Mtaalamu Msaidizi na Rubani wa ndege za kijeshi katika Jeshi la China Plt. Gao, akimfahamisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete matumizi ya kitaalam ya urushaji wa ndege ya kijeshi JW 9242 F 7 G kutoka China, wakati Rais alipotembelea kikosi cha Anga cha JWTZ Airwing Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrishi Kikwete, akiteremka kutoka kwenye ndege ya kijeshi ya JWTZ JW 9242 F 7 G kutoka china wakati alipotembelea kikosi cha Anga Airwing Dar es salaam leo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ndege ya kijeshi JW 9242 F 7 G wakati alipotembelea kikosi cha Anga cha JWTZ Airwing Dar es salaam leo.Picha na Amour Nassor VPO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. "Chadema mnaiona hii? endeleeni na uchokozi wenu tu."

    ReplyDelete
  2. sasa JK mbona unaniangusha unaendaje kutembelea Jeshi na Suti hhahahahah vaa gwanda kama za chadema bwana mbona unaleta USHARUBARO kwenye kazi

    ReplyDelete
  3. Mwaka 1978 nilikuwepo Uwanja wa Taifa DSM wakati wa sherehe ile ya kusherekea kushinda vita vya Kagera. Ndege tatu za kijeshi zilipita juu kutoa saluti. Baada ya dakika chache moja ilirudi lakini mwendo wake ulipungua halafu ilianza kulala pembeni na hatimaye kuanguka! Siwezi kusahau. Tulikabwa na moshi watoto wadogo walilia hakuna aliyejua la kufanya. Ndgee ilianguka nje ya uwanja. Marubani wawili wa JWTZ walikufa katika ajali hiyo, moja alikuwa anaitwa Karama kutoka Pemba. Nimesahau jina la huyo mwingine. Natumaini hizo ndege za sasa ni imara zaidi na zitatunzwa vizuri na jeshi letu JWTZ.`

    ReplyDelete
  4. Haswaaa babaaa,mnaiona hiyo, mambo no no-flying zone hakuna hapa...unafanya mchezoo

    ReplyDelete
  5. sijakuelewa wewe aliye toa maoni hapo juu Kwani chadema ina uhusiano gani na ndege za kijeshi chadema wapo ndani ya nchi chadema wakivunja sheria basi watashughulikiwa kisheria siyo unavyo dhani kuwa wakifanya fujo watashughulikiwa na ndege za kijeshi hapana sheria zipo

    ReplyDelete
  6. Anony wa kwanza hapo juu....
    Chadema wenyewe hata kwenye kiganja hawajai, ndege zote hizo za nn?

    ReplyDelete
  7. Yaani Michuzi unaachia hiyo comment hapo juu bila kuangalia umuhimu wake au unafurahia..Wakisema wtu wengine unaona raha ikiwa upande CCM unatupa maoni..WEwee ni mtu mmoja hatari sana. Utupe hii ujumbe umeupata

    ReplyDelete
  8. chadema hawana hadhi ya kuletewa ndege mkwara wa msajili unatosha kwao chama kinafutwa tu kirahisi na uchaguzi ujao hawatagombea vilevile na kesi ya uhaini juu nani mshindi?waendelee kupiga chapuo lao watu wanawaangalia tu unafikiri afrika kunademokrasia umafya tu ni watu wadogo sana hao waendelee kuuchonga tu wala sio wakwanza hao wamshukuru sana tuna raisi mwenye uelewa mkubwa mm nisingewakawiza kabisa wala huko walipo anzia mwanza wasingekanyaga maandamano ya amani yana matusi? na vitisho?uliona wapi mkia wambuzi ukamkuna mbuzi mgongoni?

    ReplyDelete
  9. Acha bwana kutisha watu,inahusianao gani hiyo na Chadema? ninyi ndio maleta diyo siyohumu ndani. hujui kama huyo ni amiri jesh mkuu(kwa msisitizo) "commander inchief",

    ReplyDelete
  10. HIZI NDEGE ZA KIZAMANI KWELI, ANGALIENI KWENYE YOUTUBE AU GOOGLE MTAZIONA. WACHINA WALIIGA MIG 21 ZA WARUSI, HIZI NDEGE ZINAITWA J7

    ReplyDelete
  11. Kweli kabisa mtoa maoni hapo juu, inaelekea TZ tumekuwa jalala la kutupia ndege za kizamani ambazo hata huko kwao hawazitumii tena hata kwa mafunzo tu achilia mbali mazoezi, Why??? Anyway, ni umaskini wetu ndo unaotusumbua, maana kama tunashindwa hata kununua mitambo mipya ya kuzalisha umeme tutaweza kununua ndege mpya na za kisasa!!!!

    ReplyDelete
  12. we chemi sio 1978 ile ilikua 79

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari yako . Nijaribu kufanya utafiti kuhusu hii ajari ya 1979 . Nitaipata wapi ? naomba uwasiliane nami hapa alex.office@yahoo.com au Majina wa hao Marubani

      Delete
    2. Naomba data tafadhali alex.office@yahoo.com

      Delete
  13. MHESHIMIWA RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA/TANGANYIKA "DR" J. KIKWETE UKIWA KAMA [MWANAJESHI MSTAAFU]UMEPENDEZA SANA NA SUTI YAKO. NA HII NDEGE INAPENDEZA SANA "IMEPIGWA RANGI NZURI " YA [KIJANI]"TENA KWENYE ENGINE".VIONGOZI WANAPENDA VITU "VINAVYOPENDEZA/PIGWARANGI"

    ReplyDelete
  14. Dada Chemi ile ilikuwa 1979, siku ya mashujaa wakati ule ilikuwa Septemba Mosi ndio tunaadhimisha. Ila umetukumbusha mbali sana asante kwa kumbukumbu murua ya sikukuu ya mashujaa. Nakumbuka pia Mzee Kawawa alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kwenda kwenye tukiola ajali huku farasi wakizunguka kuzuia watu kusogelea eneo la ajali. Ule moto uliowaka sijapata kuuona maishani.

    ReplyDelete
  15. Mimi nilikuwa kati kati ya uwanja nikiwa mmojawapo wa watoto walioshiriki halaiki kwenye hafla ile. Tena kulikuwa na watoto kutoka Tanzania nzima kuanzia Bukoba mpaka Pemba, na inasemekana huyo rubani alijitahidi hiyo ndege isiangukie uwanjani, yaani huo msiba wake sijui ungekuwaje. Ilikua baridi na tulipatwa na hofu ya ajabu, lakini kwa kuwa tulikuwa chini ya uangalizi wa wanajeshi shupavu na makini ambao ndio walikuwa wakufunzi wetu, hakuna mtu aliyekimbia hovyo au kutaharuki pale kati kati ya uwanja, tulitulia tuli kama tumemwagiwa maji. Hebu fikiria ingekuwa ni zama hizi za sasa watu hawaambiliki watoto hawasikii ndio kwanza wangekimbia uwanjani hovyo na watu wengi wangekufa kwa kukanyagana na kusongamana, maana hiyo siku uwanja ulikuwa umefurika!

    Mungu awarehemu marubani wale na kuwapa makazi mema peponi kwa kuokoa maisha yetu pamoja na wao walijua kuwa wanakufa.

    Mtu mwingine nakumbuka alikuwa mle ndani yeye alikuwa kamanda wa chipukizi ni Vitalis Gunda!

    ReplyDelete
  16. Haya ni za kizamani ukweli ni kuwa ndege mpya hatuwezi kuzi afford. Ndege za kivita zina bei mbaya sio sawa na magari na electronics nyingine.

    ReplyDelete
  17. Asanteni kwa sahisho ni kweli ilikuwa 1979 nikwa Form 3 Zanaki. Ingekuwa vizuri mwandishi wa habari atafute watu waliokuwepo pale uwanjani na kuwahoji. Nilikuwa katika ile kundi la Wanawake 1000. Sidhani kama tulifka 1000. Ile T-Shirt ya Pamba nzito kama Terry cloth ambayo tulilazimisha kununua na kuvaa nilikaa nayo miaka mingi!

    Kuhusu hizo ndege, kama mdau alivyosema hapo juu hawawezai kutuuzia ndege nzuri up to date.

    ReplyDelete
  18. Kwanini tusiende kujichagulia wenyewe wakati hela tunazo? Si juzi tu Soud Arabia walikua wana show ya kuonyesha vifaa vay kijeshi vipya. Na vinazoom kila kona na kuona kila kitu. Na ni the latest kama tuna million 90 za kuwakopesha wabunge means tunazo nyingi zaidi za kuinverst kwenye ulinzi.

    ReplyDelete
  19. Huyo Mwiangine aliyefariki alikuwa ni Kaka wa classmet wangu huko Cheyo primary shool Tabora . Thanks umenikumbusha mbali sana ilikuwa masikitiko sana kwa watu wote na rafiki yangu pia. Sijui hata huyo dada yupo wapi tena.

    ReplyDelete
  20. Gademu!!! tumekwisha kwa kweli - Wachina wenyewe wameacha kuzitengeneza hizi ndege mwaka 2008 baadaya kuzitengeneza kuanzia 1966. Angalau tungekuwa na tu F16 tuwili tutatu hivi tungeweza kuweka "no fly zone" siku ambayo CCM na serikali yake wakianza kutufanyia kama Gadaffi!

    Lakini kweli Rais wa Jamhuri ya Muungano alihitaji kupanda humo ndani au ndio alikuwa anatimiza 'ndoto zake' nyingine za angalau katika maisha yake ajisikie kuwa ni "pilot"?

    Tunataka kujenga taifa la kisasa lakini hatutaki kuweka ulinzi wa kisasa wa taifa hilo zaidi ya kupigana mikwara kila kukicha!

    ReplyDelete
  21. wewe michupi kuwa muazi usiwe fisadi mficha uchi hazai ukeli utabaki ukweli tu mzee abudu jumbe alinunuwa vifaa vya kivita zikiwemo ndege 6 na vitenk mwalimu aliamuru viondoshe zanzibar kwa usalama hakuna asiye juwa hili hata mama yako anajuwa muulize kama huwezi kazi ya uandishi tafuta fani nyegine muuadishi huwa anajiamini na kazi anayoifanya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...