Uncleeee.... Michuzi habari za leo?
Wiki iliyopita nilikuwa kweye kiji-vacation kidogo cha Easter huko Tukuyu Mbeya.
Naomba leo niwakumbushe Wanyambala kidogo ka-taswira ka nyumbani karibu na Kanisa la Moravian Kyimbila Mission kwa wale ambao hajafika kwa muda mrefu.
Natanguliza shukrani zangu,
Mdau Japhet.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. eeh jamani michuzi umenikumbusha kwa babu yangu mchungaji Asegelile mwankemwa , ndipo alipokuwa anasalisha hapo kyimbala moravian! asante sana kwa kutuma hizi picha za nyumbani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2011

    Asante sana umenikumbusha ujana wangu mpaka ushirika huko

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2011

    Heee yaani hapo ni pale chini kidogo karibu inapo chipuka njia au kona ya kwenda Lutengano Secondary School, duuuh ni pazuri balaaa kuna mandhali nzuri kama Sweden vile, hongera mdau kwa kutukumbusha ma-homies.
    Mpaka nasikia hamu ya kwenda huko, big up Mdau.
    Tutupie zingine jamani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2011

    Mweeh mweee jo jwani ujuh atutwalile sisyisi?, ejooh kumyitu bhamanyani, kanghi bhangumbwisye Mbushirika na mwa-Lubharisi toghaga ijolooo bho tulibhanini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2011

    kweli wengi umetukumbusha mbali miaka ya 1980, hivi yule sufiani yuko wapi walikua na mabasi pale tukuyu ya mzee mmoja wa mwananchi guest house, akina Francic mwaijumba, kweli Tukuyu enzi hizo ilikua moto, ya kale dhahabu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2011

    jamani, TKY bomba sana,nakumbuka enzi hizo nasoma Lutengano sometimes unapiga teke hadi town

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2011

    Umenikumbusha sana nikiwa chuo cha Msasani TUKUYU TTC hayo maeneo ndo tulikuwa tunavinjari sana na walimbwende wetu hahahahahaaaaaa safi sanaaaaaaa

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 11, 2011

    Huko ndo alikotokea Babu wa Loliondo Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapile

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 11, 2011

    Big up kama uoto huo ni wa asili lakini miti hiyo mirefu kama ya kigeni "HORA"

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 11, 2011

    mandhari - muafaka, unaipata Mbeya, Kagera, Kilimanjaro, Lushoto - nisihisahau Chunya. Balaaaaa tuna vitu vingi vya kuiuza nchi kwa watalii

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 12, 2011

    Anonymous wa 07:01:00pm umenichekesha,mambo ya michai chai kule chini. TCC OYEEE!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 12, 2011

    Yaani umenikumbusha mbali sana maana nimesoma kyimbila primary school huko kwenye michai tulikuwa tunapita na umande pamoja na mvua lakini namshukuru Mungu nilifaulu darasa la saba na sasa nategemea kuanza degree ya tatu (PhD), mwee kukaja kununu fijo, ndaga nkamu utukumbwisye kumyitu

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 12, 2011

    umenikumbusha mbali sana kwa bibi yangu wakati nasoma lutengano,, bibi alikuwa anakaa kiwira rodi pale jirani na kwa mwaikambo..
    enzi hizo pale standi ya mabasi... mabasi ya mzee mwamtobe ndio yalikuwa yanatamba...Tukuyu ya sasa imejaa wachaga watupu.. kwakweni nimekumbuka nyumbani..
    mwe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...