Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Henry Salewi (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Balozi Khamis Kagasheki kwenye uwanja wa Kaitaba ambaye pia alikuwa ni mmoja wa walioudhulia fainali ya Salewi Cup kati ya timu za kata za Bakoba na Bilele.
Kamanda Salewi (pili kushoto) akiteta jambo na Balozi Kagasheki wakati wa fainali ya Salewi Cup, kulia kwao ni baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kagera.
Kachero wa Jeshi la Polisi akiwa na manati aliyokuwa amemnyang'anya mmoja wa shabiki walioudhulia fainali ya Salewi Cup kati ya timu ya Bilele na timu ya Bakoba,kwenye uwanja wa Kaitaba,mjini Bukoba.
baadhi ya wachezaji wa timu za kata ya Bilele na Bakoba wakionyesha umahili wao wa kusakata kabumbu.
sehemu ya umati wa wakazi wa manispaa ya Bukoba walioshuhudia fainali ya ligi iliyoandaliwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera,Henry Salewi, fainali hiyo ilikuwa kati ya timu ya kata ya Bilele na Bakoba ambapo timu ya Bilele iliibuka na ubingwa wa ligi ya Salewi Cup kwa kuinyuka Bakoba bao 2-0, fainali hiyo ilifanyika katika uwanja wa Kaitaba,Bukoba.Picha na Audax Mutiganzi,Bukoba
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...