ARE NOT CLEANING THEIR ARE SHOES? LOOK THE PRESIDENTS KIKWETE AND MWINYI AND ALSO MR. MSEKWA THEY ARE SHOES DO NOT POLISH WELL ENOUGH AND IS LOOK DUSTING? RIP THE SON OF MSEKWA JULIUS. THANKS THAT ARE ALL TO SAY NOW BYE!

    ReplyDelete
  3. Pole Mzee Msekwa,Pole Mama Anna, Pole Jacob ndugu na jamaa wote. Ni Kipindi kigumu sana, lakini tunawaombe kwa mungu awape moyo wa subira. Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie, astarehe kwa amani. AMINA

    Mdau - Beijing.

    ReplyDelete
  4. PETER NALITOLELA, TOA VUMBI ZAKO NA WEWE HAPA KUFIWA NA KUBRASHI VIATU WAPI NA WAPI. WATU WAKO KWENYE KILIO UNATAKA WAWE SMART WANAENDA KWENYE HARUSI. USITUCHAFULIE HALI Y A HEWA. RIP JULIUS MSEKWA, BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE. POLENI SANA WAFIWA

    ReplyDelete
  5. We Peter Matolela unatoka dunia gani na unaishi dunia gani? Ulizaliwa na kukulia Tanzania au dharau ya ulikokulia nini?
    Hao waombolezaji wako Tanzania na hakuna siyejua vumbi linavyong'arisha viatu na katambuga achilia mbali kandambili za wamachinga.
    Wanakozika makaburini kuna lami?
    Ndugu Peter Matolela jaribu kuwa na upembuzi wa kiustaarabu na kusoma ishara za nyakati, mazingira na majira ili utoe comments sahihi zinazosheheni ukweli na uzito unaotakiwa. Ninyi ndo mnaoweza kuwakana wazazi wenu tokana na hali walizo nazo bila kukumbua kwamba bila wao usingekuwepo na wao ndo wamekutunza uonekane ulivyo. Kama una uchungu basi watumie brush na dawa ya kung'arishia viatu badala ya kuwaanika hadharani bila kujali msongo wa uchungu wa kuachwa na ndugu yao aliyekuwa tegemeo la familia yao.

    Poleni sana wafiwa na tukumbuka kazi ya Mungu haina makosa, na ndo sote hatima yetu ni huko alikotutangulia mwenzetu.
    Hakika hapa tunakumbushwa kuwa tayari kwani hatujui siku wala mwaka Bwana atakuja kutuchukua kuyaendea makazi yetu ya kudumu.

    ReplyDelete
  6. R.I.P Julius

    Nawapa pole wahusika wote kwa msiba wa ndugu yetu,ambao umetupata ghafla bila ya mategemeo.
    Julius atakuwa moyoni mwetu daima
    Mungu amlaze mahari pema.

    mickey jones
    mdau wa Denmark

    ReplyDelete
  7. Wewe PETER NALITOLELA hapo juu, nakushauri uka-polish kwanza english yako kabla ujaanza kuuliza kwa nini viatu having'ai kwenye msiba. Watu wako msibani hapo na sio harusini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...