Tuombe msaada kuwasaidia wenzetu ambao ni
mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu...
mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu...
Ninakuomba kama mtanzania mwenzangu tupeane hamasa ya kupendana na kusaidiana sio katika sherehe za starehe tuu, zaidi siku hizi tuzidishe kusaidiana katika shida maana sasa shida zinazidi siku hadi siku.
Katika pitapita zangu, nimekutana na mtoto huyu Abdully mwenye ulemavu wa viungo huko Kaole, Bagamoyo. Kula kwake kwa taabu, haongei, ingawa anacheka akifurahishwa, na kulia kwa kupiga kelele akiudhiwa au akiwa na maumivu ingawa hawezi kuelekeza maumivi yako wapi.
Cha kusikitisha, mama yake mzazi amemkimbia mtoto na mume, baba nae ameanza kukata tamaa ya mwanae kwa kukosa muelekeo na msaada (support). Baba (Bw. Hamoud) anaishi na mama yake mzazi ambaye ni mtu mzima mwenye matatizo ya kiafya, macho na thyrod eshafanyiwa upasuaji nk... sasa Bw Hamoud ameacha shughuli za kutafuta fedha za kukimu maisha ili aweze kumlea kijana Abdul (4) ananza asubuhi kwa kumuosha, kumlisha kifungua kinywa..... mchana kumlisha anakula kwa taabu maana ulimi hauzunguki sawa sawa kama vile umepooza, na koo halimezi vizuri.... jioni anamsafisha na kumlisha.... maisha yamekuwa duni, kwa hivyo hata malezi ya Abdul yamekuwa magumu mno...
Alishauriwa ampeleke hospitali ya CCBRT, nae baada ya kwenda hapo alishauriwa ampeleke kwa physiotherapy kila wiki, tatizo la Bw Hamoud ni usafiri kutoka Kaole hadi msasani CCBRT ni wa daladala na mtoto mwenye ulemavu wa viuongo si mchezo... mlemavu wa aina hii anaweza kuwa na haja kubwa au ndogo mahali popote wakati wowote hata mkiwa ndani ya daladala huduma yake ngumu hapo ni mtihani...
Hapo CCBRT wanaweza kushinda kutwa kabla ya kupata huduma kipindi hicho cha kusubiri mtoto amebebwa au kupakatwa, chakula hakuna, na pahala pa kumlaza aweze anaglau kunyoosha viuongo hakuna. wahudumu wanapita na kumuangalia hapo katika foleni bila kumpa tamaa au hata nasaha. Jioni usafiri wa wa kubanana ndani ya daladala kurudi Bagamoyo, pikipiki hadi Kaole.... Baba Abdul kaishiwa nguvu ameshindwa. Wapo Kaole wanasubiri hatma ya Mwenyezi Mungu.
Abdul amepewa ki "baiskeli" cha mtoto (push chair) na akiwekwa hapo lazima afungwe na khanga ndio akae kwa usalama na kwa sasa anabanwa hapo....
Hivyo basi Kama kuna wasamaria
wenye huruma na hali hii, wanaomba:
1. Wheelchair ya kawaida Abdul akae
kwa usalama na awe na nafasi viungo viwe huru
kwa usalama na awe na nafasi viungo viwe huru
2. Ushauri kwa kiafya
3. Ushauri wowote, na msaada wowote
utakaoweza kutoa afueni kwa Abdul na baba yake Hamoud
utakaoweza kutoa afueni kwa Abdul na baba yake Hamoud
mpigie simu Hamoud
+255 757 652449 na +255 787 771566
kwa msaada au ushauri. Juhudi za kufungua
akaunti maalumu zinafanywa kwa wenye
kutaka kumsaidia mtoto Abdully
+255 757 652449 na +255 787 771566
kwa msaada au ushauri. Juhudi za kufungua
akaunti maalumu zinafanywa kwa wenye
kutaka kumsaidia mtoto Abdully
Mdau Dar
Mtoto Abdully anaomba msaada wako
Abdully akiwa amebebwa na nyaya yake
Abdully anasimama na kulala kwa shida...





Inasikitisha!!!!
ReplyDeleteHali hii ndio serikali inatukandamiza tunapo lalamika na kuandamana? na police wanatumia silaha za moto! wkt garama za uukandamizaji zingeweza kusaidia wengi abduli kupata huduma muhimu.
Serikali inalipa DOWANS mabilioni ya hela kwa uzembe wa viongozi, je fedha hizo kwanini zisitumike kutatua huduma muhimu kama mahospitali, shule na usafiri?
Najua habari hii watasoma wengi wakiwemo viongozi wa serikali lkn watajidai kufumbia macho, na haswa UVCCM waliolalamika kwamba kuhusu maandamano ya Arusha! Kama wana uchungu na wanataka kuchangia na kulipa fadhila kwa wavuja jasho, mwaswala kama haya ndio walitakiwa kuyapa kipaumbele, na sio kuingilia mambo ya siasa na kutaka kuendeleza uongozi wa kurithishana na mabavu kama kawaida ya nchi za Afrika.
Yanayo ikabili family ya Abdully ni hali halisi ya taifa letu. viongozi na organisations husika please chukueni hatua mapema, kwanini watu wanateseka hivooo!!! ama mpk tuandamane?
Viongozi wa nchi kama mnaliona hili na mengine tafadhalin mchukue jitihada na njia mbadala za kuwasaidia hawa watu wenye matatizo,pesa ni za mpito katika hii dunia ila thwawabu ni za milele!CCM MUOGOPENI MUNGU!!SAIDIENI WASIOJIWEZA NA SIO KUNG'ANG'ANIA MADARAKA!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteTuwekee akaunti namba ya babake Abdul, yaani bwana Hamoud, ili sisi tusio na uwezo wa kununua hiyo wheelchair japo tumchangie pesa za kumsaidia matumizi madogo madogo.
ReplyDeleteWewe mdau wa kwanza kama ulikuwa huna la kuchangia ungesonga mbele, watu wanaomba mpaka michango ya uchangia wafu/maiti au waliokwishakufa na mapesa kibao yanatolewa seuze huyu mtoto mdogo asiye na kosa tena bado yuhai?
Mdau tuko pamoja mie masikini sina kitu lakini ntamchangia japo kidogo nilichonacho kimsaidie na mwanae. Kutoa ni moyo si utajiri!
Hongera Mdau kwa kufanya jitihada za kumtafutia mtoto huyo msaada.
ReplyDeleteWadau tuache kujinufaisha kisiasa kwa shida za watu. Huo si ustaarabu hata kidogo!
Yaani watu wa ajabu kabisa, huyo mtoto ndio wanasiasa wamchangie lakini wao kutwa kuleta matangazo ya ndugu zao walokufa wachangiwe madola kibao, hayo madola ya kusafirisha maiti huyu mtoto hata india angepelekwa lakini sisi watanzania hatunaga utamaduni wa kumsaidia mtu akiwa mzima ndio maana wadau hapo juu wameleta mambo ya siasa.
ReplyDeleteNauliza hivi mbona jamaa zenu wakifa hamuviambii vyama au wabunge wao wasafirishe maiti kutwa matangazo kwenye mablogu na kiwango cha pesa mnaweka. Acheni roho zenu mbaya za kibaguzi.
Ndugu zangu waislamu habari hii si mpaka ungoje uisikie msikitini, sisi tumeamrishwa kuwasaidia masikini na wasiojiweza shime jamani tumsaidie huyu mtoto kama dini inavyosema malipo yake ni kwa Mwenyezimungu!
Nipo tayari kumnunulia wheelchair. Michuzi weka akounti namba ya babake abduli.
ReplyDeleteMsimlaumu sana mdau kwanza , yeye amejaribu kuzungumzia mzizi wa shida zinazowapata watu kama hawa.
ReplyDeleteHamaanishi kuwa huyu asisaidiwe, kusaidia ni vizuri na ni thawabu. Serikali nyingi duniani zinakuwa na sera za kuwasaidia watu wote wenye matatizo kama haya ila ya kwetu utakuta raisi au waziri anatoa bajaj kwa mtu mmoja anayekutana naye kwenye kampeni huku akijua kuna wengine wengi tuu wako na matatizo kama hayo. Tuwe na sera za kuwasaidia wale wote wenye matatizo kama haya kuanzia serikali kuu. Sasa kama Michuzi asingetoa hii watu wangejua vipi. kumbuka kuna wengi tuu wenye shida kama hizi , wakijitokeza woote hapa kwa wakati mmija tutawasaidiaje?
Tena mie naona tuchange mchango wa hali na mali akatibiwe india kabisa, tupeni account tuweke chochote tafadhali.
ReplyDeleteplease michuzi weka akauti number sisi tulukuwepo nje ya nchi tutume hela ya matumizi kweli inauma kama mzazi nimejisikia vibaya kweli
ReplyDeleteUNCLE TAFADHALI UKIPATA ACCOUNT NUMBER ZA WAHUSIKA TUTUMIE NA SIE TULIO NJE TUCHANGIE HATA SUMNI, SHUKRAN
ReplyDeleteKAKA MICHUZI VIPI HUYU MTOTO AMEAMBIWAJE HUKO HOSPITALI ANAWEZA KUTIBIWA AU VIPI KAMA ANAWEZA BASI WAKO WATU WANAWEZA KUMFANYIA MPANGO AKAPELEKWA CANADA KWA MATIBABU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA MABULA SABULA KATIKA EMAIL HII mabusabu@yahoo.ca AU MASOUD massudalamry@yahoo.com ILITUWEZE KUMSAIDIA HUYO MTOTO.
ReplyDeleteJAMANI WADAU!!!
ReplyDeleteNilitoa mawazo yangu hapo juu, sio sbb nilikuwa nalaumu mtu! bali kama alivoeleza mdau wa 05:25 nilipoona habari hii nilisikitishwa kutokana na matukio yaliyopita, na ufafanuzi nilitoa hapa hapa lkn Mheshimiwa kabania!!!!!
Kwa kifupi nilifananisha hali ya Abdully na matukio ya wiki hii na pia baadhi ya viongozi ama watu wanaoji starehesha kwa party za kila aina( pekua habari inayofuata hapo chini mtaelewa).
Lkn tuyaache malumbano, cha muhimu ni ufumbuzi wa ttz la Abdully .
Pia naamini VIONGOZI awatafumbia macho swala hili la Abdully sbb pia wao wanapitiaga ama kupata habari zilizopo kwenye blog hii na nyinginezo.
Mr Michuzi usibanie ujumbe huuu
watu mnaombwa michango ya sherehe zote za maharusi mnatoa ili msipate aibu malaki mamilioni nini kuja humu kuongea pumba, wewe hujijui lini litakula kwako
ReplyDeletemungu awabariki wote watakaochangia na wanaochangia wengine wenye shida
huyo mama akirudi baada ya kuona pesa zinaingia mfukuzeni jamani
Inshaaaalah allah atamuafu mtt Abdully.Nina wheelchair ya marehemu mzee nyumbani TZ ambayoimetumika kwa muda mfupi sana kabla ya umauti.inshaalah kabla ya end of nxt week mtt abdul atapelekewa.Zaidi uncle Michuzi ni account number.ahsante
ReplyDeleteNashukuru kwa kutuwekea taarifa hii, Namuombea mtoto Abduly tahfif kwa hali aliyo nayo, na namuombea subra baba yake kwani ni mtihani mkubwa. Naomba utupatie account ili tuweze kutoa tutakacho jaaliwa. Naomba uniulizie kwa wahusika kama wanaweza kupokea nguo zilizokuwa za mtoto wangu wa kiume ambazo kwa sasa hazimtoshi lakini ziko ktk hali nzuri. Hali ya mtoto Abdully ni kipimo cha utu wetu. Mwenyezi Mungu atuwezeshe.
ReplyDeleteShukran
S.O.M. - UK
POLE SANA KIJANA ABDUL NA MZAZI WAKE HAMOUD KWA MATATIZO HAYO MUNGU ATAMSAIDIA KIJANA ABDUL. MAOMBI KWAKE MUUMBA YAONGEZWE KWA AJILI YA ABDUL NA WENGINE WOTE WENYE MATATIZO YANAYOFANANA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NA YA ABDUL(MAGONJWA MBALIMBALI).
ReplyDeleteTAFADHALI FUNGUA AKAUNTI TUCHANGIE KWASABABU HUWA TUNACHANGIA HARUSI KWA HELA NYINGI TU.
USHAURI AKAUNTI IFUNGULIWE KATIKA JINA LA ABDUL NA AUTHORISED OPERATOR AWE BABA YAKE ILI AKIWA MKUBWA AWEZE KUENDELEA NA AKAUNTI YAKE YEYE MWENYEWE NA ATAONA WASAMARIA WEMA WALIMCHANGIA NINI.
MARA NYINGI KTK HARUSI ZINAZONIHUSU HUWA NACHANGIA WASTANI WA TSHS.50,000.00 HIVYO NA HIYO NI AHADI YA MCHANGO WANGU KWA ABDUL NA TUAMBIWE TU PALE AKAUNTI ITAKAPOKUWA IMEFUNGULIWA ILI TUTUME HELA HIZO.
MDAU 0767528272/0655528272
Mdau wa UK mwenye nguo za mtoto sidhani kama babake Abdully atachagua maana kama ilivyoelezwa hapo juu hana kazi wala kipato kwa sasa, cha msingi wasiliana naye moja kwa moja kwa namba yake ya simu iliyotolewa hapo juu. Nafikiri hata kumpigia kumpa moyo na maneno ya faraja pia inafaa. Kama unaweza kutuma na nappies (diapers) itasaidia pia maana huko UK kidogo bei yake nafuu ukilinganisha na nyumbani.
ReplyDeleteMungu amsaidie apate msaada
ReplyDelete