Home
Unlabelled
malavi davi ya enzi zetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hii barua imenikumbusha kipindi kile mitaa ya Nyamwezi Kariakoo nilipokuwa nikimuandikia mchumba wangu wa kihindi alafu barua ikafumwa na mama wa niliemuandikia utata huo
ReplyDeleteMuhindi kaja juu anasoma barua kwenye kadamnasi wa watu.Kilizuka kicheko pale aliposoma kwamba Mwanae nampenda hata nikinywa maji namuona yeye
Mdau wa Kajificheni (Bwagamoyo)
haahahah,hiyo mi inanikumbusha morogoro wakati huo nipo darasa la nne,nimemuandikia binti halafu barua unaiweka nyuma ya jalada la daftari! Kisha nampa namwambia humo kuna mzigo wako. Hiyo ilikuwa njia muafaka ya kuwasiliana na sijawahi fumwa.Na uzuri wake demu hakuchomoa
ReplyDeletemdau aliyeleta barua hiyo kama ni 1994 mbona ilikuwa afadhali ..enzi hizo tayari kulikuwa na kamwanga kidogo MOBITEL.,TRITEL..kuna CTN,DTV na ITV ndio inaanza anza...
ReplyDeletemaneno miaka ya 80 kushuka chini.....watoto enzi hizo walitumika sana kama mesenja wa barua,...neno solemba lilianzia huko mtu unasubirishwa chini ya mwembe hadi unalala...,au unamsubiri msichana unayempenda kwenye jalala lao usiku kwa mahesabu kuwa wakishakula dona lao la yanga yeye ndie huenda kumwaga ukoko...unabug step ukoko anamwaga mama na kuishia kumwagiwa ukoko na unavumilia..tumetoka mbali..wajameni....sio siku hizi shaa sms au unapiga tu..miadi inafanikiwa....fikirieni maisha bila technology nadhani vijana wabichi wa leo hawataweza!!!
mdau..
octavian mshiu
You will never find a true love than this LOL
ReplyDeleteMAPENZI BWANA, SASA KASEMA HALALI HALAFU TENA ANASEMA ANAWEZA KULALA, KIPI NI CHA UKWELI SASA?...........!
ReplyDeleteSiku hizi fedha yako tu!
ReplyDeleteHii barua mi inanikumbusha mbali maana niliwahi kumwandikia dada mmoja tukiwa darasa la 4,huyo dada akaidondosha basi kuna mwanafunzi sijui nimuite mnoko,mpenda sifa au mwenye nia nzuri akaipeleka kwa Mwalimu tena Mkuu. Basi ikawa ni kesi nzito wakaitwa wazazi wa pande zote mbili, basi iliposomwa hiyo phrase ya 'usiku silali nakuwaza', baba yangu(RIP)alikuja juu kuwa mimi ni muongo nalala tena nalala fofofo maana kila siku yeye(baba)ndio huniamsha ili nijiandae kwenda shule.
ReplyDeleteKwa huo uongo wangu nikaongeza bakora za kuchapwa toka 6 za mwalimu na mzazi wangu akaambiwa anichape 3, na mpenzi wangu naye akapewa adhabu maana hiyo barua ilidondoka kwanini hakutoa taarifa.
Sasa hapo ndio ukawa mwanzo mzuri wa sisi kuwa wapenzi wakati tunakeleza adhabu ya kumwagilia bustani za maua kwa wiki moja.
Nimekumbuka mbali sanaaaaaaaaaaa!!!
Mie nimesoma Nganza miaka ya sabini basi sie waalimu walikuwa wanasoma hizo barua halafu unaitwa mbele ya waalimu wengine na kutukanwa kama mbwa. Ikabidi wanafunzi wadanganye majina kwa vijana wa Nsumba au Nyegezi Seminary au TTC. Nakumbuka mmoja alijiita nyegekiunoutamu basi waalimu wacha wahangaike wakaitisha mkutano wa wawanafunzi nakuuliza Nyegekiuno utamu ni nani? Kimya! Nyegekiuno ni nani ? Kimya.Waliosoma Nganza kumbukeni maisha yalivyokuwa. Siku hizi wapenzi huandikiana kwenye kitabu cha sura bila noma hadi wazazi wao wanaona. Tumetoka mbali jamani.
ReplyDeleteHahahaa asante ankali misupu kwa hii kitu, kwa kweli umetukuna wengi. Mie bwana stori yangu haikuwa kwa barua. ilikuwa wakati niliposhika pua mbele ya msichana wa kihindi tukiwa la tatu shule ya aga khan mtwara (siku hizi Shangani pr. school), basi we! Acha. mwalimu wetu Mr Karim alinitoa nduki nikaite wazazi. walipokuja akawaambia nimefanya mchezo mbaya na mwanafunzi mwenzangu. dingi kwanza alijua nimemnanihii kwa nguvu. alipoambiwa nimemshikia pua na kwa kihindi ati hiyo ni tusi, ikawa balaa. uzuri aga khan enzi hizo hakukuwa na bakora maana ukiacha kwamba wanafunzi wengi walikuwa wa kihindi, waswahili tulikuwa kama wanne hivi shule nzima. na kupata shule hapo ilibidi baba awe mtu katika jamii. dingi alikuwa bosi fulani serikalini. hivyo nikapewa adhabu ya kuandika 'i am sorry' ubaoni mara mia mbili. dah! umenikumbusha enzi za praimari wallahi. nawakumbuka kina donald msamati (kaka mkuu, halafu smati ile mbaya, na kiongozi wa gwaride), rosemary, george na josephine mwaipopo, john tembo na wamatumbi wengine wawili nimewasahau. asante sana ankal na aliyekutumia waraka huu
ReplyDeleteMINAKUMBUKA ENZI ZA SALAMA AU FITNA? NDEGE ITATUA UA UWANJA UNATOPE DUH KWELI TUMETOKA MBALI NIMFATILIA DEMU PALE KIDONGO CHEKUNDU KUMBE KAKA ZAKE WATU WA JUGNUNERO EBWANA WALINITOA NDUKI HAHAAA.
ReplyDeleteMDAU HAPO JUU UTAKUWA UMEMAANISHA JUGNU MEHU, TIMU YA MPIRA YA MTAA WA MCHIKICHI NA LIVINGSTONE (ANKAL ALIKUWA KIPA WAO, KWA MLIOCHELEWA KUJA MJINI) NA KAMA SIKOSEI ULIKUWA UNASOMA KAMA SIO GEREZANI BASI KISARAWE. NA HUYO DEMU MIE NAHISI NAMJUA. HAPO GEREZANI PEMBENI MWA SHULE YA KISARAWE PALIKUWA NA TIMU YA WATOTO WA GEREZANI (JINA NIMESAHAU) NA MMOJA WAO ALIKUWA NA DADA BOMBA ILE MBAYA ALIKUWA ANAKAA MTAA WA SOMALI KARIBU NA KWA KINA MARIJANI RAJABU. HALAFU MTAA WA AGGREY NA LIVINGSTONE (SIKU HIZI KWA BAKHRESSA) PALIKUWA NA TIMU INAITWA SANTOS, MAKAO YAKE MAKUU MJENGO WA PILI TOKA KWA BAKHRESSA, PALIKUWA NA HOTELI. USONI PA HOTELI HIYO NPALIKUWA NA KINYOZI MZEE NJOVU, BENJAMIN MKAPA ALIKUWA ANANYOA HAPO. DAH! MMENIPELEKA MBALI KWELI WALLAHI. HALAFU KULE MBELE LIVINGSTONE NA MKUNGUNI PALIKUWA NA TIMU YA GREEN EAGLES. UKIJA UPANDE WA MBELE ZAIDI MTAA WA UNGONI KULIKUWA NA TIMU INGINE (JINA NIMESAHAU) YAANI ENZI HIZO KILA MTAA ULIKUWA NA TIMU. SIO SIKU HIZI WACHINA KIBAO. WENYE KUMBUKUMBU ZAIDI HEBU TUPENI RAHA WATOTO WA KARIAKOO... BORN HIA HIA HAHAHAAAA
ReplyDeleteMambo hayo michuzi nimefurahi sana kuona barua hii na nembo yetu ya mapanzi moyo na mkuki, kule Bukoba kama kawaida yetu tlianza na neno. Kwakihaya ninkugonza, kwakiganda nkwagala na kwa kingereza I love you,
ReplyDeletena tukiamua kuwaeleza kwa mdomo tunasema NAKUTONGOLA, Maana yake ni kama kutungua embe, siunajua unachagua embe zuri.Haya ni mambo ya wakati na labda tulifanya hivyo bila kujua au nature kwani wakati huo wazazi lazima wasubiri mmelala fofo nawao wanaanza mambo yao na kwenye nyumba ya msonge husikii kitu kwani humo mbuzi na ng'ombe wanacheua usiku kucha.
mdau uk
Anonymous uliyesoma Nganza (au mkongwe kama mlivyokuwa mnaitwa enzi hizo), umenikumbusha jinsi ambavyo vijana wa Nsumba tulikuwa tunapita mlimani au kusubiri maji yakatike tukutane ziwani ili kufikisha barua kama hizo. Hizo ni enzi za mwalimu!
ReplyDeleteweee mdau wa mwanzo umenimaliza kwa kicheko.Haya jamani penzi ni kikozi, au tuseme maua popote uchanua,mdau wa mwanzo yeye ni mwafrica, mmatumbi na huyo mwengine kiasilia yeye ni muhindi, lakin ukija kwenye penzi. anakwambia sharti akinywa maji anamuona yeye, shughuli hiyo
ReplyDeleteDuh kumbe kuna wachezaji wengi wa Chelsea mnaoingia kwa Michuzi.Big pensioners.Afu cha ajabu nyie ndo mnaongoza kwa kuandika utumbo humu.haki ya nani nyie karatasi mlizoandikia hizo barua zitakuwa zile za rangi ya khaki.Nimeshaona magazeti ya 50's,60's na 70's yalikuwa si meupe.big up watoto tuliokuwa enzi za Mwinyi.hahahahahahaha.
ReplyDeleteEnzi za mwalimu penzi la kuviziana na masimango lilinoga sana
ReplyDeleteMimi niliandikiwa barua kama hiyo, mjumbe akaileta mara ile anafika tu akakutana na dingi kampokea kaifungua na kuisoma, nilitembezewa bakora, ukawa ndio wimbo wa taifa kwa baba, haki ya nani kila nikifanya kosa, ama kufanikiwa kitu kama vile kufaulu mitihani ya shule basi mshua anakumbushia si unaona yule mjinga alitaka kukuchezea na kukupotezea masomo yako ona sasa unafanya vizuri yaani hadi naingia chuo kikuu baba hajasahau anasema ungemfuata yule jamaa ungekiona chuo kikuu wewe" kaacha kunikumbushia miaka ya mwanzoni mwa 2000 nilipoolewa. Imenikumbusha mbali sana ila namshukuru mshua kwa kukomaa na mimi.
ReplyDeleteHa hahaaa hii imenikumbusha mbali sana, me niliandikiwa barua ilikuwa darasa la 5, nilikuwa muoga nikamuonyesha mwalimu bwana wee kesi ilikuwa kubwa, jamaa akatandikwa bakora na mzazi akaitwa. sasa shughuli ikawa baada ya hapo jamaa alikuwa ananivizia njiani anipige, dah nilipata tabu sana aisee!
ReplyDeletenakumbuka wakati tunacheza kombolela...tukienda kujificha tu tunadandiana hukohuko,sometimes tunashikwa lakini hivyohivyo..ilikuwa raha sana...mwendo wa dry....dah
ReplyDelete