Waheshimiwa wadau wa Globu ya Jamii,
Kama mnavyoweza kuona, Globu yenu imekuja na kuonekano mpya ambao pamoja na mambo mengine imetatua tatizo la kiufundi lililokuwepo kwa muda kiasi la kupata post za nyuma. Vinginevyo globu ni ile ile na sasa una uwezo wa kupata kila kitu ambacho utakuwa umechelewa kukiona katika wakati muafaka. Libeneke oye!

Mabadiliko haya yamekuja sio tu kwa kusikiliza amri zenu wadau kwamba huwa wanakosa uhondo wa siku za nyuma, bali pia ni kwenda na wakati. Hivyo ukiangalia vyema utakuta pia kuna links za youtube, facebook na twitter kwa ajili ya kuongeza ufanisi.

Pia tumerahisisha uwanda wa kutoa maoni (yasiyochafua hali ya hewa hahaaaaa) ambapo sasa ukishabofya neno 'maoni' utapata sehemu ya kumwaga yaliyo moyoni bila shida. Hivyo wadau kazi kwenu. Angalizo hapa ni kwamba maoni yanayotiwa kapuni ni yale yenye lengo la kujeruhi hisia za mtu/watu na sio kwa makusudi ya kuminya maoni kwa maana ya kuminya. Kuna maoni yanakuja ambayo ni kweli hayachafui hali ya hewa lakini si uwongo kwamba lengo lake ni kujeruhi hisia za mtu/watu. Tunaomba wadau mliangalie hili kwa macho na masikio mawili. Vinginevyo kuwa huru kutoa maoni kwa uhuru kama inavyojieleza...ukizingatia sera ya Globu ya Jamii ya kizuri kwa bata mzinga, kibaya kwa kuku (what's good for the goose is bad for the hen) yaani si rahisi kumridhisha kila mdau kwa kila kitu. Hivyo nawasihi wadau na tuvumiliane kwenye shida na raha.

Aidha, maoni na mawazo ya namna ya kuiboresha zaidi Globu ya Jamii yanakaribishwa. Vile vile tunaomba tutoe shukrani sana kwa wadau kwa kuendelea kuwa na imani nasi katika kuendeleza libeneke. Vile vile tunaishukuru kampuni ya MKCT kwa kuendelea kutoa huduma bora kila siku.
Usisahau kubofya juu ya
tangazo kwenda kwenye mtandao husika!

-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Hongera kaka Michuzi.
    Saleh.
    SJ Post - http://sjpost.posterous.com

    ReplyDelete
  2. Ankal hapa umepiga bao. Yaani sioni blog itayoweza kukufikia. Hakika umetoa suluhisho la wadau la muda mrefu, hasa wale waliokuwa wanalilia kupata posts za nyuma (zilizopita). ama kweli sasa Globu ya Jamii imekamilika. Na hao MKCT wanatisha kwa kweli. Hivi wao Bongo ama majuu hawa???? nawatafuta kweli niwape hongera zangu. yaaaaani, we acha tu. Globu ya jamii na libeneke Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. kazi nzuri misupu ila umesahau kurejesha saa,chonde chonde turudishie majira.

    alafu mdau naomba kama ikiwezekana idara ya maoni ifunguke kwenye page nyingine kama ilivyo kuwa hapo awali ili niendelee kula vituzzz kwa ufasaha kwenye main page.

    once again kazi nzuri misupu

    Libeneke Oyeeeee!!!!

    ReplyDelete
  4. Facebook mwisho wake ni tar.15 March 2011. Mmiliki wake amekiri kushindwa kuendesha mtandao wake kwa madai kuwa inamgharimu muda wake mwingi.

    ReplyDelete
  5. Nilikuwa sijui pa kuweka dukuduku langu kwenye blog hii. Yaani mlivyorahisisha sasa mtanikoma. Ila ankal punguza kubania maoni bana. Najua wewe ni Tanzania's top blogger ila kwenye maoni inakua si mswano. Wengine sie hatulali bila kumtukana mtu. si unajua hasira ya maboxi (hahahhaa joking). Lakini pihga ua Globu (ama blog?) ya jamii oyeeeeee. kama alivyosema mdau hapo juu, wewe ankal ni nambari wani (sio ccm lakini, mie chadema!) kilichobaki sasa ni kazi kwetu wadau. Halafu huna hiyana. Blogu (globu?) zingine zikija wala hubanii. Unapenda kweli hii social media business ikue kwa wabongo. Hongera and God Bless u kwa kutokuwa mchoyo!

    ReplyDelete
  6. Nimependa muonekano mpya. Hongera jopo lililoweza kufanikisha hili. Tunahitaji vitu kama hivi muda ukiwa unapita. Safi.

    ReplyDelete
  7. duh hii nimeipenda wangu, so organised.
    mdau

    ReplyDelete
  8. Michuzi jaribu kuitengeneza iweze kufunguka kwenye mobile phones pia bila shida..

    ReplyDelete
  9. Umezidi kubana maoni hasa yasioendana na unavyotaka wewe!

    ReplyDelete
  10. Mdau hapo juu,
    Soma angalizo kwa ufasaha. maoni yanayojeruhi mtu/watu hayawezi kuona mwanga wa jua. Hii ni Globu ya Jamii ambayo kila mtu anatakiwa afungue akijua hakuna kujeruhiana. Na si kufungua tu bali pia hata kutuma picha na maoni bila kuogopa kuchafuliwa hali ya hewa. Kwa hilo inabidi unisamhehe. kama ulivyo wewe, hata mie sipendi hali yangu ya hewa ichafuliwe. Kuna raha gani kumtoa mwenzio nishai??? Aidha kama unataka kummanga mtu/watu weka jina lako halisi na anuani. Hiyo tutairusha. hamna noma. Lakini ukijificha kama anonymous hiyo si sawa!

    -Michuzi
    (siku hizi nitajibu mapigo mwenyewe!)

    ReplyDelete
  11. Mdau Malkiory!

    Baada ya kuchunguza nimehisi hizo ni kamba kali. Tafakari!

    ReplyDelete
  12. sawa mkuu hapo umecheza cos ni juzi tu nilikutumia msg leo mambo yameenda kama nilivyotarajia yaani kama mr pesident angekua anasikiliza wananchi kama hivi basi hii nchi ingekuambali sana
    big up michuzi
    thanks

    ReplyDelete
  13. mbona hatuwezi kutuma kwa rafiki iwapo unataka utume kwa e mail? asante bro.

    ReplyDelete
  14. Yaeh but ondoa the secret word. Inachelewesha muda wa watu..Ujue sio kila mtu anatumia g4

    ReplyDelete
  15. Uncle nimekubali safi sana,libeneke oyeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!

    ReplyDelete
  16. Kwa sasa hivi libeneke liko juu sana hongera kwa hilo, lilitakiwa liwe namna hii long time kishenzi anyway better late than never ........... mdau wa man uuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  17. Halafu tunaomba sana uturudisie kile kitengo cha nyimbo unabana kama jf ati hadi uwe member haihuu... huko ni kulazimisha watu wale kitu roho haipendi kwa ajili ya kupata kitu fulani, wee tuwekee tujiachie yani naimisi ile miziki ya dini na taarabu acha tu...

    ReplyDelete
  18. Michuzi, nakubaliana na uchunguzi wako. Binafsi nilipata kwenye source hiyo uliyobandika karibuni. Sidhani kama ni source reliable sana.

    ReplyDelete
  19. Badilisha picha basi na fulanazzz au waungwana wamesema usibadilishe???

    ReplyDelete
  20. Libeneke Hoyeeeeeeeeeeeeeee.........Big up Ankali kwa kazi nzuri iliyo fanyika....haya ndio mamboziii ya 2011

    Mimi nashauri kitu kimoja tu haya maandishi ya maoni rangi imefaint sana inaumiza macho tulikua tunaomba irekebishwe....

    ReplyDelete
  21. hongera uncle ilikuwa taabu sana kwa ule muonekano wa zamani kuona older post. Safii sana!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  22. kaka Misupu ahsante kwa kazi nzuri, Vp mbona muonekano wa the Fulanazzzzzzzzz upo wkt ulitujulisha kuwa umenunuliwa na mudau huko majuu. Kwnn usiweke ile suti ambayo huwa unatinga uendapo ktk Minuso?

    ReplyDelete
  23. Hapo nimekukubalia auncle mbele kwa mbele mwaka huu. uko juu

    ReplyDelete
  24. libeneke oyeeeeee

    ReplyDelete
  25. ANKAL MICHUZI AHSANTE KWA SURA MPYA YA LIBENEKE.

    ILA MAANDISHI YA MAONI YAMEFIFIA - YANATUUMIZA MACHO. TUNAOMBA UYAKOLEZE KIDO.. AHSANTE!

    ReplyDelete
  26. Mwonekano huu ni kama wa blog ya haki ngowi http://www.haki-hakingowi.blogspot.com/ kwa miaka sasa mmekua ndo chachu ya habari nchini kama ulivyodokeza kwenye osti zako za nyuma ni kwmaba upo umuhimu kuzindua blog nyingine kama za afya elimu, ufundi na NK.
    Kwa leo nawapa pongezi sanaaa

    ReplyDelete
  27. Michuzi,

    Design nzuri. Labda tuu ufikirie kubadilisha rangi ya comments maana ya sasa inafaint hasa kwa wale wa tinted.

    ReplyDelete
  28. Naona watu wote mmeongea ila mlisahau kumpongeza Michuzi kwa hili.

    Sasa hivi kwenye globu hii huwezi kukopi neno lolote.Kuna wale mabloggers juniors ambao kazi yao ni kukopi habari toka blogu moja na kupaste kwenye blogu zao,na sasa hawataweza kukopi toka issamichuzi.blogspot.com

    Mimi ni Afisa wa IT,nimeangalia mambo ya kiufundi zaidi.Hongera bwana Issa Michuzi

    ReplyDelete
  29. Ni kweli michuzi rangi ya comment is too dull, can you make it more bold, hatuwezi soma vizuri.otherwise nice work,am loving the new look

    ReplyDelete
  30. Wezesha ku copy. Sasa text zimekaa kama image, yani huwezi kukopy wala ku highlight.. hivyo inakuwa ngumu kufungua link au ku copy na kupaste kwingine

    ReplyDelete
  31. HONGERA ANKAL KWA KUBORESHA BLOG YETU HII YA JAMII,ILA NINASHAURI KUWA
    UBADILISHE RANGI YA MAANDISHI IWE NYEUSI,MAANA RANGI HII INATUUMIZA MACHO SAAAANA HATA SISI TUNAOTUMIA MEWANI PIA NI SHIDA!!
    MDAU,WASHINGTON DC.USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...