Mh Naibu Balozi akiwa na wadau wa Reading wakati wa Carnival hiyo.
URBAN PULSE CREATIVE inawaletea picha za matukio ya Reading Carnival iliyofanyika jumatatu 30.5.11 ambayo ilikuwa ni siku ya Bank Holiday. Kwa mara ya kwanza TA Reading ikishirikiana na TANZ UK waliandaa banda la kitanzania kwa kupika chakula cha Kitanzania na kuuza kwa wadau mbalimbali waliojitokeza kutembelea banda la TA ikiwa ni mojawapo ya mradi wa kuchangia mfuko wa TA Reading. Mgeni rasmi alikuwa Mh Naibu Balozi wa Tanzania Uingereza Chabaka Kilumanga alieambatana na Afisa wa Ubalozini Amosi Msanjila. Kwa ujumla banda ka kitanzania lilitia fora kuliko mabanda yote mengine ya mataifa mbalimbali
 Watu kibao toka mataifa mbalimbali walihudhuria


 Watasha waliienda misosi ya Kibongo
 Msanii wa Zenji Fleva Berry Black (nyekundu) 
akiwa na wadau wa Reading
 Mdau Frank Eyembe wa Urban Pulse na Berry Black
 Nyama choma ilikuwa kivutio kikubwa kwenye banda la Tanzania
 Naibu Balozi Mh. Kilumanga akijiandaa kupakua ugali wa mhogo kwa mlenda
 Afisa ubalozi Amos Msanjila (kulia) akifurahi na mdau
Makuku ya kumwaga yakiandaliwa na Ankal Dello
Timu ya urban pulse ndani ya banda la TA Reading


Mdau Paul Onyango Kutoka Bongo Fleva (kushoto) akiwa na wadau wa Reading



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2011

    Wengi tulikubali TanzUK(Reading) kwa maandalizi mazuri na kuandika meza kwa lishe nzuri za kienyeji(TZ)siku hii ya Reading Carnival 2011.

    Sasa tunaomba mtuongoze vizuri na kwa kasi zaidi ili vyakula hivi tuviagize toka Tanzania kwa wingi ili mkulima mtanzania nae anufaike kama sisi.

    Yooote yanawezeka tukikaza mkanda na kupunguza uhafidhina usio wa lazima ktk taasisi husika ktk uchumi(wa soko,mpango na ushindani) wa sasa.

    Kwa Ari, Nguvu na Kasi hii tuanze mapema maandalizi ya sherehe za kumbukumbu ya Miaka 50 ya kumng'oa Mkoloni.

    MAINA A. OWINO
    UK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...