Mhe. Mustafa Haidi Mkulo, Waziri wa fedha na Uchumi wa Tanzania (shoto) akibadilishana mikataba aliyosaini na Bw. John Murray McIntire, Mkurugenzi Mkazi wa Nchi ya Tanzania, Uganda na Burundi baada ya kusainiwa kwa mkataba wa mkopo wa shilingi billioni 397.5 jijini Washington DC leoBw. John Murray McIntire akitoa ufafanuzi kuhusu msaada huo
Mhe. Mustafa Haidi Mkulo, Waziri wa fedha na Uchumi wa Tanzania, akishukuru kwa kufanikiwa kupata msaada huo Bw. John Murray McIntire wa Benki ya Dunia na ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa Nchi ya Tanzania, Uganda na Burundi akiwa na timu ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia mjini Washington D.C wakishuhudia kusainiwa kwa mkataba mkopo wa shilingi billioni 397.5 pamoja na wataalamu wa kiufundi kutoka Wizara ya fedha na uchumi.Kulia kabisa ni Bw. Omari khama akifuatiwa na Bw. John Mavura na baada ya Waziri wa fedha ni Bw. Ngosha magonya na Bw. Patrick Pima. Picha zote na mdau Ingiahedi Mduma






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. I hope mtajenga highways sasa.

    ReplyDelete
  2. Watanzania tuache lugha za miaka ya 60. Huo sio msaada ni mkopo, no more no less. Na mkopo sio wa kunyenyekea maana anayekukopesha sio amekusaidia, bali mnasaidiana maana anafahamu utarudisha.

    ReplyDelete
  3. Jamani nimempenda huyo mwanamke camerawoman tena jikamera zito hilo linaonekana! Hongera mdada.

    ReplyDelete
  4. mheshimiwa mkopo sio msaada,na huo mkopo hautaweza kulipwa.

    ReplyDelete
  5. Yale yale hata tupewe misaada yenye urefu toka duniani hadi mbinguni hakuna mabadiliko yatakayotokea kwa mwananchi wa kawaida.Hawa watu bora wangetusahau wasitupe misaada wala nini labda tungejanjaruka na kufanya mabadiliko.Napendekeza Bongo iwekewe vikwazo vya kiuchumi ili tutumie akili kuleta maendeleo kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa home.Pakiwa hakuna cha importation of foreign goods tungetumia tunachozalisha home na kuleta maendeleo pamoja na pride ya Tanzania na mali zake.

    ReplyDelete
  6. utabana sana comment zetu hila. utashindwa kwa jina la yesu.

    SHETANI TOKA! NA USHINDWE KWABISA.

    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  7. HUYO MTOA MSAADA MWENYEWE MBONA KANUNA HIVYO!! NGOJA NIJARIBU KUBUNI ANASEMAJE KICHWANI MWAKE. " THESE FOOLS GONNA CHEW DIS MONEY AGAIN " HAHAHA.

    KAKA USIBANE BASI, LEO BITHDAY YANGU!!

    ReplyDelete
  8. POINT OF CORRECTION _ HUO NI MKOPO NA SIO MSAADA.

    TUNAKOPA TUKAPRINT TENA MABANGO YA KAMPENI, HALAFU TUTALIPA MKOPO KWA KODI ZA WANANCHI.......

    ReplyDelete
  9. MSAADA ,MKOPO = SAME SAME.

    MDAU PARIS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...