Kaka Michuzi,

habari za kazi na maisha. Kwanza nakuputa hongera kwa kazi nzuri unayoifanya katika kuendeleza blog yako. Pili nakushukuru kwa kupata muda wa kuisoma mail yangu hii, naamini uko busy sana na unapata email nyingi kila siku, kwa hivyo sitochukuwa muda mrefu kueleza malengo ya email hii.

Kwa jina naitwa Ahmed Salem, kwa muda huu ninaishi na kufanya kazi hapa uk. Nilikuja kipindi na kujitahidi kujisomesha wakati huo huo nikipiga boksi. Nimefanikiwa kumaliza masomo yangu na nimekuwa nikifanya kazi katika kampuni moja ya IT hapa london kama Technical Support Field Engineer.

Kwa muda mrefu lengo langu ni kurudi nyumbani na kusaidia wanyonge wenzangu kielimu. Nahisi muda umefika wa mimi kurudi nyumbani na kutimiza lengo langu. Nakusudia kurudi nyumbani mwanzoni mwa mwezi wa januari na nataka kufanya kazi ya kusomesha vijana kwenye charity organisation.

Ninachotaka kuomba kwako na wasomaji wako walio tanzania ni msaada na muongozo wa kuweza kuwasiliana na charity organization zilizopo tanzania ambazo zinawasaidia watoto na vijana kielimu. Ningelipenda zaidi kujua organisation zilizo na base sehemu kama arusha, tanga na visiwani zanzibar.

Nakaribisha, ushauri na mawazo kutoka kwa wote.Pia napokea maoni na ushauri kupitia email hii

ahmedyoungafrican@gmail.com

ahsante sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ahmed wa Magomeni, I presume.

    ReplyDelete
  2. we m beba box vp ww! nani kakwambia anashida ya kusaidiwa na pesa zako??

    ReplyDelete
  3. Ahmed tuwasiliane kupitia mbuyanzi@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. Nakushauri anza na pale kijijini kwenu kama kweli nia na malengo yako ni ya kweli.

    ReplyDelete
  5. Bwaa Ahmed Salem, lini umefika UK? kama juzi juzi tulionana pale michenzani Zanzibar?

    Mbona unawaongopea wenzio hivyo, acha!!!!

    KK
    Magamba Coast.

    ReplyDelete
  6. Mbona unapenda charity organizesheni ili kupata pesa za bure badala ya kuanzisha charity ya kwako mwenyewe. Tusipende kupata vya dezo vilivyoandaliwa na wengine. Bora anza mradi wako mwenyewe hapo tutakuona umekamilika na lengo la kusaidia kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...