
Kama mnavyoweza kuona, Globu yenu imekuja na kuonekano mpya ambao pamoja na mambo mengine imetatua tatizo la kiufundi lililokuwepo kwa muda kiasi la kupata post za nyuma. Vinginevyo globu ni ile ile na sasa una uwezo wa kupata kila kitu ambacho utakuwa umechelewa kukiona katika wakati muafaka. Libeneke oye!
Mabadiliko haya yamekuja sio tu kwa kusikiliza amri zenu wadau kwamba huwa wanakosa uhondo wa siku za nyuma, bali pia ni kwenda na wakati. Hivyo ukiangalia vyema utakuta pia kuna links za youtube, facebook na twitter kwa ajili ya kuongeza ufanisi.
Pia tumerahisisha uwanda wa kutoa maoni (yasiyochafua hali ya hewa hahaaaaa) ambapo sasa ukishabofya neno 'maoni' utapata sehemu ya kumwaga yaliyo moyoni bila shida. Hivyo wadau kazi kwenu. Angalizo hapa ni kwamba maoni yanayotiwa kapuni ni yale yenye lengo la kujeruhi hisia za mtu/watu na sio kwa makusudi ya kuminya maoni kwa maana ya kuminya. Kuna maoni yanakuja ambayo ni kweli hayachafui hali ya hewa lakini si uwongo kwamba lengo lake ni kujeruhi hisia za mtu/watu. Tunaomba wadau mliangalie hili kwa macho na masikio mawili. Vinginevyo kuwa huru kutoa maoni kwa uhuru kama inavyojieleza...ukizingatia sera ya Globu ya Jamii ya kizuri kwa bata mzinga, kibaya kwa kuku (what's good for the goose is bad for the hen) yaani si rahisi kumridhisha kila mdau kwa kila kitu. Hivyo nawasihi wadau na tuvumiliane kwenye shida na raha.
Aidha, maoni na mawazo ya namna ya kuiboresha zaidi Globu ya Jamii yanakaribishwa. Vile vile tunaomba tutoe shukrani sana kwa wadau kwa kuendelea kuwa na imani nasi katika kuendeleza libeneke. Vile vile tunaishukuru kampuni ya MKCT kwa kuendelea kutoa huduma bora kila siku.
Usisahau kubofya juu ya
tangazo kwenda kwenye mtandao husika!
-Michuzi
Hongera kaka Michuzi.
ReplyDeleteSaleh.
SJ Post - http://sjpost.posterous.com
Ankal hapa umepiga bao. Yaani sioni blog itayoweza kukufikia. Hakika umetoa suluhisho la wadau la muda mrefu, hasa wale waliokuwa wanalilia kupata posts za nyuma (zilizopita). ama kweli sasa Globu ya Jamii imekamilika. Na hao MKCT wanatisha kwa kweli. Hivi wao Bongo ama majuu hawa???? nawatafuta kweli niwape hongera zangu. yaaaaani, we acha tu. Globu ya jamii na libeneke Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!
ReplyDeletekazi nzuri misupu ila umesahau kurejesha saa,chonde chonde turudishie majira.
ReplyDeletealafu mdau naomba kama ikiwezekana idara ya maoni ifunguke kwenye page nyingine kama ilivyo kuwa hapo awali ili niendelee kula vituzzz kwa ufasaha kwenye main page.
once again kazi nzuri misupu
Libeneke Oyeeeee!!!!
Facebook mwisho wake ni tar.15 March 2011. Mmiliki wake amekiri kushindwa kuendesha mtandao wake kwa madai kuwa inamgharimu muda wake mwingi.
ReplyDeleteNilikuwa sijui pa kuweka dukuduku langu kwenye blog hii. Yaani mlivyorahisisha sasa mtanikoma. Ila ankal punguza kubania maoni bana. Najua wewe ni Tanzania's top blogger ila kwenye maoni inakua si mswano. Wengine sie hatulali bila kumtukana mtu. si unajua hasira ya maboxi (hahahhaa joking). Lakini pihga ua Globu (ama blog?) ya jamii oyeeeeee. kama alivyosema mdau hapo juu, wewe ankal ni nambari wani (sio ccm lakini, mie chadema!) kilichobaki sasa ni kazi kwetu wadau. Halafu huna hiyana. Blogu (globu?) zingine zikija wala hubanii. Unapenda kweli hii social media business ikue kwa wabongo. Hongera and God Bless u kwa kutokuwa mchoyo!
ReplyDeleteNimependa muonekano mpya. Hongera jopo lililoweza kufanikisha hili. Tunahitaji vitu kama hivi muda ukiwa unapita. Safi.
ReplyDeleteduh hii nimeipenda wangu, so organised.
ReplyDeletemdau
Michuzi jaribu kuitengeneza iweze kufunguka kwenye mobile phones pia bila shida..
ReplyDeleteUmezidi kubana maoni hasa yasioendana na unavyotaka wewe!
ReplyDeleteMdau hapo juu,
ReplyDeleteSoma angalizo kwa ufasaha. maoni yanayojeruhi mtu/watu hayawezi kuona mwanga wa jua. Hii ni Globu ya Jamii ambayo kila mtu anatakiwa afungue akijua hakuna kujeruhiana. Na si kufungua tu bali pia hata kutuma picha na maoni bila kuogopa kuchafuliwa hali ya hewa. Kwa hilo inabidi unisamhehe. kama ulivyo wewe, hata mie sipendi hali yangu ya hewa ichafuliwe. Kuna raha gani kumtoa mwenzio nishai??? Aidha kama unataka kummanga mtu/watu weka jina lako halisi na anuani. Hiyo tutairusha. hamna noma. Lakini ukijificha kama anonymous hiyo si sawa!
-Michuzi
(siku hizi nitajibu mapigo mwenyewe!)
Mdau Malkiory!
ReplyDeleteBaada ya kuchunguza nimehisi hizo ni kamba kali. Tafakari!
niaje
ReplyDeletesawa mkuu hapo umecheza cos ni juzi tu nilikutumia msg leo mambo yameenda kama nilivyotarajia yaani kama mr pesident angekua anasikiliza wananchi kama hivi basi hii nchi ingekuambali sana
ReplyDeletebig up michuzi
thanks
mbona hatuwezi kutuma kwa rafiki iwapo unataka utume kwa e mail? asante bro.
ReplyDeleteYaeh but ondoa the secret word. Inachelewesha muda wa watu..Ujue sio kila mtu anatumia g4
ReplyDeleteUncle nimekubali safi sana,libeneke oyeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!
ReplyDeleteKwa sasa hivi libeneke liko juu sana hongera kwa hilo, lilitakiwa liwe namna hii long time kishenzi anyway better late than never ........... mdau wa man uuuuuuuuuuuu
ReplyDeleteHalafu tunaomba sana uturudisie kile kitengo cha nyimbo unabana kama jf ati hadi uwe member haihuu... huko ni kulazimisha watu wale kitu roho haipendi kwa ajili ya kupata kitu fulani, wee tuwekee tujiachie yani naimisi ile miziki ya dini na taarabu acha tu...
ReplyDeleteMichuzi, nakubaliana na uchunguzi wako. Binafsi nilipata kwenye source hiyo uliyobandika karibuni. Sidhani kama ni source reliable sana.
ReplyDeleteBadilisha picha basi na fulanazzz au waungwana wamesema usibadilishe???
ReplyDeleteLibeneke Hoyeeeeeeeeeeeeeee.........Big up Ankali kwa kazi nzuri iliyo fanyika....haya ndio mamboziii ya 2011
ReplyDeleteMimi nashauri kitu kimoja tu haya maandishi ya maoni rangi imefaint sana inaumiza macho tulikua tunaomba irekebishwe....
hongera uncle ilikuwa taabu sana kwa ule muonekano wa zamani kuona older post. Safii sana!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeletekaka Misupu ahsante kwa kazi nzuri, Vp mbona muonekano wa the Fulanazzzzzzzzz upo wkt ulitujulisha kuwa umenunuliwa na mudau huko majuu. Kwnn usiweke ile suti ambayo huwa unatinga uendapo ktk Minuso?
ReplyDeleteHapo nimekukubalia auncle mbele kwa mbele mwaka huu. uko juu
ReplyDeletelibeneke oyeeeeee
ReplyDeleteANKAL MICHUZI AHSANTE KWA SURA MPYA YA LIBENEKE.
ReplyDeleteILA MAANDISHI YA MAONI YAMEFIFIA - YANATUUMIZA MACHO. TUNAOMBA UYAKOLEZE KIDO.. AHSANTE!
Mwonekano huu ni kama wa blog ya haki ngowi http://www.haki-hakingowi.blogspot.com/ kwa miaka sasa mmekua ndo chachu ya habari nchini kama ulivyodokeza kwenye osti zako za nyuma ni kwmaba upo umuhimu kuzindua blog nyingine kama za afya elimu, ufundi na NK.
ReplyDeleteKwa leo nawapa pongezi sanaaa
Michuzi,
ReplyDeleteDesign nzuri. Labda tuu ufikirie kubadilisha rangi ya comments maana ya sasa inafaint hasa kwa wale wa tinted.
Naona watu wote mmeongea ila mlisahau kumpongeza Michuzi kwa hili.
ReplyDeleteSasa hivi kwenye globu hii huwezi kukopi neno lolote.Kuna wale mabloggers juniors ambao kazi yao ni kukopi habari toka blogu moja na kupaste kwenye blogu zao,na sasa hawataweza kukopi toka issamichuzi.blogspot.com
Mimi ni Afisa wa IT,nimeangalia mambo ya kiufundi zaidi.Hongera bwana Issa Michuzi
Ni kweli michuzi rangi ya comment is too dull, can you make it more bold, hatuwezi soma vizuri.otherwise nice work,am loving the new look
ReplyDeleteWezesha ku copy. Sasa text zimekaa kama image, yani huwezi kukopy wala ku highlight.. hivyo inakuwa ngumu kufungua link au ku copy na kupaste kwingine
ReplyDeleteHONGERA ANKAL KWA KUBORESHA BLOG YETU HII YA JAMII,ILA NINASHAURI KUWA
ReplyDeleteUBADILISHE RANGI YA MAANDISHI IWE NYEUSI,MAANA RANGI HII INATUUMIZA MACHO SAAAANA HATA SISI TUNAOTUMIA MEWANI PIA NI SHIDA!!
MDAU,WASHINGTON DC.USA.