Mazishi yakiendelea majira ya 3.45 usiku kwa kutumia mwanga wa taa na tochi za simu baada ya kupatikana kwa makubaliano kwa mme kukubali kuozeshwa maiti ya mkeweMkuu wa shule ya Star mjini Iringa Jesca Msambatavangu ambaye ni kada wa CCM (kulia) akiwa ameshika spedi kusaidia kufukia mwili wa marehemu Magreth Ray Mng'ong'oDiwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi (chadema) wa pili kulia akiwa ameongozana na ndugu wa marehemu na wananchi wakitoka kuzika majira ya saa 4 kasoro usikuBaba mzazi wa marehemu mzee Mng'ong'o akifurahia fedha za mahali alizomtoza mkwe wake baada ya mtoto wake kufariki kwa kunywa pombe na wenzake

Habari na Picha na Francis Godwin
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauni ni methali ambayo ni ngumu kuielewa iwapo halijakukuta la kukukuta ila kwa waliopatwa kukutwa kwao si methali japo si wengi wamekutana na methali hii ila kwa mwalimu Raymond Twanzihilwa wa shule ya msingi Ipogolo mjini Iringa kwake methali hii imetimia .

Kifo cha Mkewe Magreth Raymond Mng'ong'o (40) kimeweza kumthibitishia kuwa dunia ni watu na kuwa watu na viatu wasio penda ya watu baada ya leo kujikuta katika wakati mgumu zaidi baada ya baba mkwe wake kutaka kaburi lifukuliwe na maiti kurudishwa nyumbani eneo la kitwiru ili mwalimu huyo aweze kukamilisha kulipa mahali kabla ya mwili huo kuzikwa .

Utata huu ulianza majira ya saa 2 asubuhi wakati taratibu za mazishi zikifanyika na wananchi wakiwa katika harakati za kwenda kuchimba kaburi ili kumzika maheremu huyo aliyefariki ghafla kwa ugonjwa na BP akiwa nyumbani kwake Kitwiru mjini Iringa.

Baba Mkwe wa mwalimu Ray aliuambia mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao ulipata kushuhudia tukio hilo LIVE kuwa mwalimu huyo hakukamilisha mahali wakati akimuoa binti yake hivyo yeye kama baba mzazi hakuwa tayari mwili huo kuzikwa Iringa kabla ya kutolewa mahali na hivyo kutaka maiti hiyo kufukuliwa ili ikazikwe Kilimanjaro kwa ngudu zake ama Njombe ambako ni nyumbani alikozaliwa marehemu huyo na kuwa iwapo watalazimisha mwili huo kuzikwa hapo wasishangae kuukuta mwili huo katika nyumba za wale walioshiriki kuzika.

Mwalimu Ray mwenyewe akizungumza na mtandao huu alisem akuwa mzee huyo alimfanyia unyanyasaji wa hali ya juu kwani mahali yote alikuwa ameitoa toka mwaka 1990 alipomuoa mwanamke huyo na sehemu ya mahali iliyobaki ambayo ni shilingi 90,000 baba mkwe alifika Iringa na kuomba kupewa baiskeli .

Hata hivyo alisema kutokana na hatua ya mzee huyo kung'ang'ania mahali mbele za watu na kuzuia maiti hiyo kuzikwa ndipo kwa upande wake alipoamua kujifungia ndani ya nyumba yake na kutaka kujiua kabla ya wananchi kufika na kumlipia mahali ya shilingi 500,000 na ushehe .

Viongozi wa serikali ya mtaa huo wa Kitwiru na diwani wa kata ya Kitwiru Ally Mbata walisema kuwa kutokana na mgogolo huo walilazimika kutoa taarifa polisi ili kuomba ulinzi zaidi eneo hilo baada ya baadhi ya vijana kuanza kuishambulia kwa mawe nyumba yenye maiti kama njia ya kupinga hatua ya baba mkwe kutoza mahali maiti .

Huku diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi akisema kuwa alifanya jitihada za kupiga simu polisi ili kuomba ulinzi japo hajapendezwa na hatua ya polisi kuchelewa kufika eneo hilo.

Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ulishuhudia mazishi ya marehemu huyo yakifanyika bila ibada kama ilivyokuwa awali huku vijana wakifukia kaburi kwa kutumia mikono bila jembe wala spedi kwa takribani dakika 20 hivi kabla ya vifaa hivyo kupatikana .

Mwanga wa taa za chemli na tochi ndizo zilizotumika kuongeza mwanga makaburini hapo huku mbalamwezi iliyokuwepo awali ikionekana kufifia baada ya kujitokeza hali ya kisayansi katika mwezi huo na ghafla kutokea kiza katika eneo hilo.

Baada ya kurejea kutoka kuzika majira ya saa 4 usiku na mfiwa mwalimu Ray kuwashukuru wananchi zaidi ya 200 waliojitokeza kuzika maiti hiyo ,wananchi hao hasa vijana walifunga kwa muda barabara kuu ya Iringa-Mbeya huku wakizuia magari kupita likiwemo gari ya askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dr Owdernburg Mdegella ambaye alikuwa akitokea upande wa Mafinga kuja Iringa mjini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2011

    dunia imekwisha! huyo baba ana laana..

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2011

    Huu ni unyanyasaji mkumbwa kudai mahali kwa marehemu si haki hata kidogo.Mzee huyu anatamaa tu ya hela angesubiri mazishi yafanyike kwanza ndipo atoe hoja yake,ebu tazama huyo kijana mbele ya jeneza la mpenzi wake ambaye hatamwona tena na huku baba mkwe anafurahia kikombe cha pombe,huku mkwe wake anataka hata kujiua. pole sanaaaa kwa yaliokukuta.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2011

    huyu baba aliyetoza mahali marehemu siyo binadamu wa kawaida tunaambiwa tusamehe marehemu huyu baba hana roho bali ana uroho!hakika naamini huyu baba hata kufa!kwa hili alilofanya Mungu atamlipa .Pole sana mwalimu Ray haya ni ya dunia Mungu atakusaidia kipindi kizito umepita pole sana na Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu peponi aameni

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2011

    NAFIKIRI WOTE HAMJAJUA TATIZO LIPO WAPI...HUYO BABA NI MTU SANA TENA KAMA MIMI NA WEWE...HAWA NDIO WATU WANAOONGOZWA NA SERIKALI YA TANZANIA....KUNDI LOTE LILIOENDA KUZIKA BILA SHAKA KUNA WALIOSOMA JAPO MPAKA DARASA LA SABA ILA ELIMU YAO HAIJAWASAIDIA KITU....KUNA SHIDA SOMEWHERE...HASA KWENYE SEKTA YA ELIMU.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2011

    kipindi kugumu ktk maisha ni pale unapopatwa na msiba tena wa mtu wa karibu yako na wapo watakao kuumiza kwa vitendo vyao,hii ni habari ya kusikitisha sana na pole sana mwalimu Ray,nimependezwa na wadau deni ni elfu 90 na wadau wamechanga laki 5 safi na kama pesa mzee achukue na ubinadamu umekwisha,very sad.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 16, 2011

    Huyo mzee kwanza gharama ya kusafirisha maiti haijui?. Mngemuacha tuu muone kama angeweza safirisha hiyo maiti aibu tupu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 16, 2011

    Baba tamaa ya hela, utajibu maswali "juu" ukifika huko.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 16, 2011

    Pole sana Mwl. Ray, walimwengu ndivyo tulivyo, aibu hatuna, ubinadamu umeenda porini kwa wanyama!
    Malipo ni hapa hapa duniani,,,
    Mi siamini kama kweli alikuwa akidaiwa laki 5, na kama nimesoma vizuri mahari iliyobaki ilikuwa elfu 90 ambazo alinunuliwa baiskeli badala yake,
    Hizi ni tamaa tu,,
    Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!

    ReplyDelete
  9. Wote mlichangia hamjui mila za kulipa mahali.
    MATATIZO YA KUTO KULIPA MAHALI NI KAMA-
    1-Ukioa mwanamke bila kumaliza mahali ujue siku akifa mke wako,uwezi kumzika mpaka umalize mahali kwa kulipa ndipo mzike
    2-Wengine wanaoleshwa na maiti kwa sababu za kukaa na mwanamke usiye mtoa mahali kwa wazazi wake.

    MUHIMU VIJANA TULIPE MAHALI KAMA KAWAIDA NA TUSIKAE KINYUMBA NA WANAWAKE TUSIWALIPIA MAHALI JAMANI HIYO NI FUNZO KWA WATU WOTE NAOMBA MJIBU KAMA UNA HOJA ZA MSINGI

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 16, 2011

    Jamani sio MAHALI ni MAHARI kwa mujibu wa habari hii! Mahali na Mahari ni vitu viwili tofauti sana...!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 16, 2011

    mimi kama Mtanzania hapa ndio najiuliza sheria iko wapi?hapa ni inaonyesha kabisa jinsi wanawake wanavyoonewa...hakuna mtu ambaye angependa kufukuliwa in the name of dowry..a stupid price tag kept on ones' head..i think mida kama hii tuwe kama wahindi and pass a dowry prohibition act....this man is an embarrassment to all men!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 16, 2011

    WEE FRANCO KUMBUKA KUOANA NI UAMUZI WAWATU WAWILI WAZIMA NA WENYE UTASHI. HUYO MZEE NI KWAMBA AMEMPATA TU HUYO RAY. KAMA INGEKUA MIMI NA NINA HAKIKISHA CHETI CHA NDOA NINACHO NIGEMTOA NISHAI HUYO MZEE NA IMANI ZAKE ZA UCHAWI. MIMI NASHAURI VIJANA WENGI FUNGENI NDOA KWA MKUU WA WILAYA MUWE NA VYETI VYA NDOA HAPO HAMNA MTU ANAYEWEZA KUWAADHIRI KAMA HILO BABU CHAWI PUMBAVU. HAKUNA TATIZO LOLOTE KUMUOA MWANAMKE BILA KUTOA MAHALI WATASEMA MWISHO WATAZOEA TUU. KUDDA DDEKI WEE MZEE MALIPO YAKO UTAPATA HAPAHAPA DUNIANI. HUKUTAKIWA KUONGEZA WALA KUPUNGUZA IWEJE UCHUKUE LAKI TANO BADALA YA BADALA YA ALFU TISINI

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 16, 2011

    THis is unbelievable. Dunia imefika pabaya. Tamaa mbaya jamani.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 16, 2011

    HUYO MZEE NINGEMJUA NINGEMPA PONGEZI SANA AMEFANYA KITU KIZURI SANA FUNDISHO KWA SERENGETI BOYS MNAOOOA BILA KUJIPANGA SAFIIIIIIIIIII HIYO .NI HAKI YAKE KABISAAAA JAPO FEDHA NI MAKARATASI HATA SASA HIVI HANA TENA ,ILA SIO MNAFIKI

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 16, 2011

    jamani inasikitisha,hela haina utu

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 16, 2011

    watu wa Iringa ndo tabia zao, wanapenda sana mali

    ReplyDelete
  17. MBONA WATU WA BUKOBA HAMSEMI KUHUSU MAHARI JAMANI tena watu wa IRINGA NI AFADHALI KULIKO BUKOBA WAHAYA.
    Mhaya akizaa nje ya ndoa hata nyumbani kwao haendi mzazi hamkaribishi mpaka alipe faini ya mbuzi.
    MWISHO NAFURAHI MTOA HOJA MMOJA ANAJUA MTATIZO YALIYOMPATA MWL NI YA KWELI NA NYIE MNAOSEMA DUNIA INAENDA WAPI kwa mfano wewe unamtoto wako wa kike amechukuliwa na mwanamme bila kulipa mahari wewe utafurahi? kama utafurahi basi jibu hoja KWAMBA HUYO MZEE NI HAKI YAKE NA ULIZA KWA NINI WALICHANGA WATU HELA ILI MAITI IZIKWE msiwe na papara ya kujibu uliza tatizo kwa wazazi wako wakuambie MIE NAYAJUA HAYO NA NAKUSHAURI KAMA UNAISHI NA MWANAMKE USIYE MTOLEA MAHARI BASI NENDA KALIPE UCHEKI BOB HACHA YASIJE YAKAKUKUTA NA HAO SHEMEJI ZAKO AKIFA UTAWAONA WATAKAVYO KUJA MBOGO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...