Baada ya Globu ya Jamii kuanika hadharani  swiming puli la maji machafu yaliyotuama katika barabara ya Upanga kati ya YMC na Bank ABC kwa takriban mwaka mmoja, swiming puli hilo limefanyiwa kazi na kuondoka kama inavyojionesha. Tunajiuliza hivi kwa nini dimbwi hilo kubwa na mahandaki yaliyopo lilikuwepo hapo. Kumbe kazi haiwezekani kufanyika mpaka tushikiane bakora? Huu utamaduni wa uvivu na kukosekana kwa uwajibikaji inatakiwa ikome katika sekta zote, na ikiwezekana wahusika wawe wanawajibishwa kwa uzembe
 Huwezi amini kwamba hapa palikuwa na swiming puli  siku tatu zilizopita.
Wafanyakazi wakirekebisha mambo palipokuwa na swiming puli hilo. Libeneke Oye!

Kwa taswira za awali za swiming puli hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2011

    Ni vyema lakini ungetuonyesha 'before' na 'after'. Kwenye picha ya juu kuna bango jekundu linaonekana, kwenye picha ya chini limepotea na linaonekana bango jengine, jee ni sehemu ile ile kweli?

    Halafu siku hizi hawa jamaa wanafanya kazi kwa kuzima moto. Ukiwasema kwenye vyombo vya habari ndiyo wanakurupuka na kutengeneza haraka, ukinyamaza ndiyo imekula kwenu. Hivi tutafika kweli?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2011

    Congrats Globu ya jamii - wewe una special power to bring about change in our country. This was a small victory - tafadhali please fight for all the mauaji kwenye mabarabara zetu - creat a special movemenet, so that mawaziris watatusikiliza and perhaps improve transportation and save lives of tanzanians...good job michuzi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2011

    Wewe anony wa kwanza mshamba nini? Nyie ndio mnaotoka Nanjilinji na kwenda ulaya moja kwa moja bila kupata 'semina elekezi ya namna ya kuishi mjini. Yaani hata Lindi mkoani inaonesha hujafika, achilia mbali Dar. Na huko uliko kama ni London basi ni kijiji nje ya Cardiff. Sie tunaoijua Dar, yaani ma-Born hia hia tunajua hapo ndipo. Hayo mabango unayajua wewe na mjomba wako wa Nanjilinji. Mijitu mingine bwana! inabooooaaaaaaa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...