Rais wa Shirikisho la Polisi Duniani(Interpol) Bw. Khoo Boon Hui (katikati) akizungumza jana jijini Dar es salaam na makamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi juu mikakati mbalimbali ya kuimarisha usalama na jinsi ya kukaribiana na uhalifu wa kimataifa na maharamia katika mwambao wa Afrika Mashariki. Wengine katika picha ni Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Said Mwema (kushoto) na Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja(kulia). picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Hivi hao wakuu wa polisi wa kibongo ni lazima kuvaa hayo magwanda kila shemu?

    hawawezi kuvaa suti tu na wakawa na muonekano wa heshima zaidi kuliko hayo magwanda yao?

    kwani kuwa mkuu wa jeshi au mkuu wa polisi ni lazima kila kikao au unapokutana na uongozi fulani wana ulazima kuvaa magwanda?

    mbona wenzetu walioendelea wakuu wao wa majeshi au polisi hawavai magwanda kila sehemu? special wakikutana na ugeni kama huo

    kwa mfano yule mlinzi wa Mh. raisi ni lazima kuvaa magwanda?

    maana namuona mlinzi wa raisi wakati mwingine kwenye sherehe za viongozi labda viongozi wakuu wanaenjoy lakini lazima akae nyuma ya raisi na magwanda yake kwa kweli haileti picha nzuri

    utakuwa viongozi wengine wote wana walinzi wao lakini wamevaa suti na wamependeza lakini wa kwetu mmmh...

    kuwa mlinzi wa kiongozi ni vizuri zaidi kutumia mavazi ya kawaida au suti ili kuwafanya maadui wanaotaka kufanya ubaya wasiweze kukutambua na uweze kuwagundua kirahisi lakini kwetu utakuta mlinzi wa raisi ana jezi maalumu kila mechi anavaa hiyo hiyo.

    ushauri kwa wahusika wakuu wajaribu kufanya mabadiliko na kuleta muonekano mzuri kwa jamii na kwenye ulimwengu kwa maana kiongozi wetu hufika kwenye mikutano mingi mikuu huko nje ya nchi.

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu anaonesha ni jinsi gani Watanzania tunajifanya kujua kila kitu,kukosoa kila jambo, na pia kuonekana mbumbumbu kwa kila kitu na kila jambo kama huyo bwana hapo juu.

    Mpangilio wa mada yake kwanza hauko awa kama zilivyo akili zake. Kaanzia magwanda ya Afande mwema, hajamaliza karukia kwa mpambe wa Raisi.

    Hii jamani ndiyo picha halisi ya mtanzania wa kizazi kipya. ujuaji, ubishi, jazba na kujiona kaonewa hata kama hahusiki na jambo ama kitu. Halafu mbaya zaidi usikute mtu kama huyo hapo juu huenda yupo wilaya gani huko ndani na hata makao makuu ya mkoani hajafika. na kama yupo dar basi kaja majuzi na ndio kwanza anaanza kujua kwenda cafe kwenye internet na kudonoa utumbo kama huo.

    Kwa kukusaidia tu mdau, na kama ung'eng'e unapadnda. Bofya link hio chini ujue nini maana ya mpambe wa raisi ama ADC ambapo kwa muonekano wa hoja zako njiwa unadhani yuko TZ tu

    http://en.wikipedia.org/wiki/Aide-de-camp

    ReplyDelete
  3. wewe uliejaribu kunijibu hoja yangu hapo juu inaonekana wewe ndio ulikuja mjini ukiwa mkubwa

    mimi nimezaliwa dar katikati ya jiji na nimekulia dar na kwa sasa nipo nje ya nchi na maisha yangu hayafanani kabisa na njaa yako

    ukitaka kumrekebisha mtu hoja hakuna haja ya kuanza kumpa maneno ya matusi au dharau

    hao wanaoishi vijijini ni watu kama sisi na hata kama hawajafika mjini pengine sio makosa yao

    usikurupuke kuona watu wote wanaoandika maoni humu ni walala hoi kama wewe kama una matatizo weka namba yako hapa nikuite ofisini kwangu hapo dar upatiwe ajira.

    mdau mahakama kuu ya dunia.

    ReplyDelete
  4. PETER- KARDASHIAN - NALITOLELAFebruary 21, 2011

    MUSAHENI HUYO MUCHANGIAJI WA KWANZA. ANGEENDA MUZUMBE KUSOMA ANGEKUWA NA AKIRI KIDOGO. HUYU KASOMA NGUMBAO MAANA NDO MAANA YAKE. SISI TURIYOSOMA CHUO KIKUU CHA UNIVESITI CHA ECONOMY CHA KULE MOLOGOLO HATUPAYUKI HOVYO. MWEMA NI MUTU MAKINI SANA KWA MAANA KASOMA MUZUMBE BWANA. AKIRI NI NYWERE. HUYO ATAFAA ZAIDI AKIFUNGUA SARUNI YA KUNYOA NYWERE

    ReplyDelete
  5. Wewe bwana mie ndio huyo jamaa aliyekupa shua. Nasema hivi tena kwa herufi kubwa WEWE UNAISHI KIJIJINI NA HUNA EXPOSURE NA KAMA UKO DAR AMA HATA HUKO ULAYA UNAKOVUNGA UPO, ULIKIMBIA UMANDE!!!!

    Angalia hata majibu yako hapo juu yanaonesha wewe ni mtu dhaifu wa aina gani. Hao wa kijijini hawana exposure ndio maana nikawasema sio kwa ubaya kama unavyotaka kupakazia hapa.

    Halafu si kweli. kuwa wewe ulizaliwa Dar. Sie born hia hia huwa hatusemi utumb kama wako. Mie nimezaliwa na kukulia mtaa wa mbaruku. Mpira wa chandimu nimecheza karibu na kaburi la chifu Kibasila. Nitajie kiwanja hicho kiko wapi kama wewe kweli wa Dar.

    Acha ujuaji wakati hujui kitu. Na Ankal naomba hii mechi usiikate mapema, mradi hatuchafui hali ya hewa. Plizzzzzz ankal usitubanie, wengine tuna hasira a mabomu wengine (pana pua) naishi ulayaaaaaa...Allllaaaaaa!!!

    ReplyDelete
  6. wewe wacha kushindana na mimi mtoto wa livingstone nenda maskani zote za mitaa ya kariakoo ulizia utaambiwa mimi nani wacha kunitajia sehemu za kitoto

    mimi mtoto wa livingstone na mkunguni kama unatafuta ujue nilipo ili uanze kunitumia email za maombi ya kazi sina shida na mtu asiekuwa na elimu kama wewe

    wewe afadhali nimtajie ankal michuzi kwa maana itakuwa amesoma na wakubwa zangu au wamecheza pamoja enzi hizo dar kuna majina yake kama vile kiungani mchafukogwe nk.

    watoto wa mjini wakiongea wewe kachukue khanga ucheze kibao kata

    eti oooh sisi born hia hia hahaha ajira unayo lakini?

    ReplyDelete
  7. acheni kurumbana,kwa kweli hayo mavazi ya kipolisi hayapendezi kwenye international meetings, mbona mkuu wa fbi havai hayo magwanda? na huyo mkuu wa interpol ambaye ndiye mkuu wa mapolisi duniani mbona hakuvaa hayo magwanda? kwa kweli hyo magwaanda yanatia kichefuchefu !!! mimi pia ni mtoto wa mjini hapo mikocheni na niko huku ughaibuni!!

    ReplyDelete
  8. HAhahaahahahahah!!!!

    Wadau mmenichekesha sana.....

    Ankal kweli hebu waache tuone mwisho wake, lazima mmoja akubali matokeo. Amakweli BONGO kuna kila aina ya watu!!! Duh!!!! Yani FULL ubishi na ujuaji. Mmenifurahisha sana.

    MPAKA SASA MATOKEO: ALIYEZALIWA MTAA WA MBARUKU 3 - ALIYEZALIWA LIVINGSTONE 2..... mechi inaendelea

    Hao jamaa naona wamekutana, mpaka raha!!!

    NB: HAKUNA KUCHAFUA HALI YA HEWA!!!!

    ReplyDelete
  9. Narudi tena born hia hia mtaa wa Mbaruku Gerezani. Kukusaidia tu we hapo juu uwanja wetu wa mpira ulikuwa nyuma ya KAMATA (kama unapajua, maana hio Livingstone unayosema hio nyumba kulikuwa na mama mfanyabiashara ya kahawa, alikuwa na wauzaji kibao wa Kigogo anawalaza chumba cha uani, nahisi mmoja ni wewe haahahaaa). Mie pia Livingstone napajua kinyumenyume. Ulizia timu ya Green Eagles (kama unaijua ama ulikuwa umeshafika Dar wakati ipo), au nenda Gogo Vivu pale mtaa wa Ukame utaambiwa mie nani hata kabla ya kutaja jina Hahahaha upo hapo? Halafu wewe kama kweli wa Livingstone Egyptian Music club unaijua weye?

    Haki ya nani Ankal Michuzi hii mechi tuachie wenyewe. Na kama alivyosema mmdau hapo juu, mie naongoza sio 3-2 bali 4-0 kwa sababu huyo jamaa kachakachua ukaazi wake wa Dar. Anaujua mtaa wa Livingtsone tu alikokuwa anauza kahawa kwa mama nanihii (nitaje? ankal atasema nachafua hali ya hewa weweweeeeeeeeeeee bahati yako).

    Hiyo ya ajira nikuulize wewe maana nna mbwiga kama nane hivi naziweka mjini kwenye kajiofisi kangu ka Construction. Kwa taarifa yako mie naajiri, siajiriwi na hata ghorofa la karibu na ulipokuwa unauzia kahawa nimechora mimi. Upo hapo?

    Na hio mipasho ya 'kibao kata' na 'maskani' inaonekana wewe ndiyo walewale mliokimbia unguja na kudai kuna ghasia ili mjilipue. mtu wa Mrima, hasa wa Kariakoo, hataji maneno hayo. Anasema kijiweni na kibao kata ni 'nachi'. Unamjua Faruku wewe. Kitwana 'Kennedy' je. basi hao (RIP) ndio ilikuwa kazi yao. Sio kibao kata cha Unguja kwenu.

    Nasubiri majibu kwa hamu toka kwako muuza kahawa uliekuja Dar toka Dodoma na kuujua mtaa mmoja tu wa Livingstone. Ulitakiwa uuze kahawa kuanzia kuleee chini kwa kina Mkweche hadi huku juu kwetu kwa Dada Segere Matata (RIP). Kama unabisha sema. Ankal kunradhi kaka. niachie nimchane huyu mbwiga.... Haki ya nani tena sichafui hali ya hewa na wala sijeruhi hisia ya mtu/watu

    Born Hia Hia

    ReplyDelete
  10. Na wewe mtoto wa mama wa Mikocheni usidandie treni kwa mbele, utaondoka siku si zako. Wanaume wanapoongelea mambo ya town wewe katafute big G iliyotumika ule. Kwa taarifa yako Mikocheni wote mmekuja miaka ya 90. FULL STOP.

    Halafu Interpol sio polisi ya mwagwanda wala FBI. Hao kina mwema wako kazini kwao na sheria kuvaa magwanda kama wewe si kachero, sawa mtoto wa mayai wa Mikocheni?


    Born Hia Hia

    ReplyDelete
  11. Wabongo zenu nihizohizo za kuchambuana mala nina hili mala mimi ni wakuajili! sidhani kama mabomu yataturia Dar wazaliwa wenyewe nimatapeli tu wakujidanganya.Mimi naona mtanzania mwema niyule wa vijijini au machinga ndo anaekula kwa jasho lake,,na nyinyi mnaojidai kwa hivyo viji ofisi subilini mabomu ipo siku yatawanyuka.Mdau wa Kampala.

    ReplyDelete
  12. MDAU WA KAMPALA USITUTOE RAHA. WENGINE LIGI NDIYO STAREHE YETU. ULITAKA WASEME NINI NA WEWE NA UJUAJI WAKO WA UGOKONI. ACHA WATUPE DATA TUONE NANI MTOTO WA MJINI KWELI. HAYA HAYA HAYAAAAAAA DAKIKA YA 21 SASA, BORN HIA HIA FC ANAONGOZA 5-1 DHIDI YA LIVINGSTONE SC AMBAYE ANAONEKANA KAWEKA MPIRA KWAPANI.... HAHAHAA HADI RAHAAAAAAA. ILA WEWE WA BORN HIA HIA NOMA. MAANA UNATOA DATA HADI NASIKIA RAHA. MIE NILIKAA MTAA WA PEMBA KABLA YA KUHAMIA HUKU UBATANI. STORI ZAKO ZOTE ZA KWELI. UMESAHAU UWANJA WETU WA 'WIMBO' PALE MNAZI MMOJA SHULENI, NA ULE WA MNARANI AMBAKO JUGNU MEHU KIPASO WALILIKUWA WANAFANYIA TIZI. UPANDE WA PILI WA ANATOGLO KULIKUWA NA UWANJA WA MCHIKICHI BOYZ..... NANI ANA DATA ZAIDI ZA KARIAKOO WAJAMENI. TENA NASIKIA ANKAL ULICHEZEA JUGNU MEHU WEWE....KIPA!!! HAHAHHAHAHA SIAMINI!

    ReplyDelete
  13. nakuomba ankal utuachie kiwanja mimi na huyu born hia hia mpaka tujue mwisho wake

    wewe born hia hia wa bandia sikiliza sasa habari zako
    ukianza kutaja maskani ya gogo vivu pale kina seif minya marehemu makochela nk

    ukija hapo unaposema enzi hizo kunauzwa kahawa kwa yule mama wa kihehe kamwene aliweka wauza kahawa na alikuwa na bwana wake wa kidosi fundi magari hehehe hadi raha

    nitakutajia point zako zote ulizopitia

    kuhusu uwanja wa kamata ambao kwa sasa wamenunua scandnavia bus

    na kuhusu egptian music pale mtaa wa mafia

    kama unajuwa kuna alhawaa pia ipo livingstone ambayo waimbaji wake walikuwa kina abasi mzee nyimbo zao za haaaakiiika ninakupeeenda hehe



    kuhusu kuchora ramani ya gholofa la pale livingstone usijitie aibu maana mimi najuwa magholofa ya kipande kile yote kuanzia livingstone na mkunguni na nawajuwa mpaka wajenzi wake na wachora ramani wake

    nianze kutaja majina ya wamiliki wa magholofa hayo?

    1 livingstone almazrui
    2 livingstone GGS
    3 livingstone al asad kulia na kushoto kona ya mtaa wa pemba na livingstone na kona ya tandamti na livingstone tajiri mmoja

    4 mkunguni ali ablesh
    5 mkunguni bakhresa
    6 livingstone saleh mahara

    yani nakutajia magholofa yote yaliyo kipande kile unachosema umechora ramani nakutajia wamiliki wenyewe

    mpaka hapo inatosha zaidi ya hapo ni kushindana na mtu ili kumpa faida badae aje kujifanya mjuaji zaidi

    ukitaka naweza kukutajia mpaka majina ya wakazi wa mitaa zaidi ya kumi yani watu zaidi ya 1000 wa hapo kariakoo tena sio wahamiaji ni wazaliwa

    na ukitaka naweza pia kukutajia hayo magholofa yaliwahi kusimamishwa ujenzi usiendelee kwa sababu zake ambazo huwezi kuzijuwa kama huna ukaribu na wamiliki lakini kukuonyesha najuwa zaidi naweza kukutajia

    nakusubiri tena.

    ReplyDelete
  14. mkali wa livingstone nimerudi wewe unaesema umetoka mtaa wa pemba ndio utakuwa mkweli kabisa na nakukubali kwa maana utakuwa ni jirani yangu pamoja na kaka dr.riki mtaalamu wa mambo ya mipira

    na ikiwa unatokea hapo pemba basi utakubaliana na maelezo yangu na utakubali mimi ni mkali kushinda huyo born hia hia japokuwa refa anapendelea hehehe

    ReplyDelete
  15. born hia hia vp mbona kimya au umememe umekatika? hahaha kaazi kweli kweli au labda internet cafe zimefungwa

    ankal muazime laptop huyo born hia hia alete uongo wake hapa

    mimi nipo huku nilipo ndio kwanza jioni na kwa taarifa yako mimi nakutajia vitu vya hapo mitaani ambavyo miaka 10 sasa sijarudi huko

    na wewe upo hapo hapo dar unaweza kufika maeneo hayo na kuulizia data zote na ukapatiwa majibu au ukapata nafasi zaidi ya kushindana

    maana unaweza kunitajia vitu ambavyo mimi sivijui kwa sasa au nimevisahau lakini still ni mkali nakutajia vitu wakati sijapaona hapo mtaani kama miaka 10 sasa

    kama umeme umekatika subiri mgao wenu alafu kesho ujibu tena angalia tu ukisikia mizinga usifikiri ni mwaka mpya ujuwe kimewaka hehehe

    ReplyDelete
  16. We bwana maliza hela yako kupigia watu simu wakupe details tu. Mie sihitaji mamluki nakupa straight toka kichwani.

    Ukianza na Gogo Vivu unamjua Makochela tu (RIP) ambaye alikuwa anapita tu, sio mkaaji sana. mambo yote Makochela yalikuwa Ilala mtaa wa (jina kapuni nisikupe faida) na rafikie mkubwa alikuwa Norman Wage. Unamjua Norman wewe? (Nakuona unapigia wenzio simu kariakoo. unagandamizia hata mtihani mdogo hivi??? hahahahaa

    Halafu kimeo mwenzio nimekatia kwa Kitonsa muuza bangi karibu na hapo ulipokuwa unauzia kahawa (tehe tehe tehe nafurahi umekiri kwa mdomo wako kuwa unamjua mama wa Kihehe na bwana wake wa kidosi, ambaye ndiye tajiri yenu, safi sana!) Hii inathibitisha umekuja enzi hizi za maghorofa. Mie naongelea Kariakoo ya Mbavu za Mbwa baba!

    Halafu huyo Abbas Mzee alikuwa Egyptian na akiwa Awami Mohamed, aliyekuwa anafanya kazi Relwe workshop (upo hapo), na sio hio bendi uliyoita Alhawaa. Nyimbo za Abbas Mzee (RIP) ni pamoja na Yatima na Harusi. Piga, ua garagaza we bado huoni kitu (na endelea tu kuwapigia simu wakuja wenzio na majina ya maghorofa)

    Nyuma kule kwa mzee senga unakujua wewe. Kina Abbasi, Salehe na Dada zao. Mirungi kule chini Pemba hujaikuta wewe, wala hujui kwamba timu ya Green Eagle ilikuwa na makao yake pale hotelini kona na Pemba.

    Lete maneno na endelea kupigia watu simu.
    Tukmitoka kariakoo tuhamie wapi - Jangwani? Mishen kota, ama Mtaa wa Masasi kwa Mzee Rupia? Ama Congo street pale anapokaa Shaaban Dede penye timu ya Asante Tololo kina Skina Martin, Juma Kajembe, . Ama nikirudishe Kongo Mwisho timu ya Nungu?? ma kota za Relwe (Shangwe FC), ama kwa kina Kaungu, ama express ya kina gebo na peter tino na kina Aly Bay?. ama Kahe mtaa wa mchikichi, ubavuni pa simba

    Ama city boys ya Livingtsone chini, ile ya wadosi tu

    Born Hia Hia

    ReplyDelete
  17. Weweeeee nani kakwambia mie nategemea tanesco. nyumbani full jenereta na internet unlimited ya 8mps (kama unajua nini) nakwambia sina wasi na wewe na wala 10 kama wewe. jibu kwanza hizo tuhuma hapo juu za kupigia watu simu. nasubiria na wala sikuogopi...

    Born Hia Hia

    ReplyDelete
  18. KWA MPANGO HUO INAONEKANA BORN HIA HIA UMESHINDWA MAPAMBANO SASA UMEHAMIA MITAA MINGINE MWANZO ULISEMA WEWE NI MCHORA RAMANI WA MAGOLOFA NA MWINZIO KAWATAJA MPAKA MATAJIRI WENYEWE MPAKA SASA INAONEKANA WOTE NI WAZALIWA WA DAR ES SALAAM LAKINI MTOTO WA LIVINGSTONE NDIO ANAONGOZA KWA UKALI WA KUJUWA ZAIDI BIG UP HOME BOY LIVINGSTONE

    ReplyDelete
  19. wewe born hiahia wacha kushindana humuwezi huyo mtoto wa livingston hizo nyumba unazosema ni mbavu za mbwa mwinzio ndio alizozaliwa kama unajuwa lile jumba la livingston lilikuwa linafungwa mabata na kuku wengi ndio hapo kwao mimi pia nimezaliwa kariakoo na namjuwa huyo jamaa wa livingston wewe angalia amekupa maelezo kwa ufupi tu na yote ni magoli ya uhakika


    mdau usa.

    ReplyDelete
  20. NASUBIRI MPAMBANO UENDELEE, LEO RAHA TUPU......... REFA KAA SAWA MECHI INAENDELEA

    ReplyDelete
  21. hii post imeondolewa na admin.

    hee hee

    ReplyDelete
  22. Born Hia Hia hapa. Nilikuwa naongea na simu toka Bahrain, inasemekana flat yangu iko hatarini, kwani iko karibu na mapambano. Tuombe Mungu inshaallah wapangaji wangu wanusurike.

    Haya, naona Livingstone Boyz mmeamua kuja kunipiga mande. Siogopi. Njooni hata mia, sina wasi nanyi. Mechi hii ni kuhusu kuwa born hia hia Dar. Na sio kamtaa kamoja tu ka Livingstone. Jamaa wa mtaa wa Livingstone naona kaishiwa vyanzo vya habari, wengi wameuza nyumba na kuhamia aidha ulaya (anakodai aliko yeye) ama Kinyerezi huko. Njaa mbaya!

    Mie katika kuonesha ni kweli wa hapa Dar nimeenda nje ya Livingstone Street na kuhoji kama ana cha zaidi. Nyie mnadandia treni kwa mbele kutaka kumtetea. Masaa kibao hajajibu mashambulizi, bado niko langoni pake. Mnalo nyie watoto wa Livingstone kwa kina Mazolla?

    Born Hia Hia

    ReplyDelete
  23. pumba pumba tu ndio mnakazania ati na wengine wanashangilia kabisa mmh!!!
    wanaume na nguvu zenu ebu kafanyeni kazi za kajengeni taifa bana

    wakuja
    (nililetwa dar na mafuriko)

    ReplyDelete
  24. PETER- KARDASHIAN-NALITOLELAFebruary 22, 2011

    NYINYI WOTE NI MBUMBUMBU. NAMAANISHA BONI HIA HIA, NA MR. LIVINGSTONE. HAMNA LOLOTE UCHWARA TU. MIMI NIKIANZA KUMWAGA NONDO ZA CHUO KIKUU CHA UNIVESITI CHA MUZUMBE CHA KULE MOLOGOLO MTASEMA HOO, KASOMA SANA, SIJUI KITUGANI. YOU GOING TO MUZUMBE AND GET YOUR DIGILII IN ECONOMY AND NOT GO TO KALIAKOO AND SELLS KANYABOYA TO MACHINGA PEOPLE. AND COME HERE, BON HIA HIA, SIJUI LIVINGSTONE WAKATI MAJITU YAMEZALIWA MTWARA. YOURS BORING TOO MUCH MR. BONI HIA HIA. I SELLS AISKLIMU TO ALL ZE PEOPLES OF TANZANIA FROM CHINA. MAN, NO ARGUE IN BLOGS OF JAMII. GLOW UP MAN, UBISHI WA HOVYOOO

    ReplyDelete
  25. Kuvaa magwanda sio tatizo inategemea:
    1.Ilikuwa wapi?Ofisini kwa IGP au Kilanjaro Kempski?
    2.Siku gani?Jumatatu au Jumapili?
    3.Ilikuwa Ikulu au wapi?

    Kwa hiyo IGP anavaa magwanda au nguo za kiraia kutokana na matukio.Na hayo mwagwanda yanatofauti kwa rangi kutokana na matukio sio anavaa tu...

    Kwa heriiiii.Mzee wa IFAKARA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...