Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Power Pool East Africa, Machwa Kagoswe akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu juu ya eneo la kuzalishia umeme wa upepo mkoani Singida . Serikali imeingia Ubia kupitia Shiriaka la Maendeleo la Taifa (NDC) na kampuni binafsi ya Power Pool East Aftrica ili kuzalisha umeme huo kuanzia mwakani.

Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) limeingia ubia na kampuni ya Power Pool East Africa wa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida utakaogharimu takribani ya Sh Bilioni 180.

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu alisema tayari makubaliano yamesainiwa na shirika la NDC kwa niaba ya serikali itakuwa ikimiliki asilimia 51 za hisa na nyingine zitakuwa za mwekezaji binafsi.

Nyalandu alisema kwa mradi huo ambao utakuwa wa gharama nafuu katika uzalishaji utaingizwa katika gridi ya taifa na kwa kuanzia zitazalishwa megawati 50 na baadae zitaongezwa kulingana na uwezo wa wabia hao.

“Tokea kuanza kufungwa kwa mitambo itachukua takribani miezi 15 ili umeme uingie katika gridi na hii itakuwa ufumbuzi wa matatizo ya umeme kwa sasa” alisema Nyalandu.

Mkurugenzi wa Viwanda vikubwa wa NDC, Alley Mwakibolwa alieleza kuwa kwa ujenzi wa mitambo hiyo ya kutumia upepo kutasaidia kuzalisha umeme ampema kwani mitambo ya aina hiyo huchukua muda mfupi kuwekwa ikilinganishwa na ya maji ama ya gesi.

Tutajitahidi mradi huu uende kwa kasi kubwa kwani kwa kuanzia tutazalisha megawati 50 na baadae tutaongeza 50 ili kuoingia katika gridi ya taifa" alisema.

Aidha katikaeneo hilo ambalo liko ukingoni kwa bonde la ufa, upepo ni mkakli kiasi cha kufanya miti karibu yote kulalia upande mmoja na upeo huende kwa kasi ya hadi mita 21 kwa sekunde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tanzania, nchi yetu,hatma yetu ipo mikononi mwa wanasia wasiojali mateso ya wananchi. Nyalandu nakupongeza kwa juhudi zako, nakuonea huruma kwa kuwa najua bado u mgeni katika mambo ya serikali ndio maana wewe upo busy wakati wenzako wanakula kuku. Hivi ndivyo serikali yetu ilivyo, watu hawataki kuwajibika wala hawana shaka, mambo ni kwa mazoea tu. Hili ndo tatizo la kupewa kazi ki shemeji. Sisi Raia tunaona na mwisho wa siku tutasema kwa njia ya kura, nani anafaa na nani ni box

    ReplyDelete
  2. eeh wanatuletea richmond nyingine na dowans halafu waanze kusema hawakutendewa haki
    teheteh

    ReplyDelete
  3. Well done Nyalandu. Singida people need you. Remember too deforestation is a big problem in Singida. If the government can come with cheap subsidized cooking stoves instead of charcoal ones, the forest of Singida will be saved. Let say if for every power installation in a household also includes a cooking stove, a lot of trees will be saved as well as invironment. Other things I am wondering what are the strategies to remove TEMBE huts in Singida?

    ReplyDelete
  4. Hope huo ndio mwanzo mpya wa mafanikio,tunatumaini chanzo hicho kitasaidia kustabiliz bei ya umeme na kumaliza kabisa ama kupunguza kwa kiwango kikubwa cha mgawo wa umeme.Serikali basi iongeze mwendo ili kufanikisha hilo mapema.GOOD WORK NYARANDU.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...