Mhe Anne Makinda akifafanua kuhusu jina lake sasa hivi hoteli ya Millenium mjini Bagamoyo. Kulia ni Naibu Spika Mh. Job Ndugai na shoto ni Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubu Mukajanga

Spika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania Mh. Anne Makinda ametoa ufafanuzi mahususi leo kuhusu jina lake lililokuwa aidha linaandikwa Anna ama Anne, na amesema kuwa jina lake ni Anne.

Mh. Makinda ametoa ufafanuzi huo, akijibu swali la Globu ya Jamii, baada ya kufungua semina ya siku mbili ambayo Bunge limeandaa kwa waandishi wa habari katika hoteli ya Millenium mjini Bagamoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Na mimi ni Kajubi Mukajanga sio Kajubu Mukajanga.

    ReplyDelete
  2. Hii kali kuliko, maana Mheshimiwa Spikaa ANNE sio ANNA, alikuwa katika ngazi ya uongozi tangu miaka ya themanini, ENZI ZA MWALIMU, na siku zote hizo tukimjua kwa jina la ANNA MAKINDA, kuna nini ambacho kimesababisha hadi atoe ufafanuzi wa linavyotamkwa jina lake leo hii?
    Hivi hata CCM waliompitisha kugombea Uspika nao walikosea kumuweka mtu ambaye nao walikuwa hawajui kutamka jina lake?
    Kumejiri nini jamani hadi LEO 2011 atufafanulie jina lake.
    Hata hivyo hilo la ANNE nalo limekaa vizuri Mheshimiwa ANNA MAKINDA, nalitaja kwa mara ya mwisho.

    ReplyDelete
  3. hayo ni matamshi tu, jina ni lile lile.

    ReplyDelete
  4. Hilo ni jina tu na ndivyo lilivyo sema tu watu walikuwa wanaliandika kimatumbi zaidi ila yeye anataka kizungu

    ReplyDelete
  5. so what if its Anne or Anna?ina impact gani kwa maisha ya watanzania wa kawaida?

    ReplyDelete
  6. we anony Fri Mar 11, 04:20:00 PM 2011, jina la mtu ni kitambulisho muhimu mno. umuhimu wa matamshi na herufi sahihi katika jina kamwe hauwezi kuhusishwa na siasa.
    mie ni mtanzania wa kawaida lakini ukikosea jina langu tena kwa makusudi, huwa nasononeka sana.

    ReplyDelete
  7. NA MIMI NAITWA MASOUD SIO MASSUD WALA MASSUDI SAWA HAPOO

    ReplyDelete
  8. Mama ngoja tukueleweshe na wewe umri wote huo siku zote hujui kwamba ANNA na ANNE ni jina hilo hilo moja tu. Ukisema ANNE unalitamka jina hilo kwa Kifaransa na ukisema ANNA unalitamka jina hilo kwa kiingereza. Kila lugha ina jinsi ya kulitamka jina mfano Peter (kiingereza)au Pierre (kifaransa.Anthony (kiingereza)au Antoine(Kifaransa).Francis (kiingereza)au Francois (kifaransa). Mama usiseme watu wanakosea jina lako bali useme kuwa unapendelea jina lako litamkwe na kuandikwa kwa kifaransa ANNE badala ya kutamkwa na kuandikwa kwa kiingereza ANNA.

    ReplyDelete
  9. Hiyo ni pronunciation tu, Kwanza sasa hivi alivyobadilisha spelling hiyo anne kimatumbi watasema ennai au anni badala ya anne kama anavyotaka...

    well ni jina lake na ana uhuru wa kulibadili atakavyo ...ulaji kwa watunzi wa vitabu vya historia na shule b print new books...mu discontinue vyooote vyenye jina la zamani ...hhhhaaaaaa hhhh

    ReplyDelete
  10. Anna \a(n)-na\ as a girl's name is pronounced AN-ah. It is of Hebrew origin, and the meaning of Anna is "He (God) has favored me".

    ReplyDelete
  11. be out of the country you will know the meaning of correct spellings of your name,utakaponyimwa huduma muhimu kutokana na spelling moja kwenye cheti chako au viambatanisho vyako kuwa tofauti na pasport yako utaimba inde monii,utajua nini anachozungumzia

    ReplyDelete
  12. MUHESHIMIWA SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA TANZANIA/TANGAYIKA "A. MAKINDA"

    JINA NILAKO UNAHAKI YA KUBADILISHA HERUFI KWENYE JINA HAKUNA MATATIZO.

    KUMBUKA KWAMBA KUNAWATAKAO KUITA "ANNA" (WAKIMAANISHA ANNE) KUTEGEMEA NA LAFUDHI YA KABILA YAO/MAZINGIRA YAO HASWA WATANZANIA WA VIJIJINI[USIKASIRIKE]. VITABU/MAGAZETI/MAJARIDA/ VILISHAANDIKWA KWASABABU UNAHISTORIA NDEFU KWENYE SERIKALI.

    HAPO BADO WACHINA, KWASABABU WAMEJAA HAPO TANZANIA, NA SIJUI KAMA UMEWASILIANA NAO JINSI YA KULIANDIKA "KWA KICHINA NA KULITAMKA"

    SITAKI KUZUNGUMZIA "WAHIDI" JINSI WATAKAVYOLITAMKA/LIANDIKA.

    ""NAKUSIHI MWAMINI MUNGU ALIYEZIUMBA MBINGU NA NCHI"" NA HAYO MENGINE UTAZIDISHIWA.

    ReplyDelete
  13. Anony wa 10:54 Ni kweli kabisa, Lucy ni Kiingereza, Kifaransa inaandikwa Lucie lakini matamshi ni yale yale.

    ReplyDelete
  14. Ni kweli, tofauti ya herufi moja kwenye jina inaweza kukulazimu kutoa kiapo na sio nje ya nchi tu, ni suala la kisheria. Ila Mama yetu umechelewa sana kutufafanulia.

    ReplyDelete
  15. Jamani sasa yeye si anataka kuitwa ANNE hata kama ni kifaransa au kijapani. Mimi naitwa Ndunguru embu nisaidieni wadau kuliweka hili jina kifaransa zaidi...Ndunguree

    ReplyDelete
  16. Ndunguru kwa kifaransa litaatamkwa hivyo hivyo ila kimaandishi litandikwa Ndoungourou.

    ReplyDelete
  17. mbona unachagua maoni ya kuweke, unatunyima uhuru wa kuchangia hoja, hujawahi ku-post maoni yangu, kulikoni? Usichague kwani sio mawazo yako ingawa ni libeneti lako michuzi akaaaa

    ReplyDelete
  18. Nyie mnao jifanya wataalam wa lugha ni waulize mfano mtu unaenda kuomba visa ya kusoma nje,pass yako umeandika anne,dokoments za shule anna,je una fikiri watu wa ubalozi watakupa viza,no utaonekana unatumia dokoments za mtu mwingine kuomba viza,sasa ndo kusema utakuja na hizo arguments zako za lugha...acheni hizo jina ni id its should stand as it is in your birth surtificate so as other dokoments na hata magazetini,unataka kuniambia magazeti ya kifarasa yanachange jina la mtu na kuandika kifaransa au magazeti ya uk yanabadilisha jina lamtu nakuandika kidhungu no,jina linabaki kuwa vile lilivyo tokeni nu bulshit zenu za lugha

    ReplyDelete
  19. Sawa kabisa Mh. Anne, sasa mh kwenye kuapa alitamka Anne au Anna Makinda, kwahiyo inabidi waheshimiwa wangalie upya majina yao..
    Hayo yote ni matamshi tu, usichukie mheshimiwe.

    ReplyDelete
  20. Watu wana keep goodwill yeye anajitenga na jina lake ambalo lilikua linajulikana toka elfu lela ulela. Mimi nisingejua huyu ni yule yule tuliyekua wadogo tunasoma shule alikua kiongozi huko huko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...