BW. kIHWELE EMMANUEL

YAH. KUPOTELEWA NA VYETI VYA FORM IV (Living Certificate na Academic Certificate), RESULT SLEEP YA FORM SIX, CHETI CHA KUZALIWA NA CHETI CHA KIFO CHA MMOJA WA WAZAZI WAKE.
VYETI VYO VIMEPOTEA /KUSAHAULIWA KATIKA GARI (DALADALA) LINALOFANYA SAFARI ZAKE KATI YA UBUNGO - MASAKI LEO TAREHE 19/1/2011 SAA 5 ASUBUHI WAKATI MWANAFUNZI HUYO AKITOKEA BODI YA MIKOPO (TIRDO) MSASANI KUELEKEA UBUNGO.
ANAOMBA KWA YEYOTE ALIYEVIONA/KUVIOKOTA/KUVICHUKUA AMRUDISHIE KWA KUWASILIANA NAYE KWA ANWANI IFUATAYO; KIHWELE EMMANUEL D. MOB - O783 059220 na 0716001981.
AU AVIPELEKE KWENYE KITUO CHOCHOTE CHA POLISI
AU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (MLIMANI).




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Pole sana kwa mkasa huu. Lakini kumbuka hizi ni zama za ubepari (sio tena ujamaa): bila kutoa hadi ya ki-zawadi kidogo kwa mwokotaji sina uhakika kama utapata hivyo vyeti!!!!!

    ReplyDelete
  2. napenda kumpa pole kijana kwa kupotelewa na vyeti, kweli ni usumbufu kupata vyeti vingine na itachukua muda mrefu. pole sana nakupmbea uvipate.

    Napenda kusahihi kiingereza kilichotumika, ili siku nyingine tuwe makini kidogo.

    (1) "living certificate" iwe leaving certificate. ile ya mwanzo ina maana nyingine kabisaaa yaani "cheti cha kuishi...
    (2) "result sleep" iwe result slip ile ya mwanzo maana yake matokeo ya kulala.....

    Kimombo shida tupu... hata matamshi yanatofautiana jamani.

    Mdau

    ReplyDelete
  3. unafaa mdau hapo juu kuwa mwalimu wa glob tunajifunza wengi Ahsante

    ReplyDelete
  4. Bwana uliyepotelewa na vyeti pole sana.Jitahidi kuacha kutumia bahasha za khaki kuweka vyeti au documents zako kwa kuwa ni rahisi sana kusahau.Ukitumia hand bag si rahisi kuisahau.

    Kwa kuwa umetoa tangazo hapa basi natumaini utappata vitu vyako.Au kama ulitunza tiketi ya gari ulilopanda utakuwa mwanzo mzuri.

    Wewe anony wa Wed Jan 19, 11:25:00 PM 2011 sio kwamba ndugu Michuzi hajui alichokiandika na anajua sana anachojaribu ni kuonesha ni jinsi gani maneno ya kingereza yanayosomwa(pronounced) sawa yanavyoweza kuwa na maana tofauti kabisa.

    Halafu anapenda kuifanya hii blogu iwe ya kijamii ,iwe blogu shirikishi kwa wasomaji wote kushiriki kuijenga iwe nzuri zaidi.

    Kumbuka kuwa Ndugu Michuzi ni mwandishi wa gazeti la serikali la Daily News.

    ReplyDelete
  5. Pole sana uliyepotelewa na vyeti.Inshallah Mungu atakujalia utavipata

    ReplyDelete
  6. Pole sana Dogo! hila sizani aliye okota hata internet anaijua ni kitu gani! Mi na akika kaokota konda sasa , kisheria unatakiwa ulipe nauli upewe receipt sasa sijuhi kama ulilipa nauli au ulipewa hiyo receipt , kana unayo fatilia hiyo dala dala, kwani nauakika kama mtu mweka kaokota cha kwanza hatampa konda as long kulikuwa akuna pesa kama ni makaratasi tu . hatakuwa nayo konda.

    mdau bwagamoyo

    ReplyDelete
  7. wala msimtetee na hicho kiinglishi chake, elimu yetu ya bongo KUKARIRI kumezidi watu hawajui maana ya wanachosema.
    Sasa kama huyu ni mwanafunzi kamili anayeingia chuo kikuu ......
    ELimu BOngo oyeeeeee

    ReplyDelete
  8. Hiyo ni englishi ya RB aliyopewa aliporipoti kituoni?

    ReplyDelete
  9. ..pole sana jamaa, its hard for u i know..

    ReplyDelete
  10. we Mdau wa Bwagamoyo hapo juu ( anonymous 02:36:00 AM 2011 ) Tafadhali rudia comments zako kwa kiswahili tafadhali .........

    ReplyDelete
  11. Pole sana kwa kupotelewa na Vyeti......its a hard time for you, sorry.
    Sasa vyeti vikipatikana tafadhali pia mtujulishe Pia.

    ReplyDelete
  12. Niliandika mwanzo kuwa pole nashangaa sikuona comment yangu,nasema kwa watu wote wapanda daladala usiweke mzingo wako chini kwani mwendo wa daladala ni mfupi unaweza kusahau sio kama mabasi ya kwenda mikoani,kila mara katika daldala unafikilia kuteremka ni rahisi mno kusahau mzingo hasa huwo wa makaratasi ni kushika mkononi tu dogo,,Pole sana tunakuombea upate vyeti vyako masikini ni vya muhimu mno,Insha'Allah Pole sana

    ReplyDelete
  13. Dogo andika umeumia!

    ReplyDelete
  14. Nilishawahi kupotelewa na vyeti vyangu nikavipata hivyo ninauhakika kabisa utavipata vyeti vyako.Sirahisi mtu kuvitumia iwe bahati mbaya sana muokotaji asijue umuhimu wake.Pole sana kwa wakati mgumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...