Serikali imewataka wananchi wa Zanzibar kuchukua tahadhari kwa kipindi hiki kufutia kuwepo kwa uwezekano wa kutokea kwa tetemeko la ardhi baada ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam kutokea mtikisiko siku ya Ijumaa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ambayo imesainiwa na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dk Khalid Mohammed imesisitiza ulazima wa wananchi kutoa taarifa kwa Mamlaka zinazohusika wanapoona jambo si la kawaida katika shughuli zao.

Dk. Khalid amesema taarifa za kitaalamu zinaonesha kuwa upo uwezekano wa tetemeko hilo kutokea tena, hivyo ingawa tetemeko hilo halikuripotiwa katika maeneo ya Zanzibar kutokana na umbali uliopo kutoka eneo lilipoanzia tetemeko hilo hadi Zanzibar.

Amesema Juni 10 mwaka huu saa 5:28 asubuhi lilitokea tetemeko katika bahari ya Hindi umbali wa Kilomita 52 Kusini Mashariki ya Dar es Salaam na Kilomita 105 Kusini Mashariki mwa Zanzibar likiwa na ukubwa wa kipimo cha Richater 4.8 ambalo lilitokea katika kina cha kilomita 10 chini ya bahari.

Amesema bado Zanzibar ipo katika tishio la kupata tetemeko hilo endapo litatokea tena, hivyo Serikali inawataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kipindi hiki na kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika.

Katibu Mkuu huyo amesema Serikali inaendelea kufuatolia mwenendo wa matukio hayo kupitia Taasisi na vyombo vinavyohusika na itakuwa inatoa taarifa mara kwa mara. Dk Khalid alisema Serikali inaendelea kusisitiza kwamba wananchi waendelee kusikiliza na kufutialia taarifa na maelekezo yatakayotolewa juu ya suala hili na kuchukua hatua zinazostahiki.

IMETOLEWA NA:

IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR

12/06/2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2011

    Wazenji Msiogope tetemeko halitokei tena. Lile Dar lilitokana na dhambi ya uasherati aliyofanya Mboke akiwa BBA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2011

    Je serikali ya Zanzibar haina tohuti mpaka ikope ya Michuzi? Aibu banaaa!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2011

    Wacheni upumbavu wa siasa .
    Wananchi wanapaswa kufanya nini hasa, wanapoona dalili za tetemeko .
    You would expect such a serious issue to be explain clearer don't you ?
    Tuambieni how big the danger is and how are we supposed to react .
    namba gani za simu tupige, email address gani tutumie , na whether we are not suppose to sleep in houses or not during the time .
    From the government point of view this is very lazy indeed .
    Please be clearer
    Mungu atusaidie katika mashaka haya.
    Abdul Diriye

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 12, 2011

    HATUA ZIPI ZINAZOSTAHIKI NA TAHADHARI GANI ZINABIDI CHUKULIWA NA WANANCHI WA ZANZIBAR DHIDI YA TETEMEKO LA ARDHI. ITAKUWA VIZURI ZAIDI KAMA MWANDISHI WA IDARA YA HABARI KUWEKA HATUA NYETI HADHARANI KWANI KILA RAIA SI MWENYE KUJUA CHA KUFANYA DHIDI YA TETEMEKO. NCHI KAMA MAREKANI INAFUNDISHA MASHULENI AU MAKAZINI HATUA ZA KUCHUKUA DHIDI YA VIMBUNGA(TORNADO AU HURRICANE)ZINAZOWASHAMBULIA KATIKATI YA MWAKA. KWA HIVYO MAELEZO YA SERIKALI YAWE MAPANA ZAIDI ILI KUMSAIDIA MWANANCHI ANAYEJISHUGHULISHA NA KUPARA MIWA WA MCHAFUKOGE, MCHAMBAWIMA, UZINI, TUNDUNI APATE KUJUA CHA KUFANYA NA HIVYO KUSAIDIWA ZAIDI.

    THE ONE WHO CARES THE CARELESS.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2011

    At least huyo katoa taarifa angalau fupi. Huku bara hata hiyo fupi haipo! Wanataka kujenga Maghorofa 2000 eneo dogo la Upanga. Believe me the project will be a failure. Mark my words!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...