Kwanza napenda kuweka rekodi sawa, ni kweli zamani nilikuwa Yanga damu, siku hizi niko nyutro. Najua picha hii itakuwa taabu kidogo kwa wapenzi wa Simba lakini kupitiapitia makablasha ya zamani si mbaya, yana raha yake. 

Hii ilikuwa mwaka 1992 siku Yanga ilipofanya mauaji kwa mnyama uwanja wa Taifa (sasa wa Uhuru) Dar kwa goli la shuti la mbali la nahodha Ken Mkapa lililomshinda Mwameja.

Nakumbuka mechi hii ilichezwa siku chache baada ya Yanga kutoka Misri ilikokwenda menyana na Ismailia na kutoka sare ya 1-1. 

Pichani ni baadhi ya wanaume wa shoka wa Yanga. Toka kushoto ni Hamis Gaga 'Gagarino'(marehemu), Saidi Mwamba 'Kizota(marehemu), David Mwakalebela, Method Mogella(marehemu), Abeid Mziba, Ken Mkapa, Na Salum Kabunda 'Ninja'. Nyuma kwa mbali ni Stephen Nemes. 

Vizazi hivi sijui kama vitakuja tokea tena! Mungu ibariki Tanzania. Wenye kumbukumbu zaidi za mechi hii tukumbushane...
nawasilisha 

mdau
Nathan Mpangala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. MHESHIMIWA MPANGALA NI RAHA ILIOJE KUTUKUMBUSHA MAMBO YA ZAMANI KWA KWELI MIMI NI MPENZI WA SIMBA NA NAIKUMBUKA SANA MECHI HII KWANI MWENYEWE NILIISHUHUDIA KWA MACHO YANGU. NA KAMA ULIVYOSEMA KUWA WENYE KUMBUKUMBU ZAIDI TUKUMBUSHANE BASI NI KUWA YANGA ILIANZA KUCHEZA NA SIMBA KWANZA KABLA HAIJAENDA MISRI NA SIYO SAHIHI KUWA ILICHEZA NA ISMAILIA KWANZA ALAFU SIMBA.USISAHIHI NI KUWA ILIANZA NA SIMBA KWANZA NA MUDA MFUPI BAADAE NDIYO IKAKUBALI KIPIGO CHA 2-0 HAPO HAPO TAIFA KABLA HAWAJAENDA KUAMBULIA SARE YA 1-1 HUKO MISRI PIA BAO LA YANGA HUKO MISRI LILIFUNGWA NA MKAPA KWA STYLE ILE ILE ALIVYOFUNGA KWA SIMBA UWANJA WA TAIFA. MDAU MAX ABUU.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2011

    Na mimi nampongeza Nathan kwa kazi nzuri. Hata hivyo, napenda kumsahihisha mdau Max Abuu. Mechi hii ilichezwa baada ya Yanga kutoka kurudiana na Ismailia huko Misri ambako iliambulia sare ya 1-1, shukrani kwa bao la Ken Mkapa ambalo Ismailia walilisawazisha zikiwa zimesalia dakika 10.

    Baada ya kumalizana na Ismailia, Yanga ilitakiwa irudi Dar ili jumamosi inayofuata imenyane na Simba. Yanga wakaamua kubaki Misri ambapo walisaidiwa na Ismailia kuweka kambi kujiandaa na mechi ya Simba. Viongozi walipoulizwa, wakasema hawana wasiwasi kwani wangerudi siku ya jumamosi mchana kwa ndege na kuingia moja kwa moja uwanja wa Taifa kwa helocopta! Lakini ilipofika alhamisi, viongozi wa Yanga waliopo Dar wakaiomba FAT iisogeze mechi jumapili kwani walikosa ndege ya jumamosi. Simba wakatishia kugomea mchezo kwa madai kuwa FAT wanaiogopa Yanga. Hatimaye Simba wakakubali.

    Katika mechi hii Yanga walimkosa Abubakar Salum ambaye aliumia wakiwa kambini Misri, hivyo nafasi yake ikazibwa na Justine Mtekere. Hamis Gaga alipyaya sana, huku wengi wakiwa na hamu ya kumwona akicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani. Gaga akatolewa na nafasi yake ikachukuliwa na Steven Mussa (marehemu) Goli la Mkapa lilifungwa dakika ya 10.

    Jambo la kukumbukwa katika mechi hii, ni kitendo cha Yanga kuvaa jezi zenye rangi nyeusi kitu ambacho walikiacha toka mwaka 1981 (!). Niliwahi kufahamishwa na kiongozi mmoja wa Yanga kuwa jezi hizo walipewa zawadi na timu ya Ismailia mara baada ya kumaliza kambi yao Misri. Since then, Yanga wameendelea kutumia mara kadhaa, rangi nyeusi. Tumetoka mbali........

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2011

    Nilikuwa darasa la tano, namkumbuka sana marehemu Justin Mtekele, aliyekufa kwa ajali pale Mbeya......nilianza kuipenda na kuijua yanga kwa kupitia ndugu wa Justin Mtekele.....aiseee nimeipenda sana hii picha. WaKATI HUO PICHA KAMA HIZI ZILIKUWA ZINAUZWA SOKONI PALE TUKUYU MJINI. Du...enzi raha kama ukikumbuka yaliyo mema.

    Mdau Andendekisye mbije-kafanabo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2011

    Life expectancy (umri wa kuishi) yetu watanzania inasikitisha sana. Hawa jamaa wengi wamekufa wakiwa na umri wa ujana kabisa, wengi walikufa kabla hata miaka 40-45 hawajafikisha. Tungekuwa nao leo ndo wangekuwa wananusanusa miaka ya 50 hivi. Inasikitisha hasa kwenye mpira wa miguu kupoteza vipaji wakati utaalamu wao bado unahitajika sana. Mataifa makubwa wanaoendeleza soka ni wachezaji wa zamani. Ndo hao viongozi wa vyama vya soka, makocha, wachambuzi n.k, lakini wa kwetu, ukifanya kwa takwimu za haraka haraka, katika hao 7, wa-3 ni marehemu. Inasikitisha! Picha nyingi sana zinazotolewa hapa za wachezaji wa zamani, miaka ya 90 na kwenda nyuma ni R.I.P

    ReplyDelete
  5. Mdau nashukuru sana kwa kumbukumbu hii..Yanga ya enzi ya picha hii ilikuwa Yanga baada ya enzi za Kina Hamis Kinye au Joseph Fungo..Yusuph Ismail Bana ..Bado namba 2 yake haijapata mtu ; Ahmed Amasha..Namba tatu iliyotumia akili kuliko nguvu ; Fred Felix Minziro "Kataraiya" alikuwa anapiga kona zinaitwa "Banana chop" yaani kama za David Beckham; Athuman Juma Chama "Gold Smith".. Full mkoba; Isihaka Hassan "Chukwu"..Aliumia akaenda tibiwa nje..enzi zile mchezaji kitibiwa nje ilikuwa sio mchezo.; Namba Saba..Hussein Iddi..Alikuwa anapenda kukimbia na mpira sambamba na chaki ya mwisho wa uwanja; Charles Boniface Mkwasa "Kapten"; Abeid Mziba "mzee wa vichwa" Omar Hussein "keegan"; Makumbi Juma " Homa ya Jiji" ..Wengine Abubakar Salum "Sure Boy" ..Celestine "Sikinde" Mbunga..alitokea maji maji..Sanifu Lazaro "Tingisha",, Juma Mkambi "General"..alichukua mkoba wa Athuman Juma Chama..na pia kuna mchezaji wa Yanga alikuwa anaitwa.."Scania" jina nimesahau... Nawakilisha!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 03, 2011

    hakuna cha kizazi wala nn,waliipa sifa gani nchi yangu Tanzania km walikuwa na vipaji vya maana??,tuliona wana vipaji kwakuwa enzi hzo hatukuwa na sehemu ya kulinganisha.uzuri wa kitu ni mafanikio bwna na co kuwa mzuri bila mafaniko haileti maana,hakuna kumbukumbu yeyote km walikuwa wazuri hawa achezaji wetu.vizazi vyetu havina kombe wala hata kuskia kati ya wachezaji hao aliwahi kukipiga hata ulaya daraja la 2 tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 03, 2011

    Kwako Nathan, ni kweli mapenzi kwa Yanga Afrika yamekwisha au unaogopa kukosa wapenzi (wasomaji wa katuni zako)? Siamini hata siku moja kama mapenzi ya timu moja (kwa hapa Tanzania), yanaweza kuhamia kwa timu pinzani. Hata hivyo, shukrani kwa kumbukumbu nzuri, hasa kwetu wapenzi wa Yanga Afrika!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 03, 2011

    mdau umenikumbusha zamani sana enzi za akina mziba, ken mkapa pamoja na gagarino .... ama kweli ya kale dhahabu kama mdau unapicha zingine hata zile za mseto fc ya morogoro ambayo ndio ilikuwa timu ya kwanza kuchukua kikombe nje ya dar turushie hapa tupate kujikumbusha wapi tumetoka? namkubuka sana justin mtekele (R.I.P).......
    LUVIKE
    Mdau Paris

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 03, 2011

    Daaah umenikumbusha mbali saaaana. Nilikuwa kidato cha nne Old Moshi secondary school. Ushabiki wa Yanga na Simba ulikuwa juu sana kiasi kwamba mnapomfunga mpinzni wenu siku hiyo ni raha tupu kwa wapenzi wa timu hiyo. Tulizunguka mitaani tukanwa na kula nyama choma kwa furaha.

    Kwa kweli nitawakumbuka sana hao wanaume hasa hao waliotangulia mbele ya haki. Machozi yananitoka nikikumbuka kazi waliyoifanya wakiwa Yanga. Mungu awalaze mahali pema kusipokuwa na mapepo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 03, 2011

    ASANTE KAKA NATHAN KWA KAZI NZURI,KABLA YA GENERATION HII KUNA MBILI ZA NYUMA KATIKA SOKA SIJUI KAMA ZITATOKEA TENA HUSUSANI MAZINGIRA YA MAISHA YA SASA,TULIKUWA NA KIZAZI CHA KINA ELIAS MICHAEL,HASSANI MLAPA KOLO,PATRICK NYAGA,MAMBOSASA,OMARI MAHADHI,MUHIDINI,HAMISI KINYE,MWAMEJA,WAKATI ULE KWANZA KUVAA JEZI YA SIMBA AU YANGA LAZIMA UWE UNA UWEZO KWELI UWANJANI,KULIKUWA NA TIMU ZA MITAANI AMBAZO UWEZO WAO ENZI HIZO ULIKUWA MKUBWA KULIKO UWEZO WACHEZAJI WETU WA SIMBA NA YANGA SASA.ILALA TULIKUWA NA TIMU KAMA POOL ENGLAND,ASHANTI,AJAX,YOUG KENYA,SCOLAND YARD,JANGANI FRESH,CONGO UNITED SHETANI WEKUNDU,BONDE,KABAKA YEKA YA KINA MAMA SASA VIJANA.TEMEKE GOOD HOPE,EVER GREEN,CHANG'OMBE RANGERS,AFRICAN TEMEKE,KINONDONI WONDER BOYS,BLACK BROTHERS,GOLDEN ARROWS,NEW BOYS,JEMBE,TAI,TP ENGLER BELT YA MANZESE,WACHEZAJI WALIO KUWA WANACHEZEA VILABU HIVYO WALIKUWA WANA UWEZO MKUBWA KULIKO WACHEZAJI WETU WA TIMU YA TAIFA YA LEO,WIZARA YA MICHEZO LAZIMA IFIKIRIE NINI CHA KUFANYA KURUDI KATIKA HALI YETU YA ZAMANI,MOJA WAPO NI VIWANJA VYA MICHEZO KARIBU TIMU ZOTE HIZO ZILIKUWA ZINA FANYA MAZOEZI PALE JANGWANI,SHULE YA UHURU,KIDONGO CHEKUDU,GYMKANA,MAGOMENI BARAFU NA TURIANI,MAKURUMULA,TANDALE MABATINI,KARUME,KIGOGO CCM,MURAHATI SANTOSI NK.VINGI HAVIPO TENA MATOKEO SASA VIJANA WETU HAWANA PAKUFANYIA MAZOEZI WENGI WANAISHIA CHINI YA MITI KULIPULIZA MATOKEO YAKE TUNA ZALISHA WACHEZAJI WENGINE MABANGE. NANI WA KULAUMIWA IPO HAJA YA KUFANYA EFORT YA KUTATATUA TATIZO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA.MDAU BIANKA DE CONOVA SOKA DE KULUBE,FROM GUASA AMBONI A.K.A IBO FAN.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 03, 2011

    Nilikuwa nasoma DSA nikaazima tshirt ya mshikaji nikawahi uwanjani mapema sana nikaonga askari wa mbwa nikaruka ukuta upande wa kaskazinikaribu na score board nilivorukia ndani askari mwingine akanidaka nikawa sina pesa ya kumwonga kaniweka mahabusu kutaka kumtoroka nikaangusha kofia ya akari kwa bahati mbaya. jesus! nilipigwa na askari kama mwizi na wakanichania tshirt ya mshikaji.karandinga likachelewa kufika askari kaniruhusu nikakae jukwaa kuu lakini upande wa Simba. sikuweza shangilia juu ya maumivu na nilikuwa kwenye wrong stand.ila at the end it worth it.Mpaka leo nimelaaniwa huwa na commute toka Reading mpaka Manchester kwa ajili ya kuona game live.Na kila ninapoingia uwanjani huwa nasikia nywele za shingo zikinisimama na sauti inabadilika inakuwaya mkwaruzo.The feeling is better than orgasm.Shukrani kwa Yanga kwani sababu ya jezi ya green and gold ndo hapo nilianza mapenzi na Man u na Kaizer chiefs. Ya away kit ilikuwaga kijani na gold enzi za akina King Cantona.

    Michu you can change Religion but not Football Team.Hivo wewe ni yanga Damu huamini jikate kama hautatoka kijani.
    ezi hizo hawa wachezaji walikuwa siyo role model ila watakatifu na yanga Dini.By the way sikuwa Commandoo kabla hamjaanza.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 03, 2011

    wachezaji wa zamani walikuwa na maumbo mazuri kimichezo (siha) si kama wa sasa. Ni kwa nini?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 03, 2011

    aaahh! nimesahau... wachezaji wa zamani walikua na maumbo mazuri kimichezo (siha) kulinganisha na sasa lani laifu ekisipentansi yao inakua fupi. Ni kwa nini?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 03, 2011

    ...Na itutu kigi (roadmaster) yupo wapi siku hizi?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 03, 2011

    Ahsante sana Mpangala kwa kutukumbusha mbali. Hata mimi nilikuwa Yanga damu, ila nilipunguza upenzi kati ya mwaka 91/92 ilipocheza na Simba kule Z'bar na ikafungwa nadhani bao 1-0,, hapo ushabiki ukapungua kwani niliumia sana sana,,
    Namkumbuka pia mdogo wangu marehemu alikuwa anaipenda Yanga sana tena akiwa mdogo, anatoroka nyumbani kwenda kwa jirani kusikiliza mpira kwenye redio (enzi hizo hata TV hakuna).
    Mungu amrehemu!
    Pia sikuwa nimefahamu kuwa wachezaji wa zamani watatu (Kwenye picha) wametutangulia! Mungu awarehemu pia!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 03, 2011

    Michuzi hizi picha za namna hii ziko kibao kule magazeti ya Uhuru na Mzalendo.Kachukue scan uwe unazibandika(Nina uhakika hazikuwa kwenye digital format).Mwaka 1985 na 1986,1987 nilikuwa nanunua sana magazeti ya Mzalendo na uhuru kuangalia picha za wachezaji kurasa za mwisho!!Nilipipenda sana timu ya Nyota nyekundu!!Wapiga picha za magazeti enzi hizo nawakumbuka sana Mwalimu Omar,Madanga S.Madanga,Ernest Millinga,Muhidin Michuzi?Mshambuliaji hatari Ayoub Mzee(Nyota nyekundu/|Simba) yuko wapi?

    David V

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 03, 2011

    Timu hii ilikuwa ni moto wa kuotea mbali, Mnyama alikuwa analamba nyasi kila kukicha, ah YANGA raha bwana

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 03, 2011

    RIP Gagarino, bado sijampata kiungo wa aina yako.Tangu upo AFC Arusha, Simba na mwisho yanga kipaji hakikuteteleka.Ukimbiaji wako wa madaha uwanjani ulikosa mfanoe.Mungu awalaze mahala pema mliotutangulia.
    Wachezaji wetu wengi laifu yao imekatishwa na UKIMWI.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 03, 2011

    Kweli siyo mchezo mimi mwenyewe nilikuwa katoto ila sitaisahau mechi kati ya YANGA na PAMBA ya MWANZA iliyofanyika uwanja wa TAIFA,PAMBA walipiga mpira mwingi sana karibia dakika 20 za mwanzo ikabidi kipa wa YANGA(kwa kweli simkumbuki jina mwenye kukumbuka naomba msaada)ikabidi azuge kiatu kina matataizo ikasababisha mchezo usimame kwa muda baada ya kurudi tena uwanjani YANGA walibadilika wakapiga mpira mwingi sana na hadi mpira ulipoisha YANGA walishinda goli moja kwa sifuri(1-0)mfungaji alikuwa KENNETH MKAPA alienda kupiga mpira wa kona ikaingia yenyewe siyo siri hawa jamaa walikuwa na uwezo mkubwa hiyo picha bado ATHUMANI CHINA tu sijui alikuwa mbali na mpiga picha,jamani naomba kuiona picha ya ATHUMANI CHINA taswira imenitoka.Siyo siri KENNETH MKAPA,ATHUMANI CHINA,METHOD MOGELA(FUNDI)HAMISI GAGA(GAGARINO)Hawa jamaa uwezo wao ulikuwa mkubwa sana nina uhakika katika wachezaji wa sasa hakuna atakaeweza kufikia uwezo wa hawa wachache niliyoorodhesha naongezea HUSSEIN MARSHA.Nina uhakika enzi zao ingekuwa ndiyo sasa tungewaona kwenye klabu kubwa za ULAYA.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 03, 2011

    jama amis kinye bado yupo ama?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 03, 2011

    Vijana wa siku hizi hawana nguvu, sababu toka kuzaliwa wanakula chipsi na piza tu. hawapati vyakula vya asili vya kujenga mwili. wakati huo shuleni tulijifunza aina za vyakula hata kwenye kisomo cha watu wazima

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 04, 2011

    Sio kweli kwamba vijana wa siku hizi hawana nguvu , bali mpira wa sasa sio na ule wa zamani wa manguvu na, kuumizana na ukiaangalia zama hizo ni wachezaji wachache sana waliweza kucheza kwa kipindi kirefu cha zaidi ya miaka mitano,mfano sasa hivi golikipa anlindwa sana sio kama zamani alikuwa anazongwa sana nakama wewe ni beki basi unakuwa hodari sana tena unasifiwa kwa kuwaumiza wenzio,sasa hivi beki akimrudishia kipa mpira kwa mguu kipa haruhusiwi kuudaka wakati zamani aliruhusiwa kwa maana hiyo kipa na mabeki walitumia muda mwingi kupoteza wakwati na pia mpira wa zamani haukuwa na mbinu nyingi kama hivi sasa ,hivyo kufananisha na wasasa sio sawa.Ila kwa sasa michezo haithaminiwi tena kama zamani hakuna viwanja vya michezo kama zamani,hakuna park za kupumzika,hakuna michezo ya mashulekama zamani, mfano sekondari za tanzania na zambia,michezo ya urafiki wakati wa pasaka nakumbuka wachezaji wengi wazuri walitoka mashuleni.Vijana wetu wanajitahidi lakini hawana maandalizi mazuri ya kuwaendeleza kwani sehemu zote zilizokuwa za michezo hazipo tena mfano jangwani,biafra na tandika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...