Boma la Bagamoyo likipigwa sop-sop ili liwe kama mengine kibao yaliyokarabatiwa ama yanayokarabatiwa sasa na kuufanya mji huu mkongwe uwakewake na uzidi kuvutia watalii wa nje na wa ndani
mojawapo ya majengo yaliyokarabatiwa pamoja na barabara ambayo imejengwa kama iliyokuwa enzi hizo, sio kwa lami bali vitofali
Jengo lingine ambalo sasa linawaka ile mbaya baada ya
ukarabati na barabara mpya mbele yake
Hii ndiyo posta ya kwanza Afrika Mashariki karibu na bandari ya Bagamoyo. Hivi sasa inakarabatiwa na kuwa sehemu ya hoteli ya Millenium inayomalizia jengo lake kuu linaloangalia bahari kwa nyuma ya hii posta
Jengo jipya la Millenium bega kwa bega na posta ya zamani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. TUNAJUA.
    Bandari Kuu (ya kuchimba) inakuja, Kiwanja cha ndege cha kimataifa kinakuja.
    Last chance STRATEGIES. Nizubae nichekwe!!!

    ReplyDelete
  2. Tibaijuka umemwona huyo hapo posta?

    ReplyDelete
  3. Haiingii akilini... Posta ya kwanza East Africa leo inageuzwa Hoteli? Urithi wa makumbusho ya kale unaenda wapi sasa?!!! hii ni aibu sana na mi uharibifu wa vivutio vya utalii.. Hivi Bagamoyo viwanja vimeisha kiasi hicho?

    Mzozaji

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...