Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, Mfalme Mswati III wa Swaziland na Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakuu wan chi Wanachama wa Jumuiya ya uchumi Kusini Mwa Afrika SADC, leo jioni Santon,Johannesburg, Afrika ya Kusini
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akijadiana jambo na Mfalme MswatiIII wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa SADC unaofanyika SANTON, Johannesburg, Afrika ya Kusini.Katikati aliyesimama ni Mkuu wa Itifaki Balozi Antony Itatiro. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Nchi Wanachama wa Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) hivi karibuni wataanza kunufaika na fursa za kibiashara zitokanazo na kuanzishwa kwa Eneo Huru la Biashara.

Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi Wanachama za Utatu wa COMESA-EAC–SADC unaotarajiwa kufanyika kesho (tarehe 12 Juni, 2011) katika ukumbi wa Sandton Convention Centre, Johannesburg, Afrika Kusini, utazindua rasmi majadiliano ya Eneo Huru la Biashara la Utatu wa Jumuiya hizo.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi za Utatu, unatarajiwa kupitia taarifa ya Mkutano wa Pili wa Baraza la Mawaziri wa Utatu wa COMESA – EAC – SADC, Kusaini Azimio na Kuzindua Rasmi Majadiliano ya Eneo Huru la Biashara la Utatu.

Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeshiriki katika mikutano yote ya maandalizi kabla ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi. Ujumbe umeshirikisha pia Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar wakiwemo Mh. Dkt. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Mhe. Dkt. Abdulla Saadalla, Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Cyril Chami Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Nassor Ahmed Mazrui Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Zanzibar

“Nchi Wanachama wa Utatu wa COMSA-EAC-SADC zitaharakisha mchakato unaoendelea ili kufikia lengo lililokusudiwa la kuanzisha Eneo Huru la Biashara mapema iwezekanavyo, na kukuza utekelezaji wa mpango wa uendelezaji wa miundombinu na biashara” Alisisitiza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuwasili Mjini Johannesburg.

Utatu wa Jumuiya za COMESA-EAC-SADC unajumuisha Nchi Wanachama 23 ambazo ni zaidi ya nusu ya Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika. Eneo huru la biashara katika Utatu wa Jumuiya hizi lina idadi ya watu takriban millioni mia sita (Mil. 6), hii ikiwa ni fursa kubwa katika soko lililopanuka.

Nchi 19 Wanachama wa COMESA ni Burundi, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Djibouti, Egypt, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Libya, Madagascar, Malawi, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Sudan, Swaziland, Uganda, Zambia, Zimbabwe. Nchi 5 Wanachama wa EAC ni Burundi, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Muungano waTanzania na Uganda.

Nchi 15 Wanachama wa SADC ni Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo (DRC), Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Seychelles, South Africa, Swaziland, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zambia na Zimbabwe.


Imetayarishwa na   Mindi Kasiga-Tarimo, Afisa Mawasiliano Mwandamizi,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Safarini Johannesburg, Afrika Kusini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2011

    Aibu gani hii ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje hajui idadi ya nchi wanachama wa Muungano wa Afrika. Hovyo, yale yale ya Utanzania wetu. Kama huo utatu una nchi 23, basi si zaidi ya nusu ya nchi wanachama wa Muungano wa Afrika kwani wenyewe una mataifa yote ya Afrika isipokuwa Moroko, yaani, 53 - 1 = 52. Hata ukiitoa Somalia, bado unabaki na 51. Hata ukiitoa nchi yoyote nyingine, unabaki na 50. Sasa 23 kivipi ni zaidi ya nusu? Labda kama alitaka kusema 33. Kwa vyovyote vile huu ni uandishi wa kibabaishaji kwa hautaji idadi ya nchi za Muungano wa Afrika.

    Inakera mno mno.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2011

    naona bodigadi mmoja tuu!!!

    hivi tutabadilika lini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...