Ankal akiwa na DJ Luke Joe wa Globu dada ya Jamii ya Marekani ya Vijimambo baada ya kukubaliania kufanya kazi kwa ushirikiano jijini Washington DC. Vijimambo ni globu ambayo imekuja juu sana kwa habari za ughaibuni na nyumbani, ambapo mwendeshaji wake DJ Luke Joe, pamoja na kupiga boksi pia hujishughulisha na masuala ya muziki akiwa kasheheni vyombo vya kisasa na collection iliyotukuka ya Old Skul na New Skul. Katika mkataba huu DJ Luke Joe ndiye anakuwa mwakilishi wa Globu ya Jamii nchini Marekani, ambapo wadau wakitaka kuwasiliana na Globu ya Jamii kwa lolote lile, liwe habari, taswira na hata matangazo, wamwone yeye kupitia 
 Ankal na DJ Luke Joe wakiwekeana sahihi mkataba wa ushirikiano wa Globu ya Jamii na Vijimambo katika nyanja ya habari na matukio. Hafla hii fupi imefanyika kwenye ofisi za Idhaa ya Kiswahili ya Voice of America (VOA) jijini Washington DC, shuhuda akiwa mtangazaji mahiri wa idhaa hiyo Bi Aida Issa
Ankal na DJ Luke Joe wakibadilishana mikataba baada ya kuisaini, shuhuda akiwa mtangazaji wa VOA. Bi Aida Issa. Globu ya vijimambo inapatikana
http://lukemusicfactory.blogspot.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2011

    Mbona anatumia blogspot na yeye yupo ughaibuni!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2011

    kumbe anko na wewe bitozzzzz mana hilo poz nomaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2011

    Jamaa enjoy vakesheni
    Usisahau kumpa mjomba salam zetu.mwambie aje Bongo kututembelea
    PS. Usisahau kupima macho, naona wahitaji reading glasses
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2011

    Contract hiyo ni batili maana hakuna kilichoandikwa! h aha ha! Ankal miyeyusho.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2011

    MICHUZI NIKUMBUKE KWA KUNIPA SHAVU JAPO, HILO T-SHIRT KWA AJILI YA KUMBUKUKUMBU.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2011

    Ankal hiyo T-shirt naona haizeeki badala yake unazeeka wewe! Na hapo pembeni mikonoz vipi haikubaliki?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2011

    Anko mbona hufungi vifungo vya tshirt, au ndo fashion kuvaa hivyo. maana wengine hapa washamba, tumezaliwa tandahimba na kukulia huko hata mbeya tu mjini hatujawahi kufika

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 30, 2011

    Ankal kuna kipindi ulikuja na website safi sana iitwayo michuzipost.com na ukasema uko partership na mdau mmoja wa huko Ukererewe. Hata hivyo hivyo site ilipotea bila taarifa yoyote. Mkuu tunaomba ufafanuzi wa ile site. Kwa kweli ilikuwa site nzuri sana ila sijui kwa nini haipo tena hewani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...