Home
Unlabelled
dar yazidi kukwangua anga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Tibaijuka na Nyumba za NHC
ReplyDeleteNa Mwandishi wetu
1st June 2011
Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) nazo zimo katika hatari ya kuporwa kama ule uliofanywa kwenye nyumba za serikali kwa kisingizio cha kuwasaidia watumishi wa serikali, hali inayomweka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kwenye mtego mkubwa.
Safari hii mikakati imepangwa chini ya kamati maalum ya wapangaji wa nyumba za NHC wakijenga hoja mufilisi, kwamba wanastahili kuuziwa nyumba za shirika hilo kwa bei sawa na bure kwa kuwa wamekaa kwa muda mrefu katika nyumba hizo.
Uchunguzi huru wa NIPASHE na vielelezo mbalimbali vilivyokusanywa juu ya njama hizo, unaonyesha kuwa chini ya kamati hiyo, shinikizo sasa linaelekezwa kwa Waziri Tibaijuka, ili asaidie kuilazimisha NHC kuuza nyumba hizo kwa wapangaji wake kwa bei ya chee kama walivyofanyiwa watumishi wa serikali wakati awamu ya tatu.
Tayari mkutano na waziri, wapangaji na NHC umepangwa kufanyika Jumamosi wiki hii katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, ajenda ikiwa ni kuuziwa nyumba; kupunguziwa bei; na kutolewa kwa ruzuku kwa wapangaji wanaodaiwa kuwa hawana uwezo kama vile wastaafu, wajane, wagane na yatima.
Uchunguzi wa NIPASHE umeonyesha kwamba mkakati huo ingawa unajengwa kwenye dhana ya umaskini na uwezo, unasukumwa na watu wenye mitaji mikubwa nyuma ya pazia wakiwatanguliza baadhi ya watu. Kuthibitisha hili, mikakati hiyo inalenga kulazimisha NHC kuuza nyumba zake zote 800 zilizoko eneo la Upanga jijini Dar es Salaam, zikiwa zinakaliwa na familia takribani 4,000 ambazo ni sawa na watu 24,000.
NHC imepanga kuboresha makazi ya nyumba za Upanga kwa kubomoa nyumba zote hizo ili kujenga majengo mapya ya ghorofa ambayo yatakuwa na uwezo wa kuweka familia 200,000 sawa na watu zaidi ya milioni moja.
Kadhalika, uchunguzi wa kina wa NIPASHE umebaini kwamba michoro ya NHC kuhusu Upanga ni kulifanya eneo hilo kuwa la kisasa zaidi, kwa kuwa na maeneo maalum ya kuegesha magari, viwanja vya michezo na maeneo ya kupumzika kama ilivyo katika miji mingine mikubwa duniani.
Hata hivyo, katika mkakati huo, NHC ikishajenga nyumba hizo mpya kiasi cha asilimia 70 zitauzwa kwa wapangaji waliopo sasa huku asilimia 30 ikibakia chini ya miliki yake kwa nia ya kuendeleza kazi za ujenzi wa nyumba nyingine.
NHC imeingia katika mkakati huo ili kufanikisha ahadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi uliopita kwamba Shirika hilo litajenga nyumba mpya 15,000 na kuuzia wananchi kwa nia ya kuwapa wananchi makazi bora nchini.
NIPASHE imefanikiwa kuona nyaraka ambazo zimeandaliwa na kamati maalum ya wapangaji wa NHC wakijenga hoja ya kuuziwa nyumba hizo, kikubwa ni kuuziwa kwa sababu wameishi kwa muda mrefu kwenye nyumba hizo; wanataka wauziwe kwa bei ya chee kama zilivyouzwa nyumba za serikali na bila kutumia njia ya zabuni kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma; lakini pia wanataka wakopeshwe na benki ili walipie nyumba hizo na ulipaji wa mkopo uwe ni wa miaka 15 na riba chini ya asilimia 10.
Wapangaji hao wanasema kuwa nyumba zote za makazi za NHC ziuzwe bila kujali umuhimu wa shirika kubakia na nyumba za kuweka rehani ili kupata mkopo na wanaamini kwamba zikiuzwa mtaji wa mara moja wa kujenga nyumba utapatikana.
Wakati wapangaji hawa wakiendesha kampeni zao dhidi ya NHC, uchunguzi wa NIPASHE umebaini kwamba Shirika la Nyumba nchini lina uwezo wa kutoa makazi kwa asilimia 0.45 ya wapangaji wote nchini, lakini wakilipa kodi kidogo sana ikilinganishwa na nyumba binafsi katika soko.
Kwa mfano, wakati maeneo kama ya Sinza, Kijitonyama na Mwenge chumba kimoja chenye choo cha kujitegemea sasa kimefikia Sh. 150,000 kwa mwezi, nyumba nzima ya vyumba vitatu vya kulala ya NHC Upanga inalipiwa kodi ya Sh. 135,000 tu kwa mwezi.
Mkakati huu wa kutaka kuikamua NHC unafanana na ule wa serikali ya awamu ya tatu wa kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa, kwa madai kwamba watumishi wake hawakuwa na uwezo, lakini baada ya muda mfupi kupita, nyumba nyingi walizouziwa zilibomolewa na kuibuka majumba mapya ya kisasa ya bei kubwa.
CHANZO: NIPASHE
HUYO MUANDISHI WA NIPASHE INAONEKANA ANAKIZIBA CHA ROHO!KWANI WALIOISHI MIAKA MINGI NHC NA KULIPA KODI ZAIDI YA MIAKA 40 NDIO WAMESABABISHA KUJENGWA KWA NYUMBA ZA NHC MPYA,AMBAZO ZIKO MAENEO MBALI MBALI,,KUSEMA KWELI HIZO NYUMBA ZA NHC KAMA KWELI TANZANIA INAFATA HAKI ZA BINADAMU WANGESTAHILI WAPEWE BURE NA WALA SIO KUUZIWA,ZANZIBAR NYUMBA ZA MICHENZANI WALIPEWA BURE WALOKAA MIAKA MINGI,,HUWEZI KULINGANISHA VIONGOZI WA AWAMU YA 3 WALIOUZIWA HIZO NYUMBA NA WAPANGAJI WA NHC,WENGI NI MASIKINI SANA NA WENGINE WAMEISHA STAAFU,,,,HII INAONYESHA KUWA TANZANIA SISI WENYEWE KWA WENYEWE HATUTAKIANI MEMA,,KWANI HATA HUWO MJI KUPANULIWA HATA KULE KURASINI KINONDONI HATA MPAKA MBUNJU NI MJI TU,SIO LAZIMA UPANGA MAANA KUMEJIBANA MNO,JAMANI WATU WAUZIWE TU NYUMBA HIVI NI VITU VYA KAWAIDA SANA DUNIANI KUMFRAHISHA MZAWA,,ALIYETUMIKA KWA MIAKA MINGI,,NA ISTOSHE NYUMBA ZENYEWE NI MBOVU MBOVU,,KAMA KWELI KUNA NYUMBA AMBAYO INAKIWANJA KIKUBWA HAPO SAWA WANAWEZA KUBOMOA NA WAKAJENGA GHOROFA YA KUWEKA FAMILIA ZINGINE NA KUMUUZIA HUYO SEHEMU YAKE ALIYEKUWEPO KWA PESA NDOGO MNO,,,WEWE UNAFIKIRI MTU ATAKAA ANAPANGA MPAKA LINI MPAKA AINGIE KABURINI NI WAKATI SASA WAUZIWE NYUMBA HAWA WALALA HOI WA UPANGA AMBAO KWELI WENGI WAO NI MASIKINI,NYUMBA ZOTE ZA UPANGA UKISEMA ZIBOMOLEWE ZIJENGWE MPYA NI MPAKA 2030,,,,,MBONA DARAJA LA KIGAMBONI MPKA LEO BADO,,NAWAOMBEA SANA WAKAZI WA UPANGA MWENYEZI MUNGU AWAJA'ALIE WAUZIWE NYUMBA,,MUNGU IBARIKI UPANGA,TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRICA
ReplyDeleteAHLAM UK!
TATIZO NI UCHAFU. JIJI CHAFU SANA HILO, HATA KAMA VIKWANGUA ANGA VITAKUWEPO ADI MAWINGUNI NA JIJI LINANUKA KUTAKUWA MANZESE TU. AIPENDEZI WADAU, AIIBU MANISPAA ZA JIJI BADILIKENI IGENI MIFANO YA MAJIJI MENGINE.
ReplyDeleteHaki iko wapi kama wengine wanauziwa nyumba za NHC kwa bei chee eti kwa sababu wamekaa huko muda mrefu? Kwanza wao walitakiwa wasiuziwe kabisa kwa sababu walikuwa wanalipishwa kodi kidogo sana wakati sisi tunaopanga mitaani tunalipa kodi kubwa. Pili, nyumba za NHC ni mali ya watanzania wote iweje wengine wauziwe kwa bei chee? Tafakarini kwa makini. Sisi wengine mtatuuzia kitu gani kwa bei chee ili na sisi turidhike na matunda nchi?
ReplyDeletevikwangua anga wakati maji hakuna umeme mzozo maegesho ya magari kizaazaa
ReplyDeletenjia za maji machafu hakuna mvua zikinyesha hujui ni wapi pa kuweka mguu kila sehemu swimingi puli la ankali.
Wauziwe tu ni haki yao.
ReplyDeleteKama alivyosema mdau hapo juu, upanuzi siyo lazima Upanga waende nje ya mji. Kwanza wakipanua Upanga wanazidisha heka heka za traffic.
WAUZIENI WAZALENDO! WAUZIENI WAZALENDO! WAUZIENI WAZALENDO!
Ila tena yasije pita magumashi tukakuta watu wa kabila fulani ndiyo wanaomiliki hizo nyumba.
wewe mtoa maoni wa pili ni mzima kweli wewe?serikali itoe bure nyumba sasa tunakwenda wapi,makosa yaliofanywa ya kuziuza nyumba za mwanzo yafanywe tena kweli sasa watanzania tumepungukiwa akili tutakwisha tunajiona,WACHENI MAWAZO FINYU YA KIMASIKINI KAMA HAMNA CHA KU COMMENT BORA MUSIWAUDHI WANANCHI
ReplyDeleteBongo ni Bongo tu. Watu wanafikiri kuwa na vikwakungua anga ndiyo maeneleo. We angalia mji kama Dar mvua kidogo tu mabwawa (Liverpool, samahani pools) za ghafla zinajitokeza kutokana na mipangilio mibovu ya jiji. Bongo kubadirika ni ndoto au labda mpaka vizazi vyote vilivyo hapo hivi sasa vife waje watu wa nje, lakini hivi hivi, there's nothing there to be proud of!
ReplyDeleteSerikali lazima ijenge nyumba kwa raia zake wa hali ya chini. Mafisadi na waroho pekee ndio wenye uwezo wa kumiliki nyumba mijini. Mafisadi wengi ni watumishi wa serikali, ambao hawaonekani na jamii. Cashier hakupi pesa yako mpaka umkatie kitu kidogo, bosi haweki saini mpaka apewe 10%. Askari trafiki mapema anakwenda barabarani kukamata magari lakini faini zote anachukua yeye. Profesa anafelisha wanafunzi kusudi mpaka wamlipe pesa. Kila nyanja ya nchi imeoza. Vyama vya upinzani navyo vimeundwa kwa maslahi ya kabila au jimbo fulani. Hiyo ndio Tanzania.
ReplyDeleteKwanza kabisa inabidi turudi kwenye historia. Nyumba nyingi za NHC zilijengwa na watanzania wenye asili ya kiasia ambao walikuwa wafanyabiashara na wafanyakazi na sio mafisadi. Tofauti na leo viongozi wengi wanataka wafaidike bila kufanya kazi.
ReplyDeleteLakini hizo nyumba zikaja kuchukuliwa kifisadi na waliojenga wakawa wapangaji kwenye nyumba zao wenyewe, hebu fikiri haki ipo dunia hii? Wengi wao hawakupata hata fidia, na waliopata ni wachache na fidia ilikuwa kiduchu!
Ipo siku NHC wanaweza kupelekwa kortini kuhusu hilo la juu il majumba ya wapangaji warudishiwe au walipwe fidia wanayostahili!
Sasa tukija kwenye suala la nyumba za NHC kwa sasa, nataka nizungumze masuala kadhaa.
NHC wanatakiwa waangalia wapangaji waliokaa mda mrefu wauziwe nyumba. Maeneo ya kujenga maghorofa mbona yapo mengi! au kwasababu mnapata bilioni 1 kwa mwezi mnaona hapa mnaweza kupata zaidi?
Mortgage system sio suala la kurupuka. Hamjasikia huko marekani imefail? Kwingineko benki zimefilisika baada ya wapangaji kutoweza kulipa. Mnapopanga watu 200,000 wakae eneo dogo kama upanga, hiyo ni mipango miji mizuri au ni kucreate more congestion?
Je mnajua hali ya wananchi? Mkishajenga maghorofa, je mtanzania wa hali ya chini ataweza kulipa kodi kubwa ya nyumba?
Imekuaje kuhusu Satellite Cities wakati mnataka kucongest city centre, upanga na kariakoo even more. Mshafikiria miundombino nakadhalika?
Mie naona NHC wamekurupuka sana. Kwasababu wan majumba mengi Upanga wakaona hapa ndiyo penyewe. Hebu fikirieni upya otherwise the MORTGAGE SYSTEM BY NHC IS BOUND TO FAIL!
Kuuziwa nyumba kwa mwananchi sio kitu chaajabu ni sawa tu isipokuwa serikali zijenge nyumba nyingine za kuwasaidia wananchi wa hali yachini na wao wapate kulipa kodi nafuu.Lakini tukirudi nyuma serikali pia inatakiwa kuwepo na mpangilio wa majengo hayo yenye kujengwa.Mpangilio mzuri ni ule ambao ujenzi wenye kuweka maegesho ya magari ndani ya majengo hayo na wasiruhusu watu kujenga bila ya kuwa na ramani ya maegesho.Pamoja na paipu za maji machafu kwa ajili ya mvua.Kwani hata uingereza kama unaishi ktk nyumba za serikali na kama unao uwezo wa kununua basi utauziwa bila ya kipingamizi na nyingi zimeuzwa na wanaendelea kuziuza na huku wanaendelea kuzijenga kwa kuwasaidia wananchi wenye kipato kidogo.Huo ndio mfano mzuri kwa serikali ili kusaidia wananchi.
ReplyDelete