Aina Maeda (kati) ndiye mshindi wa kwanza wa Miss TZ ilipoibuka tena mwaka 1994. Wa pili alikuwa Lucy Ngongoseke (shoto) na wa tatu alikuwa Dotto Abuu
Miss Zanzibar wa kwanza na wa mwisho Hediye Khamis Mussa (kati) akiwa na washindi wa pili na watatu January 13, 1968 ambapo baada ya kuonekana mashindano hayo yanaenda kinyume na maadili ya visiwani yalipigwa marufuku na hayajawahi kufanyika tena huko Zenji
Miss Tanzania wa kwanza Theresa Shayo akipita kwenye kingo za bwawa la kuogelea la hoteli ya Kilimanjaro mwaka 1967. Wazee wa bara nao waliona hii kitu si sawa na kupiga stop mashindano ya urembo ambayo yakaja kuibuka tena mwaka 1994 na kuendelea hadi hii leo. Mjadala unakaribishwa wa je, ilikuwa sahihi kupiga marufuku mashindano haya?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Labda yafaa tuwaulize hao wazee, kama bado wapo. Kwa nini tuwapime kwa vigezo vya kisasa?

    Wazee wa Kiyunani, Kiitalia na wazee wetu wa zamani waliamini kuwa moyo wa binadamu ndio senta.

    Lakini leo hii tunaamini kuwa ubongo ndio senta. Myo ni mashini tu ya kusukuma damu. Kuna watu wamepewa na kuendelea kuishi kwa muda na mioyo ya vyuma na ya nyani.

    Lakini hakuna anayeweza kuishi kwa ubongo wa chuma au wa nyani! Labda hapo kesho, sijui!

    ReplyDelete
  2. Aaaaaaah hakuna sababu za kuzuia hiyo Miss kwa kipindi kile kwani kilikuwa hakidhalilishi.

    Ila kwa karne hii mhhhhhhhhhhhhh!

    ReplyDelete
  3. we jamaa wa kwanza hapo juu. Mtu mwenye moyo wa chuma au nguruwe hawezi kuwa na hisia sawa na mtu mwenye moyo wa mtu.

    Au labda moyo haukumaanisha moyo wa kusukuma damu kwani baiolojia ilikuwa finyu. Labda moyo maana yake ilikuwa uzindufu. ile nafasi ya akili yenye hisia na kutambua utu.

    ReplyDelete
  4. Naamini hili suala linahitaji mjadala, nami niliwahi kuchangia kidogo makala hii hapa.

    ReplyDelete
  5. Ni big business hiyo hakuna anaeweza kuzuia kwa sasa.Watunga sheria wenyewe hawana nguvu za kusimamisha hayo mambo

    ReplyDelete
  6. ungetutafutia na picha zao za sasa,tujue wako wapi?looo sana.

    ReplyDelete
  7. Maadili ya kiislamu sawa ! lkn maadili ya kiafrika ? nadhani hapo ukweli aukupimwa kwa uhakika ! tujaribu kuona ngoma zetu na mengineyo yenye kututambulisha utamaduni wetu yakoje ? kama ngoma za kwenye sherehe mbalimbali za makabila mbalimbali ya kiafrika yakoje ? jibu litapatikan !
    MZUSHI

    ReplyDelete
  8. Haya mambo yote yakishenzi shenzi ni matokeo ya FREEMASONS kuwa na influence kubwa duniani.
    Kila mtu mwenye uungwana na ustaarabu hawezi kukubali upuuzi huu.Najua ntaonekana mm naishi karne ya pili bt huu ndio ukweli.Mimi sio mshamba wala sio mjinga,naishi ulaya,nimesoma bachelor yangu ya medicine lkn siwezi kuacha imani na maadili yangu.
    Watu wengi wamekua watumwa wa mufsiduun(waharibifu wa dunia) kiasi kwamba wamepoteza uwezo wao wakutafakari mambo kwa kina nakudhani kwamba utu wa mtu hupimwa kwa uwezo wakifedha na umaarufu.Ni kwa sababu hii wengi wetu tunaona kl jambo linalofanywa nchi zilizoendelea kitekhnolojia au kl jambo linalofanywa na watu maarufu kwamba ni sahihi.Huu ni utumwa wakifikra na ulimbukeni.
    Nasema wazee walikua sahihi na ipo siku haya mambo yatakuja kuondoka duniani bcoz naamini kwamba sheria ya Mungu itatawala tena kabla kiama hakija simama.
    Na ole wenu wenye kushabikia upuuzi kwani mnajichumia dhima msizoweza na muda mfupi mtajutia kauli zenu na ushabiki wenu wakukurupuka bila kufanya tafakuri na kumkumbuka Mungu,mmefikia wakati mnashabikia na kutetea hata usenge(ushoga9...!Huu ni zaidi ya unyama...

    ReplyDelete
  9. Hao waliokataza wakati ule ndio wanafiki wakubwa. Ndio wa kwanza kuwa na nyumba ndogo, watoto wa nje ya ndoa, kutembea na wanafunzi wa kike, n.k. Kama hupendi kutazama warembo, usiende kwenye hayo mashindano, kwa sababu hulazimishwi kwenda au kutazama kwenye TV hayo mashindano. Wanafiki utawajua tu, wa kwanza kuonyesha vidole kwa wenzao wakati yao wanayaficha.

    ReplyDelete
  10. Mie naona ni bora kuacha mambo ya u miss kwa sababu mmoja kubwa hatufuati utaratibu na kanuni kijana au teenager awe na sifa zipi mpaka asimame kuwa miss mnaokota kila mtu ili mradi mzuri basi anafaa kuwa miss lazima awe anaenda shule awe mmkarimu awe na tabia njema asiwe mtu wa tamaa kuna vigezo vingi vinatakiwa kuwa na sifa ya u miss ndio matokeo yake baada ya kupewa tu umiss angalia balaa lake mtaani sijui wa tanzania kama tunajua yote hayo acheni mambo mengine angalieni kutatua umaskini kusomesha watoto yatima kuwapa elimu bora kila mtanzania kujitoa kwenye umaskini

    ReplyDelete
  11. miss wa kizenji!! Mweh
    mdau paris

    ReplyDelete
  12. MutafukurakinulwaDecember 05, 2010

    Kimsingi wa kidini...vazi la ufukweni ni just wrong!!. Hiyo sio modesty inayoongelewa na dini zetu kuu mbili Uislamu na Ukristo. Kiutamaduni....mmh, utamaduni wa nchi hubadilika na wakati, na ni wakati tu ndio unaamua kama muda umefika au haujafika wa kubadilika. Kuendelea kwa mashindano hayo tangu 1994 mpaka sasa ni ushahidi tosha kuwa huu ni wakati wake....manaake inakubalika.

    ReplyDelete
  13. Kupoteza mila na desturi ni kupoteza dira. Kupiga marufuku kitu chochote kile sio sahihi. Kilichotakiwa kufanyika ni kuhakikisha maonyesho kama haya yanafanyika kwa kuzingatia na kuimarisha mila na desturi za jamii.

    ReplyDelete
  14. Mrembo hatafutwi katika majukwaa. Hizi ni njama za watu wa magharibi katika kuwadhalilisha wanawake, na wanataka watu wote waende katika utaratibu wao. Wanawake wao tayari wanadhalilishwa kwa kuendeshwa uchi sehemu ambazo wanaume wanavaa nguo, lakini kinyume chake wanawaambia waislamu kwamba wanawake kuvaa nguo za heshima ndio kuwadhalilisha. Adhabu yake ni UKIMWI tu. Mnayaona yanayoendelea sasa hivi Tanzania huwi mrembo kama hujatoa ...

    Zanzibar wanajijua ndio maana wameendelea kupiga marufuku, kazi kwetu Tz.

    ReplyDelete
  15. hao walikuwa na akili kuzuia mambo yanayodhalilisha wanawake. na bora iwe hivyohivyo hatutaki umiss zenji. wazungu walianzisha umiss ili wauze chupi za kuogelea sasa nyinyi mna sababu gani zaidi ya kudhalilisha mabinti kwa vijihela mbuzi badala ya kuchochea maendeleo kwa kuhimiza watoto wasome nyie mmebaki na tamaa ya kuridhisha macho yenu kwa tamaa mbovu..kuna mambo kibao ya maana mbina hamyapigii debe kuigwa...

    ReplyDelete
  16. Mashindano ya urembo hayana tatizo isipokuwa pale inapotokea mshiriki akawa ni mwanano wa kumzaa au mdogo/dada yako wa damu. Mbaya zaidi akimaliza kushiriki asishinde huku jamaa wamesha mchakachua!

    ReplyDelete
  17. MICHUZI, KWANINI UNALETA MJADALA AMBAO UNAJUA JIBU LAKE NI NINI.HII NCHI SIYO IRAN INAYOONGOZWA NA SHERIA ZA KIISLAM ZA KUNYANYASA RAIA. KWANINI TUJADILI MASHINDANO AMBAYO JIBU LAKE NI KUWA YATAENDELEA TU. KAMA KUNA WATU HAWATAKI KUANGALIA...HAWALAZIMISHWI, WANAWEZA KUANGALIA VIPINDI VYA WAKULIMA WA KISASA AU UFUGAJI BORA AU WAKAJIKALIA KIMYA NA MAMBO YAO. MASHINDANO HAYA YATAENDELEA TU KWA TANZANIA BARA, HAKUNA MTU ANAYELAZIMISHWA KUANGALIA.

    ReplyDelete
  18. Mimi nakuuliza wewe kaka Michuzi mtoto wako wa kike utamruhusu ashirki katika mashindano hayo?

    ReplyDelete
  19. Kwani lazima kila mmoja ashiriki au aangalie? Kama mtu hataki kuangalia kuna channels nyingi sana za kuangalia mnaweza kuangalia. Msifanye sheria za kiislam zitutawale...Waachieni uhuru watu wafurahie wanachokitaka..kisichokupendeza si lazima kisiwapendeze wengine. Wakati wa udikteta umekwisha...je mnataka hao warembo wavae kanzu au burqa...sheria zenu zisiwe kero kwa wengine wasio waumini wa dini yenu.

    ReplyDelete
  20. zitto kiaratuDecember 05, 2010

    aliyesema kuwa walizuia yote haya ili wazungu wauze chupi sio kweli, hapa tunazungumzia uhuru wa kina mama, kwa nini sisi vibaba tuamue haki za kinamama, kama uislamu, ukristo hauruhusu yote haya hiyo ni tatizo lako/lenu, sisi tunataka uhuru wa kina mama, jamani hembu tumieni akili wenzetu wamerusha ndege hewani, wanaanza kubishana kama wanaume/wanawake wanaweza kuowana sisi bado tubishana kuhusu wanawake kuvaa chupi kwenye nchi za joto!!! hii yote ni uhuru wa kina-mama wanachotaka, haihusu uhuru wa kina-baba. haki za kina-mama zimeaanza 1975 lakini bongo leo tunazidi kurudi nyuma. nadhani tungeanza mjadala wa katiba ili wote tuwe huru kweli

    ReplyDelete
  21. hahahaaa nafikiri waliona hicho kimini na guu la miss tz ndio maana wakapiga marufuku!!

    ReplyDelete
  22. Huyo dotto ni yule wa Kassati, naona kama anafanana naye. Yupo malekani kwa sasa. Tuleteeni data za wadada wengine hapo. e.g. Saida kessy. Angalao Lucy tulimuona sana alipokuwa Multi Choice

    ReplyDelete
  23. MSUKUMAMJITADecember 05, 2010

    Kisura hana mkorogo, hana nywele za bandia, hana wembamba wakulazimisha, ngozi iko "natural", haijakwanguliwa na lotions wala cream wala moisturizers.

    HUYU NDIYE MTOTO WA MZURI WA KIKE WA KITANZANIA TUNAYEMTAKA, KUMTAMANI NA KUMPENDA!!

    ReplyDelete
  24. KILA MTU ANA FANYA APENDACHO TANZANIA NI NCHI ILIO NA HUURU,SASA MNAOTAKA KULETA MAMBO YA KINA SADAMU HUSENI PLZ PELEKENI IRAQ NA SIO BONGO,

    ReplyDelete
  25. Hili swala ni vere simpo jamanii! TZ in secular state, yaani inaruhusu uhuru wa kuabudu. Hakuna dini ambayo ina ruhusa ya kuingilia uhuru wa waumini wa dini nyingine, au siyo?

    Kama dini ya ki-islam inakataka mambo ya mamisi, mabinti wa dini hiyo wana uhuru wa kutoshiriki. Hakuna aliyelazimisha ushiriki wao. Ni hiari yao. Lakini hapa nina wasiwasi, iwapo kigezo cha ushiriki itawekwa 'WAISLAMU HAWATAKIWI KUSHIRIKI', wallah itazua purukushani kuwa inji inaendeshwa na maparoko.

    Ikumbukwe kuwa dini ni swala la imani, ni undani wa mtu na wala haijikiti katika mambo yanayoonekana mbele ya watu tu. Ndio maana ukienda Saudi Arabia ambako ni chimbuko la didi ya Uislamu, waweza kuona many'ang'unyang'u ambayo yanafanywa na waumini, huwezi kuamini. Hata ukienda VATICAN, mambo ni yaleyale, wahusika miongoni mwao ni wakuu wa dini.

    Mambo hayaishii kwenye umisi tu, hebu angalia pia swala la kilaji! Itabidi mabar yawe na mabango ya kuzuia watu wa dini fulani? Au itabidi vitambulisho (identity cards) ziainishe dini? Kama ni wa dini flani, ruksa kinywaji, vinginevyo nooo!

    Japo nilisema simpo mwanzoni, lakini naona ni kompliketedi hii ishu. Mhusika ukibania imekugusa, na ujumbe utakuwa umefika angalau kwa mtu mmoja.

    ReplyDelete
  26. Kwanza ni Ajira kwa Watanzani kuli kuwa hakuna haja ya kupiga marufuku kabisa.Lakini hao wazee walio kuwa wanatuongoza walichukulia kama ni huhuni na kuchanganya na dini na biashara.
    Hii ni biashara na kama michezo mingine siyo huhuni wala mambo mabaya kabisa.TANZANIA HATUPO SAUDI ARABIA AU AFRICANISTANI [Taliban au Alkaida] na hawa jamaa wasitulete manbo ya Kitalibani ktk nch yetu.We are free country not under TALIBAN NA ALKAIDA NEXT THINK MTASEMA TUVAE MABUGA NA MAVELI.pLSE WE LOVE OUR COUNRTY AND ALL PEOPLE LIVES THERE AMANI NA UMOJA.

    ReplyDelete
  27. As long as wanawake wenyewe wanaona raha na kuridhika kuonesha maumbile na uchi wao kwa kulipwa pesa, sioni kwa nini wadume wakate hiyo burudani! Hii haina tofauti na midume kuonesha ubabe wao kwa kutwangana na wakati mwingine kuuana katika kile kitu inaitwa "mchezo" wa ndondi/masumbwi. Ndivyo Muumba alivyoumba dunia femenine (na vionjo vyake) na masculine (na vionjo vyake). Wenye navyo acha watupatie raha nasi tuwalipe kwa kutuburudisha. the bottmline ni BURUDANI kama burudani nyingine yo yote ile.

    ReplyDelete
  28. Mdau uliyetaja freemasons hapo juu..uliyesoma medicine ulaya.. naomba nikuulize swali.
    Je unajua historia ya freemasons??unajua kwa nini wakaitwa devil worshippers?? who was the source of devil worshiping name to them??akina nani wanaweza kuwa invited kuwa freemasons maana huiingi kichwa kichwa?? je unajua nchi karibia zote duniani (ikiwemo Tz)zinatawala kwa sheria za freemasons except zenye system za ufalme na umalkia kama uingereza? tafuta historia yake ukishaijua utafahamu vyema picha tuliyonayo sisi na jinsi walivyo wao ni vitu viwili tofauti..I refused completely hadi nikanunua vitabu vya historia yao and some tv stations pia walitoa history yao kuanzia ilikotokea masons.
    Ingia amazon.com tafuta kitabu kinaitwa the freemasons. Mimi sio freemason ila at some point tuna definition mbovu kuhusu wao japo ni wakatili at some points

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...