Home
Unlabelled
JK atembelea kikosi cha Anga cha JWTZ Air wing leo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
"Chadema mnaiona hii? endeleeni na uchokozi wenu tu."
ReplyDeletesasa JK mbona unaniangusha unaendaje kutembelea Jeshi na Suti hhahahahah vaa gwanda kama za chadema bwana mbona unaleta USHARUBARO kwenye kazi
ReplyDeleteMwaka 1978 nilikuwepo Uwanja wa Taifa DSM wakati wa sherehe ile ya kusherekea kushinda vita vya Kagera. Ndege tatu za kijeshi zilipita juu kutoa saluti. Baada ya dakika chache moja ilirudi lakini mwendo wake ulipungua halafu ilianza kulala pembeni na hatimaye kuanguka! Siwezi kusahau. Tulikabwa na moshi watoto wadogo walilia hakuna aliyejua la kufanya. Ndgee ilianguka nje ya uwanja. Marubani wawili wa JWTZ walikufa katika ajali hiyo, moja alikuwa anaitwa Karama kutoka Pemba. Nimesahau jina la huyo mwingine. Natumaini hizo ndege za sasa ni imara zaidi na zitatunzwa vizuri na jeshi letu JWTZ.`
ReplyDeleteHaswaaa babaaa,mnaiona hiyo, mambo no no-flying zone hakuna hapa...unafanya mchezoo
ReplyDeletesijakuelewa wewe aliye toa maoni hapo juu Kwani chadema ina uhusiano gani na ndege za kijeshi chadema wapo ndani ya nchi chadema wakivunja sheria basi watashughulikiwa kisheria siyo unavyo dhani kuwa wakifanya fujo watashughulikiwa na ndege za kijeshi hapana sheria zipo
ReplyDeleteAnony wa kwanza hapo juu....
ReplyDeleteChadema wenyewe hata kwenye kiganja hawajai, ndege zote hizo za nn?
Yaani Michuzi unaachia hiyo comment hapo juu bila kuangalia umuhimu wake au unafurahia..Wakisema wtu wengine unaona raha ikiwa upande CCM unatupa maoni..WEwee ni mtu mmoja hatari sana. Utupe hii ujumbe umeupata
ReplyDeletechadema hawana hadhi ya kuletewa ndege mkwara wa msajili unatosha kwao chama kinafutwa tu kirahisi na uchaguzi ujao hawatagombea vilevile na kesi ya uhaini juu nani mshindi?waendelee kupiga chapuo lao watu wanawaangalia tu unafikiri afrika kunademokrasia umafya tu ni watu wadogo sana hao waendelee kuuchonga tu wala sio wakwanza hao wamshukuru sana tuna raisi mwenye uelewa mkubwa mm nisingewakawiza kabisa wala huko walipo anzia mwanza wasingekanyaga maandamano ya amani yana matusi? na vitisho?uliona wapi mkia wambuzi ukamkuna mbuzi mgongoni?
ReplyDeleteAcha bwana kutisha watu,inahusianao gani hiyo na Chadema? ninyi ndio maleta diyo siyohumu ndani. hujui kama huyo ni amiri jesh mkuu(kwa msisitizo) "commander inchief",
ReplyDeleteHIZI NDEGE ZA KIZAMANI KWELI, ANGALIENI KWENYE YOUTUBE AU GOOGLE MTAZIONA. WACHINA WALIIGA MIG 21 ZA WARUSI, HIZI NDEGE ZINAITWA J7
ReplyDeleteKweli kabisa mtoa maoni hapo juu, inaelekea TZ tumekuwa jalala la kutupia ndege za kizamani ambazo hata huko kwao hawazitumii tena hata kwa mafunzo tu achilia mbali mazoezi, Why??? Anyway, ni umaskini wetu ndo unaotusumbua, maana kama tunashindwa hata kununua mitambo mipya ya kuzalisha umeme tutaweza kununua ndege mpya na za kisasa!!!!
ReplyDeletewe chemi sio 1978 ile ilikua 79
ReplyDeleteHabari yako . Nijaribu kufanya utafiti kuhusu hii ajari ya 1979 . Nitaipata wapi ? naomba uwasiliane nami hapa alex.office@yahoo.com au Majina wa hao Marubani
DeleteNaomba data tafadhali alex.office@yahoo.com
DeleteMHESHIMIWA RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA/TANGANYIKA "DR" J. KIKWETE UKIWA KAMA [MWANAJESHI MSTAAFU]UMEPENDEZA SANA NA SUTI YAKO. NA HII NDEGE INAPENDEZA SANA "IMEPIGWA RANGI NZURI " YA [KIJANI]"TENA KWENYE ENGINE".VIONGOZI WANAPENDA VITU "VINAVYOPENDEZA/PIGWARANGI"
ReplyDeleteDada Chemi ile ilikuwa 1979, siku ya mashujaa wakati ule ilikuwa Septemba Mosi ndio tunaadhimisha. Ila umetukumbusha mbali sana asante kwa kumbukumbu murua ya sikukuu ya mashujaa. Nakumbuka pia Mzee Kawawa alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kwenda kwenye tukiola ajali huku farasi wakizunguka kuzuia watu kusogelea eneo la ajali. Ule moto uliowaka sijapata kuuona maishani.
ReplyDeleteMimi nilikuwa kati kati ya uwanja nikiwa mmojawapo wa watoto walioshiriki halaiki kwenye hafla ile. Tena kulikuwa na watoto kutoka Tanzania nzima kuanzia Bukoba mpaka Pemba, na inasemekana huyo rubani alijitahidi hiyo ndege isiangukie uwanjani, yaani huo msiba wake sijui ungekuwaje. Ilikua baridi na tulipatwa na hofu ya ajabu, lakini kwa kuwa tulikuwa chini ya uangalizi wa wanajeshi shupavu na makini ambao ndio walikuwa wakufunzi wetu, hakuna mtu aliyekimbia hovyo au kutaharuki pale kati kati ya uwanja, tulitulia tuli kama tumemwagiwa maji. Hebu fikiria ingekuwa ni zama hizi za sasa watu hawaambiliki watoto hawasikii ndio kwanza wangekimbia uwanjani hovyo na watu wengi wangekufa kwa kukanyagana na kusongamana, maana hiyo siku uwanja ulikuwa umefurika!
ReplyDeleteMungu awarehemu marubani wale na kuwapa makazi mema peponi kwa kuokoa maisha yetu pamoja na wao walijua kuwa wanakufa.
Mtu mwingine nakumbuka alikuwa mle ndani yeye alikuwa kamanda wa chipukizi ni Vitalis Gunda!
Haya ni za kizamani ukweli ni kuwa ndege mpya hatuwezi kuzi afford. Ndege za kivita zina bei mbaya sio sawa na magari na electronics nyingine.
ReplyDeleteAsanteni kwa sahisho ni kweli ilikuwa 1979 nikwa Form 3 Zanaki. Ingekuwa vizuri mwandishi wa habari atafute watu waliokuwepo pale uwanjani na kuwahoji. Nilikuwa katika ile kundi la Wanawake 1000. Sidhani kama tulifka 1000. Ile T-Shirt ya Pamba nzito kama Terry cloth ambayo tulilazimisha kununua na kuvaa nilikaa nayo miaka mingi!
ReplyDeleteKuhusu hizo ndege, kama mdau alivyosema hapo juu hawawezai kutuuzia ndege nzuri up to date.
Kwanini tusiende kujichagulia wenyewe wakati hela tunazo? Si juzi tu Soud Arabia walikua wana show ya kuonyesha vifaa vay kijeshi vipya. Na vinazoom kila kona na kuona kila kitu. Na ni the latest kama tuna million 90 za kuwakopesha wabunge means tunazo nyingi zaidi za kuinverst kwenye ulinzi.
ReplyDeleteHuyo Mwiangine aliyefariki alikuwa ni Kaka wa classmet wangu huko Cheyo primary shool Tabora . Thanks umenikumbusha mbali sana ilikuwa masikitiko sana kwa watu wote na rafiki yangu pia. Sijui hata huyo dada yupo wapi tena.
ReplyDeleteGademu!!! tumekwisha kwa kweli - Wachina wenyewe wameacha kuzitengeneza hizi ndege mwaka 2008 baadaya kuzitengeneza kuanzia 1966. Angalau tungekuwa na tu F16 tuwili tutatu hivi tungeweza kuweka "no fly zone" siku ambayo CCM na serikali yake wakianza kutufanyia kama Gadaffi!
ReplyDeleteLakini kweli Rais wa Jamhuri ya Muungano alihitaji kupanda humo ndani au ndio alikuwa anatimiza 'ndoto zake' nyingine za angalau katika maisha yake ajisikie kuwa ni "pilot"?
Tunataka kujenga taifa la kisasa lakini hatutaki kuweka ulinzi wa kisasa wa taifa hilo zaidi ya kupigana mikwara kila kukicha!
wewe michupi kuwa muazi usiwe fisadi mficha uchi hazai ukeli utabaki ukweli tu mzee abudu jumbe alinunuwa vifaa vya kivita zikiwemo ndege 6 na vitenk mwalimu aliamuru viondoshe zanzibar kwa usalama hakuna asiye juwa hili hata mama yako anajuwa muulize kama huwezi kazi ya uandishi tafuta fani nyegine muuadishi huwa anajiamini na kazi anayoifanya
ReplyDelete