Marehemu Samuel Wanjiru

Bingwa wa Olimpiki wa mbio za Marathon, Samuel Wanjiru wa Kenya. Mwanariadha huyo wa Kenya alifariki dunia Jumapili usiku nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 24. Polisi wameeleza kuwa alianguka baada ya kuruka kutoka kwenye baraza la ghorofa ya kwanza nyumbani.

Wamesema mwanariadha huyo alikuja nyumbani usiku akiandamana na mwanamke mwingine, na baadaye mke wa Wanjiru- Triza Njeri alikuja akawakuta chumbani, na kwa hasira akafunga mlango wa chumba hicho huku akimwambia mumewe anakwenda kuwaarifu polisi. Haijabainika ikiwa Wanjiru aliruka nje kujiua, au kumfuata mkewe, au kwenda kufungua mlango wa chumbani. Polisi waliwahoji wanawake hao wawili kubaini kilichotokea.

Mwezi Desemba Wanjiru alishtakiwa kwa kutishia kumuua mkewe, kumiliki bunduki kinyume cha sheria na pia kumjeruhi mlinzi wa nyumbani. Baada ya mkewe kuondolea mbali kesi inayomhusu walirudiana, na Wanjiru alitazamiwa kufika mahakamani kuhusiana na shtaka la kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Sammy Wanjiru alikuwa na umri wa miaka 21 aliposhinda medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 mjini Beijing , China, na akawa Mkenya wa kwanza kushinda dhahabu kwenye mbio za marathon za Olimpiki. Chipukizi huyo aliibuka mwaka 2004 wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 , aliposhinda mbio za marathon za Fukuoka nchini Japan.

Baada ya kushinda taji la Olimpiki, mwaka uliofuatia alishinda mbio za London na pia Chicago. Mwaka jana alitetea taji la Chicago. Ilitazamiwa na wengi kwamba mwanariadha huyo angeweza kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za Marathon ambayo kwa sasa inashikiliwa na Haile Gebreselassie wa Ethiopia.

Haile ameelezea masikitiko yake kufuatia kifo hicho. ''Najiuliza ikiwa sisi kama jamii ya wanariadha tungeweza kusaidia kuepusha tukio hilo.'', alisema Haile kwenye mtandao wa Twitter. Katibu mkuu wa chama cha riadha nchini Kenya David Okeyo amesema kifo cha Wanjiru ni pigo kubwa kwa Kenya. '' Alikuwa mwenye furaha na tulitazamia angevunja rekodi ya dunia ya mbio za marathon hivi karibuni'', alisema Okeyo.

Bingwa wa zamani wa dunia Paul Tergat pia kutoka Kenya amesema nchi hiyo imepoteza mwanariadha chipukizi mwenye kipaji. '' Ni habari za kusikitisha sana, na ni pigo. Alikuwa mwenye umri mdogo na alikuwa na nafasi ya kukimbia kwa miaka mingi. '' alisema Tergat. Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amesema kifo cha Wanjiru ni pigo kubwa kwa matazamio ya Kenya ya kushinda medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao mjini London
Marehemu akiwa na mkewe na mtoto wao enzi za uhai wake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2011

    Hao wanawake wanabidi waulizwe vizuri. Mtu aanguke na kufa kwa kujirusha kutoka gorofa ya kwanza tu? Alikua amelewa au huyo mkewe alimset up? Wakenya wakora kweli.

    Halafu huyo mwanamke anayekubali kwenda kwa nyumba ya mtu akijua kuna mke ndani na huyu ni mtu maarufu huko Kenya lazima inajulikana alikua na mke...He was too young to have a wife anyway...ndio maana haya yote yalikua yanamfuata. Alikua anaukimbiza ujana na huku nyuma ameacha familia....have one's cake and eat it too...RIP

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2011

    pole sana mjane pamoja na ndugu wa marehemu.ingekuwa ni uweza wangu mimi ningependa angekufa huyo mwanamke ambaye ni malaya aliyekubuhu,asiye kuwa na heshima,ameshindwa kumalizia mambo yake gest anaingia kwenye nyumba anayoishi mwanamke mwenzake???poor you!R.I.P SAMWEL.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2011

    Kwani si alijua ana mke kwa nini upeleke changu nyumbani kama si kumletea mkewe presha bila sababu si angeenda hotelini? radhi ya mke hiyoo malipo ni hapahapa duniani ndio mkome ufuska unapeleka changu nyumbani tena ukalale naye kitanda chako na mkeo? . ubabe gani huu lakini? hii haikubaliki. hata mie ni kimada lakini sijawahi kwenda na sitakaa niende nyumba kubwa ala tuwe na heshima kama unaiba iba kistaarabu msilete dharau!
    poleni wafiwa!
    michu hakuna kubana hii

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2011

    hakuna changu wala malaya kwani jamaa hakujua kama yeye ana mke na kwa nini lawama apate huyo kimada wakati mkosaji ni huyu marehemu. wala huyo kimada hakustahili kufa kama alivyodai mtoa maoni hapo juu. aliyekufa ndie mlengwa haswa radhi ya mke hiyo. hebu tuache kujidahlilisha wanawake jamani ndio yale ya kina Gea kushabikia fumanizi kumbe aliyefumaniwa nae ni mke halali sasa kikowapi mbona muarabu na yeye kafa? malipo hapa hapa duniani. Gea na wenzio mbona hamkwenda msibani mkarusha heka heka kama mwanzo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2011

    RIP bro pigo kubwa sana hilo duhhh na inasikitisha mnooo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2011

    Huyu kijana aliwahi kuoa, nafikiri kwa umri wake angefanya kama Ronaldo kwa kufanya mkataba na mwanamke na kumzalia mtoto kwa mbegu za kuwekwa na sindano, ili aoe na miaka kama arobaini baada ya kumaliza kipindi chake cha fani ya mbio, ndugu zetu hawa mda mwingine ni sababu ya watu wengine "kuanguka" ktk maisha na hasa kama ukikosea kuchagua.

    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...