Mama Mwapachu, mmoja wa viongozi wa TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION (TPF) akiongea na wazee wanaolelewa katika kituo cha Msimbazi jijini Dar hivi karibuni ambapo yeye na wenzake walipeleka misaada kwa wazee hao ili kupunguza makali ya maisha magumu waliyonayo
Baadhi ya wazee kwenye kituo cha Msimbazi
na misaada waliyoletewa

Misaada mbalimbali kwa wazee wetu
Mama Khalaf akikabidhi misaada kwa ajili ya wazee hao
Kila aina ya msaada unapokelewa
Baadhi ya viongozi wa TPF wakiwa kituo cha wazee Msimbazi
Sista wa kituo cha wazee cha Msimbazi akipokea misaada

Sista akishukuru wana TPF kwa misaada

Watanzania wenzetu,

Tujenge tabia ya kujitolea kusaidia sehemu ya jamii iliosahauliwa. Jamii iliokuwa pembezoni. Jamii isiojumuishwa kikamilifu katika mipango rasmi ya nchi.Tukijivunia maisha Bora, basi angalau sehemu hii ya jamii nao wapate kidogo ya ubora huu.

TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION ni NGO iso ya kiserikali, ni ya kujitolea. Azma kuu ya kikundi hiki ni kutafuta misaada mbali mbali kama vile:

1. nguo, viatu, shuka, vifaa vya jikoni viliotumika (sio viliochakaa) au vipya za wakubwa na watoto wakiume na wakike

2. vifaa vya kulimia bustani ndogo ndogo za mboga

3.magodoro na vyandarua

4.vifaa vya shule kama vitabu, madaftari na kalamu

Vitu vyote hivi ni kwa ajili ya kuwapa wazee wasio na uwezo na wengine wamejikuta wakilea wajukuu ambao wazazi wametangulia mbele ya haki.

Tumegundua wazee wengi wanaishi katika mazingira magumu na duni sana. wazee wengine wapo katika vituo na wengine wako majumbani bila msaada wowote.

Kwa maelezo zaidi tafadhali tuwasiliane kupitia info@tushikamane.com

au piga simu +255752 224688

"Haba na haba hujaza kibaba"

Mdau


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Msaaada kwa wazee ni muhimu sanaaaaaaaaaaaaaa! huo hauna kipingamizi..lakini mimi nalia na wale watoto yatima.Hawa watoto tunawasaidia ndio, lakini huwa hawana adabu. Mtoto alishafiwa na wazazi wake anajiona yeye ndie yeye, hataki kusemwa wala kuambiwa chochote kinachoweza kumjenga. Ndio maana siku hivi vituo vinakua vingi ni kwa sabb hawa wanetu hawaleleki. Ukimwambia hiki atakujibu: unasema kwa sabb mimi yatima... n.k hili neno yatima limewapa kiburi sana na wameishana kwao ni dili. Jamani tuwasaidie lakini tuwajenge kimaadili si misaada ya mali tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...