Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete

NA MWANDISHI MAALUMU, KIGOMA

MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, amesema kufanya kampeni kwa kutumia udini na ukabila ni kuhatarisha amani.

Alisema hayo juzi na jana alipozungumza kwa nyakati tofauti na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoani hapa, alipokuwa akiwaombea kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Mama Salma alisema kuwagawa Watanzania kwa misingi ya udini na ukabila ni kutaka kutowesha amani ambayo imedumu nchini kwa miaka mingi.

“Udini na ukabila utatutenganisha, tutahasimiana kwa sababu huyu ni mkristo na yule ni muislamu, haya ni yale yale ya huyu ni Mtutsi na yule ni Mhutu, jamani kina mama huko ndiko tunataka kwenda ?” Alihoji na kujibiwa “hapana”.

Mama Salma alisema, wanachama wa vyama vya siasa wana dini zao, lakini usajili wa vyama hivyo haufanyiki kwa kuangalia dini na kabila, hivyo kufanya kampeni kwa vigezo hivyo ni ukiukaji wa sheria.

Wakati akizungumzia hilo, kina mama hao walikuwa wakimwitikia kwa kusema “sema mama usiogope” kuashiria kuna baadhi ya watu wanafanya kampeni za kibaguzi kwa kutumia udini na ukabila.

Mwenyekiti huyo wa WAMA ambaye ni mke wa mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alitahadharisha kwamba, amani kuvunjika ni rahisi, kuirejesha ni kazi kubwa na mifano ipo katika baadhi ya nchi za Afrika ambazo ziliichezea na haijarejea.

Aliwaambia wananchi wa Kigoma kwamba wao ni mashahidi wa namna nchi jirani zilivyoathirika kutokana na machafuko chanzo kikiwa ni siasa za kibaguzi zilizojiegemeza kwenye udini na ukabila.

Mama Salma aliwaombea kura wagombea ubunge kwa tiketi ya CCM; Injinia Christopher Chiza (Buyungu), Jamal Tamimu (Muhambwe), Daniel Nsanzugwanko (Kasulu Vijijini), Raphael Neka (Kasulu Mjini), Robson Lembo (Kigoma Kaskazini), Peter Serukamba (Kigoma Mjini) na Gulamuhussein Kifu (Kigoma Kusini).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Ni kweli kabisa: Cha Mungu ni cha Mungu na cha Kaizari ni cha Kaizari. Tuwapuuze wale wanaojidai kuwa ni "viongozi" wa dini wanaochochea chuki wakijitia eti ni watumishi wa Bwana kumbe ni mawakala wa Lucifer.

    ReplyDelete
  2. CCM ndicho chama pekee kinachowaunganisha Watanzania wa makabila, dini na rangi zote. Copy and paste that. Morani7.

    ReplyDelete
  3. Umesema kweli mama. Mfano mzuri ni katika jimbo letu la Kigoma Kusini kuna mchungaji wa kanisa letu amekuwa akisambaza message za simu akitutaka tumchague mgombea wa dini yetu na si Gulam kwa sababu Gulam ni Mwislamu. Hata hivyo, baada ya sisi kumwambia kuwa anachofanya si kitu kizuri na hakiendani na mafunzo ya Injili amewacha mcezo huo mcafu na kukiri kuwa amekosea. Ninachosema ni kuwa sisi kondoo pia tunaweza kuwaasa wachungaji wetu kama wakipotoka, mradi tuwakosoe kwa heshima na uungwana kwa sababu wengi wao wanayo imani ambayo inawafanya watafakari na kukubali uadilifu.

    ReplyDelete
  4. ELIMU NDOGO NI TATIZO

    ReplyDelete
  5. She knows what she will miss being out of Ikulu!

    ReplyDelete
  6. Heko Michu, taswira inaendana vizuri na habari.
    Nimekuwa nikisikia viongozi wa CCM kama Salma Kikwete :) wakiongea kupiga vita kampeni za ukabila. Kinachonitatiza ni kuwa ni nani hao wanaoendesha kampeni za udini na ukabila? Kwa nini hawachukuliwi hatua? Sheria ya usajili wa vyama vya siasa inazuia usajili wa vyama vya siasa vyenye misingi ya udini na ukabila. Ina maana ukisajiliwa unaruhusiwa kupiga kampeni kwa misingi hiyo? Au ndio ile mbinu ya kampeni ya kutengeneza tatizo ambalo halipo halafu inapobainika kwamba tatizo halipo unatamba umelitatua?

    ReplyDelete
  7. Mmesha tutenganisha kati ya mafisadi na maskini.
    Mmesha geuza uraisi/uongozi ni suala la ukoo na sio la wote. Hivyo watoto wenu, Liziwani, Makamba ndio wanafaa kwa uongozi na si wengine.
    Meeshatutenganisha kiuchumi kati yenu matajiri na mtanzania wa kawaida mwenye maisha duni.
    MSITUMIE DINI NA UKABILA KUWADANGANYA WANANCHI AMBAO HAMUWAJALI NA HAMUWATUMIKII KWA HAKI.
    Acheni longolongo na kudhani watanzania ni mambumbumbu

    ReplyDelete
  8. Yeye mwenyewe ndiye mdini mkubwa, ukweli ni palepale, CCM katika uteuzi wao wamefuata udini sana. Nyinyi kina mama msidanganyike, chagueni mtu mwingine, tuondako ni kubaka, kila kona jamaa kamuweka...angalieni fungueni macho.

    ReplyDelete
  9. Huyu mama anajua fika kuwa Chama chake ndicho kimekuwa mstari wa mbele kuingiza hisia za udini.Aaanze basi kuwakemea CCM

    ReplyDelete
  10. MAMA FOR FUTURE PRESIDENT OF THE REPUBLIC

    ReplyDelete
  11. Pia kutumia migongo ya taasisi fulani ni kuhatarisha umma.

    ReplyDelete
  12. CCM HAKINA UDINI. Tangu kampeni zianze sijawahi kusikia kampeni imefanywa misikitini wala sijawahi kusikia sheikh yeyote akito agizo kwa waumini wampige kura nani. Ni juzi tu Watanzania tumemsikia Kakobe katika TV (Star na Channel 10) akiifanyia kampeni kyadema hadi kufikia hatua ya kufuta ibada ya jumapili 31 Oktoba. Mpaka leo sijasikia kiongozi yeyote wa kyadema akikemea uchanganyaji wa dini na siasa makanisani. Nyinyi watetetezi wa kyadema mnajua wazi kuwa kampeni ya kyadema imekumbwa na chuki za kidini (sms, vipeperushi, n.k.) Kama hamtaki kukubali kuwa mna ugonjwa huo basi nyinyi ni kama mbuni anayeficha kichwa chake ardhini ili asiliwe na simba!!!!!

    ReplyDelete
  13. Umenena ukweli mama Salma. Endelea kusema ukweli; kata kama "sikio la kufa (chadema) halisikii dawa".

    ReplyDelete
  14. Nyinyi wachangiaji wa Chadema mnaomwaga chuki, dharau na uongo hapa, dawa yenu tunayo: Tutawagaragaza tarehe 31/10/2010 na jeuri yenu itakatika. CCM Singida cadre.

    ReplyDelete
  15. UKabila gani? Uarabu? uzungu? Ahsante tumekusikia.
    Kumbe ni kweli unapenda kabisa haki za watu.

    ReplyDelete
  16. All we should pray for is PEACE, LOVE, UNITY....NCHI YETU NZURI YA TANZANIA IWE YA UMOJA, AMANI, UPENDO NA UTULIVU... WE STILL NEED TO BE THE 'HAVEN OF PEACE'... Hatutaki ukabila, udini wala chuki dhidi yetu vishamiri. Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardhi na kila kilichomo atuepushe na kila nuksi, fitna, shari na majungu ya kututenganisha na amani pamoja na uroho wa baadhi ya watu wachache. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki viongozi wake wawe na hekima, wabariki na uwalinde watoto wote, masikini wote na matajiri pia. Ameen!

    ReplyDelete
  17. UDINI UPO,

    CHEKI KOMENTI KADHAA ZILIVYO

    ReplyDelete
  18. Hakuna udini hapa! yale yale ya watu wenye upeo mdogo kutishiwa suala la AMANI. Wakati wa Mrema yuko juu kisiasa alishambuliwa sana na kikundi kimoja ktk msikiti mmoja maaruf, CUF ilipokua kwenye chati(juu) ikawa zamu ya upande wa pili, CCM ikadai ni chama cha kidini(Uislaam)haikukemea wakati Mrema anashambuliwa kwa Mtoro, na kweli sehemu za pwani (Tanga, Lindi, Mtwara) walipata wanachama kirahisi sana. CCM walipoona hilo jambo linawadhuru wakaacha! Again alivyoingia Kikwete, hapa katikati ameonekana kama anapigwa vita na upande wapili na viongozi wa Dini. Kuna kiongozi mzito wa dini aliwahi kushusha tuhuma/madongo ya nguvu mbele yake. Sasa.......ni kale kale kamchezo kanaendele, anaepiga kelele sana ujue kanamsaidia katika kampeni. Vinginevyo kimsingi hakuna kampeni za Udini wala Udini. Yupo mtu anaweza kutoa Data za kuaminika kuonyesha matokeo yoyote ambayo yamewahi kusababishwa au kupangika na udini?!
    Mgosi Guluguja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...