

kwenye Globu ya Jamii. Tunajua zitawafikia wahusika.
Yaani ni aibu kubwa wakazi wa Sinza “ A”, tumeachiwa matakata nyumbani kwetu kwa zaidi ya mwezi mmoja na siku kadhaa sasa. Juzi tu kabla ya krismas wakusanyaji ushuru wa matakata walipita lakini wananchi wamechukia sana sijui kama kuna hata mmoja alijitokeza kulipa.
Mapanya yaliyokufa mawiki kadhaa yaliyopita harufu zilizoko ndani majumbani kwetu inatisha. Krismas tumebakia na mitakataka ndani. Wengine wamezidiwa ndani ya magetini yao na wameweka nje ya geti zao na ni uchafu wa kutisha.
Hii picha imechukuliwa mtaa mmoja tu maeneo ya karibu na blue-bird guest house kuelekea karibu na hospitali ya kwa babu ukitokea Maeda Bara. Ninasema harufu ni ya kutisha na tumekaa nayo karibu kwa mwezi mmoja na siku kadhaa. Alikuwepo mkandarasi mzuri sana ktk siku za hivi karibu aliyekuwa anaitwa KIMANGELE. Lakini sijui nini kilitokea akaletwa mtu ambaye waliona atafanya hiyo kazi, matokeo yake ni hali hii tuliyonayo sasa.
Hivi kweli tunakwenda au tunaelekea wapi? Inamaaana suala kama hili lazima liende Ikulu ndiyo lipatiwe ufumbuzi? Watu wamechukia sana. Wanauliza uongozi uko wapi? Mwenyekiti wa serikali za mtaa hapatikani kabisa maana ameshapigiwa makelele ya kutosha na nadhani kwa usalama wake amezima simu. Sijui kama kweli anapatiwa msaada mara baada ya kuwasilisha maombi au matatizo yetu. Kama tumeshindwa kuzoa hata takataka zetu tu hivi tunakoelekea ni wapi?
Moshi, Arusha na Mwanza wanafanyaje miji yao inakuwa mizuri. Tunaomba taarifa hizi ziwafikie wahusika, na tunaomba ofisi husika ziitishe mkutano na mara nyingi tunakutana pale Meeda Bar na mara hii tunaomba ulinzi wa kutosha maana wananchi wamechukia mno. Huku ni kunyanyasana kabisa. Tunaadhibiwa kwa makusudi.
Nani ambaye hajui takataka zikinyeshewa na mvua zinanuka na kutoka wadudu? Inabidi tuchemshe maji ya moto, kumwaka ili wadudu wanaotoka kwenye matakata wasiingine ndani. Mainzi ni kila kona inabidi upigie Dawa ya MBU kama Xpel au Rungu kila siku ili kuuwa wadudu. Ukisema utoe matakataka getini geti lako litapandwa kwa harufu na watu watakuona wewe ni mchafu wa kupindukia.
Wengine wamefanya hivyo baada ya matakataka kujaa getini. Hivi tunakwenda wapi na hii Sinza yetu? Hivi lazima agizo litoke kwa Waziri Mkuu ili uchafu uzolewe? Ukitaka kujua ukweli mtu yeyote kutoka serikali anayetutakia maisha mazuri, tusipate kipindupindu aje na apite katika nyumba chache tu na ajue jinsi watu walivyoumizwa na hizi takataka. Hata mtu ukiwa msafi namna gani mainzi lazima yawe sehemu ya maisha ya kila siku kwa mlundikano huu wa takataka.
Tunaomba wahusika wafuatilie hili suala la sivyo Sinza italipuka kwa kipindupindu. Hizi picha nimechukua mtaa mmoja tu yaani ni karibu nyumba kama 8 hivi. Inatisha kwa wakazi wa Sinza A. Sijui sinza B, nk. Tunaomba tusaidiwe. Na pia tunaomba kufanyike mkutano mwingine na uongozi wa mkoa ikiwezekana.
hili nikweli , mimi ninakaa karibu na hosteli ya chuo , kulikuwa na kijana anakuja kuchukuwa taka kwa mkokoteni wiki mara 3 kwamakubaliano ya malipo ya mwezi , ifanay kazi hiyo miezi 6 vizuri , nilimsikia akisema kuna kampuni itafanay kazi hii , viongozi wa serikali wanamwambia aondoke ,sasa hatumuoni na taka zipo kibao
ReplyDeletemdau tunashea mtaa na kero juu, nasikia kimangele walitolewa kwa sababu ya fitna tu, wapo walioona wanafaidi sana na wakaamua kuleta watu wao na hatimaye hali ndio iko hivi. hilo moja lingine hao wazoa taka wana kauli chafu na si wastaarabu hasa unapowaambia kuwa kimangele walikuwa wakirudisha mifuko ya takataka wao wanchukua jumlajumla unakuta gunia lako bado zuri kabisa wanalibeba wanaondoka nalo.
ReplyDeletetumechoka na sijui viongozi wanaishi itaa gani wasiione hii kero, mtaa unanuka mtaa umeoza.
ufisadi wa wazi wazi magari ya kuzoa taka wilaya ya kinondoni wakati yanatolea viongozi wa kata ya sinza walikuwepo wanacheka cheka tu huku mtaa umeoza kupitiliza.
nchi hii....sijui tu!
hahha si mmechagua wenyewe mbunge wa chadema na madiani.na badoo
ReplyDeletesinza kwa wajanjaaa!!!!!
ReplyDeleteIlitakiwa muwakamate hao watoza ushuru na kuwakalisha juu ya hiyo mifuko ya takataka!Au muwabebesha kabisa ili wapate kupeleka ujumbe kwa wakubwa wao!
ReplyDeleteTHE LITARS IS DIRTY THE COMPOUND OF BUNGE OF TANZANIA AND MANISPAA OF KINONDONI AND THE MEYA NEEDS TO SEE DEVELOPMENT TO COLLEKTI THE LITERS TO MAKES DAR ES SALAAM CLEAN. THE MAYOR IS JOHN MYINGA OF GRADUTES OF MUZUMBE UNIVESITY OF COLLEGE OF MULOGOLO OF STUDIES THE ECONOMY CRISIS OF THE USA AND THE WIKILIKS TO STOPING THE CORRUPTION OF TAKUKURU. AND I SEE ALL CLEVER PEOPLES OF TANZANIA SAY N TO RICHMOND AND TANZANIA WILL HAVES ECONOMY AND ELESTRIKITY FOR YEARS AND NO DARK IN TANZANIA
ReplyDeleteMi mwenyewe naishi sinza A karibu na Nice pub, ila mtoza ushuru alikuja kuchua mawe yake nilimtoa nduki, lori linakuja mara moja baada ya miezi mitatu. Kimangele wameshindwa na kazi, ila pia kuna watu ambao hawatoi ushuru hapo mwanzoni ndio ilifanya hao jamaa kufulia, watu wana hela ya beer lakini kutoa buku 3tu kwa mwezi hawatoi. Wanatuma wafanyakazi waambie kuwa mwenye nyumba hayupo. We all to blame coz most of people dont pay so the company runs on loss.
ReplyDeletePoleni wana sinza, hii ndio raha ya kukaa mjini wenzenu shamba tuna mashimo ya kutupa taka.
ReplyDeleteAti vile wamechagua mbunge wa chadema kwani hao wa ccm ndo wachapa kazi mbona wapo tangu mwaka 47 na kero ndo zimezidi?? acha unafiki na aishu ya umeme ni chadema pia? nyangema wengine bwana 0 kabisa!!
ReplyDeletemimi ni mkazi wa kkoo gerezani , hata sisi kulikuwa mkandarasi mzuri tu anayezoa taka kila siku na wakati lakini hatimae juzi juzi tu kabla sikuu tukaona gari halipiti siku tatu mfululizo taka zikaanza kujaa , ikabidi tumtafute mwenye mkokoteni akazitupe akatuchaji 5000/= tukampa , sasa tukauliza vp kuhusu magari ya taka ? tukaambiwa kuwa HALMASHAURI YA ILALA inadaiwa pesa nyingi na huyo mkandalasi na pia halamashauri imemsimisha huyo mkandarasi na kuamua kuzoa taka yenyewe , sasa imeshakuwa tabu , hili gari la almashauri linapita kwa wiki mara moja , tena likipa linapita kimyaaaa hata honi halipigi kujulisha wakazi walioko majumbani kuwa gari ya taka inapita , tofauti na yule wa mwanzo alikuwa akifanya kazi yake sawa kabisa ... hii nchi ni RUSHWA imekithiri , sidhani kama JK ataweza kuitoa , hata marais 10 wajao itakuwa bado tuuu...ndo maana waotoka nje ya tanzania huwa hawataki kurudi ...
ReplyDeleteTUNAISHI KWA TABU , TUNAPATA PESA KWA TABU,TUNAZITUMIA KWA TABU ,MPAKA KUFA KWETU KWA TABU..jamani eeh
mdau KKOO
HILO TATIZO SIO SINZA TU, HATA HUKU KWETU KINONDONI MKWAJUNI. TAKA ZINAKAA MIEZI MITATU HADI SINATOA FUNZA. HAO WAZOA TAKA WANAJUA TU KUJA KUDAI HELA LAKINI HAWAJI KUCHUKUA TAKA. HUU NI UFISADI ULIOKITHIRI COZ WANALIPWA HELA KILA MWEZI KALINI HAWATOI HUDUMA. HAO WAJUMBE WA SERIKALI ZA MITAA NADHANI NAO WANAPEWA HONGO COZ HAWAENDI KUWAFUATILIA HATA WASIPOTOKEA MIEZI SITA WAO WAMEKAA KIMYA TU.
ReplyDeleteHALAFU KAKA MICHU TUNAOMBA SIKUMOJA UTUTEMBELEE HUKU KINONDONI MKWAJUNI MTAA WA MAPHERE ILI UTUFIKISHIE KERO ZETU KWA WAHUSIKA WA NGAZI ZA JUU COZ SISI TUMERIPOTI KWA MADIWANI MPAKA TUMECHOKA. MTAA HUU NI MCHAFU SANA, BARABARA INA MASHIMO MAKUBWA UTADHANI HANDAKI. GARI NDOGO ZINAPITA KWA SHIDA SANA. YANI KAMA UNA GARI NDOGO UKAFULULIZA KUPITA KWA WIKI MOJA BASI HILO GARI LITAKUA HALIFAI TENA, MVUA IKINYESHA NI KINYAA TUPU, MAJI YANATUWAMA KAMA MABWAWA. TUSAIDIE PLS KUFIKISHA HABARI HIZI KWA WAHUSIKA. TUMECHOKA JAMANI NA HUU UFISADI.
hivi hawa wakandarasi wa kuzoa taka kwanini majina ya makampuni yao yanakuwa ya ajabu ajabu mara KIMANGELE mara BUDEGE .. hamna majina mazuri ? au kwa vile mnazoa taka ?
ReplyDeleteSWALA SII KUZOATA, AU KUKU SANYA TAKA SAWLA WA ULIZE AW WAIGE MFANO WA MANISPAA YA MOSHI KILIMANJRAO KWA USAFI.
ReplyDelete1. WANANCHI AU RAIA YA MOSHI NI WAUSAFI WAMEKULIA KUTUNZA MAZINGIRA KUTO KUTUPA TAKA OVYO
2. WANANCHI WA DAR WANA TAKIWA KUWA NA VIKAO VYA MITAA KUJADILI KERO ZA MITAA YAO IKIWEMO TAKA SO WANA WEZA KU JIWEKEA UTARATIBU WA KUKU SANYA TAKA NA KUZIIFAZI MAHALA PAMOJA KULINGANA NA UKARIBU WA MITAA.
3. SWALA LA USAFI HALIITAJI U CCM AU UCHADEMA USAFI NI MTU MWENYEWE, MBONA MOSHI YA ONGOZWA NA CHADEMA NA NI SAFII?
MFANO UPO FEW YARDS AWAY... RWANDA RWANDA RWANDA RWANDA RWANDA, TUFWATE MFANO WENZETU WASAFI SANA, MJI WAO NI VERY CLEAN, LAKINI WATANZANIA!! WACHAFU SANA, SAA NYINGINE UNALIONA KABISA JITU ZIMA LINAKULA KITU LINATUPA HAPO, SASA HAPO HATA HUYO MDOGO ATAFWATA MFANO GANI HAPO? HATA NDANI YA NYUMBA ZETU, RANGI YA ELFU 5 TU KAZI!! KUTA CHAAAAFU KAMA NINI SIJUI! WHY JAMANI!? NAFIKIRI FIRST LADY ANGEVALIA NGUJA MASWALA KAMA HAYA, HATA VIPINDI VINGI VINGEKUWA VINAONYESHA DECORATIONS, USAFI, GARDENING N.K, MABADILIKO YANALETWA NA WENYEWE, ILA SERIKALI PIA IPLAY PART YAKE HAPO, KWA KUKEMEA WALE WOTE WACHAFU, NA KUPELEKA HUDUMA HARAKA, MFANO MWINGINE KAGONGWA MBWA MORROCO PALE, MPAKA MBWA ANAOZA HAPO, NA HARUFU TELE!! HAKUNA MTU ANAYEJIGUSA!! WALAHI TUMEOZA WATANZANIA.
ReplyDeleteKuna taarifa kuwa uongozi wa mtaa ulichukua 50% kama commission sasa mkondarasi anataka nao wafanye kazi ya kuwalinda ili mambo yakae sawa. Kwa hiyo ndugu zangu wa sinza hiyo ndio hali halisi, serikali yaani uongozi unashindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya mkondarasi wa kuzoa taka kwa sababu serikali ilichukua percent kubwa ambayo mkondarasi anaona kama amejenga ushirika au ubia na serikali. Nakwambia hata pafanywe vipi, uongozi pale hauna meno ya kumkaba mkondarasi
ReplyDeleteWe anony Mon Dec 27, 01:46:00 AM unapaswa kuelewa kuwa mikataba yote ya kifisadi ya kukusanya taka na 'usafi' Sinza waliingia viongozi wa serikali za mitaa wa CCM. Hii ni moja ya sababu ya kupigwa chini aliyekuwa diwani wa eneo hilo.
ReplyDeleteTuombe msaada kutoka nje , waje wataalamu kutuonyesha jinsi ya kuzoa taka. Sijui, serikali ya Marekani inaweza kutusaidia kununua malory kadhaa katika manispaa zote tatu? Yaani tutasaidiwa mpaka lini sijui. Tunaomba wafanyakazi wote wa Moshi na Arusha na Mwanza waamie Dar ili kuweka jiji liwe safi.
ReplyDeleteCHADEMA, HEBU JARIBU KUFUATILIA HILI. NAOMBA VIONGOZI WA SIASA WAFANYE PRESS CONFERENCE ILI KUTUAMBIA KILICHOJIRI. TUFANYE NINI. TUNAOMBA SINZA NZIMA TUWEKE MGOMO TUTOE TAKA NJE WOTE NA TUITE BBC WAFANYE COVERAGE. HAIWEZEKANI TUISHI KTK HALI KAMA HII. KWELI KAMA WATU WANATUTESA KIASI HIKI KWA MANUFAA YAO MWENYEZI MUNGU ATAWAONA. KWANI TUSHINDWE KULALA KWA KUACHIWA TAKATAKA NAMNA HII?LEO NIMEKUTA TAKATAK ZIMEONGEZEKA, MVUA YA ASUBUHI IMELETA MAOZO YA AJABU SANA. MAISHA YA WATOTO YAKO HATARINI. KUNA MTU MMOJA AMEAMUA KUHAMA LEO KWENDA KWEN APARTMENTS. SASA KAMA HUNA PESA YA KULIPIA HIZO APARTMENTS TUFANYEJE? KWELI WANAOISHI SHAMBA WANAFAIDI. MAANA MASHIMO YAKO YA KUMWAGA.
TUITISHE MGOMO WA UCHAFU DAR ES SALAAM NZIMA. HIVI VYOMBA VYA HABARI VIKO WAPI ZAIDI YA HII BLOG YA MICHUZI? AU MAZINGIRA HAYA HAYAWAHUSU? TBC KIMYA, ITV KIMYA, CHANNEL TEN KIMYA, HIVI MNATAFUTA HABARI GANI? HUU UCHAFU IS NOTHING TO YOU? PLEASE SAVE US FROM THIS TERRIBLE SITUATION. WE PRAY SOMEONE WILL LOOK AT THIS, AND MAY BE THE GOVERNMENT OFFICIALS WILL INTERVEN BEFORE THE PM
ReplyDeleteNi nani anaefanya kazi Dar? jieleze ni kazi gani unafanya, kama siyo kuangalia jinsi ya kuiba na rushwa, jioni ukanywe pombe. Usikimbilie kulaumu wakati wewe mwenyewe hujui unachokifanya. Kama ulivyo mzembe kazini kwako na hao wabeba taka ni mfano mzuri sana. Manjuwa kulalamika tu lakin hamju jinsi ya kutafuta chanzo cha matatizo. Nendeni Moshi< Arusha na Mwanza mkajifunze huko jinsi ya kusafisha mazingira yenu. La sivyo mtaendelea kuishi kwenye uchafu tu. Na mkomo kulala mika chukuwa hatuwa nendeni kwa wakuu wenu muwaulize maswali. Sasa badala ya kukimbilia kuakamata moja baridi na nyama choma.
ReplyDeleteMfano upo karibu tembelea Keko Mwanga ni kusafi sana. Yani nyie na kuiba kote huko sinza manshidwa kujuwa uchafu wenu muufanyie mbinu gani hii ni aibu sana.
ReplyDeleteSasa hapo ndio tutajua kama kweli Sinza ni kwa wajanja au kwa wajinga, yaani na ujanja na usomi wenu wote mlionao bado mnashindwa kutatua tatizo la takataka????!!! Eti mnaisubiri serikali???? Kweli Sinza kwa wajanja!!
ReplyDeleteLabda tunashambuliana wenyewe katika hili. ukweli ni kwamba sisi ni wakaaji, tumepanga. Tatizo hili halikuwepo kwa miaka zaidi ya 4 iliyopita, kila wiki mkandarasi aliyekuwepo wakati huo jina KIMANGELE alikuwa anazoa taka kwa wiki mara mbili. Uongozi mpya ulipoingia, sijui waliona anafaidika sana, wakamtoa wakamleta wa kwao. Kwanza walisema kuwa bei imepanda na takataka zitazolewa kwa mikokoteni ili kuwapa ajira vijana. Mara wakasema tutakuwa na mkandaras mpya, na tuliona magari mapya ya kuzoa taka karibu 10 tukasema tatizo limekwisha. Lakini kumbe sivyo , tumeachiwa matakataka hakuna mfano. Sasa kama mkaaji, tufanyeje? Leo tumeambiwa DOWANS lazima walipwe Tshs. 186billion, wewe kama mtanzania utafanya nini zaidi ya kuisubiri serikali? Kuna mambo ambayo huwezi ukayatatua hata kama ungekuwa na Phd. Tunakaa na na Prof. huku lakini prof anacheo gani zaidi ya katibu wa kata ambaye ni mwanasiasa? Wewe hujui kuwa siasa ndiyo kubwa kuliko chochote kile? Nadhani, watoto wetu lazima wajue Siasa kwanza, halafu mambo ya uchumi baadaye maana siasa inalipa hata ukiwa hujasoma. Ujanja ni kwa wanasiasa sio kwa wana-Sinza.
ReplyDeleteHONGERA MICHUZIIII, NAWE WAKAA SINZA KWA WAJANJA???
ReplyDeleteWatanzania wenzangu, nawaomba tubadilike katika namna yetu ya kufikiri, hasa tunapotafuta suluhisho mbalimbali za matatizo ya kawaida ya kila siku. Tusihame kwenye hoja kwa ajili ya kujifurahisha tu, ETI tatizo la takataka za Sinza linafanana na tatizo la Dowans!!!???, HAPANA. Wewe ndiye unayezalisha takataka kila siku!, haijalishi kama wewe ni mpangaji au mwenye nyumba, lakini cha ajabu hutaki kuwajibika kwa takataka unazozizalisha, ila unamsubiri Serikali aje kusaidia!!!??? Nani amekudanganya kwamba huyo anayeitwa 'Serikali' anakerwa na harufu za takataka (Ulizozizalisha wewe) mtaani kwako!!!???. Unataka uambiweje hadi uelewe kwamba huyo anayeitwa 'Serikali' keshajichokea, amelala na akiamka anaendelea na hamsini zake, we endelea kumsubiri tu! Kwakuwa ni wewe unayezalisha takataka wajibika katika kuziondoa, usimsubiri huyo anayeitwa 'Serikali'
ReplyDelete...Kinondoni uchafu(sic)usafi basi!
ReplyDeleteAah, kuna watu wengine wanajua mada inaongelea nini haswa na wengine hawajui so wanaishia kulaumu tu.
ReplyDeleteMimi pia ni mkazi wa Sinza A na ninakerwa sana na hao wazoa taka, kazi yao ni kuja kudai hela ya taka tu. Mi mwezi huu nimewatoa baru as watu wamefanya nje ya geti langu sehemu ya kumwaga taka zao. Usiku usiku wanatoa taka na kila asubuhi taka nakuta zimeongezeka. Uongozi uliopita ulikomesha hili maana uliwaelimisha watu kutoweka taka nje na gari lilipokuwa linapita lilikuwa linapiga honi so watu wanatoa taka zao ila uongozi mpya ni UOZO mtupu, gari halijapita zaidi ya wiki sita sasa, watu wamekaa na taka ndani kwao wameshindwa so wanaweka barabarani na kwa vile hawajazoa taka muda mrefu sana imani kwa hao watu imeisha kabisa.
Mi sitaki kabisa kuona mtu ananigongea kudai hela za taka hadi nitakapopata mkataba wa kueleweka kwenye uzoaji wa taka. Mimi sio mjinga na hela yangu naipata kwa jasho langu, siwezi nikatupa hela kwa watu wasiotekeleza majukumu yao.