Habari ya kazi Michuzi?
naomba uniwekee katangazo kangu haka, ila sio ka biashara.
Sasa nilikuwa na katatizo kadogo ka mambo ya fedha. Nikaona niuze haka ka-laptop
kangu. sasa kama Mdau yoyote anaehitaji anione. Kapo kamoja tu. nauza sh.550,000/=.
ila wasiniulize maswala ya biashara mimi siagizi
ila nimeamua kukauza kamoja tu kupata
vijisenti.

specification: 1GB Ram, HDD 120 GB intel Cerelon ,
contact: 0716-291773 or 0787-291773.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. katatizo ni kwamba hako kalaptop kako ni kaghali, halafu kametumika,pia hujasema ni ka-model gani.

    ReplyDelete
  2. aisee watu wapo kwenye core i7 wewe unaleta hako ka celeron leo hii...mpe mwanao ajifunzie computer.

    ReplyDelete
  3. Huyu nafikiri alitoka bongo siku nyingi. Huku bongo shwali kabisa tunaenda na wakati. Labda nikusaidie kuuliza dampo lililokuwa tabata lilihamia wapi ili upate pahala pa kukatupa

    ReplyDelete
  4. Kama mtu huhitaji laptop hiyo hakuna haja ya kuanza kulaani eti 'ka celeron' na i7. Watu mnatumia computer kujumlishia michango ya harusi tu halafu mnajifanya mnataka processor za core i7 sijui.

    ReplyDelete
  5. Vibaka wa laptops utawajua tuu...hawana hata aibu......X-mass hiyoooo imewasili...utampata nani usawa huu....

    ReplyDelete
  6. acha maneno ya dharau wewe, kama wewe upo ktk core i7 kimpango wako!

    ReplyDelete
  7. hahahahahaa...wabongo ni nomaa!!!

    ReplyDelete
  8. Mimi nakataka ila nini 200,000/= na email yangu ni lyimo2@yahoo.com
    kama utaafiki niambie tufanye kabiashara bana. acha wanaobeza wanao.

    ReplyDelete
  9. hamna cha dharau ni hali halisi,55oooo nyingi mno kwa laptop hiyo,laki moja nitamsaidia,sasa 1gb ram inasukuma nn tena na sijui space itakuwa ngap?

    ReplyDelete
  10. nyie waosha vinywa kwani lazima mtoe maoni ? wabongo bwana kazi kuharibia wenzenu biashara zao , roho mbaya tu zimewasakama ....khaaaa

    ReplyDelete
  11. mdau wa Tue Dec 07, 12:29:00 AM wewe ni bichwa maji na wakuja big time. core i7 ndio umeona nini? hujui hata latest version iliyopo, pia kwa taarifa yako inapokua kwenye kompyuta na laptop jambo muhimu la kuangalia ni kwa matumizi gani unataka kuitumia.

    ReplyDelete
  12. ushamba mzigo wa kuni! mtu katangaza biashara yake watu mnaanza kuchonga we kama hutaki si unyamaze kimya. Wabongo bwana hovyo kwelikweli!

    ReplyDelete
  13. Kaka bei haijakaa sawa, cerelon hata kwa matumizi ya kuchapa barua tu inasumbua, inaganda kwenye kusave. afu cerelon yenyewe used duh. anyway,sijui umeuawa kiasi gani, ila kama sio saaaana , mpe tu mdogo wako aitumie, hapa utalaliwa tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...