Waziri wa Maliasili na Utalii, na Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mh. Ezekiel Maige akiiangalia kwa umakini jinsi dhahabu inavyosafishwa na mmoja kati ya Wachimbaji wadogo wa Dhahabu wa Mwazimba alipofika mgodini hapo jana. .Waziri wa Maliasili na Utalii, na Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mh. Ezekiel Maige akinyanyuliwa mikono juu kwa furaha huku wakiimba mkombozi! mkombozi! na Wachimbaji wadogo wa Dhahabu wa Mwazimba mara baada ya kuwasili mgodini kwao jana.Waziri wa Maliasili na Utalii, na Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mh. Ezekiel Maige akinyanyuliwa mikono juu kwa furaha huku wakiimba mkombozi! mkombozi! na Wachimbaji wadogo wa Dhahabu wa Mwazimba mara baada ya kuwasili mgodini kwao jana.Wachimbaji wadogo wa Dhahabu wa Mwazimba wakiwa wamepanda juu ya mti ili kuweza kumuona Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wao wa Jimbo la Msalala, Mh. Ezekiel Maige aliyefika katika mgodi wao jana kutatua kero ya mgogoro wao na Kampuni ya Barric.

MKOMBOZI MKOMBOZI! NDIZO SAUTI ZILIZOSIKIKAWAKATI Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alipotembelea jamii ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika jimbo la uchaguzi la Msalala, ambalo yeye ni mbunge.

Waziri alitembelea eneo hilo kufuatia malalamiko ya wachimbaji hao wa Mwazimba, kudai hivi karibuni kuvamiwa na Askari Polisi na Maafisa wa BARRIC waliokuwa na silaha za moto na mabomu wakidai kwenda kuitekeleza opererasheni ya kufukia mashimo ya wachimbaji licha ya kuwepo kwa agizo la Mhe. Waziri wa Nishati na Madini, MHe. William Ngereja kutaka wachimbaji hao wasisumbuliwe katika eneo hilo.

aakihutubia wananchi hao jana, Maige alisema kuwa kuna watu wamefanya ndivyo sivyo kutokana na nguvu ya fedha ya kampuni ya BARRIC kuipoka haki ya wachimbaji wa Mwazimba na kumtaka Mhe. Ngereja kuchunguza watu wake.

Akihutubia wananchi hao Maige alisema, “Katika sakata hili sitegemei lugha tofauti, nitahakikisha kwa gharama yoyote nasema kwa uwazi hata kama utanigharimu, BARRIC hawaitakii mema serikali kwakuhangaisha wananchi wake wenye njaa, nami sitakata tama kupambana nao kwa gharama zozote, eneo hili ni halali yenu haki itendeke,” alisema Mhe. Maige.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. tunahitaji viongozi kama hawa wanaosimama upande wa wananchi katika masuala ya msingi. kama eneo ni la wachimbaji wadodo wadogo iweje hawa barrick wanaingilia. endelea bwana mh maige umasikini hauji kwa kuwasikiliza wazungu ila kwa kufanya kazi kwa upendo wa taifa letu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...