Ni simulizi ya mwandishi wa habari aliyejijengea umaarufu mkubwa kwa jamii yake kwa kuibua yaliyofichika na kuriport matukio kwa wakati muafaka"DONDA LA KICHWA MKAGUZ MKONO".Vidonda:-mauaji ya raia,madawa ya kulevya na ufisad,ufanisi wa mwandishi huyu uliacha maswali mengi kwa jamii yake,huyu ni mtu wa aina gan?anavitu gani vinavyomfanya afanye kazi kwa ufanisi?kutana na maskali(wapelelezi)waliobobea katika uchunguzi makimi na kugundua ni kinaendelea..........dont misss ur copy.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2011

    Anko Michuzi, najua nitaitwa Muosha kinywa, lakini naomba usibanie hii. Hiyo tafsiri hapo imepotoshwa kwa kiasi kikubwa hakuna hata ukaribu kati ya Darker than Night vs. Giza ni Zaidi ya Usiku. Mwandaaji acha ubahili tafuta watu wakusaidie kufanya tafsiri sahihi ili utoke na kazi bora si bora Kazi. Kama huna pesa omba msaada kwa wadau wa Lugha watakusaidieni badala ya kupotosha lugha. Hili ndio tatizo la mtayarishaji kufanya kazi zote yeye mwenyewe....NGOJA NA WENGINE WASEME, YANGU NI HAYO TU.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2011

    Mie si mpenzi wa filamu za bongo ila kuna wakati nalazimika kuziangalia hasa ninaposafiri kwa mabasi yaendayo mikoani. Mambo makubwa matatu (kasoro) ya hizi filamu ni urefu wa tukio usio wa lazima, kutokua na taaluma au ubunifu katika kuonyesha matukio ya kupigana au kurushiana risasi na tafsiri mbovu/isiyo sahihi kwa sentensi zitumiwazo.

    Ushahidi wa hilo la tatu ni hiyo tafsiri ya jina la filamu hiyo hapo juu. Hata hivyo, subtitles nyingi huwa hazizungumzi kile kinachozungumzwa na sentensi zinazotamkwa. Mfano 'you is good boy' ikiwa kama tafsiri ya 'wewe ni kijana mzuri'.

    Maoni/ushauri
    1. Hakuna haja ya kurefusha matukio ili kupata Part 1 na 2 ya filamu. Ujumbe ukifika hauna haja ya kuendelea kuonyesha kitu kile kile.

    2. Tuache kuigiza filamu za kupigana au kurushiana risasi hadi hapo tutakapokua na taaluma au vifaa. Pia, kuwe na uhalisia katika mavazi hasa ya kipolisi. Haifurahishi kuona nguo za polisi ambazo hazijapigwa pasi (la sivyo kutokunyooshwa kwa nguo hizo iwe inaleta ujumbe kusudiwa).

    3. Watengenezaji wa filamu watumie wataalamu wa lugha kwa kutafsiri. Wengine hawahitaji pesa nyingi kama inavyofikiriwa, kuandikwa jina tu katika filamu tu yatosha.

    Huwa mara nyingi najiuliza kama hizi filamu zinapitiwa (review) kabla ya kuzileta sokoni. Kama ndiyo, basi hao tuangalie sifa za hao wanaopitia filamu au vigezo wanavyotumia.

    Tutafika tu.

    Ignorant

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...