Uncle Michuzi mimi namtafuta rafiki yangu niliyesoma naye kwenye shule ya secondary SINZA WAZAZI (ITEBA) miaka ya 2003 - 2004.
Huyu jamaa tulikua tunamwita KC KABETA (Bahati mbaya sikumbuki jina lake kamili) huyu jamaa alikua maarufu saana pale sinza wazazi (iteba). Yeye kipindi hicho alikua anatokea Mburahati.
Uncle Michuzi mimi ni Mjasiria mali niliyepo huku Ughaibuni kwa sasa nataka nifungue kijimtego (Kitega uchumi) hapo Dar es salaam japo kiweze kunisaidia kujikwamua matatizo madogo madogo hapo nyumbani.
Kutokana na tabia za kijitega uchumi hiki kitafaa saaana na naamini kitaenda vyema kikiwa mikononi mwa huyu rafiki yangu KC KABETA, jamaa kwa jinsi alivyo nimependezewa niweke hiki kijitega uchumi mikononi mwake ingawa ni mda mrefu hatujawasiliana na sijui anaendelea vipi na yuko wapi naamini rafiki yangu KC KABETA atanisaidia saana kwani ana sifa zinazoendana na hiki kijitega uchumi.
KC KABETA popote ulipo usomapo ujumbe huu tafadhari tuwasiliane kaka, Ni muhimu saana.
Yeyote anaye mfahamu KC KABETA tafadhari naomba anisaidie ni vipi nitampata.
KC KABETA naomba tuwasiliane kwa email yangu hii
nimimi20@yahoo.com
Asante saana Uncle Michuzi,
Mjasiliamali wa Ughaibuni.

Haya KC KABETA popote pale ulipo zali hilo la mentali limejiseti lenyewe bila chenga!
ReplyDeleteMdau uliyeleta mada vipi mshkaji hata Facebook hapatikani? Wakamate ma-class mate wengine walioko Facebook wakutafutie hiki kiraka!
kwa maoni yangu mdau hukupaswa kuandika sababu zinazokufanya umtafute huyo rafiki yako. maelezo yako yanaelekea kuwa unadhani kuwa huyo rafiki yako mambo yake si mazuri, hivo atakuwa tayari kufanya kazi chini yako. hujuwi huyo jamaa yako yukoje sasa. je, km mambo yake ni mazuri kuliko wewe unadhani atakuwa tayari kujitokeza pamoja na hali inayoelekea kuwa umemshushia hadhi? ujumbe huu unaendeleza tabia ya watu walio nje ya nchi kudhani kuwa wote walio bongo wana maisha duni kuliko wao.
ReplyDeletelakini pia, inaelekea hamkuwa karibu kiasi hicho cha kuweza kumwamini na kumkabidhi mradi, kwa maana hata jina lake kamili hulijuwi. kwa ujumla, maelezo yako yanatia shaka. hata hivyo, nikutakie kila la heri umpate rafiki yako ili uendeleze ujasiriamali hapa kwetu.
Subiri mwenyewe mwaka wowote utakaorudi TZ ndiyo ufungue kitega uchumi wakati na wewe mwenyewe upo hapo hapo hayo mambo ya kumtegemea mshikaji utakuja kulia chonde chonde,sim-banii huyo mwanao(mshikaji/rafiki) unayemtafuta ila hali halisi naifahamu sababu hayo unayotaka kuyaanza tulishayafanya na tukaambulia hasara na maumivu.
ReplyDeletewabongo bwana, yaani mtu huna contact naye for such a long time lakini unataka kumpa business yako aisimamie?? Kama je
ReplyDeleteamedata?? umaarufu wa shule haumaanishi kua ataendelea hivyo hivyo baada ya shule.Huna ndugu au rafiki wa karibu atakayeweza kufanya hiyo business? sikufahamu ila umenishangaza kwa kweli.
Ebwana mimi nipo Libya kwa sasa nafanya kazi huku mambo yangu siyo mabaya ..ni mazuri tuuu...kwa sasa.. ila nina biashara zangu za kuuza magari nina yard tatu ziko bongo...wewe mpe mtu mwingine akufanyie kazi
ReplyDeletemimi pesa kwa sasa ninayoo ile mbaya..
Mdau wa ugaibuni angalia usije ukalia kilio cha mbwa"mdomo juu"Ujue hapa bongo watu wengi hawataki kabisa kujituma wao ni mishen town, zao ni starehe kwa kwenda mbele,kila siku mabonanza,Leaders club.Billicanas,Mango garden,msasani club nk.Ukiangalia wewe mwenyewe unapigika kufanya kazi usiku na mchana kama tujuavyo ugaibuni maisha siyo lelemama,hakuna hata muda wa kutosha kuserebuka kama bongo,ushauri wangu ni wewe kuwa muangalifu usije ukalia,usimuamini hata ndugu yako wa kuzaliwa maana nina jamaa yangu yalimkuta hayo hayo.Watu bongo hufikiri kuwa ugaibuni pesa zinapatikana kwa urahisi,si hivyo.Weka pesa zako hadi utakaporudi mwenyewe ujue cha kuanzisha ukikisimamia mwenyewe.Ni ushauri wa bure.
ReplyDeleteMdau Ugaibuni.
Wewe mtu hata jina humjui...halafu umekaa ughaibuni muda mrefu huna mawasilaino naye. Huku ndio kutaka lawama tuu? Nakupa mfano tu mimi nilikuwa na rafiki yangu wa karibu sana secondary na tulikuwa tunawasiliana yeye akatimkia Bondeni. Mwaka jana akarudi bongo tukaonana ili ku catch up kwani muda mrefu. Kuonana Yaani alikuwa mtu tofauti kabisa na kama tulivyokuwa secondary na miaka ya nyuma. Moral of story wewe unavyomfikiria huyu mshikaji sasa hivi anaweza kuwa mtu tofauti kabisa kwa hiyo sijui kwanini unataka kumpatia mradi mtu ambaye humjui.
ReplyDeleteHalafu ulizwa ndi mnakuja ku-post tena hapa kwa michuzi kuwa Bongo watu sio waaminifu. Yule mwenzio aliyelizwa kiwanja umesoma hapo juu??
ze comedi tupu!
ReplyDeleteNdugu yangu mjasiriamali wa ugaibuni fanyia kazi hayo mawazo ya waliopita hapo juu,yamkini yanaweza kukusaidia sanaaaaaa.Lakini pia nataka kumsaidia mawazo mchangiaji mmoja hapo juu alivyosema kwamba ninanukuu"maelezo yako yanaelekea kwamba huyo jamaa yako mambo yake sio mazuri"Nafikiri kuna Misinterpret.Jamaa anamtafuta rafiki yake sababu alimpenda na angependa kurudisha mahusiano ya karibu na yeye kwa kufanya biashara pamoja.Kwanini gafla ufikirie kama amemdharau?Tujifunze kuwanza positevely otherwise tutakuwa tunamiss some opportunities kisa .........
ReplyDelete