Kaka Michuzi,

Pole kwa majukumu ya kutuhabarisha Watanzania.

Kaka nia na madhumuni ya kukuandikia ni kulalamikia utendaji mbovu wa shirika letu la Tanesco. Toka siku ya jumatatu tumekuwa hatuna umeme kwasababu mashine ya Luku imekataa kupokea kadi ya luku.

Tumetoa taarifa tanesco Mikocheni toka Jumatatu lakini kila siku tunaambiwa Kesho. Jana Alhamis wamekuja watu wa Emergency wakasema tatizo ni Luku hadi waje watu wa idara husika. Sasa ni saa moja na nusu na hawajafika.

Humu ndani tuna mtoto mchanga wa wiki tatu. vyakula vimeharibika na sie wa kwenda kazini ndio tumemnufaisha dhobi.

Malalamiko yangu ni kuwa kwa nini ichukue zaidi ya siku tano kwa mteja kupata huduma anayostahili. Ama kwa kuwa wao wapi pekee yao katika utoaji huduma.

Mteja aliye gizani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. emmanuel h. lyimoSeptember 24, 2010

    pole sana kwa msukosuko..tafakari kisha chukua hatua na jua wapi pa kupeleka kura yako.

    ReplyDelete
  2. Pole sana mzee, hawa jamaa si tu kwamba wamejisahau hawajari wateja wao kulingana na mfumo uliopo hapa nchini wa wao peke yao kujimilikisha soko. Mimi kwa usmart wangu wa kutokutoa chochote nilishawahi kusotea huduma ya kuunganishiwa umeme kwa mwaka na miesi saba kisa nguzo hakuna wakati wengine wanaunganishiwa ndani ya wiki. Wewe ulishawahi kuona wapi eti ule mti wa nguzo unauziwa milioni moja na bado sio mali yako maana siku yoyote mkishindwana wanakuja wanondoka na nguzo yao na hawakurefundi pesa uliyoilipia. Nina imani flan mbovu kuwa ipo siku watajutia utendaji wao mbovu na sijui ni kwanini hata hawajifunzi kwa Posta na Simu enzi zile. It is just a matter of time, one day everything will come to an end!

    ReplyDelete
  3. kule arusha nimelipia nguzo na kila kitu wiki ya pili sasa wanadai ati hawana wire za kutoka nguzoni kwenda kwenye nyumba sasa sijui ni rushwa inatakiwa hapa au vipi nawasikilizia tu , ila kama anony hapo alivyosema iko siku watakumbuka maana tushayaona kwa wengi ,wao sasa wanajiona miungu watu lakini ni binadamu tu hawa watuwa tanesco .
    MTEJA ANAYEONEWA

    ReplyDelete
  4. Wekeni solar power kwa matumizi muhimu ni cheapest, simple, efficiency na reliable ,tabu ya nini?

    ReplyDelete
  5. Mtejagizani, hamia huku ughaibuni, huku haukatiki na ukikatika bila sababu kwa muda mrefu wanakulipa fidia.

    ReplyDelete
  6. Mteja ulie gizani, sasa nimekaa mie mwenzio najiuliza hii msg kwa kaka mithupu umeandika vipi na wewe upo gizani ? au ulitumia smart phone kufanya mambo kwa kibatari? just kidding pole sana , unajua tunapenda kuandika utani sometimes kufurahisha wana jamii, mie huwa naipenda sana hii GLOBU ya Ankal, huwa nikiwa nimechoka basi natembea globu hii natafuta habari ya kuchekesha halafu naenda kwenye comments basi huwa nacheka sanaaaaaa , mpaka nalia sometimes , hakuna habari iliyonichekesha kama ile ya BASATA kukataza watu kutembea utupu jamani nilicheka sanaaaa! mpaka nikawa naumia kwa kucheka ...

    KAka Michuzi tunakuombea kila la Keri ...

    ReplyDelete
  7. TENA HII IMEKUJA WAKATI MUAFAKA, NA IKUPE CHACHU YA KWENDA KUPIGA KURA. ASANTE.

    ReplyDelete
  8. Na nyie nyie ndiyo mnatuambia kila siku kwamba turudi bongo eti bongo ni tambalale.....

    Ng'o!!!

    ReplyDelete
  9. Kaka, pole sana. Yaani umenigusa na umenigusa na kunitonesha kidonda kilichokuwa kimeanza kupona lakini kovu bado nalihisi.
    Ilikuwa mwezi wa tano nilipatwa na tatizo kama hilo la luku ilikuwa inakata umeme kila baada ya dakika 3 na kuwaka tena kwa dakika moja, mara inakata kabisa hadi saa saba usiku ndo umeme unatulia. Nimeripoti tatizo hilo kwa mwenye nyumba kawapigia simu jamaa walokuja baada ya wiki na kudai kuwa tatizo la luku lina watu wake... Ikachukua wiki mbili watu wa luku kuja tena bila kipimo cha kugundua tatizo ilivhukua tena wiki tatu wakaja na kipimo na kuthibitisha luku ni mbovu ikanichukua wiki tena kwa kubembeleza na kuwaahidi nauli japo gari walikuwa nalo, niliwaambia waje nitawapa hela yoyote watakayohitaji ndo walikuja na luku mpya kufunga bahati mbaya/nzuri hawakunikuta nikikuwa kazini wakaona aibu kudai hayo majisenti na wakaondoka. Kipindi chote hicho nilikuwa na mtoto mchanga wa wiki zote hizo.
    Kaka, nenda tanesco, mikocheni lipoti tatizo lako kaunta, watakuelekeza chumba. Ingia..mkamate fundi mmoja chukua namba yake ongea naye aje kwa muda wake ndo shughuli itafanyika. Hakuna la zaidi ukisubiri wajikunbushe unayumia ni wewe na mtoto maraika hasiyejua chichote.
    Mimi nilifika hatua nikamchukua fundi wa kitaa, nikamlipa sh 90,000. 30 ya ufundi na 60 ya waya akaunganisha moja kwa moja toka katika nguzo, kwa risk ya kwangu mwenyewe na familia na mali zangu na nyumba ya watu. Sikujari....!
    I know how it feels!
    Bennett M. R

    ReplyDelete
  10. Mbona huku Ulaya sijawahi kusikia mita ya umeme imeharibika tena ziko nyingine kama za LUKU kwa nini?

    Kwa sababu hakuna kutemper na mita?Hakuna kununua umeme wa vichochoroni, hakuna kununua kadi za magam za wakongo sijui deal za mafundi wa Tanesco, sasa hizo mita zitakaribika vipi wakati haziwi tempered. Tuwe wakweli wajameni WATZ tumezidi mambo yasio na maana ya kutaka rahisi na dezo, matokeo yake ndio hayo. Huku bili ya umeme usisikie na huwezi kusema eti nitapikia mkaa, kuni au mafuta ya taa, nishati ni mbili tu ni umeme au gesi na hakuna kuiba wala kutemper na mita ndio maana mnaona kuna maendeleo. Mpaka tukiamua kuwa wakweli matatizo yote hayo yataisha na maendeleo yatakuja.

    ReplyDelete
  11. ha ha ha - customer service sio mbaya tu bali IMEKUFA. Lakini uongozi pia mbovu katika nyanja zote. Zanzibar walikaa kwenye Giza miezi 3 na watu hawakijali.. eti wanatumiana MSN tu za uchungu.. sasa uchaguzi huo umefika - wapigieni kura hao hao wanaotulaza kwenye giza... maana wanapiga kampeni kwa kutumia bongo flava na kijidai kukaa chini na walemavu eti kuamsha hisia za wananchi ili wapate kura.. na masikini na sisi pia tunasahau tukiona tunaburudishwa na muziki - tunawapa kura.. na siku zote elimu ndogo kwetu sisi makusudi ili tusipate kuendelea kudai haki zetu... haya mungu ibariki africa..

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2014

    pole sana kaka hao jamaa hawanaga utu wao wanachoangalia ni masrai tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...