Asalaam alaykum kaka,
natumai upo mzima bukheri na kazi zinaendelea vizuri.naomba unirushie tangazo langu hewani. Ni maulidi yatakayo fanyika Toronto, Canada.

Shukran

Wote mnakaribishwa mjumuike pamoja nasi katika siku ya furaha kubwa ya kuzaliwa kwa mtume wetu Muhammad S.A.W. Ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwake nabii wetu Muhammad S.A.W. Wake kwa Waume,Watoto kwa Wakubwa, Waislam na wasio waislam wote mnakaribishwa. Please come for love, support and cherish with us on a SPECIAL DAY like this. Kutakua na chuo ambacho kitasoma maulidi.

Siku: Sat 14/5/2011
Muda: 5:00-9:30pm
Vyakula: Mandazi,chapati,ndizi,pilau (just to name a few)
Vinywaji: Soda,Maji,Chai.

Dress code: Wanaume; Kanzu,Misuli,Suruali. No baggy pants or hats please
Women: Madira, Khanga, Long dresses (head to be covered)

I hope to see you all there, masalaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kwanza kabisa nashukuru kuona kama watanzania wa ughaibuni wanaendeleza tamaduni na dini zetu kama kawa.

    Pili. hili swala la dress code; libakie kuwa chaguo binafsi la mtu, ili mradi tuu mvaaji hasiwe uchi, kwa maana ya uchi ulivyotafsiliwa kwa mavazi ya kiislamu. Mimi binafsi sivai baggy pants na wala siyo mshabiki wa baggy pants, lakini nilizivaa sana wakati nipo katika umri wa kuvaa baggy pants.
    Ni vyema tuwaache watoto waufaidi utoto wao, na wajinga waufaidi ujinga wao. Kama mtu amevuka miaka 27 na bado anavaa baggy pants basi ujue ana matatizo asiyoyaelewa.

    ReplyDelete
  2. Hii ni nzuri kwa waislamu walio ughaibuni na duniani kote lakini itanoga zaidi pale tukifurahia siku ile ambayo kipenzi chetu Muhammad S.A.W alizaliwa na si kuadhimisha siku yoyote. Kwani hata hizo tunazosema birthday zetu au madhimisho mengine yote tunakuwa tunafanya siku ile ile lakini kuzaliwa kwa Muhammad S.A.W tunafanya tu siku yoyote pengine hata kupita ule Mfunguo aliozaliwa kipenzi chetu.
    Imekuwa si Maulid ni Halbadir inasomwa siku yoyote tu.
    Wabillah taufiq.

    ReplyDelete
  3. Mdau kwa kwanza, mtoto umleavyo ndio akuavyo! ukimzoesha kuvaa vichupi basi akikua akikuvalia usije kulia! hizi ni zama za utandawazi na dunai imeharibika sana! sio enzi kama wa huko nyuma ambapo maadili yallikuwepo! mlee mtoto katika maadili hata kesho akitokea kukushinda unaweza kuiridhisha nafsi yako kuwa ulijitahidi kumlea katika maadili! acha ushamba wa kufurahikia mambo ya magharibi!

    ReplyDelete
  4. Mdau wa Mon April 04, 03:30:00 PM; naona una stress sugu. Mdau amesema kabisa kwamba baggy pants zinavaliwa na watoto na wajinga. Na akasema kwamba yeye havai baggy pants, lakini wewe kwa kuuchukia umagharibi ukaamua kwamba eti yeye ni mshamba na anashabikia umagharibi.
    Nakushauri soma tena maoni yake, na kama huwezi kumuelewa basi tafuta mganga wa akili. Usiende loliondo lakini.

    ReplyDelete
  5. Wewe unayesema wadau wa ughaibuni wanaendeleza tamaduni za dini zetu kama kawa unajua maana ya neno ughaibuni? Hata uarabuni ni ughaibuni kwa mtu aliye Tanzania...Tamaduni za dini yeyote ni sawa sawa kama mnafuata the same foundation. Waislamu waliozaliwa Canada hawana tofauti na waislamu waliozaliwa Tanzania just so you know...

    ReplyDelete
  6. we kenge umebana meseji yangu ili iweje? paka pori we!

    ReplyDelete
  7. lol, ukiona meseji yako imebaniwa basi ujue ankal anakueleza kiheshima kwamba, takataka za kwenye ubongo wako usizimwage hapa, kwa kuwa hapa siyo jalalani.

    Hongera ankal

    DAR YOUNG AFRICAN, IN CARDIFF, UK

    ReplyDelete
  8. Nadhani kumeekwa dress code ili watu waende kwa heshma ao sio leo mtu unaenda na jersey ya boston na kofia ya lakers inahusu?. Ni bora na hiyo dress code yao hta kma huna kanzu jeans la heshma pia bora, Anony kuna watu wako 40 nabado wanavaa baggy.

    Anony wa pili huwezi jua kwanini wamechelewa kuyasoma haya mawlid lakini ni bora wanamkumbuka Muhammad (S.A.W). Mimi nawapongea sana mashallah.

    ReplyDelete
  9. Mdau wa Nane: ndio maana tukasema itanoga zaidi kama itafanyaka siku ile aliozaliwa Kipenzi chetu na sikwamba tunabeza wale wasomao maulid siku zengine.
    maasalam

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...