NA TULICHAKACHUE PATO LA BABU TAFAZALI: MJADALA
Michuzi,
Jana nilijaribu kuchakachua pato la Babu huko Loliondo nika-note yafuatayo.
Mchungaji anachaji 500/- kwa dozi moja ya dawa ambayo anaigawa ifuatavyo.
200/- Anawalipa wachimba dawa porini
200/- Anatoa kama fungu la kumi kwa kanisa lake la Kiluteri pale Usharika wa Wasso-Loliondo
100/- Ni kwa ajili ya yeye kuishi kwani kila mtenda kazi ana haki ya kipato kama biblia na katiba ya nchi vinavyosisitiza.
SASA BASI:-
Kwa sasa hivi kuna watu 8,000 kwa babu ambao wanahudumiwa kabla ya serikali kuruhusu wengine kwenda huko. hii ina maana kwamba hao watu wote wakinywa dawa, Babu ataingiza shillingi millioni nne tu (4,000,000/-) ambayo ataigawa ifuatavyo.
1,600,000/- zitaenda kwa wachimba dawa
1,600,000/- Fungu la kumi kwa kanisa lake
800,000/- (LAKI NANE TU) NDO ANABAKI NAYO.
Maswali ni mengi yanayotokana na huu mlolongo.
- Babu anahifadhi wapi pesa yake kwani
- Je TRA wanaweza kwenda kudai chao pale?
- Je kuna haja ya kudai Pay As You Earn (PAYE) kwa wachimba dawa?
- Wale wachagga walioanza kutoa huduma ya vyakula, choo na mengineyo pale nao wanapaswa kutozwa kodi? (Kumbuka sahani ya wali-nyama mwezi uliopita ilikuwa shilingi 1,000/- tu lakini sasa imepanda mpaka 3,000/-
Niachie hapa na wengine wachangie hii mada. Naomba kuwasilisha
NA MDAU DEOGRATIAS MUSHI WA DAILY NEWS
BABU PESA ANAZIIFATHI WAPI ,MBONA ATUONI. INABIDI ATAFUTE ACCOUNTANT KABISA ! KAMA KWELI DAWA INAFANYA KAZI BABU SEREKALI ITENGENEZE BARABARA NA WANAKIJIJI WAEKEWE ATMS KWENYE KIJIJI CHAKE !
ReplyDeletehata hao vijana wana kisukari?
ReplyDeleteBado kuna watu hawataki kukubali kuwa kuna watu duniani ni wateule wa mungu, wamechaguliwa kuwapatia ufumbuzi watu mbalimbali wenye matatizo. BABU WA LOLIONDO NI MMOJA WAO. Kalley
ReplyDeleteUmasikini ni kitu kibaya
ReplyDeletemaradhi ya mtu ni siri yako na dactar wewe unayeuliza kama wanakisukari any. march 16 06.10pm yanakuhuhusu nini umeambiwa babu anatibu magonjwa sugu 5. mdau wa houston
ReplyDeletekwani vijana huwa hawaugui kisukari? na kwani babu anatibu kisukari pekee? maswali mengine bwana
ReplyDeletembunge wa Loliondo huu ndo wakati wa kuinua wilaya yako
ReplyDeleteMUNGU hajabadilika ni yule yule aliyewatumia watu wa zamani kufikisha ujumbe wake anamtumia MTU huyu kuokoa watu waliokata tamaa.MUNGU mwenye enzi JINA lako libarikiwe.
ReplyDeleteNadhani kuna haja ya kuanza kumtembeza Babu mahospitalini, maana huko ndiko walipojaa wagonjwa,maana wengine hawatoweza kufuka huko, nadhani apatiwe njia ya kumuwezesha kutembelea kila mkoa na kutibia watu mahospitalini. Nadhani waganga na wachungaji wengine wanaoponya watu wajitokeze kila kona,serikali igharamie ujenzi wa barabara sehemu hizo,ndio njia pekee ya kufikisha maendelea vijijini au mnasemaje wadau?Bahati mbaya uchaguzi umepita mwakani...la sivyo babu angetekwa na wapenda madaraka.
ReplyDeleteIna maana Mungu alimpa upeo wa kutibu Babu kwa watu wenye fedha tuu, sasa kama mtu ana shida kweli na ana imani kubwa kabisa kwamba akinywa maji ya babu atapona, lakini hana pesa za kufika huko madongo poromoka na hana fedha cha chakula na maji ya bei mbaya, ata fanya nini hadi apate maji ya "Mungu" au Mungu amechagua weney uwezo wa kufika hikooooo!?
ReplyDeletekwa hali hiyo,hata na mimi kwa babu nitakwenda.wasije wakamdhuru tu babu wa watu,maana bongo wivu mwingi
ReplyDeletekama sio kisukari labda kichumvi babu toa dozi achana na serikali inakubania mchongo wako kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake
ReplyDeleteDawa ya babu haiponyi mie nilikuwa na HIV nimekwenda ili nijitibu na sasa wiki ya tatu nimepima tena na majibu ndio yale yale ya mwaka jana...sasa labda niseme imani sina ama mwenzenu ni kilio maana kufika kwa babu kumenigharimu karibu laki tatu na ndio nilikuwa nimekopa..jamani babu atanufaisha wengine na wengine tutaangamia kwa madeni na magonjwa yasiyopona..
ReplyDeleteTRA hawanatena uwezo wa kukusanya kodi. Tangu Denjamani Nkapa aondoke madarakani na TRA nayo imesinzia. Wanashindwa kukusanya kodi za bidhaa zinazoingia hapo uwani kwao (Bandarini DAR), Kariakoo, Eapoti wataweza kumfikia Babu kule Loliondo??
ReplyDeleteHiyo sahau mkuu....pia kabla hawajafanya uamuzi wa kuzipiga kodi hizo milioni nne za babu(kabla ya kutoa gharama za uendeshaji) watafute mafisadi ambao wanakula mabilioni ya nchi yetu....
HUYU MDAU ALIELETA MADA NAE ANAONEKANA BINGWA WA KUFUATILIA MAISHA YA WATU MTAANI....MAANA ALIVYOMCHAMBUA BABU MM HOI.
ReplyDeleteMIMI NAONA HATUJAJIBU HOJA YA MTOA MADA ALIYE WASILISHA. NAOMBA TUJIBU SWALI NA SIO KULETA STORY ZA ALINACHA HAPA. MASWALI ALIYOULIZA MDAU NI YA MAANA SANA. HATA SISI WENGINE UGHAIBUNI TULIKUWA NA MASWALI KAMA HAYO.
ReplyDeleteMPG BOX
UGHAIBUNI.
Ni hatari kwa sababu ana mashariti na kwamba ana idadi ya kutibu ambayo ni siri yake. Aidha anasema baada ya kumaliza kazi hiyo eti atakufa. Kutibiwa na mtu kama huyo ni hatari. Na tukumbe tu kwamba tunaishi nyakati za hatari na za mwisho hivyo shetani atafanya maigizo ya uponyaji kwa jina la Yesu. Hivyo ni kujihadhari na watu wa jinsi hiyo
ReplyDeleteMnasahau jambo muhimu la afya la hao wanaotumia vikombe kwa kushare. na kama vinaoshwa, vinaoshwa na maji ya moto au ndio hivyo tena.Maana naona vikombe vinaonyesha dalili ya kutu kwa chini.
ReplyDeleteMdau
Mbebabox UK
Kulingana na Maswali mazuri ya mdau aliyo uliza na mjadala kwa ujumla mimi naona Babu tangia ajaanza hiyo Biziness ya upako tayari alikua amesha jipanga kwa uzuri kabisa pesa ziwekwe wapi na zitatumikaje...ingawa mdau hapo umeleta maada na kuchanganua mgao wa pesa haujafafanua data umezichimbia wapi.
ReplyDeletelakini pia TRA hawana nafasi ya kwenda kwa Babu na kumtoza maana hiyo si bizness bali anatoa huduma na wanaolipa wote ni kwa imani na kama asante kwa Babu Ambilikile
Juu ya wachimba dawa mimi naona pia hapa walisha elewana kwa hiyo kulipwa ni haki yao kabisa lakin pia nauhakika kuna wengine wanajitolea kama Babu alivyo oneshwa na Mungu nae akaamua kusaidia wadau.
NA HILI SWALA LA MWISHO NDILO LA MUHIMU SANA JUU YA HUDUMA ZENGINE ZA KIJIJINI HAPO,INAONEKANA KUWA KIJIJI KIMEINGILIWA HILO LA KWANZA LAKINI LA PILI KUPANDA KWA BEI ZA CHAKULA NI SAWA HASA TUKIZINGATIA MSEMO UNAO SEMA MGENI KARIBU MWENYEJI APONE NAMAANISHA KWAMBA HATA WAKIONGEZA BEI KWA KIASI GANI BADO WATAKA HUDUMA WATALIPA TUU...KWA MANA HIYO ISHA KUWA BIZINESS HIYO...YANI CHUKUA CHAKO MAPEMA KABISAA...NA MMH...APA NAONA NI DHAHILI WANAFAIDIKA SANA..HAPO WATACHAJIWA MPAKA GHARAMA ZA MAJI YA BOMBA....
MWISHO MIMI NAWAOMBEA SANA WATU WALIO HUKO PASIJE TOKEA MAGONJWA YA MLIPUKO KAMA WATU WENGI WANAVYO WAZA...KWA PAMOJA TUWAOMBEE...
NAWATAKIA SAFARI NJEMA KWA WALE WOTE WANATARAJIA KWENDA LOLIONDO NA HII HAPA NDIO HALI HALISI
Kulala Popote
Loliondo is about 400 Km from Arusha Town and its rough road
No enough food and water,
No fancy hotels for accommodation,
No network for ease communication,
No toilets around,
Long queues may take a week to be attended.
You need at least two weeks of leave to complete your journey.
hivi jamani babu hachokiii manake kazi anayofanya ni ngumu sana hivo basi ni kweli kabisa atakuwa ametumiwa na Mungu na ndo anayempa nguvu za ziada ila nashindwa kuelewa hizo hela zake anaficha wapi jamani babu watu,pia watu muwe na imani ili muweze pona coz bila imani mtakuwa mnafnya biashara ya kuchemsha mawe wajameni
ReplyDeletetusiwe wasahaulifu walitokea watu wengi kama hawa na kudai ni wateule wa mungu na kudaganya wengi, swali je mnamkumbuka moses kulola alikuwa anaponya magonywa na vilema walitembea
ReplyDeletemponyaji ni mwenyezi mungu pekee hiyo ni kazi ya ibilis na mola wetu mlezi anaangalia nafsi zetu zitaenda wapi
ReplyDeleteMdau wa daily news acha hizo!
ReplyDeleteMbona mahesabu ya DOWANS< KAGODA n.k hujatuletea tujadili?
Mdau
Loliondo.
Baadhi yetu sisi watz ni dhaifu katika kufikiri na hili linajionesha hapa. Babu anacheza na emotions za watu waliodhaifu.
ReplyDeleteInasikitisha sana!
huyu mdau anayesema hajapona HIV me naisi analake jambo..basi tu anataka kudiscaurage watu,we huo mlolongo wote unadhani watu wenye ndugu wenye HIV waliopona kwa dawa ya babu hamna hapo.labda ulifanya ngono zembe chako kimeisha mrudie Mungu utubu.Na huna imani ndo maaana hujapona!Hata Yesu alisema Imani yako ndo itakuponya.
ReplyDeleteWewe untaka kujua anapoziweka hela ili iwe nini? Kwani wewe tunajua unaweka wapi hela zako? Watanzania kwa kufuatilia maisha ya wenzenu? Babu kapata mradi wake na wewe tafuta wa wako sio kukaa na kuanza kuangalia babu anaingiza kiasi gani!!!!!!!
ReplyDeletemdau birmingham
Mimi nasikitika sana na vitu kama hivi kwani africa siku zote watu ni rahisi kuamini kitu bila ya kuwa na uhakika. nailaumu serekali na wizara ya afya.
ReplyDeletebabu anheacha aendelee kutoa huduma lakini serikali na wizara ya afya ingewafuatilia walioprwa huduma kama wapata nafuu kutokana na magonjwa yao lakini wakikaa kimya basi wananchi wataamini.
21 century mgonjwa apimwe kabla ya matibabu na apimwe baada ya maibabu.
poor africa - no knowledge - hata huku ulaya dawa za wachina wateja wake wengi ni waafrika. dawa imeandikwa kichina na unaambiwa inatibu ulcer na unaamini kama mchina kafunga chokaa - poor african na mzungu nunua or believe kitu bila ya uchunguzi. nailaumu wizara ya afya ingefuatilia na kuwasaidia wananchi ukweli na nyia mlioko humo tanzania maneno tu mnaisaidia vipi serlika au kulaumu tu?? acheni sasa kulaumu serikali
Diaspora
London
Hivi kweli 10% ya shilingi 500 ni shilingi 200??? au hesabu zimetupiga chenga jamani?? Wakati natuma hii message, watu 23 wametuma maoni yao, na hakuna hata mmoja aliyeona hiyo??
ReplyDeleteMimi ni mdau wa Ottawa..
hi kama babu dawa zake zinaponya basi mambo mazuri ila hasiwe anchanganya na chemicles /kwani naandika hizi habari nina ushahidi wa kutosha kutoka nchini (usa)na canada na mpaka sasa kuna utata kati ya wagunduzi wa dawa na serikali, kwa hiyo niishauri serikali ifanye vipimo na cha kushangaza kingine kwa nini unanyea dawa mbele yake? nadhani kuna kitu behind the darkness
ReplyDeletewatoa mada wengi wanapoteza lengo sahihi ya mtoa mada. Kuhusu pato la babu. Mimi binafsi sioni kama kuna haja ya kulifuatilia saana kwani TRA wanaowezo wa kupata mapato yao sehemu nyingine kuliko kumfuatilia huyu babu. Pili, aliyeleta maada hii itakuwa jambo la busara kutoa ushauri kama ulioutoa kwa TRA kuchukua pato/ushuru kwa mafisadi na sio kwa mtu kama uliyetueleza ambaye anatoa huduma na ukiangalia kinacho baki mkononi mwake is nothing compare to total earnings.
ReplyDeleteMzee Deo Mushi, vipi na wewe ulienda pata kikombe kwa kujitibu nini? Au wataka punguza hizo nyama uzembe?
ReplyDeletekila mtu na imani yake! wenye kwenda na waende ambao hawana imani basi tulia. malumbano ya nini?
ReplyDeleteWEWE MTOA MADA, WAAMBIE HAO TRA WAMALIZE KUKUSANAYA KODI KWANZA DAR THEN NDO WAENDE KWA BABU,SIKU NYINGINE USILETE HOJA ZA KISHENZI SHENZI
ReplyDeleteWEWE UNAEULIZIA HELA ZA BABU INAONEKANA UNAJUA SANA HESABU !! JAPO HUNA UHAKIKA NA 10% YA SH 500 NI SH NGAPI ??!!!!
ReplyDeleteWAKATI UNAENDELEA KUTAFUTA JIBU YA SWALI LAKO ....
TUPIGIE PIA MAHESABU MENGINE MADOGO !!
GHARAMA ZA KUPANDA KWA UMEME NI ZIMETOKEA WAPI NI DOWANS WANASABABISHA AU ?
KUPANDA KWA MAFUTA (DIESEL & PETROL ) na hela tunazolipa kodi ukilinganisha ..
VITU KUPANDA BEI ,SUKARI, VYAKULA BEI ZAKE HALALI ZINAZOTAKIWA !!
ASANTE.
Sasa wewe naona unamchongea babu kwa TRA, lakini utashindwa katika damu ya Yesu.
ReplyDeleteAlafu babu hapeleki pesa bank wala nini kama mtu amechoka kuishi aende akajaribu au aende hata na wazo kama hilo atajuta
mama avisa
Huyo aliyesema alipata dawa ya babu na bado ana HIV,mwingine alituambia humu kwamba naye alipokunywa dawa alicheck baada ya siku saba kwenye hospitali ya serikali ya mount meru akakutwa NEGATIVE (hana), Mwingine alisema yeye baada ya siku 7 alicheck akakuta bado anao, hakukata tamaa akacheck tena baada ya siku 7 akakuta bado anao, hakukata tamaa akacheck tena baada ya siku 7 zingine akakuta NEGATIVE (hana) hakuamini akaenda kurudia kwenye hospitali nyingine akakuta tena NEGATIVE, Sasa hapa mnatuchanganya hiyo ipo zaidi kiimani au ni vipi?
ReplyDeletekimsingi sio fungu la kumi kama anavyosema mtoa mada babu mwenyewe hakutaja fungu la kumi bali alisema nanukuu sh 200 watachukua wachimbaji na watayarisha dawa sh 100 zake na 300 za kanisa hakutaja mambo ya fungu la kumi mtoamada fanya utafiti usikurupuke
ReplyDeletesasa ukweli ni hivi babu amenukuu dawa hizi kutoka kwenye kitabu cha dr, jim humble's ukisoma hiki kitabu hata wewe utatibu bila wasiwasi dr jim yeye alitibu kwa kemikali na tindikali babu yeye amezitafusiri hizo dawa na kutibu kwa miti sio kama hiyo miti mitatu inapatikana tu luliondo pekee, mie kwa kweli kueni macho na ndiyo maana bei iko chini kwa kutengeneza hizo ni kitu rahisi sana na babu kuna kundi la watu wako nyuma yake kwani vitbu vya dr jim vimandikwa kiinglishi sasa babu kajuaje? kama hakuna mtu nyuma yake wamepanga hiyo bei ili wapate watu wengi kwa muda mfupi,nandiyo maana anasema atakufa kwani anajua watu watakapopata side effect yeye atajiua au mikononi mwa gereza mie nimesoma vitabu vya huyu dr nae alifungua hadi kanisa lake kwa kuwa watu walimwaamini, ndiyo kuna Mungu lakini watu wamemubadilisha Mungu kwa kujilimbikizia mali kitu kingine ndugu zangu hata nasikia woga sasa kusema mbona yule dr alikuwa haunyi mara moja tu????????????na kuna vipimo vyake je babu anapima na nini ili apate 28%ya mixtures ndipo anakupa kidogo kidogo na siku zinavyozidi ndo dose inaongezwa,lakini ya babu ni siku moja poleni sana. mwisho uliza swali nitakuji kwa kupitia nakara ya hivyo vitabu .
ReplyDeleteserikali inapaswa kumuwekea ulinzi mkali sana babu kwa maana wasije kutokea watu wakamkidnap na kuanza kutoza hela nyingi ili wamuachilie
ReplyDeleteunapokunywa yale maji unakunywa babu na ndiyo maana ukienda kupita wasema negative yule anakuwa ni babu sio wewe sasa siku 21 zimepita nenda ukapime watakuta ngoma ndo imezidi kiwango, nk kumbuka uchawi wa kuvalishwa kivuli. jibu utapata.
ReplyDeletemimi nadhani hapa ni imani ya mtu ndio itakayomponya.namaanisha hata mtu kama unaumwa kichwa iwapo waamini ukinywa panadol utapona basi ukinywa kwa imani hiyo kweli utapona.Na mwingine anaamini akinywa labda mwarobaini atapona basi akinywa kwa imani yake hiyo anapona.sasa hapa maswala ni imani yako ipo wapi juu ya dawa hiyo!!!
ReplyDeleteLa msingi ni kumshukuru Mungu kwa yote maana hata wengi wetu tulishatumia madawa ya asili tena bila vipimo maalumu je,yale yamethibitishwa na TFDA???
swala ni imani.
ndio maana kama unatilia shaka basi usiende.Ushauri wangu kwa wale waliokuwa na ushuhuda basi wajitokeze kupima baada ya kunywa dawa wakipata majibu -ve wajitokeze hadharani hii itasaidia sana.
Kiukweli maswala ya imani ya mtu ni magumu jamani.Ila tu tusijisahau sana kama tu wafuatiliaji basi hata katika vitabu vya dini tunaona imeandikwa Mungu alitumia watu mbali mbali kuwapa maagaizo ya kuponya wengine.na ilikuwa.ila kwa kizazi hiki ni ngumu watu kuelewa maana hali halisi tunayoishi ni ya utata mtu.
Tuzindi kumuomba Mungu atufunulie mapokeo haya kwa namna ya kipekee ili ukweli ujulikane mapema zaidi na kuondoa utata miongoni wa wanadamu.
Jamani kwanini mnakuwa kama Tomaso?hamuamini mpaka muone sura ya Mungu?....Mnaikumbua habari ya NUHU na waliomkaidi?.....hebu kila mtu achukue dk tano kufikiri yeye ni nani,binafsi unajijua ulizaliwaje au utakufaje?....ni wengine ndio washuhudiaji. Mafumbo ya Mungu binadamu hawezi kuyafumbua...kama unaamini kuwa Mungu yupo na hujamuona na mbona usiamini kuwa anafanya mengi juu yako kwa kuwatumia wengine?Tumemsahau anataka Tumkumbuke...sisi ni wadhaifu...tuombe hekima yake
ReplyDeletewatu wengine bwana!! kwani ww unapoweka hela zako nani anakuuliza? au mchanganuo wa mapato yako ya halali na ya uwizi nani kakuuliza?? acha udaku wewe, let babu be. huamini usiende full stop. hili ni swala la imani zaidi. Hao wakina shehe yahya wakiagua nani anaenda thabitisha hospitali? why babu akiponya mnataka uthibitisho wa hospitali? nani kawahi kumuuliza shehe yahya au mganga yoyote mapato yake? au wapi wanaweka. stop hating jamani.MUNGU YUPO!!!
ReplyDeletenakuja na hili babu kasema anawasaidizi kumi na yeye wa kumi na mo hata akifa bado tuna hawa kumi mpaka kumi wafe basi kila mtanzania atakuwa amepata dawa!!!!!na pia kabla ajafa mwambie babu amrithishe mtumishi mmoja najua tatizo la babu, anawaondoa wakati wa kuchanganya hizi dawa tatu. na wote kumi wakifa basi ndipo mie nitakuja kutoa ila nitakuwa mjini na ninahitaji eneo kubwa kwani gharama zangu itakuwa mbuzi mmoja tu ,na babu kama anitengei fungu langu basi mie na yeye kwani kaiba haki miliki.
ReplyDeleteHIVI HII SERIKALI YA WATANZANIA HAINA MAABARA ZA KUWEZA KUJARIBU HIZI DAWA KUHAKIKISHA UBORA NA USALAMA WAKE?
ReplyDeleteje wewe unaijua vizuri computer?kama unajua basi nitakuonyesha web site usome dawa za babu ukisha soma ndo utajua ukweli huko wapi sasa hivi naondoka kwenda kunywa gahawa kidogo nitarudi baadae.thx
ReplyDeleteMi naona babu asilipe income tax sababu yeye ni Mstaafu ila kanisa lilipe 10% ya kipato wanacholipwa na babu au zitumike kutengeneza vyumba vya wagonjwa wanaosubiri tiba. Wale watafuta dawa ni vibarua ambao hawalipi kodi sababu ni off book job.
ReplyDeleteWenye mahotel hao ndo wakamatwe hasa, wapangiwe bei ya vyakula na wakizidisha wafungiwe biashara zao ila kodi walipishwe kila siku kama wale wa sokoni. Wenye usafiri wapangiwe bei kabisa ili wasidhurumu. Na wale wanaopata tiba waweke fungu zaidi ambalo si la babu bali ni kama hasante kwa kijiji ambalo litanufaisha wakazi wa pale na mazingira. Hayo ndo mawazo yangu mdau.
Yesu aliwalisha watu maelfu mikate na samaki iweje babu ashindwe kuwatibu watu wa Mungu mmezoea kudanganywa muacheni Mungu aitwe Mungu amemteua mtumishi wake kuokoa watu wake.george k
ReplyDeleteMnakumbuka ya kina Kibwetere,Georgetown,Waco Texas etc?
ReplyDeletenimerudi ,hata kwenye vitabu vya dr, kuna masharti ya dawa kuwa husinye citrus juices wakati unapokunywa dawa kwamba inanutrolize dawa ,ukija kwa babu anasema husinye pombe ukizichambua hizi story mbili zote zinamaana moja,kitu kingine nimegundua babu amenda shule ila alihamua kurudi maisha ya chini(mwanakijiji) hii ya babu iliibuka nchini mali miaka minne iliyopita nadhani tayaari alikuwa amenunua kitabu cha dr.
ReplyDeletenaungana na mdau wa diresbora wa london, kuwa sisi kuamini ni sec kwani hata yule dr alipendekeza kuwa dawa yake ya kwanza inatibu maralia ni kwamba alitarget africa na njaa zetu tutanunua tu na baadae alipopata soko akasema inatibu magonjwa yote yaliyoshindikana nyie kunyuni tu mfano indosia kuna maajabu sana mtu anaota mti mwilini nakuota mizizi si ndo dawa zenyewe hizo.
ReplyDeleteSerikali itengeneze utaratibu...kwanza priority wapewe watu ambao ni wagonjwa sana.Halafu kwa watanzania ndo wapewe kipaumbele.Si unajua sisi watanzania ndo wenye matatizo mazito zaidi kuliko mataifa mengine
ReplyDeleteWabongo ndio maana tunanywishwa dawa zisizo na mbele wala nyuma. Mtu kauliza swali zuri sana kuhusu kodi ya mapato ambayo huwa ni ya ajabu na wengine hawalipi kabisa ndio maana hatuendelei. Majibu ya wengi ni yakujiuliza with this attitude tutafika kweli? Mnakalia hela za mafisadi mafisadi....Tuanze na kila mahali...Kila mtu alipe share yake...Transactions bongo za cash cash in millions ni za kusikitisha....Mtu ananunua gari million 60 cash ...Je alilipa ushuru kweli? aliipata wapi hiyo hela na aliilipia ushuru? Vitu viiingi ndio vinatufanya tuwe nyuma tu...WEnzetu wanajenga nchi zao kwa koi siye twangoja misaada
ReplyDeleteMimi naamini sana lakini kuna mambo ambayo sitayaamini kama hiyo dawa ni ya kuchimba angeficha recipe na kuwaambia watu unywe na na umwombe Mungu akuesaidie kwa vile hata dawa za hospital bila Mungu huwezi kupona. Lakini kitendo cha kuwanywisha watu dawa tu na kuendelea na safari hivi? Kwanini asifanye kwa watu wachache tu halafu tuone majiibu baada ya muda ndio iwe hivi? kwanini watu wooote hawa kwa mara moja tu.....Na tusubiri miezi sita mje mtupe majibu...Huyu babu anachezea desperate people...
Imani ya mtu ndo-itakayomponya. MZALENDO WA UK unayetaka serikali iingilie kati-swali... kwani hizo dawa zinazonyweka kwa waganga wa kienyeji zinapimwana nani? na mbona baadhi ya watu kutokana na imani yao wanakunywa na wanapona....! acha hizo au kwasababu unabeba mabox huko unadharau wataalamu wa home...
ReplyDelete