Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini Elifuraha Mtowe akipiga simu katika Kijiji cha Samunge Loliondo kupata taarifa za zali ya huduma na barabara kabla ya kuruhusu basi la SHOBNAZ Coach kuanza safari na abiria 80 wakiwemo watoto 20. Kundi hilo lilifika salama Loliondo na kurejea salama. Pembeni yake ni mwaandishi Grace Macha anayeandikia Gazeti la Tanzania Daima.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini Rashid Magoma akiongea na waandishi wa Habari kuhusu umuhimu wa kuwasaidia wananchi wenye uhitaji na jinsi Chama hicho kitakavyotekeleza majukumu yake kwa wapiga kura wao kwa kuwashirikisha wapiga kura wenyewe kwa michango mbalimbali, aidha aliwashukuru watu wote waliojitolea kufanikisha safari hiyo. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini Elifuraha Paul Mtowe (Mwenye suti Nyeusi na shati la Pinki) akiongea na waandishi wa Habari mbele ya baadhi ya wananchi waliopatiwa msaada na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mh. Godbless Lema na Taasisi hiyo ili kwenda Samunge kupata tiba ya maajabu inayotolewa na Mchungaji mstaafu Ambilikil

Wananchi wakazi wa Jimbo la Arusha Mjini waliopatiwa Msaada wa kwenda Samunge wakiwa kwenye basi la SHOBNAZ Coach Namba T.239 AEG tayari kuanza safari ya kuelekea Kijiji cha Samunge Loliondo kupata Kikombe.
Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini (ArDF) wamefanikiwa kupeleka watu 182 wenye magonjwa mbalimbali katika Kijiji cha Samunge Loliondo ili kupata dawa ya Maajabu inayosadikiwa kuponya maradhi sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapila.
Idadi hiyo ya watu inafuatia Makundi matatu kuondoka kwa awamu tofauti ikiwa ni la watu 47 waliondoka mmoja mmoja kwa msaada wa Mbunge wa Jimbo hilo, kundi la pili la watu 80 wakiwemo watoto 20 walioondoka Alhamisi tarehe 12 kwa basi la SHOBNAZ Coach lenye Namba T.239 AEG na kundi jingine la watu 60 walioondoka leo Jumapili.
Akiongea katika tukio la kugawa msaada wa tiketi kwa wakazi wa jimbo la Arusha waliopewa msaada kufuatia kukosa uwezo wa kujigaramia safari ya kwenda Samunge, Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini, Elifuraha Paul Mtowe alisema wingi wa watu unaokwenda Kijiji cha Samunge kupatiwa tiba kunaonyesha ni jinsi gani Watanzania wanavyosumbuliwa na maradhi, amesema hali inaonyesha Wananchi na Viongozi wa Tanzania kwa kiasi kikubwa wanaumwa maradhi yanayofana na mengi yakitokana na uwezo duni wa kimaisha na mifumo duni ya utabibu na matibabu isiyoweza kuwahudumia watu na hasa watu masikini.
Amesema watu masikini wamekata tamaa kufuatia gharama kubwa za kujitibu magonjwa ya kudumu, hivyo kitendo cha kupatikana dawa hiyo ya muujiza ni suluhisho kwa watu wengi wenye uwezo duni wa Nchi ya Tanzania, amesema maradhi kwa kiasi kikubwa yanachelewesha ufanisi na kudumisha uchumi wa Nchi na ni busara kwa wanaoamini kikombe cha Babu kwenda kukitumia ili waweze kurejea katika shughuli zao za ujenzi wa Taifa.
Akiongea kuhusu Imani amesema, ni ngumu kufikiria au kuhoji uwezo wa Mungu au fomula zake anapofanya vitu vyake, amesema Mungu hutenda miujiza katika namna nyingi na hata mambo makubwa aliyoyafanya yalibakia kuwa maajabu na hakuna anayejua yalivyofanyika, akitoa mfano alisema hakuna mtu anayejua ni fomula gani iliyotumika kwa Yesu Kristo kumfufua Lazaro au kujeuza maji kuwa Divai au kumponya kipofu kwa kuchanganya mate na udongo.
Akiongea kwa niaba ya Mbunge wa Arusha Mjini, Mwenyekiti huyo amewashukuru wananchi waliochangia gharama za safari kwa wananchi wenzao wasiokuwa na uwezo na pia alimshukuru Mchungaji Mwasapila kwa kutoa dawa hiyo kwa gharama nafuu na kusema Mungu amelitendea jambo jema Taifa la Tanzania kwa kuufanya Muujiza huo kutokea katika nchi yetu hali itakayoweza kusaidia watu wengi wenye Imani na dawa hiyo kuitumia kwa gharama nafuu hata kama ni kwa kusaidiwa na wananchi wen

Namuona dada anamavazi ya kiislam na ameingia mtego huuu wa kuona Mungu anaongea na huyo mzee..inasikitisha sana
ReplyDeletesi atasema shahad upya tatizo liko wapi? au anaweza kuwa wa dini nyengine kwani nani kasema ni waislamu tuu ndo wavaa hivyo?
ReplyDelete