
Habari ya kazi Michuzi?
naomba uniwekee katangazo kangu haka, ila sio ka biashara.
Sasa nilikuwa na katatizo kadogo ka mambo ya fedha. Nikaona niuze haka ka-laptop
kangu. sasa kama Mdau yoyote anaehitaji anione. Kapo kamoja tu. nauza sh.550,000/=.
ila wasiniulize maswala ya biashara mimi siagizi
ila nimeamua kukauza kamoja tu kupata
vijisenti.
specification: 1GB Ram, HDD 120 GB intel Cerelon ,
contact: 0716-291773 or 0787-291773.
katatizo ni kwamba hako kalaptop kako ni kaghali, halafu kametumika,pia hujasema ni ka-model gani.
ReplyDeleteaisee watu wapo kwenye core i7 wewe unaleta hako ka celeron leo hii...mpe mwanao ajifunzie computer.
ReplyDeleteHuyu nafikiri alitoka bongo siku nyingi. Huku bongo shwali kabisa tunaenda na wakati. Labda nikusaidie kuuliza dampo lililokuwa tabata lilihamia wapi ili upate pahala pa kukatupa
ReplyDeleteKama mtu huhitaji laptop hiyo hakuna haja ya kuanza kulaani eti 'ka celeron' na i7. Watu mnatumia computer kujumlishia michango ya harusi tu halafu mnajifanya mnataka processor za core i7 sijui.
ReplyDeleteVibaka wa laptops utawajua tuu...hawana hata aibu......X-mass hiyoooo imewasili...utampata nani usawa huu....
ReplyDeleteacha maneno ya dharau wewe, kama wewe upo ktk core i7 kimpango wako!
ReplyDeletehahahahahaa...wabongo ni nomaa!!!
ReplyDeleteMimi nakataka ila nini 200,000/= na email yangu ni lyimo2@yahoo.com
ReplyDeletekama utaafiki niambie tufanye kabiashara bana. acha wanaobeza wanao.
hamna cha dharau ni hali halisi,55oooo nyingi mno kwa laptop hiyo,laki moja nitamsaidia,sasa 1gb ram inasukuma nn tena na sijui space itakuwa ngap?
ReplyDeletenyie waosha vinywa kwani lazima mtoe maoni ? wabongo bwana kazi kuharibia wenzenu biashara zao , roho mbaya tu zimewasakama ....khaaaa
ReplyDeletemdau wa Tue Dec 07, 12:29:00 AM wewe ni bichwa maji na wakuja big time. core i7 ndio umeona nini? hujui hata latest version iliyopo, pia kwa taarifa yako inapokua kwenye kompyuta na laptop jambo muhimu la kuangalia ni kwa matumizi gani unataka kuitumia.
ReplyDeleteushamba mzigo wa kuni! mtu katangaza biashara yake watu mnaanza kuchonga we kama hutaki si unyamaze kimya. Wabongo bwana hovyo kwelikweli!
ReplyDeleteKaka bei haijakaa sawa, cerelon hata kwa matumizi ya kuchapa barua tu inasumbua, inaganda kwenye kusave. afu cerelon yenyewe used duh. anyway,sijui umeuawa kiasi gani, ila kama sio saaaana , mpe tu mdogo wako aitumie, hapa utalaliwa tu.
ReplyDelete